Virusi vya corona: Madaktari wa Afrika Kusini wanatumia dawa ambayo haijathibitishwa kutibu Covid-19

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
3,382
2,000
Ivermectin imekuwa ikitumiwa kutibu virusi vya corona katika Amerika Kusini lakini bado haijathibitishwa kwa matibabu.

Dawa ya Ivermectin, ambayo imewagusa wengi kama dawa yenye ufanisi kwa tiba ya virusi vya corona ingawa haijaidhinishwa kimatibabu, imekuwa kitovu cha makabiliano ya kisheria nchini Afrika Kusini huku baadhi ya madaktari walitaka ihalalishwe kwa kupata kibali cha kutumiwa kwa binadamu.

Raia wengi wa Afrika Kusini wanahangaika kupata kitu ambacho kinaweza kupunguza athari za wimbi la tatu la maambukizi ya virusi vya corona.

Huku kukiwa na mpango wa utoaji wa chanjo ambao bado haujawafikia watu wote walio katika hatari ya kuambukizwa, kuna hofu kwamba nchi hiyo iliyoathriwa zaidi na corona barani Afrika inaweza kuumia zaidi wakati vipimo vya joto vitakaposhuka wakati wa msimu wa majira ya baridi.

Zaidi ya watu 52,000 wamekufa kutokana na virusi vya corona na ingawa maambukizi mapya kwa sasa yako chini, kwa ujumla maambukizi hayatoweki.

Ni katika muktadha huu ambao Ivermectin - dawa ambayo inatumiwa kuua minyoo-imepata imepota umaarufu. Baadhi ya madaktari wamekuwa wakiitoa kwa wagonjwa wenye virusi vya corona, wakisema kuwa wameona ushahidi kwamba inaweza kuondoa athari mbaya zaidi za Covid-19.

Hatahivyo, wadhibiti wa viwango vya dawa, watengenezaji wa dawa na baadhi ya wanasayansi wa ngazi juu nchini humo wote wameonya dhidi ya matumizi ya dawa hiyo ya minyoo katika kutibu virusi vya corona.

Baadhi ya raia wa Afrika Kusini wamekua wakidai kwamba mamlaka ziruhusu Ivermectin itumiwe

Imekuwa sasa maarufu katika masoko haramu-mamilioni ya tembe yamekuwa yakikamatwa nchini Afrika Kusini tangu mwanzoni mwa mwaka huu huku mitandao haramu ya uuzaji wa dawa hizo ikiendelea kuongezeka hadi katika mataifa ya China na India.

Kabla haijahusishwa na virusi vya corona, tembe 10 za Ivermectin zilikuwa zinauzwa kwa dola $4 -lakini sasa bei yake imeanda mara 15 katika soko hilo hilo.

Lakini matumizi ya Ivermectin kwa ajili ya virusi vya corona yameibua maoni tofauti nchini humo.

Tembe hizo hazijaidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya binadamu na Mamlaka ya udhibiti wa viwango vya afya (Sahpra), imesajiliwa kama tiba ya minyoo ya wanyama.

Licha ya haya, baadhi ya madaktari walianza kutumia hawa hii wakati Afrika Kusini ilipokuwa na viwango vya juu zaidi vya maambukizi ya corona mwezi Julai mwaka jana.

'Watu walikua wanakufa'

Profesa Nathi Mdladla, mkuu wa kituo cha tiba ya dharura katika Hospitali ya chuo cha George Mukhari Academic , ni mojawapo ya madaktari ambao wamekuwa wakitoa wito wa matumizi ya dawa ya Ivermectin katika visa vibaya vua corona.

"Wakati maambukizi yalipokuwa ya juu zaidi katika wimbi la kwanza, hospitali zote za umma na za kibinafsi pamoja na madaktari wa kibinafsi nchini Afrika Kusini walikuwa wakitumia dawa ya Ivermectin," Dkt Mdladla aliiambia BBC.

"Watu walikua wakifa na madaktari walikuwa wanaangalia aina mbalimbali za tiba kujaribu kunusuru maisha ya watu. Ivermectin ilikuwa ni moja ya madawa ambayo yalitumiwa na madaktari ."

