Wanaotangaza CCM wameiba kura wathibitishe

mansoorsaid

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2014
Posts
1,498
Reaction score
286
Naomba sheria itumike wanaosema CCM wanaiba kura wathibitishe kama si kweli wachukuliwe hatua stahiki.

Huku ni kupandikiza chuki kwa wananchi imefikia kupiga kura majimbo yaliobakia hawapigi kura eti CCM wanaiba kura.

Wanavyotuhumiwa CCM hata tume inatuhumiwa vile vile.Kwa taarifa kura haziibwi jamani watanzania wanaipenda CCM yao kwahiyo msikichafue CCM kwa chuki za kushindwa uchaguzi.
 
Hwawezi siunajua wanajificha kwenye kwapa la kuwa hawawezi kupinga mahakamani???

Hivyo waache waendelee kubwabwaja mitaani mwisho watachoka sio mda mrefu...na mwaka huu hakuna kwenda Ikulu kunywa juice.
 
  • Thanks
Reactions: nao
Ni muhimu pia serikali iwafungulie mashitaka watu wanaozusha uwongo kuhusu kuibiwa kura ili wakathibitishe makahani jinsi walivyoibiwa majimbo yote.
 
mtoa mada kwakweli hili linanikera sana hii tabia chafu sana msimu uliopita walisema ccm wamechakachua sasa wanasema neno baya kabisa ccm wameiba kura
 
Hicho ni kitu hata wewe mwenyewe unaweza kufanya na ukathibitisha, hauhitaji kuthibitishiwa. Ngoja nikupe njia, Chukua jumla ya kura zote halali zilizopigwa, kisha jumlisha kura za wagombea wote halafu uone kama idadi itakuwa sawa. Kama ni sawa wanaodai wameiba watakuwa ni waongo, kama si sawa wanaodai zimeibwa watakuwa ni wakweli.
 
Hwawezi siunajua wanajificha kwenye kwapa la kuwa hawawezi kupinga mahakamani???

Hivyo waache waendelee kubwabwaja mitaani mwisho watachoka sio mda mrefu...na mwaka huu hakuna kwenda Ikulu kunywa juice

uthibitisho ni kurandaranda kwa majeshi mtaani kulinda wezi wa kura tusiwadhuru
 
Lowasa alisema njia zote za wizi anazjua sasa vipii? Mfa maji haish kutapatapa na 2020 tukiwa hai tutamnyooosha tena
 
  • Thanks
Reactions: nao
Naomba sheria itumike wanaosema CCM wanaiba kura wathibitishe kama si kweli wachukuliwe hatua stahiki.

Huku ni kupandikiza chuki kwa wananchi imefikia kupiga kura majimbo yaliobakia hawapigi kura eti CCM wanaiba kura.

Wanavyotuhumiwa CCM hata tume inatuhumiwa vile vile.Kwa taarifa kura haziibwi jamani watanzania wanaipenda CCM yao kwahiyo msikichafue CCM kwa chuki za kushindwa uchaguzi.
Unataka wathibitishe kwako?
Kama unajua wanadanganya si mkawafungulie mashtaka maana ushaihidi si mnao?
Wahi mahakamani mkawashitaki.
 
Wapinzani hasa UKAWA ni watu wa kulalamika kila siku. Kama walijua kwa Katiba iliyopo kuwa Tume haitakuwa huru kwanini walishiriki uchaguzi? Burundi wapinzani walisusia uchaguzi uliofanyika hivi karibuni kwasababu walijua haki haitatendeka. UKAWA walitoka katika Bunge la Katiba kwasababu walidai maoni ya wananchi hayakuzingatiwa kama yalivyo kwenye Rasimu ya Warioba. Kwa ari ile ile nilitegemea wasingeshiriki uchaguzi huu kwasababu vyama vilikubaliana kuleta Mswada Bungeni wa kurekebisha Katiba ya sasa ili matokeo ya urais yapingwe mahakamani, mgombea binafsi na Tume huru ya Uchaguzi iundwe upya! Lakini hayo hawakufanya na kwa uroho wao walikubali kuingia kwenye ligi wakifikiri watashinda kwa kuwatumia marefa walewale na washika vibendera walewale. Walifikiri Lowassa ndiyo Messi wao ambaye atawapa ushindi bila kurekebisha Katiba! Hapo walitegemea nini? Sasa hivi imekula kwao, wahesabu hasara hadi Katiba ya Warioba ijadiliwe na siyo ya Chenge.
 
Nnaunga mkono hoja, wanaosema CCM wameiba kura wafikishwe mahakamani ili wathibitishe hilo na wakishindwa wachukuliwe hatua kali za kisheria.

Tusicheke nao tena hawa.
 
Naomba sheria itumike wanaosema CCM wanaiba kura wathibitishe kama si kweli wachukuliwe hatua stahiki.

Huku ni kupandikiza chuki kwa wananchi imefikia kupiga kura majimbo yaliobakia hawapigi kura eti CCM wanaiba kura.

