Wanaovaa vimini Kanisani kuvalishwa vitenge

diana chumbikino

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2018
Posts
428
Reaction score
368
b205f27ed024862c6fa8b471626c04b2.jpg

WAUMINI wa Kanisa Katoliki Parokia ya Ilomba Jimbo Kuu la Mbeya hawatoruhusiwa kuingia kanisani iwapo hawatatii agizo la kuvaa mavazi yenye heshima na yasiyodhalilisha utu wa mwanadamu. Kanisa hilo limesisitiza kuwa halitomwonea aibu mtu yeyote, atakayetaka kuingia kwenye ibada za Misa Takatifu akiwa na mavazi yasiyo staha, kwa kuwa mavazi ni sehemu ya ibada.

Kutokana na hali, inakusudia kuwavalisha kanzu, vitenge na khanga maalumu ili kukomesha tabia hiyo. Paroko wa parokia hiyo, Padri Peter Mambo alisisitiza hayo wakati akihubiri katika Ibada ya Misa Takatifu ya Jumapili, akieleza kuwa waumini wanapaswa kutofautisha aina ya mavazi wanayovaa na matukio. Padri Mambo amesema kumekuwepo na baadhi ya waumini wa kanisa hilo, ambao wamekuwa wakienda kushiriki ibada kanisani pasipo kuangalia aina ya mavazi waliyovaa, akisema wengi wao wanavaa nguo zinazodhalilisha utu wa binadamu na kutopendeza kuvaliwa wakati wa misa takatifu. “Lazima mtambue kuwa kuna mavazi ya disko, ufukweni, kwenye mikutano maalumu, maosini na hata kanisani ...kila vazi livaliwe sehemu yake...Ukivaa vazi la mkutanoni au kanisani wakati uko ufukweni utaonekana wa ajabu, vivyo hivyo na unapotuvalia nguo za disko au ufukweni kwenye ibada tunakushangaa,” ameseme Padri Mambo.

“Waumini mnapaswa kuelewa hilo sio kuvaa mavazi ambayo wewe mwenyewe yanakusumbua wakati ulivaa mwenyewe tafadhali tuheshimu misingi na taratibu za kanisa kwa kuvaa mavazi yenye staha,” amesisitiza. Amebainisha kuwa wapo waumini ambao mavazi yao yamekuwa yanawanyima, hata uhuru wa kukaa na hata kupiga magoti mbele ya altare, hivyo kutokidhi matakwa ya kuhudhuria misa kutokana na aina ya mavazi wanayotumia. Kwa upande wake, mmoja wa watawa ambaye jina lake halikupatikana mara moja, alisema ili kudhibiti uingiaji na mavazi yasiyopendeza kanisani utaratibu maalumu, unaandaliwa ili kuwadhibiti waumini wenye tabia kama hiyo.

Mtawa huyo amesema uvaaji wa mavazi yasiyohitajika kwenye nyumba za ibada, si kwa wanawake pekee, kwani wapo pia wanaume wanaova suruali chini ya makalio. Lakini aliongeza kuwa kwa wanawake wanaovaa nguo fupi na zenye kubana na kuonesha maumbile yao, utaratibu utakuwa kuwavalisha vitenge na khanga mlangoni, kabla hawajaingia kanisani, sambamba na kuwashonea kanzu maalumu wanaume.

“Ili kuwadhibiti watu wanaovaa nguo fupi na zinazobana tutakuwa tunakaa mlangoni na kuwavalisha vitenge kwa wanawake huku wanaume tukiwaandalia makanzu maalumu ili kanisani wote tuwe katika lengo moja la kusali na kumuabudu Mungu,” amesema. Amesema uvaaji wa mavazi hayo, sio tu unadhalilisha utu wa binadamu, bali pia humharibia utaratibu wa ibada muumini mwingine, kwani wakati mwingi watu wanajikita katika kumshangaa, badala ya kusikiliza neno la Mungu
 
View attachment 996627

I can not subject my life to illusions!
 
Naunga mkono kwa asilimia mia moja hoja hiyo. Huendi kanisani kuonyesha mwili wako. Unawafanya hata wengine waliokuja kusali waanze kufikiria mambo mengine. By the way, hilo kanisa ulilolitaja ni moja tu katika makanisa mengi yanayokuwa na msimamo kama huo. Mimi ni Mkatoliki na mlangoni mwa kanisa ninalosali zimebandikwa picha za mavazi yasiyoruhusiwa kuingia nayo kanisani.
 
