Wanaotangaza CCM wameiba kura wathibitishe

Wanaotangaza CCM wameiba kura wathibitishe

Hivi hujui nyumbu huambiwa jambo nao bila kulifikiria wanaitikia kwa pamoja ndio mzee hapo Mbowe kawaambia kura zimeibiwa nao ndio zimeibiwa pfyuuuuuu
 
Wapinzani hasa UKAWA ni watu wa kulalamika kila siku. Kama walijua kwa Katiba iliyopo kuwa Tume haitakuwa huru kwanini walishiriki uchaguzi? Burundi wapinzani walisusia uchaguzi uliofanyika hivi karibuni kwasababu walijua haki haitatendeka. UKAWA walitoka katika Bunge la Katiba kwasababu walidai maoni ya wananchi hayakuzingatiwa kama yalivyo kwenye Rasimu ya Warioba. Kwa ari ile ile nilitegemea wasingeshiriki uchaguzi huu kwasababu vyama vilikubaliana kuleta Mswada Bungeni wa kurekebisha Katiba ya sasa ili matokeo ya urais yapingwe mahakamani, mgombea binafsi na Tume huru ya Uchaguzi iundwe upya! Lakini hayo hawakufanya na kwa uroho wao walikubali kuingia kwenye ligi wakifikiri watashinda kwa kuwatumia marefa walewale na washika vibendera walewale. Walifikiri Lowassa ndiyo Messi wao ambaye atawapa ushindi bila kurekebisha Katiba! Hapo walitegemea nini? Sasa hivi imekula kwao, wahesabu hasara hadi Katiba ya Warioba ijadiliwe na siyo ya Chenge.

Kwa ninavyojua ukitaka kukamata paka mwizi jifanye siku moja umesahau mlango wazi weka na samaki juu ya meza halafu unamtia samaki sumu..paka lilivyo jinga litakuja na kula yule samaki bila kupiga hesabu kwamba kwanini mlango umeachwa wazi na samaki akasahaulika juu ya meza?.
Ndicho kilichowatokea hawa jamaa zetu, walifikiri wanakula samaki tena wa Mwaka huu angekua papa kumbe mzee mwenye nyumba anawajua tabia zao kawawekea tego na sumu juu. Sasa tunaangalia wanavyojinyonganyonga kabla hawajakata roho. Na sumu isipowamaliza kabisa basi mwaka 2020 watakua na ulemavu wa kuwafanya washindwe kuingia hata ndani kuokota makombo!
 
Nnaunga mkono hoja, wanaosema CCM wameiba kura wafikishwe mahakamani ili wathibitishe hilo na wakishindwa wachukuliwe hatua kali za kisheria.

Tusicheke nao tena hawa.
maccm wa wizi tu wamekubuu, ukikaa vibaya na wewe unaweza kuibiwa.
 
Mliambiwa katiba itayotumika ni ya 1977 kelele za nini?na wabunge walioshinda wa ukawa na wao waseme siyo halali ukawa wanatafuta huruma wajipange kwa 2020
 
Subiri tu utayaona. Sasa hivi ni utawala mwengine kabisa.

#HapaKaziTu

Hamna lolote jipya hapo- it's the failed governance system. It's sad that Mr. President went to Muhimbili last week to give directives of such and such have to be rectified - among the directives was to service and maintenance of MRI and CT Scan machines.

Nasikia hizo mashine zimeharibika tena...... AIBU KUBWA na that proves the failed presidential directives hence the failure of Mr. President's directives.

Tunajipanga kwa miaka mingine kumi ya maumivu... YARABI TUEPUSHE WAJA WAKO ADHABU YA MIAKA ILIYOPITA INATOSHA.
 
Watu wanaongea nyama wewe unaleta utumbo.

Huyo unaemuomba tulimuomba nasisi kasikia dua zetu ndiyo katuepusha na akina Lowassa na Mbowe kututawala.

AlhamduliLlah.
 
Naomba sheria itumike wanaosema CCM wanaiba kura wathibitishe kama si kweli wachukuliwe hatua stahiki.

Huku ni kupandikiza chuki kwa wananchi imefikia kupiga kura majimbo yaliobakia hawapigi kura eti CCM wanaiba kura.

Wanavyotuhumiwa CCM hata tume inatuhumiwa vile vile.Kwa taarifa kura haziibwi jamani watanzania wanaipenda CCM yao kwahiyo msikichafue CCM kwa chuki za kushindwa uchaguzi.

