Wanaompuuza Makonda nawashangaa, ipo siku mtamkumbuka

Wanaompuuza Makonda nawashangaa, ipo siku mtamkumbuka

Wakuu salaam,
1. Mnakumbuka zile kelele za watu wengi dhidi ya waziri wa afya kutaka atumbuliwe kwa kudanganya umma kwamba dawa zipo wakati hazipo? Hapa wananchi walitaka hatua ileile ya kumtumbua Anna kilango kwa 'uongo' wake ichukuliwe pia kwa huyu waziri lakini matokeo yake wote tunayajua.

2. Mnakumbuka ishu ya Gambo vs Lema? Tulipiga kelele sana lakini mwisho wa siku tuliona alichokifanya malaika mkuu.

3. Mnakumbuka yale maigizo ya picha ya yule dc wa iringa? Watu walipiga kelele kuhusu yale maigizo lakini malaika mkuu akabariki yale maigizo.

Inshort, Mikelele yenu inamsumbua malaika mkuu na yeye huwa hapendi kelele na kwa vile yeye ni mtu wa visasi kwenye haya makelele dhidi ya Makonda atawakomesha kwa kumpandisha cheo ili mkome kiherehere chenu.
Na wewe pia kiherehere kwa kuandika uherehere huu
 
Wakuu salaam,
1. Mnakumbuka zile kelele za watu wengi dhidi ya waziri wa afya kutaka atumbuliwe kwa kudanganya umma kwamba dawa zipo wakati hazipo? Hapa wananchi walitaka hatua ileile ya kumtumbua Anna kilango kwa 'uongo' wake ichukuliwe pia kwa huyu waziri lakini matokeo yake wote tunayajua.

2. Mnakumbuka ishu ya Gambo vs Lema? Tulipiga kelele sana lakini mwisho wa siku tuliona alichokifanya malaika mkuu.

3. Mnakumbuka yale maigizo ya picha ya yule dc wa iringa? Watu walipiga kelele kuhusu yale maigizo lakini malaika mkuu akabariki yale maigizo.

Inshort, Mikelele yenu inamsumbua malaika mkuu na yeye huwa hapendi kelele na kwa vile yeye ni mtu wa visasi kwenye haya makelele dhidi ya Makonda atawakomesha kwa kumpandisha cheo ili mkome kiherehere chenu.
Katumbuliwa Kitwanga!
Itakuwa Makonda!
 
Hata akitumbuliwa si tatizo, wasema kweli na wapenda haki watakuwa nyuma yake kama shujaa wao, namkubali sana Paul Makonda, aendelee na moyo wake wa ujasiri na usema kweli na Mwenyezi Mungu atamlinda na kumbariki siku zote. Love you my brother Paul Makonda.
 
Awamu hii watu hawajui kutumia fursa,we kila siku watukane wapinzani hadharani,baada ya mwaka kama hujaukwaa udc basi una laana.
 
Inshort, Mikelele yenu inamsumbua malaika mkuu na yeye huwa hapendi kelele na kwa vile yeye ni mtu wa visasi kwenye haya makelele dhidi ya Makonda atawakomesha kwa kumpandisha cheo ili mkome kiherehere chenu.
Nakubaliana na wewe na hasa kutokana matamshi yake mwenyewe alioyatoa kwenye mahojiano na TV Clouds. Kuwa ameletwa na YESU kuja kuwanyoosha watu anaowaongoza.Tamko kama hili limewahi kutolewa na Field Marshal John Okello alioteshwa kwa aya za Biblia kuja Zanzibar kitovu na chimbuko la uislamu chini ya jangwa la sahara kuja kuudhibiti uislamu kuenea kwa kuwachinja na kuwauwa waislamu,wenye umri kuanzia miaka 18.Sasa hizi ndoto za aina hii kutoka Biblia na chaguo teule kutoka kwa YESU lazima ziheshimiwe au zitatupeleka pabaya!Huko ndiko Tanzania ya viwanda tunako elekea.
 
Serikali isiyokuwa na "job description" wala si ya kujivunia.
 
Mpaka akija kusema vibali vinatoka ikulu ndiyo watachukua hatua, maana kama amemshutumu waziri mkuu mpaka akafedheheka kuwa wanasema wewe ndiyo umewaruhusu kuuza shisha ina maana bado ofisi moja tu, nayo ni ikulu
 
Wakati Makonda anateuliwa Mkulu alisema moja ya sababu ya kumteuwa ni baada ya kusikia Makonda akipigwa pigwa vita..!!

Kwaiyo Makonda kuadhibiwa na mamlaka ya uteuzi ni kama ndoto.