Wao lilikuja kutoka America Kusini ambako madaktari walikuwa wakiitumia. Hivi karibuni zaidi, baadhi ya tafiti zilionesha kuwa inaweza kuwa ya ufanisi lakini utafiti zaidi unahitajika.

Lakini haikujulikana hadi mwishoni mwa mwaka jana ndipo wakaanza kuzuia matumizi yake, wakiwalazimisha madaktari ambao walikuwa wakiitoa kuacha kutoa dawa hii, kwa kuhofia kuwekewa vikwazo na mamlaka , Dkt Mdladla alisema.

Anaamini jibu hili halisaidii, hususan kwa familia ambazo haziwezi kununua tiba ambayo ni ghali.

Afrika Kusini ilianza mpango wa chanjo kwa umma mwezi Februari.

Sasa, vikundi vya utetezi, madaktari pande zote za mjadala na Sahpra watalazimika kutoa kesi yao mbele ya Mahakama Kuu ya Gauteng katika usikilizaji uliopangwa kutokea hivi karibuni.

"Mapambano ni juu ya ubora wa masomo ambayo yamefanywa hadi sasa. Tunachosema ni kwamba katika janga hilo, huwezi kamwe kuwa katika nafasi ya kutoa masomo haya ya kiwango cha juu na marefu, kwa sababu inamaanisha katika wakati huo huo, unaangalia watu wakifa, "anasema Dk Mdladla.

Madaktari wanaotetea kuruhusiwa matibabu hayo kwa ugonjwa wa coronavirus wanasema kwamba dawa hiyo haina tisho lolote kwa usalama.

Madhara mengine ya kawaida ni pamoja na kizunguzungu, kichefuchefu, kuhara, maumivu ya tumbo na upele wa ngozi, kulingana na Mamlaka ya kusimamia Chakula na Dawa ya Marekani.

Nchini Afrika Kusini imekuwa ikitumika kwa wanyama, lakini imependekezwa tu kwa matumizi ya binadamu na Shirika la Afya Ulimwenguni kutibu aina fulani ya upofu.

Walakini, Sahpra ina wasiwasi kuwa hakuna utafiti wa kutosha juu ya jinsi inavyoathiri wagonjwa wanaosumbuliwa na coronavirus na kwa hivyo inaogopa kuidhinisha matumizi yake.

Mnamo Desemba, ilikataza utumiaji wa dawa hiyo kwa watu isipokuwa madaktari wakitoa idhini kupitia maombi maalum ya "matumizi ya huruma" - hii inaruhusu dawa isiyoidhinishwa kutumiwa katika hali mbaya.

Uvaaji wa barakoa na kutosogeleana 'vinaweza kudumu kwa miaka '

Kwanini baadhi ya watu hupata corona kati ya dozi ya kwanza na ya pili ya chanjo.

Ikiwa inatumika katika visa hivi basi madaktari wanahitaji kutoa habari juu ya jinsi mgonjwa anavyoendelea.

Nadharia moja kwa nini inaweza kuonekana kuwa nzuri kwa wagonjwa walio na virusi vya corona ni kwamba inaweza kutibu vimelea vyovyote walivyobeba na hivyo kuwafanya kuwa na nguvu, bila kushughulikia virusi ambavyo husababisha Covid-19.

Lakini kwa vyovyote vile, mdhibiti wa dawa nchini Afrika Kusini alionya kuwa: "Hakuna ushahidi wa kutosha kuhusu au dhidi ya matumizi ya Ivermectin katika kuzuia au kutibu Covid-19."

Sahpra pia ilielezea wasiwasi wake juu ya utumiaji wa Ivermectin inayopatikana kutoka soko haramu, akisema "ubora hauwezi kuhakikishiwa".

Kampuni iliyotengeza dawa hiyo , Merck, pia imeonya dhidi ya utumiaji wa dawa hiyo kutibu coronavirus, ikisema: "Hatuamini kwamba data inayopatikana inasaidia usalama na ufanisi wa Ivermectin zaidi ya kipimo na idadi ya watu iliyoonyeshwa katika wakala wa kisheria aliyeidhinishwa kuagiza habari . "

Ni jambo ambalo Prof Abdool Karim, mmoja wa madaktari anayeongoza majibu ya virusi vya corona ya Afrika Kusini, pia ameangazia.

