Wanaomtetea Prof. Muhongo Sospeter 'Wanaangamia kwa kukosa maarifa'

Wanaomtetea Prof. Muhongo Sospeter 'Wanaangamia kwa kukosa maarifa'

Mods naomba huu uzi msiuhamishe, msiuchanganye na mwingine. Acha tuujadili ukweli!

Kumekuwa na jitihada za makusudi za kumtetea waziri wa nishati na madini Prof. Sospeter Muhongo eti kwa kuwa ni mtendaji bora basi asiwajibishwe kutokana na wizi wa mali ya umma. Huu ni ukosefu wa maarifa na kutokutumia akili kuliko kithiri!

Kwanza kabisa Muhongo Sospeter siyo mtendaji mzuri.

Pili ni mtu wa kujiamulia mambo bila kufuata taratibu na sheria kitu ambacho kimeligharimu taifa kwa kiasi kikubwa!

Je, mnaomtetea Muhongo mna habari kuwa ndiye aliyechangia 13% ya deni la taifa tunaloliona sasa?

Je mnajua kuwa Prof. Muhongo aliwajibishwa na kamati ya maadili ya bunge kwa kuwa aliituhumu POAC iliyokuwa ikiongozwa naZitto Kabwe kabla ya kuvunjwa ambapo alisema kuwa POAC imepewa hongo na Reginald Mengi ili iikwamishe bajeti ya wizara yake kwa mwaka
2014/15?

Baadaye Prof. Muhongo alijieleza mbele ya spika Makinda na kamati ya maadili ya bunge ambapo alikiri mwenyewe kuwa alifanya hivyo ili bajeti ya wizara yake ipite kirahisi eti kwamba hakuitaji usumbufu kutoka kwa aliowaita kuwa wajuaji na hakukuwa na tuhuma zozote za Zitto na kamati yake kupewa rushwa na Reginald Mengi. Makinda akajilaumu sana kwa kuivunja kamati ya Zitto! Muhongo akasamehewa yakafanywa siri, yakapita!

Kama hamjui basi nawaeleza kuwa Prof. Muhongo amekuwa akituhumiwa mara kwa mara ndani ya kikao cha baraza la mawaziri kuwa ni mtu anayelitia hasara taifa kutokana na maamuzi yake ya hovyo na kutokufuata sheria na taratibu za mikataba na manunizi ya umma.

Hafuati sheria za manunuzi ya umma, ni mtu asiyepokea ushauri na amekuwa akilazimisha serikali nzima kusahau mambo mengine kwa ajili ya wizara yake!

Prof. Muhongo amekuwa akitoa takwimu za uongo kwa makusudi mbele ya bunge..Mathalan deni la Tanesco limekuwa likizidi mara mbili kila mwaka na sasa Tanesco
inadaiwa bilioni 100 za Kitanzania ambapo yeye aliingia wizarani Tanesco ikiwa na deni la bilioni 10 pekee hilo analifanya kuwa siri na kutoa takwimu za uongo eti fedha za ESCROW zilibadilishwa kuwa deni la Tanesco kwa IPTL! Utendaji wa huyu mtu uko wapi?

IPTL imekuwa ikizidishiwa malipo kila siku tangu aingie madarakani hilo kaamua kulifumbia macho kwa makusudi kwa kuwa tayari alishakiuka taratibu za mauzo ya IPTL kwa PAP!

Wapo wanaosema kuwa amefanikisha kupeleka umeme vijijini kupitia REA, fine. Je wanajua ni kiasi gani Prof. Muhongo ameidanganya serikali kwa takwimu za uongo na kupikwa ili serikali ihamishie rasilimali zake nyingi REA? REA imepewa kiasi kikubwa sana cha fedha kuliko ambavyo inazalisha! Hilo wanalifahamu?

Ukweli ni kuwa Muhongo amekuwa akitoa taarifa za uongo kwa serikali ili kufanikisha mpango wake wa kuchota fedha, ametoa takwimu na taarifa za uongo bungeni toka alipoteuliwa kuwa waziri! Spika wa bunge kila bunge la bajeti linapoisha amekuwa akimpeleka Prof. Muhongo mbele ya kamati ya maadili ya bunge kutokana na taarifa za uongo ila hilo limekuwa likifanywa siri!

