Wanaomtetea Prof. Muhongo Sospeter 'Wanaangamia kwa kukosa maarifa'

Wanaomtetea Prof. Muhongo Sospeter 'Wanaangamia kwa kukosa maarifa'

Majenereta yamedoda na yataozea stooni,wafanyabiashara wamekosa vitalu vya gesi,kampuni ya mkono and advocates imekatiwa mirija,Lowasa ameahidi vyeo kwa wajumbe wa PAC,mahela ya mengi kumbuka kumzomea tu prof 3mil,ukichangia na kushinikiza atoke mil 20,mkono kuwakodishia ndege Zitto na wenzake kwenda kwenye harus ya kafulila,Zitto kupewa bil 1.5 na kupewa jukumu la kutafuta wabunge wenye ushawishi kushinikiza prof na katibu wake waondoke,

Tatizo letu watanzania njaa zinatusumbua tunadanganyika na vitu vidogo vidogo tu, leo hii ukiniambia majenereta yataozea stoo ni kama tunajidanganya kwani mgao ni kama unaendelea. kanga ,fulana na kofia ndiyo zinavyofanya watu wampigie debe. Profesa amemwaga hele sana mpaka kwenye vyombo vya habari watu wamtetee.
 
Watakomaje Fununua waone tabia za ndani za Mjiolojia ukichanganya na katabia ka wasu yego waika atiki!!!Ndolelalaa Ndolelalaaa Mamaa Ndolelelaa Chaseleleka !!!!Bamulaemweee Nchimbusi chamala Ubutaghaa Mwitaleee ....
 
Kumtetea huyu Professor ni pathetic. Labda kama ni wale wanaotoka kwenye familia yake maana yeye ni breadwinner.

Kila mtu anayekuja hapa ana hoja ya utendaji wake. Najiuliza upi? Hakuna mwenye majibu. Hebu tuvute matukio machache yanayomhusu:
(1) Alipoingia kwa mara ya kwanza kama waziri alitutangazia mgawo sasa hautakuwepo. Kauli hii ilimtoka tu bila hata kufanya utafiti kwa nini kunatokea mgawo. As a result Muhongo amelazimisha kutimiza kauli hii kwa gharama kubwa sana. Ikiwa na pamoja na kuilazimisha Tanesco kuingia hasara kubwa ya mafuta ya mitambo ili kuzalisha umeme hata kama ni wa gharama kubwa. Kuongezeka kwa hasara ya tanesco zaidi ya mara 4 kwa kipindi chake kunatokana na hili.
(2) alituambia kuwa umeme hautapanda bei ili kumuumiza mwananchi. Wakati anaingia TZS 10,000 ilikuwa inanunua units 25 sasa fedha hiyo hiyo unapata units 8.7 mara tatu chini zaidi. Utendaji uko wapi?
 
mwizi huyooooooooo
dalali huyooooooooooo
atokeeeeee atokeeeeeeeee hatumtaki ng'oooo
 
Mtahangaika sana mwaka huu. Mliuaminisha umma kuwa Prof Muhongo amekwapua fedha za escrow lakini report ya CAG haijaonesha kuwa alilipwa fedha hizo. Watanzania tuweni na tabia ya kusema na kutenda haki.

kasababisha hasara yaani kafanikisha wizi badala ya kulinda mali ye ndo anasababisha ziibwe
 
We chizi endeleeni na fisadi lenu mengi ndiyo mnamuona mungu wenu wakati jizi muhongo ni kiboko ya mafisadi ukiwemo wewe kitasa.
 
kasababisha hasara yaani kafanikisha wizi badala ya kulinda mali ye ndo anasababisha ziibwe
We kidumu unaweza weka bayana hasara gani ambazo kasababisha ukiacha ile ya mengi kunyimwa kitaru cha gesi kwa kutaka apewe bure eti kisa mzawa.
 
Mods naomba huu uzi msiuhamishe, msiuchanganye na mwingine. Acha tuujadili ukweli!

Kumekuwa na jitihada za makusudi za kumtetea waziri wa nishati na madini Prof. Sospeter Muhongo eti kwa kuwa ni mtendaji bora basi asiwajibishwe kutokana na wizi wa mali ya umma. Huu ni ukosefu wa maarifa na kutokutumia akili kuliko kithiri!

Kwanza kabisa Muhongo Sospeter siyo mtendaji mzuri.

Pili ni mtu wa kujiamulia mambo bila kufuata taratibu na sheria kitu ambacho kimeligharimu taifa kwa kiasi kikubwa!

Je, mnaomtetea Muhongo mna habari kuwa ndiye aliyechangia 13% ya deni la taifa tunaloliona sasa?