View attachment 996627

WAUMINI wa Kanisa Katoliki Parokia ya Ilomba Jimbo Kuu la Mbeya hawatoruhusiwa kuingia kanisani iwapo hawatatii agizo la kuvaa mavazi yenye heshima na yasiyodhalilisha utu wa mwanadamu. Kanisa hilo limesisitiza kuwa halitomwonea aibu mtu yeyote, atakayetaka kuingia kwenye ibada za Misa Takatifu akiwa na mavazi yasiyo staha, kwa kuwa mavazi ni sehemu ya ibada.

Kutokana na hali, inakusudia kuwavalisha kanzu, vitenge na khanga maalumu ili kukomesha tabia hiyo. Paroko wa parokia hiyo, Padri Peter Mambo alisisitiza hayo wakati akihubiri katika Ibada ya Misa Takatifu ya Jumapili, akieleza kuwa waumini wanapaswa kutofautisha aina ya mavazi wanayovaa na matukio. Padri Mambo amesema kumekuwepo na baadhi ya waumini wa kanisa hilo, ambao wamekuwa wakienda kushiriki ibada kanisani pasipo kuangalia aina ya mavazi waliyovaa, akisema wengi wao wanavaa nguo zinazodhalilisha utu wa binadamu na kutopendeza kuvaliwa wakati wa misa takatifu. “Lazima mtambue kuwa kuna mavazi ya disko, ufukweni, kwenye mikutano maalumu, maosini na hata kanisani ...kila vazi livaliwe sehemu yake...Ukivaa vazi la mkutanoni au kanisani wakati uko ufukweni utaonekana wa ajabu, vivyo hivyo na unapotuvalia nguo za disko au ufukweni kwenye ibada tunakushangaa,” ameseme Padri Mambo.

“Waumini mnapaswa kuelewa hilo sio kuvaa mavazi ambayo wewe mwenyewe yanakusumbua wakati ulivaa mwenyewe tafadhali tuheshimu misingi na taratibu za kanisa kwa kuvaa mavazi yenye staha,” amesisitiza. Amebainisha kuwa wapo waumini ambao mavazi yao yamekuwa yanawanyima, hata uhuru wa kukaa na hata kupiga magoti mbele ya altare, hivyo kutokidhi matakwa ya kuhudhuria misa kutokana na aina ya mavazi wanayotumia. Kwa upande wake, mmoja wa watawa ambaye jina lake halikupatikana mara moja, alisema ili kudhibiti uingiaji na mavazi yasiyopendeza kanisani utaratibu maalumu, unaandaliwa ili kuwadhibiti waumini wenye tabia kama hiyo.

Mtawa huyo amesema uvaaji wa mavazi yasiyohitajika kwenye nyumba za ibada, si kwa wanawake pekee, kwani wapo pia wanaume wanaova suruali chini ya makalio. Lakini aliongeza kuwa kwa wanawake wanaovaa nguo fupi na zenye kubana na kuonesha maumbile yao, utaratibu utakuwa kuwavalisha vitenge na khanga mlangoni, kabla hawajaingia kanisani, sambamba na kuwashonea kanzu maalumu wanaume.

“Ili kuwadhibiti watu wanaovaa nguo fupi na zinazobana tutakuwa tunakaa mlangoni na kuwavalisha vitenge kwa wanawake huku wanaume tukiwaandalia makanzu maalumu ili kanisani wote tuwe katika lengo moja la kusali na kumuabudu Mungu,” amesema. Amesema uvaaji wa mavazi hayo, sio tu unadhalilisha utu wa binadamu, bali pia humharibia utaratibu wa ibada muumini mwingine, kwani wakati mwingi watu wanajikita katika kumshangaa, badala ya kusikiliza neno la Mungu
Naunga Mkono, Ni Lazma Tufike Mahali Tumheshimu Mungu Hasa Ktk Mazingira Ya Ibada. Nimekuwa Nikiona Makanisa Mengi Hasa Katoliki Wakilisimamia Sana Hili. Big Up Kwao,, Kwakulisimamia Hili Kwani Linawaondoa Hata Waumini Wengine Ndani Ya Ibada Kifkra Ktk Kuelekeza Fikra Zao Kwa Ibada Badala Yake, Kukaa Kuangalia Maumbile Ya Watu Waliovaa Nusu Uchi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zamani wanawake walikuwa wanakaa upande wao lakini siku hizi wanakuja kujichanganya kwa wanaume hata Kama upande wao Kuna viti empty, unakuta amekaa mbele yako vimbwanga tupu mpaka unajiuliza nimekuja kufanya nini.. wanatuharibia sana ibada.

Suluhisho: watengewe upande wao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom