Wanaomtetea Prof. Muhongo Sospeter 'Wanaangamia kwa kukosa maarifa'

Wanaomtetea Prof. Muhongo Sospeter 'Wanaangamia kwa kukosa maarifa'

Right. Kwa mawazo yako chief, unafikiri nani anapaswa kuwajibika kwa sakala hili la ESCROW?

Mwanasheria mkuu wa serikali kwa kuzipotosha idara na wizara zote zilizohusika kwenye huu mchakato. Ikumbukwe kuwa mwanasheria mkuu wa serikali ndio mwenye sauti kuhusiana na masuala ya kisheria ya serikali ikiwemo mikataba.
 
utaonaje wakati wewe ni kipofu wa akili

Teh teh teh huwa nacheka sana ninapokutana na michango ya watu kama wewe mnaojifanya mna akili kuliko watu wengine.
 
Nyie akina M acheni mzee wetu Muhongo ni nn jaman kwan Kikwete hamjui?mmeshupaa kama wanya mbeya?
 
Ewe Mungu baba yetu wa Mbinguni, tupe maarifa na hekima ya utambuzi, wenye elimu na wasio nayo maana hakika watu wako Tanzania tunaangamia kwa kukosa maarifa. Ni binadamu asiye na maarifa ama anayejitoa ufahamu anayeweza kusema muhongo na jk wanajenga uchumi. Watanzania tumeshauzwa marekani, China na kwingineko duniani. Kwa sasa deni la taifa ni karibu trilioni 40 wakati jk anaingia Ikulu lilikuwa chini ya trilioni 10. Hadi mifuko ya jamii (akiba ya wafanyakazi) zaidi ya trilioni 8 imekopwa. Msifahamu mambo mazito ya nchi hii tulieni haya mambo yanauma sana. Anayetetea vitalu vya gesi hana tofauti na aliyetetea uwekezaji katika sekta ya madini miaka 10 iliyopita. Sekta ya madini tayari ni laana kwa taifa letu na NDIVYO itakavyokuwa sibirini myaone. Vinginevyo tuungane kumlilia Mungu afute laana na viongozi laana katika nchi akiwemo prof muongo.
 
kijijini kwangu nimepata umeme kwa elfu 30, nimchukie muhongo kwa lipi? tanesco wana ceo wao nabodi yao kamahawana mikakati yakibiashara muhongo afanyeje sasa.
 
kasababisha hasara yaani kafanikisha wizi badala ya kulinda mali ye ndo anasababisha ziibwe

watu wengine washenzi kweli, fedha za iptl zilikuwa bot sasa muhogo kahusikaje? muulizeni mwigulu na gavana wa bot ziliko pesa.
 
g sam hata mimi ninamtetea na nitamtetea kwa nguvu zote profesa kwa sababu natambua wazi kuwa ninyi mnaompiga vita ni kundi moja na mnao ufadhili wa mtu ambaye aliambiwa ukweli kuhusu umiliki wa visima vya gesi na mafuta...Profesa hana hatia na hawezi kubebeshwa lawama za kisiasa . Kumbuka yeye hakuwahi kugombea wala kuomba nafsi ya kisiasa bali ameombwa asaidie wizara ile hasa wakati huu tunagundua gesi na mafuta...sasa kwa kuwa ninyi mnayo ajenda ya ubinafsi zadi ndio maana mnafanya juhudi zote ili aondolewe...Kwa nini msiache mamlaka yake ya uteuzi ifanye uamuzi sahihi..wewe na wenzako mnachopaswa kufanya ni kumpinga kwa nguvu zote humu mitandaoni na sisi tutamtetea kwa nguvu zote lakini mwisho wa siku mwenye mamlaka ndiye ataamua bila shinikizo
Mods naomba huu uzi msiuhamishe, msiuchanganye na mwingine. Acha tuujadili ukweli!

Kumekuwa na jitihada za makusudi za kumtetea waziri wa nishati na madini Prof. Sospeter Muhongo eti kwa kuwa ni mtendaji bora basi asiwajibishwe kutokana na wizi wa mali ya umma. Huu ni ukosefu wa maarifa na kutokutumia akili kuliko kithiri!

