Wanaotaka dawa za kienyeji (asili ) zitolewe kwenye hospitali za Serikali ni vema wakaruhusu pia kupiga Chale na ramli

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,689
218,192
Maadam tumeamua kwa kauli moja kuirejesha nchi yetu kwenye zama za mawe na ujima ( God must be crazy ) , basi ni vema tukaruhusu na msingi mkubwa wa miti shamba hiyo ambao ni uchawi na ushirikina , ramli na kupigana Chale .

Hii itasaidia wachawi wengi wa Sumbawanga na kwingineko nchi nzima kujitokeza kizalendo ili kusaidiana na viongozi wa nchi yetu katika kutokomeza corona .

Mungu ibariki Tanzania

Nakala : Mshana Jr
 
Hizo siyo dawa mkuu.Hizo ni lishe.Kuna tofauti kubwa sana kati ya lishe na dawa ndiyo maana kwa mfano mtu mwenye ukosefu wa vitamin B twelve complex huwa anapewa vidonge akameze na siyo kuambiwa kuwa akale lishe yenye vitamini B twelve complex.

Ni Tanzania pekee yake maprofesa wanatengeneza lishe na kuiita kuwa ni dawa.Dawa ni kitu chenye specific
antidotes with specific ingredients kwa ajili ya kushambulia specific antigens!
 
Watu wa "ni yeye" wamechanganyikiwa hawajui kuna asili na kisasa, hawajui broiler na yule kuku anayeitwa wa kienyeji wote ni kuku ila wanatofautiana tu malezi na faida.
Wengi wazazi wao wamekulia vijijini ambako hata zahanati hamna, na wazazi wao wamewazaa huko huko, leo hii wanakuja kukejeli dawa asili hapa lahaula!

Natamani niwape kisa cha tabibu wa asili (mganga wa jadi) wa Serbia aliyetibu wachezaji 'mabilionea' wa ligi maarufu duniani kwa muda mfupi, kuliko hata hizo hospitali mnazoziita za kisasa
 
Maadam tumeamua kwa kauli moja kuirejesha nchi yetu kwenye zama za mawe na ujima ( God must be crazy ) , basi ni vema tukaruhusu na msingi mkubwa wa miti shamba hiyo ambao ni uchawi na ushirikina , ramli na kupigana Chale .

Hii itasaidia wachawi wengi wa Sumbawanga na kwingineko nchi nzima kujitokeza kizalendo ili kusaidiana na viongozi wa nchi yetu katika kutokomeza corona .

Mungu ibariki Tanzania

Nakala : Mshana Jr
Kwahiyo kutumia dawa za viwandani ndio God must be inteligent?
 
Kaka tembea uone kwa mfano China kuna hospitali zenye vitengo vya dawa za asili na zinatumika sana ,kwa hiyo sio kitu kipya kama hujui kitu uliza kwanza
Nimewahi kutibiwa Nanjing (China) kwa dawa hizo, sio ajabu kwa kweli.
Tatizo ndugu zetu wanaamin sana Panadol iliyotokana na mwarobaini au aroe vera lakin ukimpa mwarobaini au aroe vera anakataa kutumia
 
Kaka tembea uone kwa mfano China kuna hospitali zenye vitengo vya dawa za asili na zinatumika sana ,kwa hiyo sio kitu kipya kama hujui kitu uliza kwanza
Umecheki ulivyojibiwa kigreat thinker kwenye comment #3 na mleta mada?

Mkishabugia na kushindilia viporo vya kande iliyochacha mnapurupuka tu na kujifanya wajuaji mnajikuta mnapokea za uso.

Kamoooonn
 
Wastani wa umri wa kuishi wa Mtanzania ni Miaka 65, Japan ni miaka 85,Uingereza 81,Israel 82. Kwa nini unafikiri kuna utofauti huo?
Watu wa "ni yeye" wamechanganyikiwa hawajui kuna asili na kisasa, hawajui broiler na yule kuku anayeitwa wa kienyeji wote ni kuku ila wanatofautiana tu malezi na faida.
Wengi wazazi wao wamekulia vijijini ambako hata zahanati hamna, na wazazi wao wamewazaa huko huko, leo hii wanakuja kukejeli dawa asili hapa lahaula!

