Kwanza kabisa, unaelewa kwamba swali siyo kuwa kashindwa, bali kwa nini hakuumba ulimwengu ambao hauwezekani kuwa na mabaya?
Naona unazunguka pale pale na jibu nimeshakupa. Nakusaidia kwa mtindo huu. Allah ni muweza wa yote.
Nakupa mfano wa namna ambavyo Allah anafanya mambo yake, kwa hekima na kwa malengo maalumu. Anasema Allah aliye juu katika Qur'aan :
51. Na tungeli taka tungeli peleka katika kila mji Mwonyaji. (al-Furqaan : 51)
Leo hii kuna jambo kuhusu kwanini hakuna Mtume muafrika au kwanini au hakutoka Afrika. Allah anajibu kwa mtindo huo. Huo ni mfano tu.
Hili swali nilishakujibu tangu ulipo niuliza sababu ni mtu wa kupoteza muda na kutokuwa na hoja unarudia swali lile lile. Allah ndiye ameruhusu au anaruhusu mabaya yatokee, sababu ana hekima zake na ndiyo utaratibu wake ameuweka na ndiyo bora zaidi. Unapo taka iwe unavyotaka mambo mengi yasingekuwepo na mngetaka iwe kinyume chake sababu Allah anatujua waja wake.
Ulimwengu ambao hauna mabaya angetaka kuumba angeumba ila ameumba ulimwengu ambai ndani yake ameruhusu mabaya yatokee kwa sababu ambazo nimeshakutajia huko juu.
Labda nikupe kazi jaribu juelezea au kuweka picha ya ulimwengu ambao mabaya yasikuwepo, ungekuwaje ulimwengu huo ?
Ulimwengu huo ungekuwa logically consistent na Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na ujuzi wote
Thibitisha hilo kisha nikuulize maswali ujibu, maana naona unakimbia maswali yangu. Kingine utuambie umejuaje kama ungekuwa "Logically consistent" wakati haujaudiriki ?
Ulimwengu huu tunaouona unaoruhusu mabaya hauko logically consistent na Mungu huyo. Unaonesha Mungu huyo hayupo.
Hilo nimeshakwambia ni uchachefu wako wa maarifa na kufikiria kwako kitoto ndiyo maana unaona hivyo kama unavyodai, ndiyo maana hiyo mantiki unayoitumia inashindwa kuthibitisha ya kuwa Mola hayupo. Hili nalo nilikueleza huko nyuma.
Kingine siyo ulimwengu ndiyo unao ruhusu bali ni Allah ndiye anaye ruhusu na kutaka iwe hivyo, na kama asingetaka isingekuwa hivyo. Yeye ndiyo muweza wa kila kitu.
Unaonyeshaje Mola hayupo ? Shida yako unashindwa kuelezea mchakato unavyo kwenda mpaka kufikia hatua ya kuthibitisha ya kuwa Mola hayupo, yaani unasema tu. Ngoja nikupe mfano, majanga au mabaya huwa yanadumu au hayadumu ? Yanapo ondoka majanga nani huyaondoa majanga hayo ? Je kuondoka kwa majanga na kuja faraja huashiria nini ?
Mimi nataka unionyeshe mtiririko wa hitimisho lako umeanzia wapi na umeishia.
Kwanini Mungu atumie mabaya kutukumbusha? Watoto wafe, magonjwa yaenee, matetemeko ya ardhi, mafuriko etc?
Maisha hayaishii duniani. Mfano mzuri watu wenye akili huwa wanajiuliza hivi, hivi ni kweli sisi tupo duniani tu tuishi halafu tufe iwe basi ? Vipi kuhusu mafisadi vipi kuhusu wenye kufanya dhuluma na kuwaua watu bila hatia ? Jibu linakuja ya kuwa tunaishi kwa malengo maalumu na maisha hayaishii duniani bali kuna siku ya malipo.
Safi kabisa, sababu ni mambo yanagusa hisia za watu moja kwa moja na kwa haraka sana. Watoto kufa, hufa kwa wakati wao unapofika na maisha hayaishii kwenye kufa tu, kadhalika ameleta kila ugonjwa na dawa zake, ndiyo maana kuna ugonjwa na dawa zake, na maradhi ni sababu ya kufutiw mtu madhambi yake.
Unapoleta mafuriko na ndiyo yeye mwenyewe huyaondoa hayo mafuriko, kadhalika matetemeko.
Hii dunia inayoruhusu maovu inapingana na nature yake ya upendo wote.
Kwa nini hakuumba ulimwengu ambao maovu hayawezekani kuwapo, na watu bado wanamkumbuka?
Dunia hairuhusu, bali Allah ndiyo anaruhusu na kutaka iwe hivi ilivyo, huo ndio uwezo wa Allah mtukufu.
Sababu amejaalia kila jambo na sababu zake.
Kingine cha kustaajabisha, nataka nikuonyeshe ujinga wako ulipo katika hili hili swali, jalia kwamba hajaumba huo ulimwengu unao utaka wewe, vipi kupitia majanga na maovu kuwepo kuthibitishe ya kuwa Mola hayupo ?