Ulitaka kumjua Nyerere, ukaenda kusoma vitabu vya Nyerere, na "kupitia maandiko yake sijaona jambo baya"!... nilifanikiwa kusoma vitabu vyake na hata kumwona. Kupitia maandiko yake sijaona jambo baya
Nyerere kama mwanadamu hakosi sura mbili . Sura hizi ni ya yale mema aliyofanya na yale mabaya aliyofanya. Mema yana sura moja ya wema, mabaya yan sura mbili za ubaya, kwanza ni je, ubaya ulikuwa wa dhamira na pili, ni kwa makosa ya kibinadamu!
.
Nafuatilia mijadala mingi kuhusu Nyerere. Kuna kitu watu wanakiificha au hawataki kukikubali. Nyerere kama mwanadamu hakosi sura mbili . Sura hizi ni ya yale mema aliyofanya na yale mabaya aliyofanya. Mema yana sura moja ya wema, mabaya yan sura mbili za ubaya, kwanza ni je, ubaya ulikuwa wa dhamira na pili, ni kwa makosa ya kibinadamu!
Wengi ambao kwa kusema ukweli hawasomi au hawakuwahi kuishi nyakati za Nyerere wanadiriki kuongelea ya Nyerere bila kuwa na reference kwasababu tu wanahubiriwa au kufundishwa. Mapungufu haya ambayo ni sehemu kubwa ya udhahifu wetu watanzania ndiyo chanzo cha watu kuanzisha topic ile ile kila kukicha. Inashangaza wasio Watanzania wanaweza kuandika na wanaufahamu mkubwa sana kuliko sisi kuhusu Nyerere ambaye tuna access na nyaraka zote ikiwa ni pamoja na majarida, vitabu na hata watu waliofanya kazi naye kwa ukaribu sana.
Matokeo ya kusikia au kusimuliwa yanadhihirika kwa watu kushindwa kutetea hoja zao kwa ushahidi. Wengi wanapenda kujadili kwa hisia tu ili waweke nadharia zao lakini inapowekwa nyaraka ya kuthibitisha hawana uwezo wa kuitetea.
Tumeona hapa JF kila ikiwekwa nyaraka inayomhusu Nyerere watu wanakimbia na kesho yake unakuta Thread mpya iliyoanzishwa kwa nadharia. Fikiria mtu anaposema Nyerere aling'oa reli ya Dar -Mtwara hapa ni nini kama si masimulizi bila ya utafiti au uthibitisho wa aina yoyote.
Nyerere kama Icon na Beacon anachambuliwa kuliko viongozi wengine na hiyo ndiyo privilege ya great personality. Nina mambo ninayoyaeleza kila siku kuhusu mapungufu ya mwalimu, lakini hayo siwezi kuyatumia kuficha mema aliyoyafanya. Hakuna ushindani bali ni ushindanishi wa hoja.
Lile kundi linalomtetea Mwalimu, sio lazima kuwa linampenda bali linatetea rekodi yake inayoharibiwa makusudi ili kuunda rekodi iliyokusudiwa na si iliyopo. Kundi linalomchukia Nyerere linaongozwa na chuki na linatumia mbinu za kutafuta makosa ya kweli na ya uongo ili kujenga hoja zinazoshabihiana na lengo hilo. Tofauti ya makundi haya mawili ni kuwa kundi la kwanza lipo tayari kusimama na ushahidi kutetea hoja. Kundi la pili kwa bahati mbaya halipendi mjadala wenye data, takwimu au ushahidi, bali kujenga nadharia ambayo mara nyingi haiwezi kuitetea.
Mfano, mtu atasema Nyerere alikuwa dikteta, well and good! prove it, no answer. Yaani tuamini tu kwasababu imesemwa.
Nyerere alikuwa mdini, hapa amekuja Mohamed Said mwenye takwimu, hakuweza kuthibitisha zaidi ya kudai wazee wake wengine walifariki siku moja kabla hajawahoji. Mohamed said ameshindwa, kama wasivyoweza kutetea wanao amini nadharia ya udini wa Nyerere.