Natamani niwape kisa cha tabibu wa asili (mganga wa jadi) wa Serbia aliyetibu wachezaji 'mabilionea' wa ligi maarufu duniani kwa muda mfupi, kuliko hata hizo hospitali mnazoziita za kisasa
 
Maadam tumeamua kwa kauli moja kuirejesha nchi yetu kwenye zama za mawe na ujima ( God must be crazy ) , basi ni vema tukaruhusu na msingi mkubwa wa miti shamba hiyo ambao ni uchawi na ushirikina , ramli na kupigana Chale .

Hii itasaidia wachawi wengi wa Sumbawanga na kwingineko nchi nzima kujitokeza kizalendo ili kusaidiana na viongozi wa nchi yetu katika kutokomeza corona .

Mungu ibariki Tanzania

Nakala : Mshana Jr
Muhimbili kulikuwa na kitengo cha dawa asili sijui kama bado kipo! Nakumbuka kuna mwaka walidai wangeweza kumtibu mtoto aliyevimba jicho, baada ya jicho kuendelea kuvimba waganga wakaingia kwenye manyanga na tunguri! Ikabidi wasimamishwe kumtibu.
 
Wastani wa umri wa kuishi wa Mtanzania ni Miaka 65, Japan ni miaka 85,Uingereza 81,Israel 82. Kwa nini unafikiri kuna utofauti huo?
Very simple, ni uwezo wa kiuchumi. Wenzetu wakifika umri mkubwa wa uzee wanapelekwa kwenye vituo maalum vya kulea wazee. Huko wanapewa kila kitu mpaka wanapokufa, na ajira za kuwahudumia ndizo ambazo wabongo wengi na waafrika wengine wanazipata.

Huku mzee ana miaka 70 bado anashika jembe, anauza kashata kwenye jua kali lazima akate moto mapema.

Raisi mstaafu Mwenyi ana 90 plus, warioba, mama nyerere, nk wengi waliokua well off wanadunda
 
Dawa za asili na na ramli ni ndugu wawili wa mbali sana hawana hata mahusiano,yani ni sawa na samaki na mjusi.
 
Maadam tumeamua kwa kauli moja kuirejesha nchi yetu kwenye zama za mawe na ujima ( God must be crazy ) , basi ni vema tukaruhusu na msingi mkubwa wa miti shamba hiyo ambao ni uchawi na ushirikina , ramli na kupigana Chale .

Hii itasaidia wachawi wengi wa Sumbawanga na kwingineko nchi nzima kujitokeza kizalendo ili kusaidiana na viongozi wa nchi yetu katika kutokomeza corona .

Mungu ibariki Tanzania

Nakala : Mshana Jr
Kwa muelekeo huu inawezekana tiba za kisasa zikapigwa marufuku na vyuo vya tiba vikafundisha usangoma.
 
Watu wa "ni yeye" wamechanganyikiwa hawajui kuna asili na kisasa, hawajui broiler na yule kuku anayeitwa wa kienyeji wote ni kuku ila wanatofautiana tu malezi na faida.
Wengi wazazi wao wamekulia vijijini ambako hata zahanati hamna, na wazazi wao wamewazaa huko huko, leo hii wanakuja kukejeli dawa asili hapa lahaula!

Natamani niwape kisa cha tabibu wa asili (mganga wa jadi) wa Serbia aliyetibu wachezaji 'mabilionea' wa ligi maarufu duniani kwa muda mfupi, kuliko hata hizo hospitali mnazoziita za kisasa

Sent from my Android using JamiiForums mobile app
Mkuu shusha vitu
 
Back
Top Bottom