Je mnajua kuwa Prof. Muhongo aliwajibishwa na kamati ya maadili ya bunge kwa kuwa aliituhumu POAC iliyokuwa ikiongozwa naZitto Kabwe kabla ya kuvunjwa ambapo alisema kuwa POAC imepewa hongo na Reginald Mengi ili iikwamishe bajeti ya wizara yake kwa mwaka
2014/15?

Baadaye Prof. Muhongo alijieleza mbele ya spika Makinda na kamati ya maadili ya bunge ambapo alikiri mwenyewe kuwa alifanya hivyo ili bajeti ya wizara yake ipite kirahisi eti kwamba hakuitaji usumbufu kutoka kwa aliowaita kuwa wajuaji na hakukuwa na tuhuma zozote za Zitto na kamati yake kupewa rushwa na Reginald Mengi. Makinda akajilaumu sana kwa kuivunja kamati ya Zitto! Muhongo akasamehewa yakafanywa siri, yakapita!

Kama hamjui basi nawaeleza kuwa Prof. Muhongo amekuwa akituhumiwa mara kwa mara ndani ya kikao cha baraza la mawaziri kuwa ni mtu anayelitia hasara taifa kutokana na maamuzi yake ya hovyo na kutokifuata sheria na taratibu za mikataba na manunizi ya umma.


Hafuati sheria za manunuzi ya umma, ni mtu asiyepokea ushauri na amekuwa akilazimisha serikali nzima kusahau mambo mengine kwa ajili ya wizara yake!

Prof. Muhongo amekuwa akitoa takwimu za uongo kwa makusudi mbele ya bunge..Marhalan deni la Tanesco limekuwa likizidi mara mbili kila mwaka na sasa Tanesco
inadaiwa bilioni 100 za Kitanzania ambapo yeye aliingia wizarani Tanesco ikiwa na deni la bilioni 10 pekee hilo analifanya kuwa siri na kutoa takwimu za uongo eti fedha za ESCROW zilibadilishwa kuwa deni la Tanesco kwa IPTL! Utendaji wa huyu mtu uko wapi?

IPTL imekuwa ikizidishiwa malipo kila siku tangu aingie madarakani hilo kaamua kulifumbia macho kwa makusudi kwa kuwa tayari alishakiuka taratibu za mauzo ya IPTL kwa PAP!

Wapo wanaosema kuwa amefanikisha kupeleka umeme vijijini kupitia REA, fine. Je wanajua ni kiasi gani Prof. Muhongo ameidanganya serikali kwa takwimu za uongo na kupikwa ili serikali ihamishie rasilimali zake nyingi REA? REA imepewa kiasi kikubwa sana cha fedha kuliko ambavyo inazalisha! Hilo wanalifahamu?

Ukweli ni kuwa Muhongo amekuwa akitoa taarifa za uongo kwa serikali ili kufanikisha mpango wake wa kuchota fedha, ametoa takwimu na taarifa za uongo bungeni toka alipoteuliwa kuwa waziri! Spika wa bunge kila bunge la bajeti linapoisha amekuwa akimpeleka Prof. Muhongo mbele ya kamati ya maadili ya bunge kutokana na taarifa za uongo ila hilo limekuwa likifanywa siri!

Jifanye kama mengi siyo ndugu yako halafu soma hapa vizuri utaelewa kitu lakini undugu wako na mengi ukiuweka mbele hutaelewa somo.

Mh. Rais, Usimuondoe Waziri wa Nishati na Madini kuhudumu katika Wizara husika
Wanabodi niwasalimu nyote habari za jioni,


kwanza kabisa nianze kuwapa pole na shughuri za siku nzima imani yangu tunaafya njema kadri ya mapenzi ya mmwenyezi mungu alivyopendezwa ziwe.


siku chache zilizopita nchi yetu ilikuwa kwenye mjadala mkali kuhusu miamara ya utoaji wa fedha katika A/c ya Tegeta Escrow mjadala ambao uliisha kwa bunge kupendekeza kuchukuliwa kwa hatua mbali mbali kwa wale wote waliohusika kwa namna moja ama nyingine,hii ni pamoja na taasisi mbalimbali ambazo zitaonekana kuhusika katika utoaji wa fedha hizo bila kufuata utaratibu.


Miongoni mwa hatua zilizopendekezwa kuchukuliwa ni pamoja na kuwajibishwa kwa baadhi ya viongozi akiwemo mwanasheria mkuu,waziri wa nishati na madini,waziri nyumba na maendeleo ya makazi pamoja na katibu mkuu wizara ya nishati na madini.