Nakubaliana na wewe 100%, profesa muongo kuliko maprofesa wote duniani hata ripoti yake ya utetezi bungeni ilijaa uongo, uongo mkubwa ni yale aliyoyasema kuhusu Bw. Gwilina aliyekuwa mwanasheria wa Tanesco aliyekwenda Malaysia kufanya "Due diligence" ya Mechmar, wengi wetu hapa wanaangalia uzuri wa cover ya kitabu sio content yake na hawataki kusoma katikati ya mistari, na hawataki kifikiri nje ya kisanduku, most are mesmerised by the professors lengthy an confusing CV! Muhongo ni muongo A & O, hafai kusimamia ofisi ya umma, aondoke akafungue wizara binafsi ya miamba awe waziri wa maisha. The pitiable profesa of rocks nd other inanimate objects is a pathological lier, Aondoke period
 
Povu linakutoka kwa kutetea upumbavu wako unatumwa tu na bwana wako na wewe bila kufikiri kwa kuwa unaongozwa na upumbavu kichwani mwakp unatuletea upuuzi wako humi.Nenda kamwambie bwana wako aliyekutuma umtetee humu kuwa kazi aliyokupa ni ngumu akupe nyingine kulingana na upuuzi wako.

wewe ndo unayelipwaa kuchafua watu wapige hela wengine mpakazie wengine. leta fact sio maneno ya kwenye mbege.
 
Halafu kuna wapumbavu kama wakina Eddy na wenzake wanatetea upuuzi,kweli wajinga nchi hii wako wengi kuliko inavyodhaniwa mkuu.

upuuzi mnauleta nyie mnaolipwa kwa kazi ya kipumbavu na washenzi wenu.
 
Halafu kuna wapumbavu kama wakina Eddy na wenzake wanatetea upuuzi,kweli wajinga nchi hii wako wengi kuliko inavyodhaniwa mkuu.

waambieni mabwana zenu wamguse gavana waone watakavyoaibika.
 
Nakubaliana na wewe 100%, profesa muongo kuliko maprofesa wote duniani hata ripoti yake ya utetezi bungeni ilijaa uongo, uongo mkubwa ni yale aliyoyasema kuhusu Bw. Gwilina aliyekuwa mwanasheria wa Tanesco aliyekwenda Malaysia kufanya "Due diligence" ya Mechmar, wengi wetu hapa wanaangalia uzuri wa cover ya kitabu sio content yake na hawataki kusoma katikati ya mistari, na hawataki kifikiri nje ya kisanduku, most are mesmerised by the professors lengthy an confusing CV! Muhongo ni muongo A & O, hafai kusimamia ofisi ya umma, aondoke akafungue wizara binafsi ya miamba awe waziri wa maisha. The pitiable profesa of rocks nd other inanimate objects is a pathological lier, Aondoke period

Mkuu leo hii hakina asiyejua Prof Muhongo ni Prof wa Uongo duniani yaani wasiejua hilo ni wale wanaolipwa humu jukwaani kwa kumtetea
 
upuuzi mnauleta nyie mnaolipwa kwa kazi ya kipumbavu na washenzi wenu.

Dunia nzima inajua bwana wenu Prof Muhongo ni Prof wa Uongo kupindukia ambaye hajawahi kutokea duniani kabla.
 
Tusipende KUAMINISHA UMMA KWAMBA KILA ANAYEMTETEA MUHONGO N MWANA C C M.KWA MTU YEYOTE MWENYE UTIMAMAU WA AKILI ATAKUBALIANA NA UKWELI KUWA KWENYE BARAZA LA MAWAZIRI,HAKUNA WAZIRI MCHAPA KAZI NA MWENYE AKILI KAMA MUHONGO.NI WAJINGA KWA WATU KUKUBALI KUSHKWA MASHKIO NA MENGI.

Wewe ni mmoja wa watanzania wajinga kabisa. Hivi unatumia vigezo gani kupima utendaji wa Muhongo. Mbona hakuna mabadiliko chanya pale wizara ya nishati na madini?
Hivi ukimuweka kwenye mizania huyu Muongo na Dr Pombe nani atakuwa na weight kubwaa. Kama wampenda sana mpe tiGo yako basi. Lakini huyu hana cha kujivunia ktk utendaji wa wizara hiyo. Sana sana amekuwa middleman wa akina Singa Singa huku akiplot dili kubwa kubwa za mabilioni kutoka kwa wawekezaji wa nje kwa maslahi yake. Bado kuna scandal la bomba la gas hapo ndipo utakapomuona Muhongo katika muktadha wake halisi.
 