Nyerere alikuwa mkabali, inawezekana!!!, prove it, hakuna jibu, ila tuamini tu kwasababu fulani kasema.
Nyerere ndio chanzo cha mgao wa umeme, ok! prove it, ah ooh unajua ujamaa, kambona etc, ili mradi tu hakuna hoja bali kumsingizia.
Hakujenga viwanda, then prove vilivyojengwa baada yake, aahh aoooh unajua may be, hakuna jibu.
Kumewekwa nyaraka ya mpango wa maendeleo 1963.... wote wanaomchukia mwalimu wameingia mitini. Hakuna hata mmoja aliyethubutu kuonyesha, ukanda, ukabila au udini wa mwalimu.
Makosa ya mwalimu yasemwe, mazuri yasemwe na ikibidi yawekwe kwenye mizani, lakini tungo, mashairi yenye vibwagizo hayatusaidiii hata kidogo.
Tuangalie hoja bila kuongozwa na chuki zetu za kibinadamu au kufundishwa. Tuangalie kazi yake na tuichambue bila kuangali umbo lake.
Tujadili hoja kwa ushahidi si kusadikika, nadharia, majungu, ngano, mashairi au simulizi.
Wanaomkosoa Nyerere wanazo hoja, nyingi na za kuvutia; wanapata shida linapokuja suala la kuzipa ushahidi na nguvu hoja zao kwani tatizo siyo hoja, ni ushahidi wa kimantiki, kivitu, na kihistoria wa hoja hizo. Ndio maana kule Bungeni mtu akisema hoja fulani ambayo anashindwa kuiback up anaambiwa "alete ushahidi"..
a. Hadi leo hii hakuna mtu ambaye ameweza kutoa waraka, barua au maelekezo yoyote ya Nyerere ya kuwakandamiza Waislamu au kupendelea watu wa makabila fulani ili kukandamiza makabila mengine. NONE.
b. Hadi hivi sasa hakuna mtu ambaye ameweza kuthibitisha kuwa Nyerere aliwahi kuchukua uamuzi wowote bila kushirikisha viongozi wenzake, mijadala na bila kuzingatia sheria iliyokuwepo. Kwa mfano mara mbili kumekuwa na mashtaka dhidi ya uhaini. Na mara zote kesi zilikuwa wazi, ushahidi ukaletwa wazi na walioachililwa waliachiliwa na waliokutwa na hatia walikutwa na hatia.
c. Hadi hivi sasa hakuna mtu ambaye ameweza kuthibitisha kuwa Nyerere "aliua watu" ili kujilazimisha madarakani.
d. Hakuna mtu ambaye ameweza kututhibitishia kuwa Nyerere alikuwa hakubali kukosolewa au kuandikwa vibaya. Ushahidi wote uliopo ni kuwa Nyerere hakutaka Tanzania changa iparaganyike na hivyo hakumvumilia mtu yeyote. Leo hii wale wanaokubali "kukosolewa" ndio wanalivunja taifa letu mchana kweupe wakiwa waoga kulitetea!
n.k so wakosoaji wana hoja, tatizo ni katika kuzithibitisha hoja hizo.
FJM, ndiyo maana niliandika hapo awali kuwa pro-Nyerere wanakitu cha kuonyesha na wanataka waonyeshwe. Ant-Nyerere hawana kitu cha kuonyesha ila wanataka dhana na fikra zao zichukue nafasi ya ukweli.FJM;2175832]@Nguruvi3 kwenye red - spot on! & thank you!
Na mazungumzo au studies za ubaya wa Mwl (wengine Mzee) Nyerere umekuja mara baada ya wananchi kuanza kuuliza tunaelekea wapi kama nchi? (national leadership). How coincidental? Badala ya kutoa majibu ya maswali tunayouliza sisi wananchi, tunaandikiwa essays na kupewa lectures za ubaya, u-dikteta, udini, ukabila wa 'Mzee' Nyerere.