Anasema kuwa dozi zinazopewa watu zinaweza hata kuwa na sumu.

"Lazima isemwe wazi kwamba Ivermectin haiui virusi kwa kipimo ambacho binadamu anaweza kuvumilia. Kiasi cha dawa inayohitajika kuua virusi ni sumu kwa wanadamu. Chochote kinachofanya, sio kuua virusi," tovuti ya TimesLive inamnukuu akisema.
 
Bukyanagandi

JF-Expert Member
Jun 24, 2009
8,995
2,000
Legalize it.......
Tatizo hapo, dawa hiyo ni so cheap ndio maana Makampuni makubwa ya kuzalisha chanjo wana ipiga vita/hujumu dawa ya ivermectin hisitumike kutibu wagonjwa wa kovid - Big Pharma Companies Zina honga media za magharibi vitoe habari za kutisha watu Duniani ili waogope kutumia dawa hizo bafala yake wakubali chanjo ambazo bei zake ni za ghali sana.
 
Stefano Mtangoo

Verified Member
Oct 25, 2012
4,831
2,000
Nani aithibitishe wakati wao tayari ni madaktari? Mthibitishaji hatakuwa daktari kama wao?
Hili swali bahati mbaya wengi hawajiulizi. Tumetoa haki ya kuthibitisha usalama wa afya zetu kwenda kwa global agencies ambazo hazina uchungu na watu wetu kabisa.

Usishangae watu wakawapinga madaktari wao wenyewe wakawaamini akina Ted ambao hawana uchungu nao.

Ivermectin na Hydroxylchroloquine zinaonekana ni nzuri kupambana na huyu mdudu. Ila wakithibitisha maana yake si pandemic is over? Chanjo watamuuzia nani? Hasara atabeba nani?
 
Bambushka

JF-Expert Member
Jan 9, 2020
2,516
2,000
Bongo ipo na tunaitumia. Ipo pharmacy kubwa Mwenge, na pharmacy ingine ina matawi Mlimani city.

Kuna mawili uokoe maisha ya mpendwa wako au usubirie sijui mamlaka zije na wiki ya nyungu na juice za pilipili kichaa.

Sijui kwanini sijamuona field marshall wa afya akiingia wenye machine za kujifukiza Muhimbili?

Everyday is Saturday............................... :cool:
 
Shadow7

JF-Expert Member
Sep 28, 2020
4,437
2,000
Dawa ya Ivermectin, ambayo imewagusa wengi kama dawa yenye ufanisi kwa tiba ya virusi vya corona ingawa haijaidhinishwa kimatibabu, imekuwuwa katika makabiliano ya kisheria nchini Afrika Kusini huku baadhi ya madaktari wakitaka ihalalishwe kwa kupata kibali cha kutumiwa kwa binadamu.

image.jpg

Baadhi ya madaktari wamekuwa wakiitoa kwa wagonjwa wenye virusi vya corona, wakisema kuwa wameona ushahidi kwamba inaweza kuondoa athari mbaya zaidi za Covid-19.

Ni katika muktadha huu ambao Ivermectin – dawa ambayo inatumiwa kuua minyoo-imepata umaarufu. Hatahivyo, wadhibiti wa viwango vya dawa, watengenezaji wa dawa na baadhi ya wanasayansi wa ngazi juu nchini humo wote wameonya dhidi ya matumizi ya dawa hiyo ya minyoo katika kutibu virusi vya corona.

Imekuwa sasa maarufu katika masoko haramu-mamilioni ya tembe yamekuwa yakikamatwa nchini Afrika Kusini tangu mwanzoni mwa mwaka huu huku mitandao haramu ya uuzaji wa dawa hizo ikiendelea kuongezeka hadi katika mataifa ya China na India.

Raia wengi wa Afrika Kusini wanahangaika kupata kitu ambacho kinaweza kupunguza athari za wimbi la tatu la maambukizi ya virusi vya corona.