Pamoja na kuwepo kwa viongozi takribani wanne waliopendekezwa kuwajibishwa mimi nitazungumzia waziri wa nishati na madini prf sospeter muhongo kutokana na umhimu wake kwenye wizara ya nishati na madini pamoja na kazi kubwa alizofanya kwenye wizara husika kwa mda mchache ambao ni takribani miaka miwili tu lakini ameweza kufanya mambo makubwa ambayo yako bayana kwa kila mpenda maendeleo.


kwasasa wizara ya nishati na madini chini ya uongozi wa muhongo inafanya uwekezaji mkubwa kila sehemu wenye lengo la kuifanya wizara iweze kujitegemea pasipo kutegemea ruzuku ya serikali,wizara chini ya uongozi wa muhongo sasa inasomeaha watanzania wengi nje ya nchi kwenye taluma za mafuta na gesi kitu amabacho hakijawahi kufanywa na uongozi wowote wa wizara ila muhongo kathubutu,aidha muhongo na jopo lake la uongozi ameipa uhai Tanesco mpaka sasa umeme unakwenda kila kijiji na kupunguza kwa kiasi kikubwa kukatika kwa umeme.


wizara ya nishati na madini chini ya uongozi wa muhongo ipo kwenye uwekezaji mkubwa na plani za mda mrefu ambazo zinapaswa kuungwa mkono na watanzania wote hasa kwenye mradi wa uwekezaji kwenye mafuta na gesi huko mtwara ambao kwa sasa umefika hatua nzuri sana hivyo ni vema waziri muhongo akaendelea kuwepo ili kutimiza ndoto na mipango yake aliyonayo kwenye wizara.


uhusika wa muhongo kwenye kashifa ya EScrow A/C.


Nimefanikiwa kupata tarifa ya CAG sijaona mahala popote muhongo ametajwa kuhusika kwenye hiyo kashifa iwe kwa maneno au kwa vitendo hakuna mahala popote anapotiwa hatiani na ripoti hiyo,kwamantiki hiyo napata shida kuamini mawazo na maoni ya kamati ya PAC ambayo wanadai waliyatoa kwenye ripoti ya CAG mimi nasema hapana ila nahisi siasa imechukua nafasi kubwa zaidi kuliko ukweli na uhalisia wa jambo.


Baada ya kuzungumza na watu wa aina tofautitofauti nimebaini yafuatayo,
waziri wa nishati na madini mh muhongo anachukiwa na baadhi ya watu ambao amewabana wakashindwa kupenyeza mirija yao pale wizarani hasa tanesco na kwenye vitaru vya gesi hapa unamkuta mbunge wa msoma vijijini mh Nimrod mkono na mfanya biashara marufu na mmiliki wa vyombo vya habari kadhaa hapa nchini hawa waliapa kuwa muhongo lazima aondoke kwa namna yoyote ile hapa ndipo nguvu ya pesa nilipoiona kumbe mtu yupo tayari kuacha kulipa watumishi wake kwa miezi miwili ili pesa hiyo iende kumuangusha muhongo nimeshangaa sana.


Lakini pia nimekuta chuki binafsi ndani ya chama cha mapinuzi kwa baadhi ya wabunge kudhani kuwa baraza la mawaziri likibadilishwa wanaweza kuukwaa uwaziri wapo waliofanya jitihada kubwa kuhakikisha kuwa muhongo aondoke kwakuwa nao ni wasomi tena wenye ngazi ya profesa kama muhongo waliamini kabisa akiondoka watapewa wao ikizingatiwa kuwa waliwahi kuwa mawaziri wa hiyo wizara enzi hizi ikiitwa wizara ya maji nishati na madini hapa mtamkuta mzee wetu waziri asiyeshika popote na mbunge wa jimbo mojawapo kule mbeya.


Lakini pia nimekuta msukumo mkubwa wa mashirika kadhaa ya mafuta na gesi yakiwemo simbioni na mengine nao wameshindwa kuchota tena pesa kutoka tanesco kiujanja kama zamani nao walimwaga pesa ya kutosha ili muhongo aondoke kwa namna yoyote ile pesa hizi zilimwagwa kwa wabunge wengi wakiwemo wa chama tawala na upinzani.


kwa upande mwingine nimekuta ugomvi binafsi baina ya mbunge wa simanjiro mh Ole sendeka na Muhongo,kama mtakumbuka muhongo na sendeka wanaugomvi wao binafsi ambao kila mtu anafahamu kuwa sendeke aliwahi kuomba rushwa akiwa kwenye kamati ya kudumu ya bunge ya nishati na madini muhongo akamlipua bungeni ndipo sendeka akaapa kumfanyia kazi muhongo na maswi mpaka waondoke,Lakini walienda mbali zaidi kwa muhongo kutoa cheti cha matokeo ya sendeka aliyokuwa amepata sifuri ndipo ugomvi ulikolea zaidi lakini ugomvi huo mwanzo ulikuwa ni kama utani baina ya watu hao hatukutegemea kuwa sendeka atauingiza mpaka kwenye kuathiri utekelezaji wa mipango ya maendeleo.


chuki kwa muhongo,
Muhongo amechukiwa na baadhi ya watu hasa wafanyabiashara na wanasiasa walioshindwa kupenyeza mambo yao wizarani hasa tanesco na kwenye vitaru vya gesi Lakini pia muhongo anachukiwa na wachache hao kwa kuwa muwazi kitu ambacho watanzania wachache hasa mafisadi hawajazoea kuusikia lakini muhongo alikuwa anausema.


