Wanaoomuamini Mungu, wana nini cha kujivunia?

Hoja yako ipo juu juu tu na wala haina mantiki yoyote ile.

Faith isn't about having a better life now , it's about having eternal purpose beyond now. Usidharau nguvu ya imani kwa kipimo cha dunia kinachopita.
 
Kwa akili zako unaona alifanya kazi ya maaana! Huo mua unaouona mtamu, kuna mwingine kwake ni mchungu. Kuna na mwingine haujui. Vinginevyo tungeuliza aliekupa mkongoto wengine wakapewa mashimo; au aliekupa akili finyu, wengine wakajaziwa. Nilichouliza mimi, nani ana haki ya kumdhihaki mwenzie kisa imani! We kama unaamini, ni juu yako, una sababu zako, na wasioamini, wana sababu zao.
Heshimu mtazamo wako, lakini kumbuka,si kila mtu anaona mambo kwa jicho lako. That’s your personal lens, not a universal fact. Watu wanaamini kwa misingi tofauti, usiwavalie watu fikra zako as if ni sare.
 
Wanajiona wana monopoly of truth.

Ukiamini Mungu wako ni wa kweli ni lazima uamini uko kwenye upande wenye monopoly hii.
Siyo sahihi kusema mtu ana monopoly of truth kwa sababu anaamini Mungu wake ni wa kweli. Belief in truth is not the same as claiming exclusive ownership of it. Watu wengi wana imani tofauti, na hiyo haimaanishi wote wanadai kuwa wao pekee ndio wako sahihi.

Kama kila mtu ana uhuru wa kuamini anachokiona kuwa kweli, basi hakuna mwenye monopoly , kuna tofauti za kiimani. Truth, by nature, invites sincere search, not arrogant possession.
 
Ukishaamini Mungu wako ndiye wa kweli, lazima utaona wale wote wasioamini Mungu wako hawaujui ukweli.

Na ukiamini kuwa wasioamini Mungu wako wanaamini kweli, basi imani yako kwa Mungu wako si ya kweli, una shaka.

This is a mutually exclusive proposition.

Huwezi kuamini Yesu ndiye njia pekee ya kwenda mbinguni kwenye uzima wa milele halafu hapo hapo ukaamini kuwa hata Buddha naye anaweza kukufikisha mbinguni kwenye uzima wa milele.

That is a contradiction.

Huelewi wapi?
 
Uabudu ng'ombe au jua tusikushangae? Lazima tukushangae kukuona umepotea njia.
 
Heshimu mtazamo wako, lakini kumbuka,si kila mtu anaona mambo kwa jicho lako. That’s your personal lens, not a universal fact. Watu wanaamini kwa misingi tofauti, usiwavalie watu fikra zako as if ni sare.
Mkuu, hii imetokana na majibu yake, wala swali nililouliza halihusiani na haya. Mi nimeuliza kwa nini wanaoamini, wanawaona wasioamini kama vituko. Majibu aliyonipa, ndo yaliyopelekea huko kote. Wala si kwamba namforce mtu aamini navyoamini mimi.
 
Ukishaamini Mungu wako ndiye wa kweli, lazima utaona wale wote wasioamini Mungu wako hawaujui ukweli.

Na ukiamini kuwa wasioamini Mungu wako wanaamini kweli, basi imani yako kwa Mungu wako si ya kweli, una shaka.

This is a mutually exclusive proposition.

Huwezi kuamini Yesu ndiye njia pekee ya kwenda mbinguni kwenye uzima wa milele halafu hapo hapo ukaamini kuwa hata Buddha naye anaweza kukufikisha mbinguni kwenye uzima wa milele.

That is a contradiction.

Huelewi wapi?
Hoja yako inaonekana kama black or white thinking, si lazima imani yangu iwe ya kutengwa na imani za wengine. Inawezekana Mungu ana njia nyingi za kuwapata watu, na imani tofauti zinaweza kuwa njia tofauti za kuuelekea ukweli mmoja. Hii si shaka bali ni mtazamo mpana zaidi wa ukweli, ambao haupimwi kwa kufunga akili kwenye sentensi moja tu.

Faith in one truth doesn't mean denying all others , ukweli unaweza kuwa na nyenzo tofauti, si lazima ziwe contradictory.
 
Uabudu ng'ombe au jua tusikushangae? Lazima tukushangae kukuona umepotea njia.
Ndo hapo sasa. Je, kwa ninin mimi nisieamini, nisiwaone nyie mnaoamini mmepotea njia? Hili swali lina mabishano hakika. Swali lilikuwa kwa nini sasa, muwaone wamepotea njia, na wao wakiwaona nyie, wanaona ni kawaida, hawajishughulishi na kuwaconvice musiamini? Af wanaoamini, wanataka waonekane wao ndo wako sahihi
 
Mkuu, hii imetokana na majibu yake, wala swali nililouliza halihusiani na haya. Mi nimeuliza kwa nini wanaoamini, wanawaona wasioamini kama vituko. Majibu aliyonipa, ndo yaliyopelekea huko kote. Wala si kwamba namforce mtu aamini navyoamini mimi.
Mkuu kumwona asiyeamini kama kichekesho si tabia ya waumini wa kweli, bali ni udhaifu wa binadamu kujiinua kwa kuwadharau wengine.

Waumini wa kweli hawako hivyo.
 
