Wanaomhujumu Rais Magufuli hawa hapa

Wanaomhujumu Rais Magufuli hawa hapa

Walio pamoja na Magufuli ni wengi kwa idadi na wana nguvu kubwa kuliko walio kinyume na Magufuli.Wampingao hawatafanikiwa ila wataona mambo yao yakiharibika siku baada ya siku maana wanashindana na mtu ambaye mamlaka zilizomuweka si za wanadamu.
MNA HOFU YA NINI SASA; BY THE WAY ANAJIHUJUMU MWENYEWE
 
Mkuu Jana nlitoa uzi wa demokrasia kwa upana wake zaidi inaonekana haukuisoma kwa kuwa mode iliificha ila nitaandika tena ujifunze maana ya demokrasia naona hauijui kabisaaa
Ningeuona labda ningejua ufahamu wako kuhusu demokrasia otherwise bias zinaweza kutumika kuupindisha ukweli kama viongozi wa dini wanapotumia vitabi vya dini kuhalisha dhambi zao
 
Tunakoelekea mi naona giza tu huku mkiendelea kutuaminisha uongo. Akitokea mtu kaongea ukweli anaonekana mchochezi na mvunjifu wa amani. Tuache unafki wakujipendekeza ili tupate vyeo huku wengi wakiteseka
 
Ningeuona labda ningejua ufahamu wako kuhusu demokrasia otherwise bias zinaweza kutumika kuupindisha ukweli kama viongozi wa dini wanapotumia vitabi vya dini kuhalisha dhambi zao
Ipo siku utaniona na nitakufundisha maana ya demokrasia maana nyie mnaitamka tuu bila kuijua kwa upana wake
 
Yote uliyoyaandika ni sahihi kabisa, Nilichokuwa sijui ni WAFADHILI wa akina Yeriko, Ben na Mtatiro, umenifungua milango ya fahamu.
 
Yote uliyoyaandika ni sahihi kabisa, Nilichokuwa sijui ni WAFADHILI wa akina Yeriko, Ben na Mtatiro, umenifungua milango ya fahamu.
Rudia kusoma vizuri haujelewa kilichoandikwa usikurupuke
 
Naunga mkono kabisa,hao ndo wahujum wa nchi kwa asilimia mia.
Wanaokataa ni mazuzu nyerere huwaita.
kimoja umekisahau tu....
Nacho ni kimoja.
KATIBA.

Mfumo wote wa kuwalea wahujum uchumi ni katiba tuliyonayo.Tungepata katiba mpya itayoondoa malalamiko yanayowafanya walamilike hususan wanasiasa.
Katiba mpya ingeondoa uwezekano wa rais kuwa dikteta kungekuwa hakuna huo unaoita uhujum uchumi.
Makam wa spika kateuliwa na rais.Vip tukipata katiba km ya rasim ya warioba.Watasema?
Au JAJI MKUU kuteuliwa na rais....
imekaaje hapo?

Huoni kweli katiba inaweza kumtengeneza mtu udikteta?KATIBA YETU INATUHUJUM PIA
 
Serikali yenye kila kitu; mgambo, polisi, jeshi la wananchi na fyoko fyoko zote itahujumiwaje?

Ifikie wakati tukiri tu kuwa juhudi haziwezi kuzidi uwezo .
 
Hii sijui tuiite ni hadithi, umbeya au majungu. Unaweza kutuletea majina ya hao walioondoa hela kwenye mabenki kwaajili kuihujumu serikali?
 
Nyie Mnaandika Makala za kujipendekeza Ndio wasaliti wakubwa!! Jiulize umefanya nini Kulikwamua Taifa Lako badala ya kuandika makala zako za kugawa watu!! Je unalipwa na nani??
 
MNA HOFU YA NINI SASA; BY THE WAY ANAJIHUJUMU MWENYEWE

UNAOTA.SISI TUNAITWA KIZUNGU NO FEAR HERE .
kama unabisha tikisa kibiriti uone cha mtemakuni.Magufuli hajaribiwi na mwanadamu yeyoye kama ambavyo Yesu hajawahi jaribiwa na binadamu yeyote ALIJARIBIWA NA SHETANI TU NA SHETANI MWENYEWE YESU alimwonyesha cha mtema kuni
 
You are so biased na hadithi yako! Hutakiwi kuitwa Msomi!! Ila shida iliyopo katika taifa kila mtu anajiona Mchumi sijajua wachumi wa ukweli wamekwenda wapi??
 
unasema wanafanya vikao kwa usiri mkubwa sana,sasa wewe umejuaje? unaendekeza udaku hadi unajiovateki.
 