Wito wangu kwa mh Rais na mamlaka ya uteuzi kwa ujumla sisi wazalendo na wapenda maendeleo tunaomba muhongo asiondolewe ili atuondoe kwenye dunia ya tatu kwa kutimiza ndoto zake kwenye miradi kadhaa ya uwekezaji ambayo ameianzisha,


Muhongo ni binadamu hawezi kukosa mapungufu na mazuri pia lakini ukipima mapungufu na mazuri ya muhongo mazuri yake ni mengi kuliko mapungufu kwani mapungufu yake yanavumilika wala hayana madhara katika ujenzi wa jamii mpya kwani hata uongo anaotuhumiwa kuusema bungeni unamadhara gani kwenye maendeleo ya ujenzi wa jamii mpya? Tunamhitaji sana muhongo kwa wakati huu kuliko wakati wowote,mh Rais usimuondoe waziri wa Nishati na Madini tunamhitaji sisi watanzania wapenda maendeleo tusiotoka kwenye familia za kifisadi.
 
Kumtetea huyu Professor ni pathetic. Labda kama ni wale wanaotoka kwenye familia yake maana yeye ni breadwinner.

Kila mtu anayekuja hapa ana hoja ya utendaji wake. Najiuliza upi? Hakuna mwenye majibu. Hebu tuvute matukio machache yanayomhusu:
(1) Alipoingia kwa mara ya kwanza kama waziri alitutangazia mgawo sasa hautakuwepo. Kauli hii ilimtoka tu bila hata kufanya utafiti kwa nini kunatokea mgawo. As a result Muhongo amelazimisha kutimiza kauli hii kwa gharama kubwa sana. Ikiwa na pamoja na kuilazimisha Tanesco kuingia hasara kubwa ya mafuta ya mitambo ili kuzalisha umeme hata kama ni wa gharama kubwa. Kuongezeka kwa hasara ya tanesco zaidi ya mara 4 kwa kipindi chake kunatokana na hili.
(2) alituambia kuwa umeme hautapanda bei ili kumuumiza mwananchi. Wakati anaingia TZS 10,000 ilikuwa inanunua units 25 sasa fedha hiyo hiyo unapata units 8.7 mara tatu chini zaidi. Utendaji uko wapi?

aisee!!!!
 
Tatizo unaongozwa kwa shinikizo la tumbo utaishia kuwatumikia mabwana mafisadi hadi mwisho wako.
Kama mengi angepewa kitaru cha gesi bure kama alivyotaka sasahivi msingekuwa mnaandika haya lakini kwa vile alikosa ndiyo shida yake hii.
 
Kama mengi angepewa kitaru cha gesi bure kama alivyotaka sasahivi msingekuwa mnaandika haya lakini kwa vile alikosa ndiyo shida yake hii.

Ni wapumbavu pekee hasa watanzania kama nyie ambao wako radhi mtu wa nje aje aibe rasimali apeleke kwao kuliko mtanzania mwenzake apate,hats kama ana vigezo vyote.Roho yako mbaya inakuuwa bila kujijua.
 
Huyu Muhongo mbona ana wafuasi wengi hivi?kwa nini? Au ndio watu wa wizarani?
Hii wizara ina mamluki kweli. Mnakumbuka walivyosukuma gari ya katibu wao yule mwizi na wakamfanyia sherehe?dadeki

Hadi Waziri William Mganga Ngeleja naye alisukuma gari la katibu wake
 
We kidumu unaweza weka bayana hasara gani ambazo kasababisha ukiacha ile ya mengi kunyimwa kitaru cha gesi kwa kutaka apewe bure eti kisa mzawa.

we hawara wa muhongo punguza hasira muhongo kuambiwa atole uwaziri sio kwamba atakosa hela ya kukuhonga. visenti anavyo utahongwa tu
 
Muhongo ametulindia gesi yetu isiporwe na majambazi
 
Hii nchi imejaa wajinga na prof Muhongo analijua hilo ndio maana anawageuza wadanganyika kama samaki kwenye kikaango.
Usemi wako umemaliza kila kitu nchi hii tusingekuwa wajinga leo hii tusingekuwa na wakumtete wala wakumhukumu kwani kusingekuwa na furusa ya kuwafanyia watu haya ambayo tunayaona leo
 
Back
Top Bottom