Wanaomhujumu Rais Magufuli hawa hapa

Wanaomhujumu Rais Magufuli hawa hapa

Mungu ndiye kwanza alihakikisha hao wapiga kura siku ya kupiga kura wako hai hawajafa kwa ukimwi ,malaria,ajali nk pia akawaongoza kupiga kura wampigie nani na wamwache nani
Mungu wa wapi na yukoje na anakaa wapi??? Imani siyo kuwa na proofs haiwezi kuwa referenced before the law!!!!
 
Walio pamoja na Magufuli ni wengi kwa idadi na wana nguvu kubwa kuliko walio kinyume na Magufuli.Wampingao hawatafanikiwa ila wataona mambo yao yakiharibika siku baada ya siku maana wanashindana na mtu ambaye mamlaka zilizomuweka si za wanadamu.
Hakika mamlaka zilizomuweka si za mwanadamu YEHOYADA.
Kuna mamlaka kuu mbili ukitoa za wanadamu. Kama umeshindwa taja hizo mamlaka zilizomuweka madarakani,inamaana kuwa ama huzijui hizo mamlaka au huna uhakika ni mamlaka gani imemuweka. Kati ya hizo mamlaka,moja ni mbaya na nyingine ni nzuri. Kawaida ya binadamu huwa tunapenda kuwaelezea vizuri na kuwapamba watu wetu tunaowashabikia kwa sifa zote nzuri na kuwaweka upande mzuri hata kama ndani ya mioyo yetu tunaamini si sahihi. Mbona umeshindwa fanya hivyo leo?
 
Naona umejiandika jina na namba kabisa ili mtukufu asipate tabu kukuteua
 
Vipi Buku 7 umeshapokea leo?.
Akili yako hapo imefika mwisho basi haina budi kukulaumu kwa kuwa upo kwenye giza nene mno mkuu!!! ila inabidi tukuelemishe hatuwezi kukuacha hivihivi
 
Kaumiza kichwa wee kuandka uongo mtupu, haya mnayofanya yanamwsho jaman. Kuuadaa uma wa Tanzania kwa maneno ya kutumwa kuna mwisho jaman, utashangaa n kjana ambae hata 40 ajafksha anakuja kuleta porojo hapa INAUMA SANA
 
Kama alivyoibuka kidedea kwenye mbio za urais ndivyo atakavyoibuka kidedea mwaka 2020! Ninyi mwapiga domo yeye achapa kazi.
kinachotakiwa ni ufanisi, sijali Rais anatoka chama gani mkuu
 
I am sure hata Magu akiona hoja za mleta thread anweza akatapika kwa hasira na fadhaa

Post imejaa personal attacks, shoddy analysis na mbaya zaidi inaonekana imeandikwa na mtu mwenye mental illness

Hujawataja wakwepa kodi lakini ukakomaa na vidagaa kama Malisa... waaay
 
Kuna mamlaka kuu mbili ukitoa za wanadamu. Kama umeshindwa taja hizo mamlaka zilizomuweka madarakani,inamaana kuwa ama huzijui hizo mamlaka au huna uhakika ni mamlaka gani imemuweka. Kati ya hizo mamlaka,moja ni mbaya na nyingine ni nzuri.

Kiufupi hiyo mamlaka iliyomuweka Magufuli ni kubwa mno na ina nguvu kubwa kushinda ile mamlaka ya mgombea Uraisi wa UKAWA.Ni mamlaka iliyoipiga mateke na kuibamiza chini mamlaka ya chini iliyomweka huyo mgombea wa UKAWA na mamlaka hiyo kuu iliyoicharaza vibao hiyo mamlaka ya chini ndiyo mamlaka nzuri.Hiyo nyingine ni mamlaka mbaya

LOWASA.jpg
 
  • Thanks
Reactions: MC7
Mkuu Jana nlitoa uzi wa demokrasia kwa upana wake zaidi inaonekana haukuisoma kwa kuwa mode iliificha ila nitaandika tena ujifunze maana ya demokrasia naona hauijui kabisaaa

mkuu kwa matapishi hujachacha. Mpaka sasa kuna mikataba nchi imeingia kupitia serekali ya ccm, kila siku mnaambiwa muipeleke bungeni ijadiliwe hamtaki. Leo unakuja na propaganda za kizee eti mataifa ya nje, je hiyo mikataba ya kinyonyaji imeingiwa na mataifa yapi ambayo leo unasema unayaogopa? unadhani bado wananchi walio wengi wanaamini kwenye hayo matapishi uliyoleta hapa?
 
