Wanaotembea kwenda Ikulu wamevaa magunia

Wanaotembea kwenda Ikulu wamevaa magunia

Nawashauri Wakikaribia Magogoni Wavae Magome Ya Miti,,, Kiashilio Cha Enzi Za Harakati Za Ukombozi Mpya Wa Nchi Yetu!!
 
Hivi ni kwa nini ccm mnaonyesha unyama na uzimwi wenu hadharani bila hata chembe ya uzalendo? Ujumbe waliobeba hawa vijana kwenu hauwahusu ama ninyi ni mizoga inayotembea?

Watu wamevaa magunia si kwamba hawana nguo. Kuvaa magunia ni dalili ya maombolezo makali yanayogusa mioyo yao ya ndani na maumivu yake hayana faraja. Sintashangaa wakinyoa nywele zote za vichwa vyao kuashiria kwamba hawana faraja wala furaha yoyote kwa msiba unaolikumba taifa.

Hata kama hamna utu, iweni na akili. Mtu mwenye akilil timamu hawezi kuwadhihaki watu waliojitoa mhanga kwa kuomboleza kukubwa namna hii kwa ajili ya taifa.

Ccm mnakera sana. Tutaanza kuwatafuta kwa sababu ya usaliti na dhihaka zenu kwa wanyonge ili mlipe!.

Wajipake na majivu usoni kuonyesha msisitizo!
 
Hofu ni je JK atakuwepo? mana Colambus hakawii kuruka nnje! asipowapokea magogoni leo, laana iwe kwake na vizazi vyake hata cha tatu! GT WOTE TUSEME AMEN!
 
Mtu mwenyewe huyo huwa anayasikiliza na kuyafanyia kazi mawazo ya wasio na kitu kwa pocket?
 
Nimepishana nao hapo kibaha mida ya saa moja asubuhi. Kumbe kweli walikuwa wanaenda ikulu.
 
Leo kupitia Channel 10 asubuhi hii, wale vijana watatu wanaotembea toka Mwanza kwenda Ikulu wameongea kwa njia ya simu na mtangazaji na kusema hivi sasa wako Kibaha na wanaelekea Ikulu na wamekiri kuvaa magunia.

Walipoulizwa na mtangazaji ni kwanini wamevaa magunia, walijibu kuwa ni kuonyesha hisia zao na pia walipoulizwa kama wataruhusiwa kuingia Ikulu huku wamevaa magunia;vijana hao wamejibu kuwa hakuna "dressing code" ya kuingia Ikulu.

Baadhi ya hoja walizobeba ni kupinga ufisadi na kushuka kwa maadili katika nchi.

Maoni yangu:
Maadam wengi wamekaribishwa Ikulu na JK,basi hana budi kuwapokea na hawa pia kwani nao ni watanzania kama kina Diamond,Ray C na wengineo.
10676157_590112594421802_2726790791109930056_n.jpg


Naaaam saa ya ukombozi imewadia,amen
 
Sasa hivi wamefika maeneo ya mapipa .a wapo na escot ya polis inaonekana ujio wao una taarifa ,wapo vijana kadhaa wanawasapoti.
 
kikukweli wana stahili kupokelewa na kuingua ikulu....mbona kuna maboya tu wanaikaribishwa state house.....
 
wanastahili pongezi sana na hata wasipopokelewa ikulu ujumbe waliobeba utakuwa umefika kwa Watanganyika!
 
Back
Top Bottom