Kwanza kabisa Muhongo Sospeter siyo mtendaji mzuri.

Pili ni mtu wa kujiamulia mambo bila kufuata taratibu na sheria kitu ambacho kimeligharimu taifa kwa kiasi kikubwa!

Je, mnaomtetea Muhongo mna habari kuwa ndiye aliyechangia 13% ya deni la taifa tunaloliona sasa?

Je mnajua kuwa Prof. Muhongo aliwajibishwa na kamati ya maadili ya bunge kwa kuwa aliituhumu POAC iliyokuwa ikiongozwa naZitto Kabwe kabla ya kuvunjwa ambapo alisema kuwa POAC imepewa hongo na Reginald Mengi ili iikwamishe bajeti ya wizara yake kwa mwaka
2014/15?

Baadaye Prof. Muhongo alijieleza mbele ya spika Makinda na kamati ya maadili ya bunge ambapo alikiri mwenyewe kuwa alifanya hivyo ili bajeti ya wizara yake ipite kirahisi eti kwamba hakuitaji usumbufu kutoka kwa aliowaita kuwa wajuaji na hakukuwa na tuhuma zozote za Zitto na kamati yake kupewa rushwa na Reginald Mengi. Makinda akajilaumu sana kwa kuivunja kamati ya Zitto! Muhongo akasamehewa yakafanywa siri, yakapita!

Kama hamjui basi nawaeleza kuwa Prof. Muhongo amekuwa akituhumiwa mara kwa mara ndani ya kikao cha baraza la mawaziri kuwa ni mtu anayelitia hasara taifa kutokana na maamuzi yake ya hovyo na kutokufuata sheria na taratibu za mikataba na manunizi ya umma.

Hafuati sheria za manunuzi ya umma, ni mtu asiyepokea ushauri na amekuwa akilazimisha serikali nzima kusahau mambo mengine kwa ajili ya wizara yake!

Prof. Muhongo amekuwa akitoa takwimu za uongo kwa makusudi mbele ya bunge..Mathalan deni la Tanesco limekuwa likizidi mara mbili kila mwaka na sasa Tanesco
inadaiwa bilioni 100 za Kitanzania ambapo yeye aliingia wizarani Tanesco ikiwa na deni la bilioni 10 pekee hilo analifanya kuwa siri na kutoa takwimu za uongo eti fedha za ESCROW zilibadilishwa kuwa deni la Tanesco kwa IPTL! Utendaji wa huyu mtu uko wapi?

IPTL imekuwa ikizidishiwa malipo kila siku tangu aingie madarakani hilo kaamua kulifumbia macho kwa makusudi kwa kuwa tayari alishakiuka taratibu za mauzo ya IPTL kwa PAP!

Wapo wanaosema kuwa amefanikisha kupeleka umeme vijijini kupitia REA, fine. Je wanajua ni kiasi gani Prof. Muhongo ameidanganya serikali kwa takwimu za uongo na kupikwa ili serikali ihamishie rasilimali zake nyingi REA? REA imepewa kiasi kikubwa sana cha fedha kuliko ambavyo inazalisha! Hilo wanalifahamu?

Ukweli ni kuwa Muhongo amekuwa akitoa taarifa za uongo kwa serikali ili kufanikisha mpango wake wa kuchota fedha, ametoa takwimu na taarifa za uongo bungeni toka alipoteuliwa kuwa waziri! Spika wa bunge kila bunge la bajeti linapoisha amekuwa akimpeleka Prof. Muhongo mbele ya kamati ya maadili ya bunge kutokana na taarifa za uongo ila hilo limekuwa likifanywa siri!
 
Ni wapumbavu pekee hasa watanzania kama nyie ambao wako radhi mtu wa nje aje aibe rasimali apeleke kwao kuliko mtanzania mwenzake apate,hats kama ana vigezo vyote.Roho yako mbaya inakuuwa bila kujijua.

wewe ndo mpumbavu namba moja. nenda bonite uone wahindi walivyojazana kwa mengi wachimbaji wadogo wanakosa maeneo yote kajimilikisha mengi. hebu muulizeni ippmining imefia wapi? kama hawezi kuchimba arudishe leseni zetu.
 
