Wanaopona CoronaVurus wanapona kwa dawa ipi?

Wanaopona CoronaVurus wanapona kwa dawa ipi?

kidadari

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2012
Posts
8,646
Reaction score
9,623
Mpaka sasa imeripotiwa vifo takriban 1,803 huku maambukizi yakifikia 73,000.
Katika hali ya kushangaza kuna wagonjwa 9,000+ wamepona na kuruhusiwa kurudi nyumbani.
Cha kushangaza dunia haizungumzii hao waliopona na dawa gani imetumika ili kunusuru hali ya taharuki duniani tofauti na hapo habari zinazovuma ni maambukizi mapya na idadi ya vifo.

Kuna nini ndani ya #CoronaVirus?
 
Ni jambo la kushangaza sana kutangaza watu wanaokufa, inabidi taarifa zote za pande zote Zitangazwe, kuna watu wengi wanapona,Lakini wao wanatuhaminisha kuwa ukipata Covid-19 ni kama death sentence! vyombo vya magharibi viko vitani na China.
 
Inawezekana kabisa wametibiwa na kupona,nilishawahi kusikia hili pia kwenye mlipuko wa Ebola ,wagonjwa wengine walitibiwa na kupona,ingawa sijui hasa kitaalamu nini kinafanyika...
 
Wanatibu dalili, na kuacha Kinga ya mwili ipambane dhidi ya virusi. Hakuna dawa ya virusi, mwili ukishindwa ku-fight ndio Basi.
 
Anayepashwa kujibu hilo ni China because it is the country currently hosting the deadly virus and a good number of victims.
 
Wanatibu dalili, na kuacha Kinga ya mwili ipambane dhidi ya virusi. Hakuna dawa ya virusi, mwili ukishindwa ku-fight ndio Basi.
Sasa kwa mini hiyo kinga isitumike kwenye ukimwi maana ni. Virus pia
 
Sasa kwa mini hiyo kinga isitumike kwenye ukimwi maana ni. Virus pia
Mkuu unajua kirefu Cha Ukimwi au ulimaanisha VVU ?.

Kwa sababu Mimi siyo mtaalamu wa Afya, Ila Nina Basic knowledge ya baadhi ya magonjwa kutokana na kujisomea na kuperuzi humu JF na sehemu zingine.

Magonjwa ya virusi yanatofautiana kulingana na Aina ya kirusi na sehemu kinapo shambulia.

Mkuu ulishawahi kushuuhudia mtu aliyeugua magonjwa Aina hii mfano;

- Lubela
- Surua
- mafua ya Aina yeyote

Magonjwa hayo hapo juu kwa uchache yana-sababishwa na virusi/virus. Kwa mfano ukiona mtu anaegua Surua ametokelezea mapele, dawa atakazopewa zinatamsaidia kutibu hayo mapele , lakini Kinga ya mwili ndio itakayomponesha.

Mkuu ukisikia mtu anapewa Kinga/chanjo ya Surua/Lubela ujue anachoma kirusi kabisa Cha huo ugonjwa lakini hakina madhara(hapa utahitaji usaidizi wa wataalam ili wakupe ufafanuzi), Lengo nikuufanya mwili uwe aware na hao virus na kuuandaa Askari, so siku utakapo upata ugonjwa wenyewe mwili unakuwa unawafahamu hao virus na kupigana nao.

N.b mkuu naomba niishe hapo swali la nyongeza sitaweza kujibu maana naweza nikadanganya. Sehemu ambayo nimekosea kwa wale wataalamu ruksa kunirekebisha.
 
Ni jambo la kushangaza sana kutangaza watu wanaokufa, inabidi taarifa zote za pande zote Zitangazwe, kuna watu wengi wanapona,Lakini wao wanatuhaminisha kuwa ukipata Covid-19 ni kama death sentence! vyombo vya magharibi viko vitani na China.
Ndege inayoruka na kutua salama huwa haitangazwi,zinazotangazwa ni zile zilizopata ajali. Wako sawa kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa kwa mini hiyo kinga isitumike kwenye ukimwi maana ni. Virus pia
Shida ya ukimwi inakuja pale virusi vinapojizalisha maana vinatumia seli za muathirika ili kuendelea kujiongeza sasa hapo ukitaka kuvimaliza kabisa inakua ngumu maana itabidi na seli zako mwenyewe uziue hapo ndo mwanzo wa kujiua....arv inachofanya ni kupunguza kasi tu ya hivo virusi kuzaliana ili idadi yake isizidi ya zile seli nyeupe za kinga ya mwili.....na hizo seli za kinga ya mwili zinashindwa kuvimaliza virusi vya ukimwi sababu kuna virusi vinakua vimeingia ndani ya seli za aina nyingine za muathirika sasa zile seli nyeupe za kinga haziwezi kushambulia seli nyingine na kile kirusi kikitoka kwenye seli kilipoingia kinatoka kimejiongeza tena ....seli nyeupe inashambulia tu virusi ambavyo vipo nje ya seli
 
Wametengeneza kwa ustadi wa hali ya juu!
 
Hizo habari za wanaotibiwa wakapona hawatangazwi unazipata wapi?! Mbona kila siku wanatangaza na jana tu wameripoti.
 
Hata ebola wapo waliopona hapahapa Afrika!
 
Ilishasemwa kwamba kuna uwezekano wa Mtu kupona bila kutumia dawa.

Nadhani inategemea na kinga/uwezo wa kuhimili wa mwili wa muhusika.
 
Back
Top Bottom