Hujui unachokifanya wewe acha akili za kitoto Mimi namaanisha na nilimaanisha harakati zenu za kumpinga magufuli kama yeye ndo alizaliwa ili afe kwa ajili ya nchi yetu maana kila anapojitaidi mnamkwamisha kila kukicha kwa propaganda zenu hizihizi
Daaah! Yaani mtu amezaliwa ili afe kwa akili ya hii nchii!!!?
Halafu tena unasema kuwa watu wanamuhujumu kwa propaganda zao!!!? Wewe ni kiumbe wa ajabu sana. Kwa kuwa umeweka namba yako ya simu,basi nitakutafuta nilete group la watalii wa kampuni yangu waje kushangaa kiumbe wewe.
 
Walio pamoja na Magufuli ni wengi kwa idadi na wana nguvu kubwa kuliko walio kinyume na Magufuli.Wampingao hawatafanikiwa ila wataona mambo yao yakiharibika siku baada ya siku maana wanashindana na mtu ambaye mamlaka zilizomuweka si za wanadamu.
Na kwelu sii za binadamu , ni za kishetani
 
Ha ha ha.. Propaganda katika ubora wake.. Visigizio kibaooo.. Sambaratishen huo mtandao
 
Nani ana muhujumu km siye yy na uongozi wake?
Utasema mbowe kazuia ajira mpya?
Utasema Mbowe kazuia fao la kujitoa?
Utasema Mbowe kapandisha VAT & TAX?
Utasema Mbowe kafanya maisha yawe magumu mtaani?
Utasema Mbowe kasababisha wafanyakazi hewa?
Utasema Mbowe kasababisha rushwa na ufisadi?
Utasema Mbowe kaficha pesa?
Utasema Mbowe kasababisha deni la taifa lifike 51%?
Acheni unafiki. Mnapewa hela kuja kutuaminisha hapa.
Mfanye kazi na siyo kulilia hapa. Mnashindwa kutoa ajira mpya halafu mnasema mnahujumiwa. Nani kawahujumu km siyo wenyew
 
Naona umeweka namba ya simu ili upigiwe upewe hata ka cheo kidogo hahahahaha njaa mbaya sana
NImecheka sana aisee

Jamaa kaona ameshamjulia mkuu wa nchi... wacha aimpress, aweke namba hapo ili atafutwe badae apewe shavu... kwikwikwikwi!!

I respect JPM efforts mno, na he is doing well, ila post kama za huyu nyangarika mleta hoja kwakweli imeniacha hoi

Niliifungua nikijua kuna some serious content... kumbe kaput kabisa
 
Kiufupi hiyo mamlaka iliyomuweka Magufuli ni kubwa mno na ina nguvu kubwa kushinda ile mamlaka ya mgombea Uraisi wa UKAWA.Ni mamlaka iliyoipiga mateke na kuibamiza chini mamlaka ya chini iliyomweka huyo mgombea wa UKAWA na mamlaka hiyo kuu iliyoicharaza vibao hiyo mamlaka ya chini ndiyo mamlaka nzuri.Hiyo nyingine ni mamlaka mbaya

LOWASA.jpg
Mamlaka ipi nzuri isiyotajika?
Mimi ni mfuasi wa ukweli na si propaganda,na sina chama zaidi ya kupenda kuona ustawi wa Tanzania kwenda mbele,bila ya kujali ni nani anatupeleka mbele (kasoro tu shetani). Mambo ya kuchafuana hayo nawaachia nyie wanapropaganda,maana hata kusikia na kuona pia watu fulani wakifanya mambo fulani tumeona na kusikia.
 
mkuu kwa matapishi hujachacha. Mpaka sasa kuna mikataba nchi imeingia kupitia serekali ya ccm, kila siku mnaambiwa muipeleke bungeni ijadiliwe hamtaki. Leo unakuja na propaganda za kizee eti mataifa ya nje, je hiyo mikataba ya kinyonyaji imeingiwa na mataifa yapi ambayo leo unasema unayaogopa? unadhani bado wananchi walio wengi wanaamini kwenye hayo matapishi uliyoleta hapa?
Huna hoja zaidi ya kukashifu au kukejeli ila nitakufundisha vizuri na nitakuelimisha vizuri sanaaa naona bado unatamani kushindana na Mimi lakini huna hoja yenye mvuto Bali upo kunikashifu lakini nakwambia Mimi ni mtu mwingine
 