Wanavyotuhumiwa CCM hata tume inatuhumiwa vile vile.Kwa taarifa kura haziibwi jamani watanzania wanaipenda CCM yao kwahiyo msikichafue CCM kwa chuki za kushindwa uchaguzi.
Wapiga kura wanajua kuwa kuwa kura zao zinaibiwa; hapo wezi lazima wajipange kupigiwa kura
 
Nnaunga mkono hoja, wanaosema CCM wameiba kura wafikishwe mahakamani ili wathibitishe hilo na wakishindwa wachukuliwe hatua kali za kisheria.

Tusicheke nao tena hawa.
Mwambie Mwanasheria mkuu na viongozi wa CCM wapeleke hili mahakamani haraka. Naunga mkono hoja
 
Hicho ni kitu hata wewe mwenyewe unaweza kufanya na ukathibitisha, hauhitaji kuthibitishiwa. Ngoja nikupe njia, Chukua jumla ya kura zote halali zilizopigwa, kisha jumlisha kura za wagombea wote halafu uone kama idadi itakuwa sawa. Kama ni sawa wanaodai wameiba watakuwa ni waongo, kama si sawa wanaodai zimeibwa watakuwa ni wakweli.

Yaani kazi ya tume iliishaisha kitambo unataka tena leo tuanze upya? kwani wao wslipojumlisha walipata ngapi? hicho ndo kitu tunawataka waweke wazi ili tuanzie hapo kwasababu wanasema wanao ushaidi
 
Jamani kwa kuanzia tuanze na Godbless Lema tumkate, alafu 2020 Halmashauri ya jiji la Arusha tuirudishe ccm pamoja na kirimanjaro. Naamini rais wetu atarudisha heshima ya chama chetu, iliyotaka kupotezwa na mafisadi wachache. Ng'ombe na zichungwe kiroho safi. Eti naamuru tume isimame mara moja kutangaza matokeo, we nani? Hapo Lubuva ndo kaweka pamba masikioni, utasikia jimbo la Geita mjini....................!
 
Hicho ni kitu hata wewe mwenyewe unaweza kufanya na ukathibitisha, hauhitaji kuthibitishiwa. Ngoja nikupe njia, Chukua jumla ya kura zote halali zilizopigwa, kisha jumlisha kura za wagombea wote halafu uone kama idadi itakuwa sawa. Kama ni sawa wanaodai wameiba watakuwa ni waongo, kama si sawa wanaodai zimeibwa watakuwa ni wakweli.

Kwa akili yako unadhani huyu aliyetuletea haya matapishi hapa ana akili hiyo? Ataendelea tu kukubishia kwa kuwa tayari moyoni mwake ana kitu anapenda. Kama watu wanaipenda CCM, zi wapi shamra shamra za ushindi?

Wakitaka kujua nini Watanzania wanapenda, ngoja ifike hiyo siku ya kuapishwa Maalim Seif halafu uone jinsi watu watasherehekea ndio ionekane tofauti ya chaguo la wananchi na chaguo la tume.
 
Waliopiga kura wanajua walimchagua nani na kwa wingi gani. Lisemwalo lipo! Hata 2010 system ilifanya mambo yake lakini yote haya yana mwisho hata kama ni baada ya miaka 100 ijayo! Mabadiliko tunayotaka au kutegemea hayawezi kuletwa na chama tawala yataletwa na wananchi wenyewe kwa kushirikiana na serikali mbadala sio CCM. Mtajaribu lakini hamtafka mbali mioyo ya watu ina msononeko wa yaliyotokea. Kama kura zilihesabiwa vituoni na kubandikwa si kila mtu ajumlishe? Ya nini kurudia kuhesabu kata au kwa mkurugenzi kama hakuna namna?
 
Ushahidi ni uchaguzi wa Zanzibar. Zaidi ya hapo kamuulize jechaa.
 
Naomba sheria itumike wanaosema CCM wanaiba kura wathibitishe kama si kweli wachukuliwe hatua stahiki.

Huku ni kupandikiza chuki kwa wananchi imefikia kupiga kura majimbo yaliobakia hawapigi kura eti CCM wanaiba kura.

Wanavyotuhumiwa CCM hata tume inatuhumiwa vile vile.Kwa taarifa kura haziibwi jamani watanzania wanaipenda CCM yao kwahiyo msikichafue CCM kwa chuki za kushindwa uchaguzi.

Na kwa Wasira na Bulaya nako unasemaje..??
 
Hicho ni kitu hata wewe mwenyewe unaweza kufanya na ukathibitisha, hauhitaji kuthibitishiwa. Ngoja nikupe njia, Chukua jumla ya kura zote halali zilizopigwa, kisha jumlisha kura za wagombea wote halafu uone kama idadi itakuwa sawa. Kama ni sawa wanaodai wameiba watakuwa ni waongo, kama si sawa wanaodai zimeibwa watakuwa ni wakweli.
Kwa hiyo kutokana na hiyo hesabu ndio una thibitisha kuwa CCM ndio wameiba kura?kwanini iwe ni CCM tu wakati kuna Chadema,CUF?
 
Back
Top Bottom