2. Mwl Nyerere anaweza akawa hakujenga shule kila kata lakini alicha nchi ikiwa na literacy rate approx. 90%
3. Mwl. Nyerere anaweza akawa hakujenga mfumo 'mzuri' wa kusamehe kodi ili kuwepo na EPZ madhubuti na kuvutia uwekezaji lakini aliacha Mwatex, Kiltex, Tanganyika Packers, Tanneries, General Tyres, Machine tools, Tanzania Fertilizers company (TFC), Coffee Curing, Tanzania Railway Company, Air Tanzania (with physical aircrafts), Ranchi za Taifa, Kiwanda cha kutengeza magunia, just to mention a few!
4. Mwl Nyerere anaweza asiwe na nguvu za ziada (super-man) lakini alijenga bwawa la Mtera na kipindi chake mvua za kutosha zilinyesha na kujaza hilo bwawa! maajabu!
5. Mwl Nyerere anaweza akawa anavaa miwani ya giza saa zote na hivyo kutowaona wezi wote, lakini hakuna mtu aliweza kuchota fedha toka central Bank kwa maana ya BOT! EPA, Kagoda hawakufurukuta!
7.Mwl Nyerere hakutatua matatizo yetu yote lakini alitoa elimu bure (huku akiacha rasimali zote nzima kama alivyozikuwa) ili tuwe na uwezo wa kutatua wenyewe. Kwa maneno mengine he empowered Tanzania to solve thier solve thier problem.
8. Mwl. Nyerere anaweza akanunua rada ya kizamani sana- pengine ya kuona ndege ikiwa umbali wa mita 3 tu! lakini ndege za kivita toka nchi nyingine hazikutuwa kwenye viwanja vyetu na kuchukua wanyama bila rada kuwaona!10.Mwisho. Mwl. Nyerere anaweza kuwa Dikteta in the strongest terms possible lakini hakuondelewa madarakani na NATO au kwa 'mazungumzo' ya amani!
Mwl Julias Kambarage Nyerere - RIP.
Mfano mzuri wa wanaomchukia mwalimu(haki yao) shamu.Hebu tunaomba ufafanue yafuatayo kwa uthibiti na mifano si nadharia au hadithi.Shamu;2177074]Miaka zaidi 25 aliotawala, bila ya demokrasia, ubabe, bado unataka prove kama alikuwa Dictator? Let's be honest.
Ushahidi wa mauaji? Azimio la Arusha. WTZ walikuwa wanalazimishwa kwenda vijijini bila ya kuwepo kwa misingi bora kama jinsi ya kupata maji.
Kulikuwa na maandamano wakati wa utawala wa Nyerere, na ushahidi upo ktk moja ya video niliyoipost.
Ktk hiyo video niliyoipost inaonesha ushahidi tosha kabisa na maneno yake mwenyewe Nyerere, "I have sufficient power, under the Constitution to be a Dictator..." Ushahidi gani unataka ya zaidi ya maneno yake mwenyewe Nyerere. Nyeree alitumia lugha hiyo kuwatisha wale wanaondamana.
Hii Kauli ya " I have sufficient power, under the Constitution to be a Dictator" ina maana gani kwako?
Naona hukuwepo enzi za Arusha Declaration. Maandamano yote yaliyofanyika yalikuwa yanaunga mkono Azimio. Lete kingineHii ni threat. Ni sawa na mtu akimwambia mtu anaembisha kwamba "nina bastola yenye kuua" Nyerere katumia hiyo lugha kuwatisha wale wanaondamana dhidi yake.
Mfano mzuri wa wanaomchukia mwalimu(haki yao) shamu.Hebu tunaomba ufafanue yafuatayo kwa uthibiti na mifano si nadharia au hadithi. 1. Je Mwalimu alitawala miaka 25 kama unavyodai? 2. Alitawala vipi bila ya demokrasi said:1.Ok 20 na,
2. Hiyo article niliyoipost inaeleza vizuri. Halafu ushahidi tosha ktk Azimio la Arusha. WTZ walilazimishwa kwenda vijijini bila ya matakwa yao. Wafanyabiashara, WTZ walipokonywa haki zao bila ya matakwa yao kwa ajili ya kufuata Ujamaa ideology . Ushahidi upi unoataka wewe?
