Wanaotumia Udart ni moja ya kundi lenye maisha ya shida sana hapa Dar

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
13,111
18,327
Tuwaonee huruma wananchi wanao tumia usafiri unajulikana kama mwendokasi.

1. Mabasi hayana muda rasmi
2. Unaweza kaa kituoni hadi masaa 2
3. Basi likipita limejaa kiasi kwamba hata kutoka tuu kwenye basi inabidi uwe umeshiba.
4. Huduma kwa wateja haipo.. hata namba zikuhizi haipo.
5. Dereva anaweza pitiliza kituo kwa sababu zake tuu zisizo na mashiko

Hivi vitu vya kizungu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna siku nikipitilizwa kituo nitaenda dirisha la dereva na kumpiga ngumi ya sikio, unakuta anakupitiliza alafu anakwambia panda lingine kwa tiketi hiyo hiyo ukashuke kituo chako, sijui na muda nao anaonipotezea anamirudishiaje!
 
Ile Barabara ya Mwendokasi ingekwepo kama kawaida ila zipite daladala tu bila magari mengine,iwe Strictly daladala tu.
Itakuwa fujo kuwahi hesabu. Mwendokasi hawana fujo barabarani kupitana sababu wao wanalipwa mshahara mwisho wa mwezi na hela hawashiki ktk mlango kuingia basini.
Logistically wazo lako ni gumu upande wa ukisanyaji nauli.
 
Kinachonishangaza mimi kuliko yote huduma ya Express basi halisimami kituo cha Ubungo Bus Terminal lakini linasimama Ubungo Maji!
 
Back
Top Bottom