ENGLISH TUTORIAL: Jifunze aina za sentensi na jinsi ya kuziunda kwa lugha ya kingereza

Da'Vinci

JF-Expert Member
Dec 1, 2016
35,673
106,768
ENGLISH TUTORIAL

Mate,
tatizo la kuelewa kuandika na kuongea na lugha ya kingereza ni suala mtumbuka. Wengi wetu hasa tuliopita shule za uswahilini bado lugha yetu haipo sawa. Hivyo basi ningependa kushea nanyi module hii japo kwa uchache. Nitazungumzia zaidi upande wa sentesi.

NB. Ili nieleweke vizuri nitatumia lugha ya Kiswahili na kiingereza katika kufundisha, karibu.

SENTENCES

Ni kundi la maneno ambalo hutoa maelezo yenye maana au ni kundi la maneno lenye kutoa ujumbe wenye maana. Hivyo basi maneno ili yaitwe sentesi lazima yatoe maana yenye kueleweka.

Examples:

Hello there, My name is Da’Vinci

I’m Jf Expert member

FRAGMET

Ni kundi la maneno ambalo linafanana na sentence lakini hua halina maana yoyote.

Examples:

Nilipojiunga JF member wote wa FB wakaanza kulia, ndipo magari yalipogongana huku waumini wakipiga makofi kushangilia goli lililofungwa pale barababara ya lami.

She is handsome himself me why?

TYPES OF SENTENCES

Katika aina za sentensi, sentence zimegawanywa katika makundi mawili ambayo makundi hayo ugawanywaji wake utatokana na mahitaji yako wewe mtumiaji wa sentesi hii. Sentensi zimegawanywa kwa kuzingatia matumizi na maundo wa sentensi.

Kwa kuzingatia matumizi (function/purpose) ya sentensi, sentensi imegawanywa katika makundi haya.

Kwa kuzingatia matumizi ya sentensi, sentensi zimegawanywa katika makundi haya.

DECLERATIVE SENTENCE

Are the sentences that tell about facts,opnions and other statement.

Examples:

Da’Vinci is Jf expert member.

Da’Vinci loves you all.

IMPERATIVE SENTENCES

Ni aina ya sentensi ambayo hutoa amri au ombi Fulani. Mara nyingi sentensi hizi huishia na alama ya mshangao(!)

Examples:

Close the door.

Get out.

Please sir may I come in!

INTEROGATIVE SENTENCES

Ni aina ya sentensi ambayo lengo lake ni kupata maelezo Fulani kwa kuuliza swali au ni sentensi inayouliza swali. Siku zote huishia na alama ya kiulizo (?) katika aina hii ya sentensi tunajikita zaidi katika WH question, wh question ni kipengele kipana hivyo tutagusa mifano tu juu juu.

Examples:

What is jamiiForum?

Who is Da’vinci?

Are you jf member?

Do you know?

EXCLAMATORY SENTENCE

Ni aina ya sentensi ambayo huonyesha hisia, siku zote huishia na alama ya mshangao (!)

Examples:

Oooh! My God she died

I love you!

I hate you!

The End…

Point to ponder

Cluase

Ni sentensi zilizoundwa na mtenda/kiima(subject) na kitenzi (verb)

Independent Clause

Ni aina ya sentensi ambayo inaweza kusimama pekee yake na kuleta maana bila ktegemea sentensi nyingine.

Example

I’m writing.

They are coming.

Dependent Clause

Ni aina ya sentensi ambazo hua hazitoi maana kamili ya santensi hivyo hutegemea sentensi nyingine ili ziweze kuleta maana iliyokusudiwa.

Examples:

If you can work on Sunday

Then his sister came

After that I started to fall in love

Kwa mifano michache hiyo unaweza kuona katika sentesi hizo kuna habari Fulani imekosekana hivyo hazileti maana au inakua ngumu kujua kusudi sahihi la sentesi hiyo.

Kwa kuzingatia muundo (structure) wa sentensi, sentensi imegawanywa katika makundi haya.

SIMPLE SENTENCE

Hii ni aina ya sentensi ambayo huundwa na Independent clause moja. Technically Independent sentence ndio simple sentence

Example…

Life is Unfair

I have studied

Life is good.