Huyu Muhongo kama hataki kujiuzulu dawa ni kumtafutia basha, atajiuzulu mbona bila kupenda...
 
Haishauriwi kumchinja kuku anayetaga

huenda ni kweli siyo vizuri kumchinjia mgeni kuku anayetaga lakini kuku huyo akiwa na ugonjwa usiopona unamwacha afe,Prof wenu anaugonjwa usiopona.
 
Kitendo cha mada yako kumtaja REGINALD MENGI najiondoa kwa sababu hata sakata la ESCROW MENGI anahusika sana tu.
 
huenda ni kweli siyo vizuri kumchinjia mgeni kuku anayetaga lakini kuku huyo akiwa na ugonjwa usiopona unamwacha afe,Prof wenu anaugonjwa usiopona.
Ugonjwa wa kusingiziwa siyo ugonjwa.
 
Wewe mitu ya Kilimanjaro unatuchosha. REGINALD MENGI anawalipa shilingi ngapi kumchafua MUHONGO?
 
Wewe ni mmoja wa watanzania wajinga kabisa. Hivi unatumia vigezo gani kupima utendaji wa Muhongo. Mbona hakuna mabadiliko chanya pale wizara ya nishati na madini?
Hivi ukimuweka kwenye mizania huyu Muongo na Dr Pombe nani atakuwa na weight kubwaa. Kama wampenda sana mpe tiGo yako basi. Lakini huyu hana cha kujivunia ktk utendaji wa wizara hiyo. Sana sana amekuwa middleman wa akina Singa Singa huku akiplot dili kubwa kubwa za mabilioni kutoka kwa wawekezaji wa nje kwa maslahi yake. Bado kuna scandal la bomba la gas hapo ndipo utakapomuona Muhongo katika muktadha wake halisi.
Mabadiliko hayaonekani wizarani bali kwa wananchi, tangu tupate uhuru mwaka huu ndiyo nimeona umeme kwenye vijiji vya kwetu. Hayo ndiyo mabadiliko yenyewe tunayoyataka wananchi.
 
upuuzi mnauleta nyie mnaolipwa kwa kazi ya kipumbavu na washenzi wenu.
Ila sidhani wataweza kumshawishi JK amfukuze kazi huyu mzee ambaye kiukweli ameonekana kuleta mageuzi makubwa ndani ya Wizara ya Nishati na Madini
 
Hawana mpya hawa Profesa Muhongo ni jembe. hata mfanyaje hamna hoja za msingi dhidi ya Muhongo ni bla bla bla tu! Muhongo oyeee! kule kigoma tunasema Muhongo ni mwisho wa rubishi ya batoto. Sabato Masalia tunaendesha maombi maaulumu kwakeb Mungu ibariki prof. Muhongo Mungu ibariki Tanzania.
 
Dunia nzima inajua bwana wenu Prof Muhongo ni Prof wa Uongo kupindukia ambaye hajawahi kutokea duniani kabla.
Dunia nzima inajua Prof. Anasingiziwa kutokana na misimamo yake ndani ya Wizara yake, watu walizoea vya mteremko
 
mfalme juha jamani someni vitabu watu kama muhongo wako wengi tz
 
Hawana mpya hawa Profesa Muhongo ni jembe. hata mfanyaje hamna hoja za msingi dhidi ya Muhongo ni bla bla bla tu! Muhongo oyeee! kule kigoma tunasema Muhongo ni mwisho wa rubishi ya batoto. Sabato Masalia tunaendesha maombi maaulumu kwakeb Mungu ibariki prof. Muhongo Mungu ibariki Tanzania.

hawa jamaa zitto kawapiga chenga ya mwili kesi za ag bot na brela kawasakizia kwa muhongo majuha yanashupaa tu. anawadanganya wataifishe mitambo ili mzee wa kofia ya mreli apate dili jingine.
 
Back
Top Bottom