Ndugu wanajamvi sisi kama wazalendo na wanaharakati ambao sote tunaipigania nchi yetu kwenda kwenye uchumi wa kati lazima tupaze sauti zetu kila Mara kupinga hujuma mbalimbali zinazofanywa na watu Fulani Fulani kuhakikisha RAIS MAGUFULI anakwama lakini kibaya zaidi hawajui hii nchi ni yetu sote na siyo MAGUFULI peke yakee.
Ndugu wanabodi hakika sasa hivi kuna mambo mengi yanayosemwa kwa RAIS wetu kuhusu utawala wake lakini kuna kitu kimejificha nyuma ya pazia ,na huu ni mtandao unaupinga utawala wa awamu ya tano au kwa lugha nyingine wanaomuhujumu RAIS magufuli na hapa wapo watu wa makundi mbali mbali na taasisi mbali ila ngojea nianze kuyachambua kama ifuatavyo;

1: Wafanya biashara ambao walikuwa hawalipikodi;hawa wameunda mtandao wao kwa usiri Mkubwa mno ili kuhakikisha kwa kila namna huu utawala ufe, kwa kuwa walizoea kuishi bila kulipa kodi lakini sasa hivi lazima ulipe kodi kitu ambacho kinawanyima usingizi.Juzi tumesikia kuwa RAIS MAGUFULI analalamika kuna watu wametoa hela benki wameficha nyumbani eti kuzuia mzunguko wa hela inasadikika kuwa kundi hili limo kwenye hii harufu mbaya.

Mfano moja tuu niwape juzi tumemsikia RAIS wa ufilipino Rodrigo Durteze analalamika kuwa anahujumiwa na wafanyabiashara wa madawa ya kulevya waliounda mtandao wao kuhakikisha huyu RAIS anafeli katika utawala wake kwa kuwa alitangaza operation ya kuwanyonga hawa mabwenyenye. Lakini akawa na wakati mgumu kwa sababu huu mtandao ulikuwa mpana sanaaa hadi Marekani ameingilia kati kabisa kwa kigezo cha haki za kibinadamu. Swali ni je Marekani hawajawahi kuwanyonga watuhumiwa wa madawa ya kulevya?

Utakuta ni majibu nyepesi kwenye masuala magumu kama haya ukikaa na kufikiri kwa undani utakuta Kuna maslahi ya watu hapa ndo maana wanaingilia mambo yasiyowahusu kwani nani asiyejua athari za madawa ya kulevya inavoangamiza vijana na vizazi katika taifa. Lakini huyu Rais alipoingia madarakani aliivalia njuga kama MAGUFULI alivyolivalia njuga swala la mafisadi na kulipa kodi.

2: Ni genge la watu Wanaodai demokrasia ambayo hata demokrasia yenyewe hawaijui maana yake, eti kwao demokrasia ni kufanya mkutano wa kisiasa na maandamano ambao hauna faida kwa wananchi. Na hapa ndipo kuna upotoshaji mkubwa unaotaka kugawa serikali na wananchi wake, na viongozi wa hii genge hasa ni MBOWE na MAALIM SEIF ambao kwao demokrasia ni ubavu ndani ya vyama vyao na kutunishana msuli usio na faida kwenye ujenzi wa vyama vyao.

Wamejitahidi kutumia vijana wao kama YERIKO NYERERE,MALISA G,BENSAANANE,JULIUS MTATIRO,katika kuupotosha umma kwenye mtandao wa kijamii kama JF,Facebook na Twiter kuhusu dhana ya demokrasia na wanaenda mbali na kusahau kabisa kuwa wao ndo vijana wa kulisaidia taifa hii kwenda kwenye uchumi wa kati.

Niwasihi hawa vijana waache maramoja kuupotosha umma kuhusu neno demokrasia kama mawazo yao yalivofikia waaache utashi wa kisiasa bali wajenge hoja zenye mantiki ya kutuunganisha sisi wananchi kwenda kwenye uchumi wa kati kwa kuwa Mimi naamini RAIS MAGUFULI angekuwa dikteta wasingetamka hadharani kama wanavolitamka kwa nyakati tofauti Bali huu ni uchochezi wa hali ya juu kuwahi kutokea katika taifa hili.

Kwakuwa hili kundi linasadikika kuwa inapata support kutoka kwenye mtandao wa wafanyabiashara ambao kodi kwao kulipa hawataki na pia inapata support kutoka kwa mtandao wa mabwenyenye wa mataifa ya magharibi wenye mrengo tofauti na RAIS MAGUFULI ambao kwao lengo kubwa ni kutaka kuchuna rasimali zetu na mkakati huu ulianza tokea uchaguzi wa 2015 ambao hawa mabwenyenye wana kiu sanaa na rasimali zetu ndipo wanaungana na mtandao wenye mrengo kama ya kwao wenye kujiita wana demokrasia.

3. Ni taasisi Fulani Fulani zisizo za kiserikali ambao wanatumiwa na wana siasa kwa nyakati tofauti kuja kupotosha umma kuhusu dhana ya demokrasia na utawala wa RAIS MAGUFULI zipo taasisi za kidini na zisizo za kidini kama mnafuatilia mambo kiundani mmemsikia padri Fulani kwa nyakati tofauti amesikika kuupinga utawala wa MAGUFULI hadharani lakini siyo kosa lake ni kosa la waliomtuma.
Hili kundi lina ushirikiano mkubwa na kundi la pili kwa kuwa waga kuna vikao wanafanya kwa usiri Mkubwa na ndipo wakishapewa au wakishaaidiwa vitu Fulani unawasikia wakiropoka bila ata mantiki ya kutuunganisha sisi wananchi hivyo nitoe rai yangu kuvionya hizi taasisi ambao wanashirikiana kwa namna moja au nyingine na hii genge la MBOWE na wenzake kuacha Mara moja kwa kuwa wao ni taasisi bila kujali ya serikali au siyo ya ki serikali kazi yao ni kutuunganisha na si kutugawa na kuleta uchochezi.

4. Baadhi ya vyombo vya habari hapa utakuta kuna media zimenunuliwa na kuna wana habari pia na magazeti yamenunuliwa ili kupambana na serikali ya awamu ya tano juzi tuu ni mfano halisi baada ya waziri NAPE kuvifungia baadhi za station za radio zilizoripoti habari za kichochezi na hili kundi hushirikiana kwa karibu na kundi la pili kwa nyakati na sehemu tofauti.

Kila siku ukisoma gazeti Fulani ambye mmiliki wake ni kiongozi wa chama Fulani utaona na kujiiridhisha kuwa wanapambana na serikali ya awamu ya tano. Rai yangu kwa wanahabari wote kuacha mara moja mambo au kutoripoti kabisa habari za kichochezi zenye mrengo wa kutugawa katika taifa letu pia niwaonye wamiliki wa vyombo vya habari kuacha utashi wa kisiasa kuvitumia vyombo vyao kuripoti au kuandika habari za kichochezi zenye mrengo wa kuligawa taifa letu.

Safari ya kuelekea kwenye uchumi wa kati bado inaendelea:

Ni wako kijana mtiifu,mzalendo na mwanaharakati wa kweli.

SIMON MATO-0762189733.
Wapo wafanyakazi wa serikali,wapo wanaojiita wanachama wa CCM waliovaa ngozi ya CCM lakini ndani ni mbwa mwitu wakali.Wapo pia viongozi mbalimbali waliokuwa kwenye awamu ya nne,hawa ndio wabaya kuliko wote.Magufuli asipowashuhulikia hawa atakwama.
 
Huna hoja zaidi ya kukashifu au kukejeli ila nitakufundisha vizuri na nitakuelimisha vizuri sanaaa naona bado unatamani kushindana na Mimi lakini huna hoja yenye mvuto Bali upo kunikashifu lakini nakwambia Mimi ni mtu mwingine

mkuu njaa ni kitu hatari, shikilia hapohapo maana umetoa mpaka namba ya simu. ngoja tukupe ukweli mchungu maana huwezi pata cheo kirahisibila kupambana hata kama ni kwa kujitoa ufahamu na kuchafua watu unaotofautiana nao kiitikadi.
 
Back
Top Bottom