Huku kukiwa na mpango wa utoaji wa chanjo ambao bado haujawafikia watu wote walio katika hatari ya kuambukizwa, kuna hofu kwamba nchi hiyo iliyoathriwa zaidi na corona barani Afrika inaweza kuumia zaidi wakati vipimo vya joto vitakaposhuka wakati wa msimu wa majira ya baridi.

Zaidi ya watu 52,000 wamekufa kutokana na virusi vya corona na ingawa maambukizi mapya kwa sasa yako chini, kwa ujumla maambukizi hayatoweki.

Woman getting vaccinated

Kabla haijahusishwa na virusi vya corona, tembe 10 za Ivermectin zilikuwa zinauzwa kwa dola $4 -lakini sasa bei yake imeanda mara 15 katika soko hilo hilo.

Lakini matumizi ya Ivermectin kwa ajili ya virusi vya corona yameibua maoni tofauti nchini humo.
Tembe hizo hazijaidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya binadamu na Mamlaka ya udhibiti wa viwango vya afya (Sahpra), imesajiliwa kama tiba ya minyoo ya wanyama.

Licha ya haya, baadhi ya madaktari walianza kutumia hawa hii wakati Afrika Kusini ilipokuwa na viwango vya juu zaidi vya maambukizi ya corona mwezi Julai mwaka jana.

Watu walikua wanakufa‘
Profesa Nathi Mdladla, mkuu wa kituo cha tiba ya dharura katika Hospitali ya chuo cha George Mukhari Academic , ni mojawapo ya madaktari ambao wamekuwa wakitoa wito wa matumizi ya dawa ya Ivermectin katika visa vibaya vua corona.

“Wakati maambukizi yalipokuwa ya juu zaidi katika wimbi la kwanza, hospitali zote za umma na za kibinafsi pamoja na madaktari wa kibinafsi nchini Afrika Kusini walikuwa wakitumia dawa ya Ivermectin,” Dkt Mdladla aliiambia BBC.

“Watu walikua wakifa na madaktari walikuwa wanaangalia aina mbalimbali za tiba kujaribu kunusuru maisha ya watu. Ivermectin ilikuwa ni moja ya madawa ambayo yalitumiwa na madaktari .”

Wao lilikuja kutoka America Kusini ambako madaktari walikuwa wakiitumia. Hivi karibuni zaidi, baadhi ya tafiti zilionesha kuwa inaweza kuwa ya ufanisi lakini utafiti zaidi unahitajika.

Lakini haikujulikana hadi mwishoni mwa mwaka jana ndipo wakaanza kuzuia matumizi yake, wakiwalazimisha madaktari ambao walikuwa wakiitoa kuacha kutoa dawa hii, kwa kuhofia kuwekewa vikwazo na mamlaka , Dkt Mdladla alisema.

Anaamini jibu hili halisaidii, hususan kwa familia ambazo haziwezi kununua tiba ambayo ni ghali.
Sasa, vikundi vya utetezi, madaktari pande zote za mjadala na Sahpra watalazimika kutoa kesi yao mbele ya Mahakama Kuu ya Gauteng katika usikilizaji uliopangwa kutokea hivi karibuni.

“Mapambano ni juu ya ubora wa masomo ambayo yamefanywa hadi sasa. Tunachosema ni kwamba katika janga hilo, huwezi kamwe kuwa katika nafasi ya kutoa masomo haya ya kiwango cha juu na marefu, kwa sababu inamaanisha katika wakati huo huo, unaangalia watu wakifa, “anasema Dk Mdladla.

Madaktari wanaotetea kuruhusiwa matibabu hayo kwa ugonjwa wa coronavirus wanasema kwamba dawa hiyo haina tisho lolote kwa usalama.

Madhara mengine ya kawaida ni pamoja na kizunguzungu, kichefuchefu, kuhara, maumivu ya tumbo na upele wa ngozi, kulingana na Mamlaka ya kusimamia Chakula na Dawa ya Marekani.

Nchini Afrika Kusini imekuwa ikitumika kwa wanyama, lakini imependekezwa tu kwa matumizi ya binadamu na Shirika la Afya Ulimwenguni kutibu aina fulani ya upofu.