COMPOUND SENTENCES

Ni aina ya sentensi ambyo huundwa kwa independent clause mbili ambazo huunganishwa kwa kutumia mkato na viunganishi (conjuction). Kwa wataalamu wa aina za maneno kwenye part ya conjuctions hapa tutatumia aina zote mbili za viunganishi ambavyo coordinating na subordinating conjuction. (F.A.N.B.O.Y.S/A.A.A.W.W.U.B.B.I.S)

Examples of compound sentnces

He studied hard but he failed

JF is for GreatThinker while FB is for kids

COMPLEX SENTENCE

Hii ni aina ya sentensi ambayo imeundwa kutumia independent clause moja na dependent clause moja au zaidi.

Examples

It was raining that’s why the football match was cancelled

Although he was so wealthy, he was still unhappy

He died because he was sick.

The End…

QUESTION TAG

Kwa wale wazee wa tookn’t you? Loven’t you? Eikeiei Question tag I got you covered, karibia kila tukivunja yai letu adhimu la lugha ya Kiswahili hua tunatumia Question tag bila kujua au tukiwa tunajua.

Q Tag ni swali ambalo huulizwa mwisho wa sentensi ili kupata ufafanuzi na uthibitisho wa sentensi iliyozungumzwa au itakayozungumzwa(clarification and confirmation of sentence), Mfano:

umependeza au sio?

Utakuja au hauji?

Unanipenda au huinipendi?

Ushakula au hujala?

HATUA ZA KUZINGATIA WAKATI WA KUUNDA QUESTION TAG
  • Tambua kitenzi (Verb) kipo wapi katika sentensi yako​
Mfano: go, eat,is,are, do , etc
  • Tambua aina ya kitenzi kinachopatika kwenye sentensi yako kama ni​
  • Auxiliary Verb; hapa utapata vitenzi visaidizi ambavyo ni..​
  • HAVE: has, had,have,haven’t ,hadn’t hasn’t​
  • DO: Do, does,did,didn’t to do​
  • BE: Is, are, am, was,were, been.​
  • Main Verb; hapa utaangalia angalia kama sentensi yako ina kitenzi kikuu ambavyo tunavifahamu. Kama go,run,eat etc​
  • Tambua sentensi yako ipo katika aina gani ya nyakati (Tense)​
  • Kama sentensi yako ipo katika muda uliopo (present tense) tambua nafsi ya kwanza na nafsi ya tatu umoja (1st and 3rd person singular)kwenye nafasi ya tatu umoja yaani he,she,it,name, weka Does.​
  • Kama sentensi ipo katika wakati uliopita (past tense) tumia vitenzi saidizi Be na Do. Angalia hatua ya pili kwenye Auxiliary verbs​
  • Tambua kama sentensi ni hasi au chanya (affirmative or negative)​
  • Weka alama ya kiulizo (?)​
Mifano mnaweza kuongezea kwnye comments……..
Vinjii​
 
Lugha ni ufanisi ahsante kwa somo kichwa yangu naijua tu!
Kitaalumu wanawake wanauwezo mkubwa zaidi ktk lugha kushinda sisi. Coz ubongo wao wa kushoto na kulia unachakata lugha isipokuwa sisi ni upande mmoja!..

Nini maana ya komenti yangu..?
Ni kutaka kupatia mwanga watu ili kujua ni njia ipi itakuwa nzuri zaidi kwako ukitaka kujua lugha yoyote.. Kuna watu niwepesi na wanauwezo wa kuzingatia hizo sheria sijui za grama na miundo ya sentensi n.k lengo kubwa ni kutaka mtu ajichunguze na kupi kutakuwa kwepesi kwake ktk kujua lugha husika... Wapo wengine ukiwafundisha hizo aina za sentensi sijui na nini hawayashiki!
Coz lugha kwa wengine ni kitu cha kuadapt ni Kama tabia! Na hapa ndipo ushauri wangu ulipo! Ila lengo langu si kupinga mada bali nakazia zaidi.. ni hivi ukishajua A B C za lugha fulani basi we unachofanya ni kutafuta watu Kama kina da Vinci wanaoijua hiyo lugha uanze kuongea nao kwa kutumia lugha husika.. kwa muda fulani utajajikuta umebeba Mambo mengi sana maana lugha ni kama urithi.. hizo grama zitagramika automatic tu maana hapo ni sawa umekaa kwenye gari na utaifata tu inavyoenda.. na Hilo ndo angalizo langu sorry Kama nimeenda nje na mada binadamu wengine ndo tulivyo mtusamehe bure tu.. ila msingi jijue wepesi wako ktk udokozi upi utakufanya udokoe mengi zaidi ktk lugha husika.
 