Hoja yako inaonekana kama black or white thinking, si lazima imani yangu iwe ya kutengwa na imani za wengine. Inawezekana Mungu ana njia nyingi za kuwapata watu, na imani tofauti zinaweza kuwa njia tofauti za kuuelekea ukweli mmoja. Hii si shaka bali ni mtazamo mpana zaidi wa ukweli, ambao haupimwi kwa kufunga akili kwenye sentensi moja tu.

Faith in one truth doesn't mean denying all others , ukweli unaweza kuwa na nyenzo tofauti, si lazima ziwe contradictory.
Ukishaqmini imani tofauti zinaweza kuwa za ukweli ndiyo by definition umeweka shaka kwenye imani yako.

Kwamba wewe huna monopoly ya ukweli, na wale wanaweza kuwa na ukweli.

Huelewi wapi?
 
Juzi nimeona hii video, jamaa anawahubiria wayahudi huko Israeli.

Anawasomea Isaya 53 ile "alidharauliwa alikataliwa alijeruhiwa kwa ajili ya dhambi zetu", anawauliza hiyo mistari ni ya agano jipya au la kale? WOTE hadi mbabu wamesema ni agano jipya kwasababu inamuongelea Yesu ! ! !

View: https://youtube.com/shorts/PhRvfkg_Dts?si=wVsUGS-72IX6HZRP

They missed the Messiah! ! He's written all over their books and they didn't and still don't see him.....but they will soon, and they will call upon the name of the Lord Jesus, and he'll finally arrive!
 
Kuna rafiki yangu mpendwa,jana alinipigia simu anahitaji kijana kuna ofisi anahitaji kufungua,hakika hiyo sio ofisi yake ya kwanza ni almost kama ya 5 kwa biashara tofauti

Aliniambia anahitaji kijana,lakini sharti la kwanza ni kuwa muislam
Hakika nilimjibu mbona unaleta udini ndugu???

Alijibu kwakweli siwezi pangua hilo,nilimuacha aende zake maana nilitambua ata mimi ni vile anapenda mawazo yangu na michango yangu kwenye maswala tofauti lakini si rafiki kama ninavyomchukulia hakika, na anajua kuhusu mimi na maswala ya imani

Hakika yule sio rafiki tena bali mimi ndiye nilidhani ni rafiki,ni mengi kanisaidia lakini nahisi nilikuwa nikidanganya akili yangu
Watu wengi hushindwa kutofautisha kazi na iman na hii ni shida kubwa sana
 
Ukishaqmini imani tofauti zinaweza kuwa za ukweli ndiyo by definition umeweka shaka kwenye imani yako.

Kwamba wewe huna monopoly ya ukweli, na wale wanaweza kuwa na ukweli.

Huelewi wapi?
Kukubali kuwa imani tofauti zinaweza kuwa na chembe chembe za ukweli si sawa na kuwa na shaka kwenye imani yako, bali ni kuwa na unyenyekevu wa kiakili (intellectual humility).

Kushikilia imani yako kwa dhati huku ukitambua kuwa wengine pia wanaweza kuwa na nuru fulani si udhaifu wa imani, ni hekima ya kutambua mipaka ya uelewa wa binadamu mbele ya mambo ya kiroho yasiyopimika.

Ukweli hauhitaji kuwa wa mtu mmoja pekee ili uwe wa kweli.

Huelewi wapi mkuu?
 
Mtu anayeamini kabisa 100% kuwa Mungu wake ndiye wa kweli hatakiwi kuwa na intellectual humility.

Intellectual humility ni shaka, ni kukubali kuwa inawezekana umekosea. Hiyo si imani 100% kwamba Mungu wako ndiye wa ukweli.
 
Si kweli kwamba intellectual humility ni sawa na shaka katika imani. Mtu anaweza kuwa na imani thabiti 100% kuwa Mungu wake ndiye wa kweli, at the same time akawa na intellectual humility, yaani, utayari wa kusikiliza wengine kwa heshima, si kwa sababu anashuku, bali kwa sababu anatambua kuwa binadamu wote tuna mipaka ya maarifa.

Kuwa mnyenyekevu kiakili (intellectually humble) si kusema nimekosea, bali kusema najua niaminicho, lakini sihitaji kudharau walio na mtazamo tofauti ili kuimarisha imani yangu. Imani ya kweli haipaswi kuwa na hofu ya maswali, bali inajiamini hata mbele ya hoja pinzani.
 
Sasa mtu anayeamini Mungu wake ni wa kweli 100% na anamuongoza atamsikiliza vipi binadamu tu kwa kuwa binadamu tuna mipaka ya maarifa?

Kwa nini unataja mipaka ya maarifa ya binadamu wakati mwenzako anaamini 100% anamtegemea Mungu na hamtegemei binadamu?
 
Hakika kwa sasa najitahidi kudanganya watu kwa mfano nilikuwa tabora,watu wakawa makundi kwa maelfu wakiniuliza dini yangu

Nikasema sina dini,nilionekana kana kwamba kituko,jamii kwa mbali ikaanzs kunikataa na mambo yangu yakaanza kugoma

Ikabidi nijifanye nimesilimishwa,hakika jamii walifurahi sana nikaendelea kuungwa mkono kwa kile nilikuwa nafanya kwa asilimia kubwa

Hakika dini ni ugonjwa
Uchizi kabisa 🙌 😂
 
Back
Top Bottom