Kwa sehemu nyingine yoyote, ile statement aliyosema juzi Makonda kwamba " nilipowauliza mbona Shisha inauzwa wakanijibu Waziri Mkuu ameruhusu..", Zile zilikuwa ni serious allegations kwa PM na kwa namna yoyote lazima Makonda angewajibishwa kwa kumtuhumu PM hadharani kwa namna ile.
Kisha waziri Mkuu huyo huyo ndiye aliyekuja na malalamiko kuwa biashara ya SHISHA mbona ina shmili ndani ya jiji wakati kiuhalisia inatakiwa kuwa imekwisha.Ndio kusema Waziri Mkuu alikua anajua na alitaka kujua kuwa Mkuu wa MKoa anapambaa vipi na jambo hilo kwa kuwa liko kwenye ngazi yake...Sasa ndani yake Makonda anamwambia ...waliniambia wewe ndio umetoa Kibali....utapata picha game lilivyokuwa linachezwa kwa kutumia ngazi ya Waziri Mkuu kuruhusu biashara ya Shisha kuendelea wakijua Makonda awezi fikia kwa Waziri Mkuu na yeye Waziri Mkuu kwa kuona maagzio yake ya biashara ya Shisha kufungwa Dar alipoona yanaendelea akambana aliyemkabidhi dhamana ya jiji..kumbe wajanja wanaendelea kuwatwisha Watanzania madhala 19 yanayotokana na shisha ikiwemo TB...kwa kutumia mgongo wa Waziri Mkuu..

Sasa kazi ipo nani aliyemwambia Makonda ruksa imetoka kwa Waziri Mkuu?Je pale polisi walipokua wakiagizwa na Makonda kila alipozungukia vijiwe vya Shisha jijini na kukuta vinnaendelea akiwapigia simu wanao husika ama kuwaona uso kwa uso wakamatji wa shisha na kuwaambia mwndendelezo wa biashara ya shisha kuwa sokoni inaendelea ndio Je hapo walipokua wanatoa jibu la kuwa Mh Waziri Mkuu karuhusu au yeye mwenyewe Makonda alikua anawafuata wauzaji nao wanamjibu wanakibali toka kwa Waziri Mkuu....Hapo ngoma inogile
 
Tamko kama hili limewahi kutolewa na Field Marshal John Okello alioteshwa kwa aya za Biblia kuja Zanzibar kitovu na chimbuko la uislamu chini ya jangwa la sahara kuja kuudhibiti uislamu kuenea kwa kuwachinja na kuwauwa waislamu,wenye umri kuanzia miaka 18.
Wapemba mmeanza...
 
Katumbuliwa Kitwanga!
Itakuwa Makonda!
Ndo hapo nashangaa kitwanga alikuwa friend Wa mkulu before day one na kamtumbua sasa huyu makonda aliejuana naye juzi tu siasani akishindwa nitamshangaa mkulu aisee .

Ila makonda daaah [emoji3]
 
Wakati kesho jumamosi Mkuu wetu Wa mkoa akitalajia kuwepo katika ziara ya mkoa Kigamboni kusikiliza kero za wananchi naomba kusema machache!..

Kusema ukweli kumlidhisha myahudi wa kizazi hiki yataka moyo!
Mh; PAUL MAKONDA; Ni miongoni mwa wakuu Wa mikoa vijana wachapakazi Wa kupigiwa mfano!

Kwa kifupi Makonda;
Makonda ana uthubutu wa hali ya juu kufanikisha jambo!
Ikumbukwe makonda anawasaidizi na watendaji katika halimashauri na sekta zingine wanaopaswa kumuunga mkono!

WANAO MNANGA KUHUSU CRO!
1. Makonda aliamua kusema hadharani ili kuondoa unafiki katika jambo la shisha; maana tayali kulikuwa na tetesi za watu kuwa shisha imeruhusiwa.

2. Makonda tayari siku nyingi kwa nafasi yake alishapeleka mahali husika majina ya waliotaka kumhonga.

3. Makonda hana ugomvi na mtu yeyote Bali anatetea maslahi yako wewe mtanzania.

4. Makonda anaangushwa na baadhi ya watendaji kutoendana na kasi yake.
***************
Nawashauri watu tumpe muda mkuu wa mkoa wetu afanye kazi.

Kuna watu wanafikiri kazi ya ukuu wa mkoa ni ndogo! Wamesahau " kuongoza ni kazi hata kwenye familia hutokea kupingwa"

Naunga sana jitihada zake huyu Makonda; wanaompinga wengi wamejaa chuki binafsi tu.

Umasikini ukitawala huuharibu Moyo!
Moyo ulioharibiwa na Umaskini huzaa chuki ya kwanini!

Maskini hawezi mtakia mema mwenzake kwasabu chuki ipo moyoni kwake!
Tujifunze kuwaunga mkono viongozi wachapakazi kama makonda.
MAKONDA ANATHUBUTU NA ATAWEZA!

Natangaza rasmi kumuunga makonda mkuu wetu Wa mkoa!

IPO SIKU MTAMKUMBUKA HUYU KAKA! JIFUNZENI KUSHUKURU
"MOYO USIOKUWA NA SHUKRANI HUKAUSHA MEMA YOTE"
MAKONDA go! go! go!


Kweli Mkuu tutamkumbuka kwa kutowafichua walotaka kumpa rushwa, maana huenda ingekuwa ni dawa ya kuzuia na kupambana na shisha, lakini wafanyakaz wenzake anawachomekea kwa viongozi wa juu.
 
Kosa lake liko wapi; alichoamua kusema pale hadharani ni kuondoa ule unafiki uliokuwa umeanza kujitokeza
Serikali haifanyi kazi kwa kutangaza hadharani, bali hutenda hadharani. Makonda anatafuta cheap popularity. Haya ndiyo makosa yake. Ipo siku mteuzi wake atamwona kaa la moto. Atamtupa. Muda ni hakimu mzuri. Kitwanga rafiki yake mkubwa na mkulu yuko wapi
 
20161119_142559.png
 
Back
Top Bottom