Walakini, Sahpra ina wasiwasi kuwa hakuna utafiti wa kutosha juu ya jinsi inavyoathiri wagonjwa wanaosumbuliwa na coronavirus na kwa hivyo inaogopa kuidhinisha matumizi yake.

Mnamo Desemba, ilikataza utumiaji wa dawa hiyo kwa watu isipokuwa madaktari wakitoa idhini kupitia maombi maalum ya “matumizi ya huruma” – hii inaruhusu dawa isiyoidhinishwa kutumiwa katika hali mbaya.

Ikiwa inatumika katika visa hivi basi madaktari wanahitaji kutoa habari juu ya jinsi mgonjwa anavyoendelea.
Nadharia moja kwa nini inaweza kuonekana kuwa nzuri kwa wagonjwa walio na virusi vya corona ni kwamba inaweza kutibu vimelea vyovyote walivyobeba na hivyo kuwafanya kuwa na nguvu, bila kushughulikia virusi ambavyo husababisha Covid-19.

Lakini kwa vyovyote vile, mdhibiti wa dawa nchini Afrika Kusini alionya kuwa: “Hakuna ushahidi wa kutosha kuhusu au dhidi ya matumizi ya Ivermectin katika kuzuia au kutibu Covid-19.”

Sahpra pia ilielezea wasiwasi wake juu ya utumiaji wa Ivermectin inayopatikana kutoka soko haramu, akisema “ubora hauwezi kuhakikishiwa”. Kampuni iliyotengeza dawa hiyo , Merck, pia imeonya dhidi ya utumiaji wa dawa hiyo kutibu coronavirus, ikisema:

“Hatuamini kwamba data inayopatikana inasaidia usalama na ufanisi wa Ivermectin zaidi ya kipimo na idadi ya watu iliyoonyeshwa katika wakala wa kisheria aliyeidhinishwa kuagiza habari . “

Ni jambo ambalo Prof Abdool Karim, mmoja wa madaktari anayeongoza majibu ya virusi vya corona ya Afrika Kusini, pia ameangazia.

Anasema kuwa dozi zinazopewa watu zinaweza hata kuwa na sumu. “Lazima isemwe wazi kwamba Ivermectin haiui virusi kwa kipimo ambacho binadamu anaweza kuvumilia. Kiasi cha dawa inayohitajika kuua virusi ni sumu kwa wanadamu. Chochote kinachofanya, sio kuua virusi,” tovuti ya TimesLive ina mnukuu akisema.
 
TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
7,887
2,000
Hebu tuvute muda tuone nini kitafuata baada ya hizi tembe kuruhusiwa au kukataliwa.
 
Mlenge

Verified Member
Oct 31, 2006
2,047
2,000
Heeee kumbe kuna ivermectin ya kidonge??mi naijua ya Maji ambayo hua tunatumia kutibia minyoo ya Nguruwe.
Zipo, na Tanzania zimekuwa zikitumika kutibu mabusha/matende. Kwenye wimbi linaloishilia la korona, zimejipatia umashuhuri nchini kote katika kupambana na korona.

Gama

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
12,219
2,000
.
Tembe hizo hazijaidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya binadamu na Mamlaka ya udhibiti wa viwango vya afya (Sahpra), imesajiliwa kama tiba ya minyoo ya wanyama
Dawa hii imesajiliqa kote duniani kama dawa ya binadamu pia kwa miongo mingi. Hii ndiyo dawa bora ya kutibu elephantiasis. Kwa tanzania imekuwa ikitolewa kama dawa yankinga ya matende na mabusha.

Kuhusu kitibu covid; india na australia zimeshaanza kuitumia, kenya pia imetumika kwaafanikio
 
Shadow7

JF-Expert Member
Sep 28, 2020
4,437
2,000
Zipo, na Tanzania zimekuwa zikitumika kutibu mabusha/matende. Kwenye wimbi linaloishilia la korona, zimejipatia umashuhuri nchini kote katika kupambana na korona.