Ewe Mungu baba yetu wa Mbinguni, tupe maarifa na hekima ya utambuzi, wenye elimu na wasio nayo maana hakika watu wako Tanzania tunaangamia kwa kukosa maarifa. Ni binadamu asiye na maarifa ama anayejitoa ufahamu anayeweza kusema muhongo na jk wanajenga uchumi. Watanzania tumeshauzwa marekani, China na kwingineko duniani. Kwa sasa deni la taifa ni karibu trilioni 40 wakati jk anaingia Ikulu lilikuwa chini ya trilioni 10. Hadi mifuko ya jamii (akiba ya wafanyakazi) zaidi ya trilioni 8 imekopwa. Msifahamu mambo mazito ya nchi hii tulieni haya mambo yanauma sana. Anayetetea vitalu vya gesi hana tofauti na aliyetetea uwekezaji katika sekta ya madini miaka 10 iliyopita. Sekta ya madini tayari ni laana kwa taifa letu na NDIVYO itakavyokuwa sibirini myaone. Vinginevyo tuungane kumlilia Mungu afute laana na viongozi laana katika nchi akiwemo prof muongo.

haya maneno peleka himo kwenye mbege
 
wewe ndo mpumbavu namba moja. nenda bonite uone wahindi walivyojazana kwa mengi wachimbaji wadogo wanakosa maeneo yote kajimilikisha mengi. hebu muulizeni ippmining imefia wapi? kama hawezi kuchimba arudishe leseni zetu.

Wewe ni mpumbavu na mjinga kuliko wote,kwa hiyo bora apate mtu wa nje achime akajenge uchumi wao kuliko mtanzania,kweli.mpumbavu hata umuweke kwenye kinu umtwange ili upumbavu umuishe ukimtoa bado ataendelea kuwa na upumbavu wake.Kamwambie bwana wenu Muongo kuwa udalali umemponza hafai hata kuongoza kuku atadalalia woote.
 
Huyu Muhongo mbona ana wafuasi wengi hivi?kwa nini? Au ndio watu wa wizarani?
Hii wizara ina mamluki kweli. Mnakumbuka walivyosukuma gari ya katibu wao yule mwizi na wakamfanyia sherehe?dadeki

1.kama ameweza kusema kodi ya bilion 21 kwenye Akaunti ya Tegeta ESCROW sio hela ya umma sijui huko kwenye mikataba ya gesi na madini kasamehe bilion ngapi? 2. Watanzania tuna uwezo wa kuwekeza kwenye juice ila sio gesi wakati huo 70% ya hisa za IPTL zinauzwa kwa milion 6 tu,kwa bei hiyo hata mm ningeweza kumiliki mitambo ya IPTL.
 
Wewe ni mpumbavu na mjinga kuliko wote,kwa hiyo bora apate mtu wa nje achime akajenge uchumi wao kuliko mtanzania,kweli.mpumbavu hata umuweke kwenye kinu umtwange ili upumbavu umuishe ukimtoa bado ataendelea kuwa na upumbavu wake.Kamwambie bwana wenu Muongo kuwa udalali umemponza hafai hata kuongoza kuku atadalalia woote.

usituletee porojo za kipumbavu hapa, fomu za kuomba vitalu zipo tpdc akajaze afanyiwe rating kama anasifa apewe kama hana akanunue hisa swala. maswala ya escow kamuulizeni gavana, yeye ndo anajua miamala yote iliendaje.
 
1.kama ameweza kusema kodi ya bilion 21 kwenye Akaunti ya Tegeta ESCROW sio hela ya umma sijui huko kwenye mikataba ya gesi na madini kasamehe bilion ngapi? 2. Watanzania tuna uwezo wa kuwekeza kwenye juice ila sio gesi wakati huo 70% ya hisa za IPTL zinauzwa kwa milion 6 tu,kwa bei hiyo hata mm ningeweza kumiliki mitambo ya IPTL.

wewe ndo kituko kweli, kwa hiyo brela sikuhizi iko chini ya muhongo! tra wako chini ya muhongo! leta hoja zenye mashiko.
 