Grammar zitagramika zenyewe😄😄
 
Lugha ni ufanisi ahsante kwa somo kichwa yangu naijua tu!
Kitaalumu wanawake wanauwezo mkubwa zaidi ktk lugha kushinda sisi. Coz ubongo wao wa kushoto na kulia unachakata lugha isipokuwa sisi ni upande mmoja!..
NI kweli kabisa wanawake waponfasta kwenye kunasa na kuchakata vitu akilini mwao. Lakini tuliopita kwenye saikolojia ya watoto tuhaamini kati ya miaka 2 hadi 8 mtoto anauwezo miubwa wa kuelewa na kushika lugha yoyote atakayofundishwa. Zaidi tafuta maandiko ya Maria Montessori utapata mengi zaidi.
Nini maana ya komenti yangu..?
Ni kutaka kupatia mwanga watu ili kujua ni njia ipi itakuwa nzuri zaidi kwako ukitaka kujua lugha yoyote.. Kuna watu niwepesi na wanauwezo wa kuzingatia hizo sheria sijui za grama na miundo ya sentensi n.k lengo kubwa ni kutaka mtu ajichunguze na kupi kutakuwa kwepesi kwake ktk kujua lugha husika... Wapo wengine ukiwafundisha hizo aina za sentensi sijui na nini hawayashiki!
Kuha wengine ni wajuzi wa kuandika wengine kuongea zaidi
Coz lugha kwa wengine ni kitu cha kuadapt ni Kama tabia! Na hapa ndipo ushauri wangu ulipo! Ila lengo langu si kupinga mada bali nakazia zaidi.. ni hivi ukishajua A B C za lugha fulani basi we unachofanya ni kutafuta watu Kama kina da Vinci wanaoijua hiyo lugha uanze kuongea nao kwa kutumia lugha husika.. kwa muda fulani utajajikuta umebeba Mambo mengi sana maana lugha ni kama urithi.. hizo grama zitagramika automatic tu maana hapo ni sawa umekaa kwenye gari na utaifata tu inavyoenda.. na Hilo ndo angalizo langu sorry Kama nimeenda nje na mada binadamu wengine ndo tulivyo mtusamehe bure tu.. ila msingi jijue wepesi wako ktk udokozi upi utakufanya udokoe mengi zaidi ktk lugha husika.
No need to sorry mate.
Kwakweli ukitoka st kayumba unaweza kuongea hii lugha kwa ufasaha kiasi au kuandika si kazi nyepesi
 
Naona umebase zaidi kwenye Syntax . Ila hii lugha ni pana sana. Kuna ma phonology na semantics n.k

Ungegusia na huko mkuu kama phonology (matamshi) wengi wetu tumeathiriwa na lugha mama.
 
Naona umebase zaidi kwenye Syntax . Ila hii lugha ni pana sana. Kuna ma phonology na semantics n.k

Ungegusia na huko mkuu kama phonology (matamshi) wengi wetu tumeathiriwa na lugha mama.
Nikweli mkuu. Nilitamani nifike huko lakini hua napenda nielezee vitu clearly. Ingenibidi niweke michiro fulani ya jinsi ya kuumba maeno kwenye koo na ulimi. So nikaona nitawachaganya watu..
Kama vile elimu ya Do Re Mi Fa... Ti Do
 
Ni kweli mkuu, shukrani kwa somo
 
Ili tuelewe english lazima tufundishwe kwa kiswahili,yaani kutoka kwenye lugha fahamika kwenda kwenye lugha isiyofahamika.

Tumia lugha husika inayofahamika kufundisha lugha isiyofahamika.

Ila sisi kayumba tulikaririshwa ili tujibu mtihani sio tuweze kuongea,najifunza kizungu sasa hivi sitaki kukariri yaani unaelewa vizuri.

Sio kama zamani tulikosoma sisi unaambiwa ukoona too...to ukiona so .... that.

Kwa hyo ikitungwa sentensi wewe hauna haja ya kujua maana unaangalia tu kuna too hapo kati ? Ndio basi najaza to mbele ,tumesoma hivyo..
 
Dah kuongea tatizo ila kiukweli kuomgea ndo njia tamu zsidi
Kwakweli kuongea najua ika ugonjwa wangu Up kwenye kujieleza. Kiswahili tu shida kuongea mbele za watu english je?? Nikifungua mdomo tu kila kitu kinapotea ndio maana natumia muda mwingi kuandika zaidi
 
Back
Top Bottom