Kumbe inatibu na busha :oops: :oops:
 
Shadow7

JF-Expert Member
Sep 28, 2020
4,437
2,000
Dawa hii imesajiliqa kote duniani kama dawa ya binadamu pia kwa miongo mingi. Hii ndiyo dawa bora ya kutibu elephantiasis. Kwa tanzania imekuwa ikitolewa kama dawa yankinga ya matende na mabusha.

Kuhusu kitibu covid; india na australia zimeshaanza kuitumia, kenya pia imetumika kwaafanikio
Sawa mkuu
 
Nafaka

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
5,828
2,000
image.jpg

Baadhi ya madaktari wamekuwa wakiitoa kutoa masomo haya ya kiwango cha juu na marefu, kwa sababu inamaanisha katika wakati huo huo, unaangalia watu wakifa, “anasema Dk Mdladla.

Madaktari wanaotetea kuruhusiwa matibabu hayo kwa ugonjwa wa coronavirus wanasema kwamba dawa hiyo haina tisho lolote kwa usalama.

Madhara mengine ya kawaida ni pamoja na kizunguzungu, kichefuchefu, kuhara, maumivu ya tumbo na upele wa ngozi, kulingana na Mamlaka ya kusimamia Chakula na Dawa ya Marekani.

Nchini Afrika Kusini imekuwa ikitumika kwa wanyama, lakini imependekezwa tu kwa matumizi ya binadamu na Shirika la Afya Ulimwenguni kutibu aina fulani ya upofu.

Walakini, Sahpra ina wasiwasi kuwa hakuna utafiti wa kutosha juu ya jinsi inavyoathiri wagonjwa wanaosumbuliwa na coronavirus na kwa hivyo inaogopa kuidhinisha matumizi yake.

Mnamo Desemba, ilikataza utumiaji wa dawa hiyo kwa watu isipokuwa madaktari wakitoa idhini kupitia maombi maalum ya “matumizi ya huruma” – hii inaruhusu dawa isiyoidhinishwa kutumiwa katika hali mbaya.

Ikiwa inatumika katika visa hivi basi madaktari wanahitaji kutoa habari juu ya jinsi mgonjwa anavyoendelea.
Nadharia moja kwa nini inaweza kuonekana kuwa nzuri kwa wagonjwa walio na virusi vya corona ni kwamba inaweza kutibu vimelea vyovyote walivyobeba na hivyo kuwafanya kuwa na nguvu, bila kushughulikia virusi ambavyo husababisha Covid-19.

Lakini kwa vyovyote vile, mdhibiti wa dawa nchini Afrika Kusini alionya kuwa: “Hakuna ushahidi wa kutosha kuhusu au dhidi ya matumizi ya Ivermectin katika kuzuia au kutibu Covid-19.”

Sahpra pia ilielezea wasiwasi wake juu ya utumiaji wa Ivermectin inayopatikana kutoka soko haramu, akisema “ubora hauwezi kuhakikishiwa”. Kampuni iliyotengeza dawa hiyo , Merck, pia imeonya dhidi ya utumiaji wa dawa hiyo kutibu coronavirus, ikisema:

“Hatuamini kwamba data inayopatikana inasaidia usalama na ufanisi wa Ivermectin zaidi ya kipimo na idadi ya watu iliyoonyeshwa katika wakala wa kisheria aliyeidhinishwa kuagiza habari . “

Ni jambo ambalo Prof Abdool Karim, mmoja wa madaktari anayeongoza majibu ya virusi vya corona ya Afrika Kusini, pia ameangazia.

Anasema kuwa dozi zinazopewa watu zinaweza hata kuwa na sumu. “Lazima isemwe wazi kwamba Ivermectin haiui virusi kwa kipimo ambacho binadamu anaweza kuvumilia. Kiasi cha dawa inayohitajika kuua virusi ni sumu kwa wanadamu. Chochote kinachofanya, sio kuua virusi,” tovuti ya TimesLive ina mnukuu akisema.
Pia wanadai inaua mbu wa malaria wafyonza damu kutoka kwa mtu aliyeitumia na kuna utafiti unaitwa Bohemia unafanyika Rufiji muda huu kuona kama ni kweli.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom