Wanaopenda kula kula kwani hamshibi?

Jitu unakuta umepanda nalo basi ktk safari mara limenunua mahindi ya kuchemsha linamenya maganda linakula.
Mara mishikaki, mara juisi daah alafu lina mwili mkubwa.
Hivi ni kwa nini mtu usile ukashiba halafu utulie!
Yani watu wa hivi wananikera...mwisho utasikia dereva naomba nijisaidie! Huku maushuzi yanamtoka...
 
Kula ni starehe wewe kama starehe nyingine na hakuna starehe nzuri kama kula na kingine ujue duniani kuna mamilioni ya aina za chakula kuna vyakula ukila wewe mwenyewe utasema mungu anapenda

Off course mimi binafsi napenda kulakula ila tatizo pesa mfano kuna Karanga za mayai ningekuwa na Uhuru wa kifedha ningekula ata nane kwa siku ,kuna maziwa nayapenda vibaya ,nikienda kula ubwabwa napenda niweke na nyama au samaki nk kwaiyo ningekuwa na pesa mimi kwasiku ningekuwa nina spend pesa nyingi katika kula ila tatizo pesa

Pia akuna mtu asiyekuwa na interest ya kulakula ila tatizo ni kwamba hauna Uhuru wa kifedha tu nandomana mara nyingi unakula kitu kutokana na bei yake ila sio kutokana na kukipenda

Yani usiponde kabisa kula nina sababu nyingi za kutafuta mafanikio kwenye maisha yangu ila moja wapo ni kula

NB: sio kwamba upendi kulakula,kuvaa vizuri nk ila tatizo hauna uhuru wa fedha ndomana kuna kauri inasema pata pesa tujue tabia yako
 
Tofauti wao na mimi mimi silagi safarini au ovyo i mean njee ya home mpaka iwe home au pawe pasafi.
 
Tatizo munachanganya vitu amuelewi mada yenu kuna kulakula arafu kuna kulakula bila ya ustaarabu munachokizungimzia nyie sasa kulakula bila ustaarabu mfano kwenye gari
 
Kama kuna uwiano na ratiba ya kuhudhuria maliwato, basi wale tu.
 
Ata mazuri ya pepo yakitajwa vyakula aviachwi utasikia kuna mito ya kuririsha maziwa mala nyama ya ndege kula starehe ya halali
 
Habari wadau,

Aisee wakuu, kuna watu wanapenda kula kula yani utakuta ratiba yake ya siku ameshakula makorokoro kibao.

Utakuta asubuhi saa 1 kanywa chai na kiporo , alafu ikifika saa 4 anakunywa supu na chapati 2, ikifika saa 5 anakula sambusa 2 na soda.

Ikifika mchana saa 8 anakula ugali na samaki na juice, ikifika saa 8 anakula karanga au keki ikifika saa 10 akikutana na muhindi anakula.

Usiku anakula tena lisahani la wali na nyama na juice.

Wadau nini chanzo cha kulakula kila saa? Ni ulafi au?
Anatumia hela yako??
Au huwa anakuja kuazima tumbo lako atunzie chakula??

Hivi wabongo ni lini mtaacha kufwatilia mambo yasiyowahusu??
 
Anatumia hela yako??
Au huwa anakuja kuazima tumbo lako atunzie chakula??

Hivi wabongo ni lini mtaacha kufwatilia mambo yasiyowahusu??
We mbona unawasemea wanaokula wewe yanakuhusu nini...pita hiviii...
 
Mie nakula mnoo kama nipo na stress,kula inanipunguzia stress,yaan naweza malizo pkt zima la soseji ndani ya siku moja,nna ndizi za kukaanga,supu,ubuyu yaan nakua nacheza na friji!! Nakua km mbuzi natafuna tafuna tu.Ila stress zikiishaa arrgh nakula milo mitatu tu naridhika.
 
Habari wadau,

Aisee wakuu, kuna watu wanapenda kula kula yani utakuta ratiba yake ya siku ameshakula makorokoro kibao.

Utakuta asubuhi saa 1 kanywa chai na kiporo , alafu ikifika saa 4 anakunywa supu na chapati 2, ikifika saa 5 anakula sambusa 2 na soda.

Ikifika mchana saa 8 anakula ugali na samaki na juice, ikifika saa 8 anakula karanga au keki ikifika saa 10 akikutana na muhindi anakula.

Usiku anakula tena lisahani la wali na nyama na juice.

Wadau nini chanzo cha kulakula kila saa? Ni ulafi au?
Watu wa namna hii lazima wawe na minyoo tumboni
 
Napenda kula na sio kula tu bali vile vizuri na vitamu soseji, kuku choma, nyama choma, sanbusa za nyama, pizza, burger, zege mishkaki, maziwa, soda, mijuisi mikubwa, eat sam moo, nk nk

Ila tatizo pesa na ndio mana nataka kuwa na pesa nyingi sana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom