Vitambulisho vya Rais Magufuli kwa wajasiriamali viwezeshwe ku-cover mpaka N.H.I.F Community Health Fund. Itaongeza ushawishi zaidi

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
12,044
2,000
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa JamiiForums.

Mimi mdogo wenu Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Leo ninapenda kuuliza hivi:

Vitambulisho vya Rais Magufuli kwa wajasiriamali viwezeshwe ku-cover mpaka N.H.I.F Community Health Fund. Itaongeza ushawishi zaidi.

Idea yangu ni kwamba, mjasiriamali mdogo anapolipia pesa ya kitambulisho 20,000/= anakuwa anaweza pia kutumia kitambulisho hicho katika kupata matibabu kwenye zahanati iliyopo ndani ya locality yake kwa muda wa mwaka mzima pasipo kuhitajika kulipa tena 5,000/= gharama ya CHF.

Kuongeza benefit hii inaweza kuwashawishi wajasiriamali wengi kujitokeza na kuchukua vitambulisho hivi kwa wingi sana.

Hili ni wazo langu tu and I STAND TO BE CORRECTED.

OUR MOTTO: KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.

IMG_20181203_121456_984.jpg


VODACOM WAMECHUKUA WAZO LANGU
 

dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
13,444
2,000
Good idea. Vinaweza kupandishwa bei kidogo hadi 50,000, kwa mfano, then vika-cover huduma nyingi zaidi kama hiyo ya NHIF. Na hii itakuwa njia rahisi ya vitambulisho "kujiuza" vyenyewe bila kuhitaji nguvu ya dola, wakuu wa wilaya au mikoa. Yaani mjasiriamali ashawishike na thamani halisi atakayoipata ikiwapo suala la afya yake. You are really a GT!
 

Extrovert

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
32,625
2,000
Kwani kitambulisho hicho kimetengenezwa kwa madhumuni gani ? kama kuna mjasiriamali anaona haimfai basi asilazimishwe aiache tu.
Dhumuni ni kukusanya mapato yatokanayo na biashara anayofanya machinga ambae hana location maalum. Ilikuwa ngumu kukusanya kodi kwao nadhani 500 kila siku maana walikuwa wanahama hama sana na kukulupushwa na migambo wa city.

Ila kwa sasa ukilipa 20,000 unapiga kazi mwaka mzima bila kusumbuliwa na migambo. Utalipia hela kidogo kama ushuru kwa manispaa kwa ajili ya maintanance ya maeneo na usafi ila so far inapunguza kero ya kufuatwa fuatwa na ma afisa kodi wa TRA.
 

Extrovert

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
32,625
2,000
Good idea. Vinaweza kupandishwa bei kidogo hadi 50,000, kwa mfano, then vika-cover huduma nyingi zaidi kama hiyo ya NHIF. Na hii itakuwa njia rahisi ya vitambulisho "kujiuza" vyenyewe bila kuhitaji nguvu ya dola, wakuu wa wilaya au mikoa. Yaani wajasiriamali washawishike na thamani halisi atakayoipata ikiwapo suala la afya yake. You are really a GT!
Yeah ila hii itakuwa kama kubwa sana kwa wafanyabiashara wadogo. Nzuri ni walau 30,000 hapo.
 

dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
13,444
2,000
Yeah ila hii itakuwa kama kubwa sana kwa wafanyabiashara wadogo. Nzuri ni walau 30,000 hapo.
... sure! Ni mfano tu nimetoa. Muhimu iwe figure ambayo haitamuumiza "mnyonge" wakati huo huo akiona thamani halisi ya kitambulisho chake zaidi ya kuwa safe dhidi ya mgambo wa jiji.
 

Extrovert

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
32,625
2,000
... sure! Ni mfano tu nimetoa. Muhimu iwe figure ambayo haitamuumiza "mnyonge" wakati huo huo akiona thamani halisi ya kitambulisho chake zaidi ya kuwa safe dhidi ya mgambo wa jiji.
Wazo zuri, tuombe Rc Makonda alifanyie kazi kama mfano.
 

Lucky Star

JF-Expert Member
Jul 16, 2017
1,152
2,000
Mawazo kama haya ndiyo yanayotakiwa ili kujenga jamii salama na iliyostaarabika.

Ni faraja siku moja kuona wazo kama hili limefanyiwa kazi.

Kikubwa wasiweke gharama kubwa ikawa nafasi yao tena kukidhi matakwa yasiyokuwa na tija kwa mmiliki wa kitambulisho

Sent using Jamii Forums mobile app
 

mwakijembe

JF-Expert Member
Mar 20, 2017
1,451
2,000
Infantry Soldier,

Mmeshindwa kutupatia vitambulisho vya taifa, saa hii mnatuuzia viplastik card kwa 20,000 ambavyo haviko havifiki hata shilingi 3,000. Hizo 20,000 kwanza zinaingia mfuko gani na ni nani anazikagua makusanyo na matumizi yake? Acheni wizi wa kitoto.
 

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
32,653
2,000
Nadhani first step ni kuwatambua kwanza. Kusema 20000 itumike kucover matibabu kwa mwaka huo ni uongo wa mchana.la msingi watambulike then wawe organised kama vikundi vya wafanyabiashara wadogo wawezeshwe kwa mikopo na fursa mbalimbali. Tusije tukaiua NHIF kwa reasons za kisiasa. Let everyone know kwamba afya ni muhimu na ni ghali na kamwe afya isiwekwe kama hitaji la hiari bali hitaji la msingi.

Asiyetaka kuchukua kitambulisho asifanye kazi ya umachinga full stop.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom