Wanaotembea kwenda Ikulu wamevaa magunia

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
52,788
Reaction score
165,484
Leo kupitia Channel 10 asubuhi hii, wale vijana watatu wanaotembea toka Mwanza kwenda Ikulu wameongea kwa njia ya simu na mtangazaji na kusema hivi sasa wako Kibaha na wanaelekea Ikulu na wamekiri kuvaa magunia.

Walipoulizwa na mtangazaji ni kwanini wamevaa magunia, walijibu kuwa ni kuonyesha hisia zao na pia walipoulizwa kama wataruhusiwa kuingia Ikulu huku wamevaa magunia;vijana hao wamejibu kuwa hakuna "dressing code" ya kuingia Ikulu.

Baadhi ya hoja walizobeba ni kupinga ufisadi na kushuka kwa maadili katika nchi.

Maoni yangu:
Maadam wengi wamekaribishwa Ikulu na JK,basi hana budi kuwapokea na hawa pia kwani nao ni watanzania kama kina Diamond,Ray C na wengineo.
10676157_590112594421802_2726790791109930056_n.jpg

Yule jamaa wa Mwanza alikamatwa na polisi kabla hata hajamuona mkuu wa mkoa.. Hawa watafanywaje...
 
Hivi pesa ya kurudi Mwanza wanayo au watarudi kwa mguu tena?
 
waende pale ufipa kwenye ofisi zao ikulu haiwez kuwa inapokea wahuniwahuni hivyo
 
Leo kupitia Channel 10 asubuhi hii, wale vijana watatu wanaotembea toka Mwanza kwenda Ikulu wameongea kwa njia ya simu na mtangazaji na kusema hivi sasa wako Kibaha na wanaelekea Ikulu na wamekiri kuvaa magunia.

Walipoulizwa na mtangazaji ni kwanini wamevaa magunia, walijibu kuwa ni kuonyesha hisia zao na pia walipoulizwa kama wataruhusiwa kuingia Ikulu huku wamevaa magunia;vijana hao wamejibu kuwa hakuna "dressing code" ya kuingia Ikulu.

Baadhi ya hoja walizobeba ni kupinga ufisadi na kushuka kwa maadili katika nchi.

Maoni yangu:
Maadam wengi wamekaribishwa Ikulu na JK,basi hana budi kuwapokea na hawa pia kwani nao ni watanzania kama kina Diamond,Ray C na wengineo.

hii habari niliiona kwenye wall ya tundu lissu kuleeee fb sasa niona hapa inamaana wewe ndio lissu
 
Maoni yangu:
Maadam wengi wamekaribishwa Ikulu na JK,basi hana budi kuwapokea na hawa pia kwani nao ni watanzania kama kina Diamond,Ray C na wengineo.
Kama waliomba appointment ya kuonana na raisi kabla ya kwenda wakakubaliwa basi watamwona.Kuna njia mbili za kumwona Raisi ya kwanza anakwambia mwenyewe njoo ya pili unaweka appointment akikubali ukijibiwa sawa nitakuwa na muda siku fulani na muda fulani basi unaenda kumwona.Ila hawa kama katika hizo mbili hawamo wakila virungu wasimlaumu mtu.Ikulu sio choo cha baa ambacho kila mtu aweza ingia akijisikia haja.
 
Kama wanaenda kiofisi watapewa jinsi ya kuvaa hili liko wazi!!
Wanaoalikwa kwa social matters wanavaa watakavyo kwa mujibu wa hadhi ya wanakoenda so wajiandae kwa lolote
 
Kama waliomba appointment ya kuonana na raisi kabla ya kwenda wakakubaliwa basi watamwona.Kuna njia mbili za kumwona Raisi ya kwanza anakwambia mwenyewe njoo ya pili unaweka appointment akikubali ukijibiwa sawa nitakuwa na muda siku fulani na muda fulani basi unaenda kumwona.Ila hawa kama katika hizo mbili hawamo wakila virungu wasimlaumu mtu.Ikulu sio choo cha baa ambacho kila mtu aweza ingia akijisikia haja.

Harbinder Singh Seth alipoenda Ikulu hivi karibuni alikuwa na appointment?
 
Hivi ni kwa nini ccm mnaonyesha unyama na uzimwi wenu hadharani bila hata chembe ya uzalendo? Ujumbe waliobeba hawa vijana kwenu hauwahusu ama ninyi ni mizoga inayotembea?

Watu wamevaa magunia si kwamba hawana nguo. Kuvaa magunia ni dalili ya maombolezo makali yanayogusa mioyo yao ya ndani na maumivu yake hayana faraja. Sintashangaa wakinyoa nywele zote za vichwa vyao kuashiria kwamba hawana faraja wala furaha yoyote kwa msiba unaolikumba taifa.

Hata kama hamna utu, iweni na akili. Mtu mwenye akilil timamu hawezi kuwadhihaki watu waliojitoa mhanga kwa kuomboleza kukubwa namna hii kwa ajili ya taifa.

Ccm mnakera sana. Tutaanza kuwatafuta kwa sababu ya usaliti na dhihaka zenu kwa wanyonge ili mlipe!.
 
Harbinder Singh Seth alipoenda Ikulu hivi karibuni alikuwa na appointment?

Kama hakiwa nayo we thibitisha tu mkuu ili mjadala ufe!!!
Kwa level yake hawezi kwenda bila taarifa labda iwe sasa ni taarifa ipi na kwa njia gani na kwa muda upi???!!

Much as host alikuwepo na (walionana??????) basi hapo hoja inakuwa tofauti
 
Tatizo kubwa la ccm ni kujiona kuwa wana hati miliki na nchi hii. Mungu naomba uniweke hai niweze kuiona ccm watakavyokuwa wapinzani bunge la december.
 
Si wanaenda kumuona mhuni mwenzao Ikulu!!!!

We utakuwa ulikosa malezi mazuri kutoka kwa wazazi wako, huwezi kumdhalilisha raisi wako, raisi wa dr slaa na watanzania mil 45 kiasi hicho
 
Kama waliomba appointment ya kuonana na raisi kabla ya kwenda wakakubaliwa basi watamwona.Kuna njia mbili za kumwona Raisi ya kwanza anakwambia mwenyewe njoo ya pili unaweka appointment akikubali ukijibiwa sawa nitakuwa na muda siku fulani na muda fulani basi unaenda kumwona.Ila hawa kama katika hizo mbili hawamo wakila virungu wasimlaumu mtu.Ikulu sio choo cha baa ambacho kila mtu aweza ingia akijisikia haja.

Njia ya tatu ya kumuona Rais wakati ule January yupo pale ni kumpa ada ya Dola mia moja mpaka mbili anakuandalia mchongo mpaka unamuona Rais. Njia hii ilijulikana sana hasa kwa wafanya biashara ambao wengine walikuwa wanaongeza dau.
Kweli Ikulu sasa ni pango la walaghai.
 
Back
Top Bottom