3. Nyerere kwa makusudi aliweza kuwanyima haki za msingi WTZ kama freedom, freedom of press, nk. Ushahidi upi unaotaka wewe?
Naona hukuwepo enzi za Arusha Declaration. Maandamano yote yaliyofanyika yalikuwa yanaunga mkono Azimio. Lete kingine
Hii ni threat. Ni sawa na mtu akimwambia mtu anaembisha kwamba "nina bastola yenye kuua" Nyerere katumia hiyo lugha kuwatisha wale wanaondamana dhidi yake.
Kwanini unachukulia kuwa ni thread instead of a statement of fact?
Mtu akisema
"Nina bunduki mkononi ambayo naweza kuitumia vizuri tu"
"Nina Bunduki mkononi ambayo naweza kuitumia dhidi yako"
ipi kati ya hizo ni tishio dhahiri?
Kwanini unachukulia kuwa ni thread instead of a statement of fact?
Mtu akisema
"Nina bunduki mkononi ambayo naweza kuitumia vizuri tu"
"Nina Bunduki mkononi ambayo naweza kuitumia dhidi yako"
ipi kati ya hizo ni tishio dhahiri?
ninavykumbuka mimi, nilimsikia akionesha dosari ya katiba yetu tuliyo nayo na si kutishia wananchi wake."I have sufficient power, under the Constitution to be a Dictator..."
Hivi Bwana Kambota unaweza japo kidogo kuzingatia busara ya usemi kuwa akili nyepesi hujadili mtoa hoja ilhali akili zilizotanuka hujadili mada husika?Ni vigezo gani ulivyotumia kutambua kuwa baadhi ya wanaomkosoa Nyerere wanatafuta umaarufu?Nilikuhoji katika jibu langu la awali, "hivi mtu anapataje umaarufu kwa kumkosoa Nyerere",so far hujajibu bali unaendelea kuhukumu.Kama kumsoa ni kusaka umaarufu,je wanaomsifia wanasaka nini?
Na unaponyooshea watu kidole,kumbuka kidole kingine kinalenga kwako pia.Hivi tukikubaliana nawe kuwa baadhi ya critics wa Nyerere wanafanya hivyo kusaka umaarufu,hudhani kuwa na wewe unayewakosoa hao critics wa Nyerere unaweza kutuhumiwa kuwa unasaka umaarufu kwa kudandia hoja za wengine?
Halafu maswali mengine unayouliza yanaweza kutia mawaa harakati zako za kuwa mchambuzi mahiri.Unauliza kwanini Nyerere anakosolewa sasa?Jibu jepesi ni kuwa mfumo wa siasa hadi Nyerere anaondoka madarakani haukuruhusu maoni/mawazo mbadala.Kumkosoa Nyerere zama hizo ilikuwa ni sawa na uhaini.
Pengine jibu jingine la "why now" ni sehemu ya kuangalia mustakabali wa taifa letu,kwa minajili ya wapi tulikwenda kombo na kwa sababu zipi basi tufikie katika mazingira haya ya viongozi miungu-watu na mafisadi sugu.Kuuliza maswali magumu kuhusu taifa letu na uongozi si dhambi just like isivyo dhambi kusoma historia ya nchi.Tunapaswa pia kutambua siasa si dini: kwenye dini cha muhimu ni imani,na kuhoji imani ni kujichumia dhambi za bure.Siasa,on the other hand,ni tofauti.Unless unaishi katika mfumo wa kidhalimu usioruhusu muhimu na kukosoa bali kupongeza pekee,wadau wa maendeleo ya nchi wana haki na uhuru-kupitia Katiba-kufanya hivyo (muhimu,kukosoa,etc).Ndio freedom of expression ambayo wenzetu mnatafsiri kuwa ni kusaka umaarufu (which is fine kwani kwa kufanya hivyo nanyi mna-exercise freedom of expression).