Wanaomiliki vitambulisho vya Rais Magufuli kwa wajasiriamali wanapaswa kulipa nusu ya kiingilio Timu ya Taifa inapocheza nyumbani. Itaongeza ushawishi

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,891
16,319
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums. Mimi mdogo wenu Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to the Almighty. Leo wazo langu lipo kama hivi;

Wanaomiliki vitambulisho vya Rais Magufuli kwa wajasiriamali walipaswa kulipa nusu ya kiingilio mechi ya Tanzania Vs Uganda. Itaongeza ushawishi zaidi.

Hili suala litaongeza ushawishi zaidi kwa wajasiriamali wadogo kwa maana kwamba ukiongelea ushabiki wa soccer kindakindaki hapa unaongelea watu wa kipato cha chini wanaokaa kule juu kabisa wanaojichora rangi za uzalendo za bendera usoni pamoja na kubeba mabango ya ukereketwa wa soccer.

Kama kiingilio cha bei ya chini kabisa ni shillings 10,000 basi mjasiriamali anayemiliki kitambulisho anaweza kulipia let's say 5,000 ili kuongeza ushawishi na hamasa kwa wajasiriamali wadogo wengi kuchukua vitambulisho hivi kwa manufaa mapana yao na biashara zao.

Hili ni wazo langu tu na nipo tayari kusahihishwa. This is my own idea and I stand to be corrected.

KIJANA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA.
IMG_20181203_121456_984.jpg
 
Hivi ni vitambulisho au tiketi ya kupata huduma na starehe bure sasa? Sababu kwa vitambulisho hivi hivi unataka wenye navyo wapate bima ya afya bure, unataka waingie navyo uwanja wa taifa, baadaye utataka wapande navyo drimulaina bure ili kuleta ushawishi?
Ulipaswa tu kujua hizi ni propoganda nyepesi za siasa ya kodi kwani anayewadai wamachinga kodi ni serikali na anayepiga marufuku kodi hiyo kupitia vitambulisho ni hiyo hiyo serikali,sasa ilibidi za kuambiwa uchanganye na za kwako.
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums. Mimi mdogo wenu Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to the Almighty. Leo wazo langu lipo kama hivi;

Wanaomiliki vitambulisho vya Rais Magufuli kwa wajasiriamali walipaswa kulipa nusu ya kiingilio mechi ya Tanzania Vs Uganda. Itaongeza ushawishi zaidi.

Hili suala litaongeza ushawishi zaidi kwa wajasiriamali wadogo kwa maana kwamba ukiongelea ushabiki wa soccer kindakindaki hapa unaongelea watu wa kipato cha chini wanaokaa kule juu kabisa wanaojichora rangi za uzalendo za bendera usoni pamoja na kubeba mabango ya ukereketwa wa soccer.

Kama kiingilio cha bei ya chini kabisa ni shillings 10,000 basi mjasiriamali anayemiliki kitambulisho anaweza kulipia let's say 5,000 ili kuongeza ushawishi na hamasa kwa wajasiriamali wadogo wengi kuchukua vitambulisho hivi kwa manufaa mapana yao na biashara zao.

Hili ni wazo langu tu na nipo tayari kusahihishwa. This is my own idea and I stand to be corrected.

KIJANA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA.
View attachment 1050659

Loyalty To country Alyways,To government When it deserves
 
Good kua umekiunga mkono hoja au ?
Ila ametoa hoja ya kijinga sana ;alienunua kutambukisho kwa kukopa pesa 20000/ kisa hana huo uwezo leo aache kutembeza mboga za majani akaangalie mpira tena ?
Rais atambue kua Hizi Vitambulisho vimekua kero sana kwa wananchi....wananchi hawatainuka kwa kuletewa vitu vya kipuuzi kama Hizi vitambulisho.
 
Inakuwa kama ni promotion. Kwani National Team inacheza uwanja wa nyumbani mara ngapi kwa mwaka? Wajasiriamali ni lazima washawishiwe kuchukua hivi vitambulisho kwa manufaa yao na biashara zao
Unaposema kwa manufaa ya biashara zao unamaanisha kitu gani ? mtu mwenye mtaji wa 2000/ ananunua kitambulisho cha 20000/ Mara moja..huyu mtu atafanya biashara kwa muda gani mpaka arudishe pesa ya itambulisho ?
 
Hujaelewa kuwa ubongo wako umefungiwa kwenye box dima utajiona kuwa wewe ni mnyonge na maskini. Maskini na mnyonge mpira unauambia nini? Kwanza wote wanao tegemea hivi vitambulisho nikupe hawana mchango wowote kwauchumi wataifa zaidi yakuchafua mazingira nakuharibu muonekano wamiji.
Good kua umekiunga mkono hoja au ?
Ila ametoa hoja ya kijinga sana ;alienunua kutambukisho kwa kukopa pesa 20000/ kisa hana huo uwezo leo aache kutembeza mboga za majani akaangalie mpira tena ?
Rais atambue kua Hizi Vitambulisho vimekua kero sana kwa wananchi....wananchi hawatainuka kwa kuletewa vitu vya kipuuzi kama Hizi vitambulisho.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom