Hata wabaya kwa siku ya ubaya

Hata wabaya kwa siku ya ubaya

a sinner saved by Christ

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2017
Posts
3,331
Reaction score
3,812
KUTOKUSAMEHE KUHIFADHI UCHUNGU MOYONI*
Mfano 1.
muonekano wa nje*
Mama G huyu mama wa watoto 4 mwenye umri wa miaka 56..anatumikia kanisani kwa miaka 20 sasa,anaimba kwaya,anafundisha anahubiri injili,anatoa sadaka ,ni mtumishi anatumikia kanisa kwa uaminifu kwa miaka yote zaidi ya 20

muonekano wa ndani

Mume wake alimuacha miaka 20 iliyopita akaondoka na nusu ya mali walizochuma pamoja kwenda kuoa kabinti kadogo dogo kabichi akawatelekeza yeye mama G na watoto, na watoto waliumia sana kuachwa na baba yao.

Moyo wa mama G unavyoonekana katika ulimwengu wa roho
--umejaa kinyongo ma majeraha makubwa ya mauchungu chuki kisasi juu ya baba G ..ambao aliapa hatasamehe mpaka kufa anasema alimuumiza sana yeye pamoja na watoto,aliwatelekeza na akachukua nusu ya mali akaenda kuoa mwanamke mwingine.

askofu mmoja
muonekano wa nje
nitumishi anayetumika kwa viwango vikubwa makatifu kabisa...

muonekano wa ndani moyoni mwake
kuna muumini mmoja ambaye ni kiongozi mmojawapo wa kamati , huwa anampinga sana wazi wazi kwenye maswala mbali mbali yanayohusu yanayohusu miradi ya maendeleo ya ,kwa kumkosoa waziwazi..

moyoni mwake amejaa chuki na kinyongo juu ya kukosolewa kwa muda mrefu ,kinyongo..maheraha ya moyo.

Tusichokijua Mungu haangalii kama sisi wanadamu ,yeye anaangalia NJE NA NDANI?

Tendo hilo dogo tu la kutokusamehe peke yake linatosha kukuzuia usiingie mbinguni .

SHERIA YA MUNGU IPO WAZI...INASEMA

1)Mt 6:14-15
Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi. Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu

2)Ebr 12:14
Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao

3)LUKA 6:27
Sikieni niwaambie, wapendeni adui zenu. Watendeeni mema wanaowachukia. 28 Wabarikini wanaowalaani, waombeeni mema wanaowaumiza

4).Mt 5:44-45
lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi, ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.

Na kingine cha muhimu hata watu wabaya ni Mungu amewaumba kwa makusudi yake
SAULO alishiriki kumpiga mawe stefano baadae akaja kuwa PAULO, ..je kama stefano asingemsamehe alipokuwa anapigwa mawe..

Yesu mwenyewe aliwasamehe waliomsulibisha pale msalabani ambao ni mimi na wewe alijeruhiwa na kuchubuliwa kwa makosa yetu.

Mfano mzuri ni wale watu watatu waliotupwa kwenye tanuru liwakalo moto walipokataa kusujudia sanamu ,mfalme akashangaa walitupa watu watatu lakini wameongezeka wamekuwa wanne..daniel,meshack anediego shedrack..

lakini pamoja na mfalme kuwafanyia uovu ubaya ..wao walimsemesha vizuri..uishi milele ewe mfalme(wakimuombea dua njema) ..wakaendelea kusema kuwa BWANA hakuona hatia ndani yetu akamtuma malaika wake atuokoe na huu moto..

Ayubu pia aliwaombea rafiki zake waliomuudhi..na kwa kufanya hivyo uteka wake ukamtoka.akapona.


HATA WATU WABAYA MUNGU amewaumba kwa siku ya ubaya

Mungu alifanya moyo wa Farao kuwa mgumu kama fundisho ili BWANA apate kutukuzwa..

Mit 16:4 SUV
BWANA amefanya kila kitu kwa kusudi lake; Naam, hata wabaya kwa siku ya ubaya
Source: Wingu la Mashahidi – NAAM, HATA WABAYA KWA SIKU YA UBAYA. – Site title
 
Samehe samehe huleta dharau sana mkuu
kinyongo ni sumu inayomdhuru aliyebeba ,kuondoa sumu ya kinyongo moyoni mwako huimarisha afya kwako.
 

Attachments

  • FJWGvWaVQAI2GZ7.jpg
    FJWGvWaVQAI2GZ7.jpg
    68.3 KB · Views: 14
Amelala sahivi,anawahi sana kulala….kesho nishtue nimtag …mi sifumbi maji mdomoni
mtag tu tumalizane nae leo,, hayo ya kesho anayajua muumba,,, kwenye kufumba na maji mdomoni hata mi nishashindwa🙃
 
🤣niumie? Are you sure? Yaan mi mtu aliyeniumiza moyo ni yule aliyening’ata kisimi kwa maksudi kabisa
Ila c yalikuwa maumivu na mautamu juu yake, hvy hakuna maumivu hapo
 
mtag tu tumalizane nae leo,, hayo ya kesho anayajua muumba,,, kwenye kufumba na maji mdomoni hata mi nishashindwa🙃
🤣🤣achana naye bhana,yaan kwa ninavyomwogopa…hakika nishamsamehe🙌🏾
 
🤣niumie? Are you sure? Yaan mi mtu aliyeniumiza moyo ni yule aliyening’ata kisimi kwa maksudi kabisa
alooo hivi hii issue ni kweli au unatania?,, kuna siku nimeiona mahali umereply nikahisi unachangamsha genge tu 😄😄😄
 
alooo hivi hii issue ni kweli au unatania?,, kuna siku nimeiona mahali umereply nikahisi unachangamsha genge tu 😄😄😄
🤣🤣niwe mkweli,sijawahi kuwa serious na kitu chochote….sema napenda tu kuongelea hizi mambo mpenzi.
 
🤣🤣niwe mkweli,sijawahi kuwa serious na kitu chochote….sema napenda tu kuongelea hizi mambo mpenzi.
na mimi nilihisi hivyo,, nimezikumbuka zile enzi za usiku wa manane tulivyokua tunamtania shadow😄😄,, ile cycle ilikuaga poa sana asee saiv ndo hamna kila kitu😪
 
Back
Top Bottom