EMT
Platinum Member
- Jan 13, 2010
- 14,477
- 15,357
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Morogoro limesema halitawafungisha ndoa watarajiwa watakaoingia kwenye ibada wakiwa wamevalia mavazi yanayodhalilisha hasa kwa wanawake kuonesha sehemu ya matiti nje na migongo wazi.
Makamu wa Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania ( KKKT) Dayosisi ya Morogoro, Mchungaji George Pindua, alitoa agizo hilo kwa niaba ya uongozi wa Kanisa kabla ya Askofu Jacob Paulo ole Mameo kumkaribisha Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa kuendesha harambee.
''Kanisa limeshindwa kuvumilia tabia iliyojengeka ya kuona mavazi yanayovaliwa hasa kwa wanawake ya kuacha matiti yakionekana ...hili sasa ni agizo kwenye ibada hasa ya ndoa, wanaovaa mavazi hayo, wachungaji msiruhusu ndoa hiyo ifungwe'' alisema Makamu wa Askofu.
''Wazee wa Kanisa sasa muwe na vitenge maalumu vya kuwafunika hawa mabibi harusi wenye kuvaa magauni yanayoacha sehemu ya matiti wazi...hili haturuhusu kuendelea kufanyika'' alisema Makamu wa Askofu.
Alisema ''Tunawaheshimu mama zetu, mmetulea, lakini kwa hili la kuacha sehemu ya maziwa kuonekana wazi, hatutalikubali kuanzia sasa, yafuateni haya maagizo, msiwakwaze wachungaji '' aliongeza kusema.
Pamoja na kuzuia uvaaji wa nguo zinazoonesha sehemu ya matiti wazi, alizitaja nguo nyingine ambazo hazitakiwi kuvaliwa kanisani ni zile za kulalia ambazo ni suruali zinazobana na kuonesha mapaja.
"Ni budi sisi waumini tuheshimu maadili ya kumcha Mungu na moja ni uvaaji wa mavazi ya heshima mbele ya Mungu ...zile suruali zinazoonesha maumbile yote ya ndani zisitumike kuingia kwenye ibada '' alisisitiza Makamu wa Askofu.
http://www.habarileo.co.tz/index.php/habari-za-kitaifa/8683-wanaoonesha-matiti-kutofungishwa-ndoa