einstein newton
JF-Expert Member
- Oct 18, 2015
- 1,969
- 2,672
hivi wanasarufi katika isimu ya lugha ya kiswahili,hii sentensi ni sahihi au si sahihi? "samahani kaka,naweza kukuuliza swali?" NB:katika fikra zangu,nimeona kuwa hii sentensi ina makosa ya "kisemantiki",yaani haijafata mtiririko wa kimawazo au logic,haiwezekani mtenda wa hiyo sentensi aombe kuuliza swali wakati huohuo ameshauliza swali.naweza kuwa sahihi?na kama nipo sahihi na sentensi ikaonekana ina makosa/kosa nililolitaja hapo juu,je muundo sahihi wa hii sentensi ulitakiwa uweje?kazi kwenu wakuu.