Mwambie Jecha akupe ushahidi maana mpaka sasa amefuta matokeo lakini hajatoa ushahidi!!
 
Hicho ni kitu hata wewe mwenyewe unaweza kufanya na ukathibitisha, hauhitaji kuthibitishiwa. Ngoja nikupe njia, Chukua jumla ya kura zote halali zilizopigwa, kisha jumlisha kura za wagombea wote halafu uone kama idadi itakuwa sawa. Kama ni sawa wanaodai wameiba watakuwa ni waongo, kama si sawa wanaodai zimeibwa watakuwa ni wakweli.

nenda mahakamani kiongozi ushahidi si unao
 
Tanzania hakuna uchaguz tunafanya maigizo tu, kwani kuna kikudi cha watu wanajigawia madaraka na kuanza kuudanganya ulimwengu eti kuna demokrasia.. Tanzania chini ya ccm hakuna utawala bora wala demokrasia hakuna, kuna ubabaishaji tu..
 
Wapinzani hasa UKAWA ni watu wa kulalamika kila siku. Kama walijua kwa Katiba iliyopo kuwa Tume haitakuwa huru kwanini walishiriki uchaguzi? Burundi wapinzani walisusia uchaguzi uliofanyika hivi karibuni kwasababu walijua haki haitatendeka. UKAWA walitoka katika Bunge la Katiba kwasababu walidai maoni ya wananchi hayakuzingatiwa kama yalivyo kwenye Rasimu ya Warioba. Kwa ari ile ile nilitegemea wasingeshiriki uchaguzi huu kwasababu vyama vilikubaliana kuleta Mswada Bungeni wa kurekebisha Katiba ya sasa ili matokeo ya urais yapingwe mahakamani, mgombea binafsi na Tume huru ya Uchaguzi iundwe upya! Lakini hayo hawakufanya na kwa uroho wao walikubali kuingia kwenye ligi wakifikiri watashinda kwa kuwatumia marefa walewale na washika vibendera walewale. Walifikiri Lowassa ndiyo Messi wao ambaye atawapa ushindi bila kurekebisha Katiba! Hapo walitegemea nini? Sasa hivi imekula kwao, wahesabu hasara hadi Katiba ya Warioba ijadiliwe na siyo ya Chenge.

Tukiacha kulalamika mtahama mitaa!
 
Nakumbuka lorry lilokuwa limejaa mabox yenye kura ambazo tayari zishapigwa
 
Hapa kazi tu, mtaibiwaje kura za uraisi wakati mmeambulia wabunge thelasini na kidogo wakati ccm kimepata wabunge zaidi ya 180, hamjafikisha hata robo ya wabunge manyumbu nyie. na urais tofauti ya kura zaidi ya milioni mbili na ushee halaf bado mnasema mmeibiwa. Shida yenu manyumbu majigambo na mashauzi meengi wakati wenye akili zao wanajua watampigia nani, tena kimyA kimya. hapa kazi tu na endeleeni kuisoma namba.
 
Swali langu kwa watanzania wenzangu ni hili; Mgombea mmoja amejishusha kwa wananchi akazunguka kwa barabara nchi nzima na kuonana na watu wengi zaidi ya mgombea mwingine ambaye alijipandisha na kusafiri na CHOPA huku akiwapita wapiga kura walio wengi kwa juu,je unategemea mgombea yupi ashinde?
Jibu ni rahisi; AJISHUSHAYE HUPANDISHWA NA AJIPANDISHAYE HUSHUSHWA.Acheni kulia lia kajipangeni mjaribu tena baadae.
 
Wizi wa kura ulianzia kwenye kura za maoni sasa sijui ushahidi wa kura zepe
 
Kwasababu UKAWA wamenyamaza baada ya kuibiwa kura wametuona mafala lakini watambue kwamba UKAWA wameongoza ktk kulinda amani ya nchi hii. Mwisho wa ubabe utafika tu hata km sio leo.
 
Wana JF.

Tunawaomba viongozi wa Chadema watuwekee idadi za kura za rais walizopata majimboni ili watanzania wapenda amani waone na kupima kama kweli wameibiwa kura.

Viongozi wa Chadema wamekuwa wakilalamika kwenye vyombo vya habari wameibiwa kura zao za urais bila kuweka ushahidi.

Chadema wanasema mgombea wao Lowassa amepata kura milioni 10 bila kuweka data zozote hii inakuwa ngumu watanzania na jumuiya za kimataifa kuwaelewa.

Kwa faida ya watanzania wote wapenda amani sikilizeni kilio chetu.
 
Back
Top Bottom