Wanaomtetea Prof. Muhongo Sospeter 'Wanaangamia kwa kukosa maarifa'

Wanaomtetea Prof. Muhongo Sospeter 'Wanaangamia kwa kukosa maarifa'

Namsupport Mhongo 100% Zitto na Mkono wajipange upya movie ya pili hii inakosa mashabiki.
 
kwani ndie aliewatuma wagawane pesa zetu? ukifuatilia hizo za huyo singasinga ni wakina nani walichukua utakuta na wakina Muhongo wamo, tusubir maamuzi ya jk ila hili swala ni mtego sana kwa chama
 
Dunia nzima inajua Prof. Anasingiziwa kutokana na misimamo yake ndani ya Wizara yake, watu walizoea vya mteremko

Dunia nzima especial tanzania inajua Prof Muhongo ni Ptof Muongo kuliko wote katika dunia hii,rejea kauli yake aliyoitoa bungeni wakati wa bajeti "kuna wabunge wamelipwa na Dr Mengi ili wakwamishe bejeti ya wizara yangu" alipoitwa kwenye kamati ya Ngwilizi alimaanisha nini akajitetea kwamba sio kweli kuwa kuna wabunge walihongwa ila alisema ili bajeti yake ipite bila kikwazo.Huyu ni waziri wa hovyo na muongo kutokea katika Taifa linaloitwa Tanganyika toka haijapata uhuru.
 
Kumbe kina Asumpta Mshamu wako wengi hata JF nilidhani watu wa aina tunawakuta kule ambako sifa ya kuwa huko ni kujua kusoma na kuandika wakati dreva wako anapashwa kuwa amemaliza darasa la kumi na mbili.
Kweli inahitaji moyo kumetetea Prof anayewadhihaki nakuwadharau waajiri wake.
 
Kabla ya kuendelea kumjadili Muongo je huyu jamaa ametahiriwa kweli? anayofanya na anayoendelea kufanya ni utoto kabisa!
 
Sikuomba UWAZIRI,Nilibembelezwa kuwa WAZIRI-Hata Leo nikiacha Narudi PRETORIA kuna KAZI YANGU Inaeleweka-PROF MUONGO!
 
kasababisha hasara yaani kafanikisha wizi badala ya kulinda mali ye ndo anasababisha ziibwe

Endeleeni kuyageuzageuza tu lakini ukweli ni kwamba mnaendeleza kampeni dhidi ya watu wazuri.
 
Mods naomba huu uzi msiuhamishe, msiuchanganye na mwingine. Acha tuujadili ukweli!

Kumekuwa na jitihada za makusudi za kumtetea waziri wa nishati na madini Prof. Sospeter Muhongo eti kwa kuwa ni mtendaji bora basi asiwajibishwe kutokana na wizi wa mali ya umma. Huu ni ukosefu wa maarifa na kutokutumia akili kuliko kithiri!

Kwanza kabisa Muhongo Sospeter siyo mtendaji mzuri.

Pili ni mtu wa kujiamulia mambo bila kufuata taratibu na sheria kitu ambacho kimeligharimu taifa kwa kiasi kikubwa!

Je, mnaomtetea Muhongo mna habari kuwa ndiye aliyechangia 13% ya deni la taifa tunaloliona sasa?

Je mnajua kuwa Prof. Muhongo aliwajibishwa na kamati ya maadili ya bunge kwa kuwa aliituhumu POAC iliyokuwa ikiongozwa naZitto Kabwe kabla ya kuvunjwa ambapo alisema kuwa POAC imepewa hongo na Reginald Mengi ili iikwamishe bajeti ya wizara yake kwa mwaka
2014/15?

Baadaye Prof. Muhongo alijieleza mbele ya spika Makinda na kamati ya maadili ya bunge ambapo alikiri mwenyewe kuwa alifanya hivyo ili bajeti ya wizara yake ipite kirahisi eti kwamba hakuitaji usumbufu kutoka kwa aliowaita kuwa wajuaji na hakukuwa na tuhuma zozote za Zitto na kamati yake kupewa rushwa na Reginald Mengi. Makinda akajilaumu sana kwa kuivunja kamati ya Zitto! Muhongo akasamehewa yakafanywa siri, yakapita!

Kama hamjui basi nawaeleza kuwa Prof. Muhongo amekuwa akituhumiwa mara kwa mara ndani ya kikao cha baraza la mawaziri kuwa ni mtu anayelitia hasara taifa kutokana na maamuzi yake ya hovyo na kutokufuata sheria na taratibu za mikataba na manunizi ya umma.


Hafuati sheria za manunuzi ya umma, ni mtu asiyepokea ushauri na amekuwa akilazimisha serikali nzima kusahau mambo mengine kwa ajili ya wizara yake!

Prof. Muhongo amekuwa akitoa takwimu za uongo kwa makusudi mbele ya bunge..Mathalan deni la Tanesco limekuwa likizidi mara mbili kila mwaka na sasa Tanesco
inadaiwa bilioni 100 za Kitanzania ambapo yeye aliingia wizarani Tanesco ikiwa na deni la bilioni 10 pekee hilo analifanya kuwa siri na kutoa takwimu za uongo eti fedha za ESCROW zilibadilishwa kuwa deni la Tanesco kwa IPTL! Utendaji wa huyu mtu uko wapi?

IPTL imekuwa ikizidishiwa malipo kila siku tangu aingie madarakani hilo kaamua kulifumbia macho kwa makusudi kwa kuwa tayari alishakiuka taratibu za mauzo ya IPTL kwa PAP!

Wapo wanaosema kuwa amefanikisha kupeleka umeme vijijini kupitia REA, fine. Je wanajua ni kiasi gani Prof. Muhongo ameidanganya serikali kwa takwimu za uongo na kupikwa ili serikali ihamishie rasilimali zake nyingi REA? REA imepewa kiasi kikubwa sana cha fedha kuliko ambavyo inazalisha! Hilo wanalifahamu?

Ukweli ni kuwa Muhongo amekuwa akitoa taarifa za uongo kwa serikali ili kufanikisha mpango wake wa kuchota fedha, ametoa takwimu na taarifa za uongo bungeni toka alipoteuliwa kuwa waziri! Spika wa bunge kila bunge la bajeti linapoisha amekuwa akimpeleka Prof. Muhongo mbele ya kamati ya maadili ya bunge kutokana na taarifa za uongo ila hilo limekuwa likifanywa siri!

Hizi hoja zako zinafanana na za yule mfadhili wa vikoba na sasa kaingia mitini kwa sababu fedha zake zimeelekezwa kumpiga vita muhongo .
 
Back
Top Bottom