1.kama ameweza kusema kodi ya bilion 21 kwenye Akaunti ya Tegeta ESCROW sio hela ya umma sijui huko kwenye mikataba ya gesi na madini kasamehe bilion ngapi? 2. Watanzania tuna uwezo wa kuwekeza kwenye juice ila sio gesi wakati huo 70% ya hisa za IPTL zinauzwa kwa milion 6 tu,kwa bei hiyo hata mm ningeweza kumiliki mitambo ya IPTL.

Million sita ndio bei yake halisi kwa mujibu wa capital yake.
Iptl ina assets ya mitambo ya kufulia umeme na assets nyengine zisizodi $120m.Lakini madeni ya bank ni zaidi ya million 400$
Na mapato ya mashaka kutokana na mashaka ya uzalishaji na ugomvi na Tanesco. Hivyo kwa melchar hawakuwa na maslahi tena na mitambo ile.
Na huwezi kumpangia mtu bei ni uamuzi wake.
 
Jibu hoja sio kusema kichwa kimejaa matope. Hapo hujajibu hoja kichwa chako kinakuwaje tofauti na mtoa hoja kama unavyomtuhumu wewe?
we hujui kitu kichwa chako kimejaa matope hata tukueleze nini hutaweza kufahamu
 
usituletee porojo za kipumbavu hapa, fomu za kuomba vitalu zipo tpdc akajaze afanyiwe rating kama anasifa apewe kama hana akanunue hisa swala. maswala ya escow kamuulizeni gavana, yeye ndo anajua miamala yote iliendaje.

Povu linakutoka kwa kutetea upumbavu wako unatumwa tu na bwana wako na wewe bila kufikiri kwa kuwa unaongozwa na upumbavu kichwani mwakp unatuletea upuuzi wako humi.Nenda kamwambie bwana wako aliyekutuma umtetee humu kuwa kazi aliyokupa ni ngumu akupe nyingine kulingana na upuuzi wako.
 
1.kama ameweza kusema kodi ya bilion 21 kwenye Akaunti ya Tegeta ESCROW sio hela ya umma sijui huko kwenye mikataba ya gesi na madini kasamehe bilion ngapi? 2. Watanzania tuna uwezo wa kuwekeza kwenye juice ila sio gesi wakati huo 70% ya hisa za IPTL zinauzwa kwa milion 6 tu,kwa bei hiyo hata mm ningeweza kumiliki mitambo ya IPTL.

Halafu kuna wapumbavu kama wakina Eddy na wenzake wanatetea upuuzi,kweli wajinga nchi hii wako wengi kuliko inavyodhaniwa mkuu.
 
Kwani hata Kagasheki si alikua mtu safi na mtendaji mzuri sana pale wizara ya maliasili na utalii na hakufanya kosa lolote lakini ilibidi a step down kwa makosa ya watendaji wengine. Wala hakushika bunduki wakati wa oparesheni tokomeza lakini kiongozi sifa yake kubwa ni kuhakikisha idara au wizara yake iko vizuri katika kutimiza wajibu wake. Muhongo si mbaya na inawezekana alikua na nina nzuri tu katika hili lakini kwa sababu wananchi wamekosa imani na wizara yake hana budi kuachia ngazi japo ana sifa zote. tusiwe na na double standard kwenye kuwajibishana

Tusipende KUAMINISHA UMMA KWAMBA KILA ANAYEMTETEA MUHONGO N MWANA C C M.KWA MTU YEYOTE MWENYE UTIMAMAU WA AKILI ATAKUBALIANA NA UKWELI KUWA KWENYE BARAZA LA MAWAZIRI,HAKUNA WAZIRI MCHAPA KAZI NA MWENYE AKILI KAMA MUHONGO.NI WAJINGA KWA WATU KUKUBALI KUSHKWA MASHKIO NA MENGI.
 
Back
Top Bottom