Ndugu wanajamvi sisi kama wazalendo na wanaharakati ambao sote tunaipigania nchi yetu kwenda kwenye uchumi wa kati lazima tupaze sauti zetu kila Mara kupinga hujuma mbalimbali zinazofanywa na watu Fulani Fulani kuhakikisha RAIS MAGUFULI anakwama lakini kibaya zaidi hawajui hii nchi ni yetu sote na siyo MAGUFULI peke yakee.
Ndugu wanabodi hakika sasa hivi kuna mambo mengi yanayosemwa kwa RAIS wetu kuhusu utawala wake lakini kuna kitu kimejificha nyuma ya pazia ,na huu ni mtandao unaupinga utawala wa awamu ya tano au kwa lugha nyingine wanaomuhujumu RAIS magufuli na hapa wapo watu wa makundi mbali mbali na taasisi mbali ila ngojea nianze kuyachambua kama ifuatavyo;

1: Wafanya biashara ambao walikuwa hawalipikodi;hawa wameunda mtandao wao kwa usiri Mkubwa mno ili kuhakikisha kwa kila namna huu utawala ufe, kwa kuwa walizoea kuishi bila kulipa kodi lakini sasa hivi lazima ulipe kodi kitu ambacho kinawanyima usingizi.Juzi tumesikia kuwa RAIS MAGUFULI analalamika kuna watu wametoa hela benki wameficha nyumbani eti kuzuia mzunguko wa hela inasadikika kuwa kundi hili limo kwenye hii harufu mbaya.

Mfano moja tuu niwape juzi tumemsikia RAIS wa ufilipino Rodrigo Durteze analalamika kuwa anahujumiwa na wafanyabiashara wa madawa ya kulevya waliounda mtandao wao kuhakikisha huyu RAIS anafeli katika utawala wake kwa kuwa alitangaza operation ya kuwanyonga hawa mabwenyenye. Lakini akawa na wakati mgumu kwa sababu huu mtandao ulikuwa mpana sanaaa hadi Marekani ameingilia kati kabisa kwa kigezo cha haki za kibinadamu. Swali ni je Marekani hawajawahi kuwanyonga watuhumiwa wa madawa ya kulevya?

Utakuta ni majibu nyepesi kwenye masuala magumu kama haya ukikaa na kufikiri kwa undani utakuta Kuna maslahi ya watu hapa ndo maana wanaingilia mambo yasiyowahusu kwani nani asiyejua athari za madawa ya kulevya inavoangamiza vijana na vizazi katika taifa. Lakini huyu Rais alipoingia madarakani aliivalia njuga kama MAGUFULI alivyolivalia njuga swala la mafisadi na kulipa kodi.

2: Ni genge la watu Wanaodai demokrasia ambayo hata demokrasia yenyewe hawaijui maana yake, eti kwao demokrasia ni kufanya mkutano wa kisiasa na maandamano ambao hauna faida kwa wananchi. Na hapa ndipo kuna upotoshaji mkubwa unaotaka kugawa serikali na wananchi wake, na viongozi wa hii genge hasa ni MBOWE na MAALIM SEIF ambao kwao demokrasia ni ubavu ndani ya vyama vyao na kutunishana msuli usio na faida kwenye ujenzi wa vyama vyao.

Wamejitahidi kutumia vijana wao kama YERIKO NYERERE,MALISA G,BENSAANANE,JULIUS MTATIRO,katika kuupotosha umma kwenye mtandao wa kijamii kama JF,Facebook na Twiter kuhusu dhana ya demokrasia na wanaenda mbali na kusahau kabisa kuwa wao ndo vijana wa kulisaidia taifa hii kwenda kwenye uchumi wa kati.

Niwasihi hawa vijana waache maramoja kuupotosha umma kuhusu neno demokrasia kama mawazo yao yalivofikia waaache utashi wa kisiasa bali wajenge hoja zenye mantiki ya kutuunganisha sisi wananchi kwenda kwenye uchumi wa kati kwa kuwa Mimi naamini RAIS MAGUFULI angekuwa dikteta wasingetamka hadharani kama wanavolitamka kwa nyakati tofauti Bali huu ni uchochezi wa hali ya juu kuwahi kutokea katika taifa hili.

Kwakuwa hili kundi linasadikika kuwa inapata support kutoka kwenye mtandao wa wafanyabiashara ambao kodi kwao kulipa hawataki na pia inapata support kutoka kwa mtandao wa mabwenyenye wa mataifa ya magharibi wenye mrengo tofauti na RAIS MAGUFULI ambao kwao lengo kubwa ni kutaka kuchuna rasimali zetu na mkakati huu ulianza tokea uchaguzi wa 2015 ambao hawa mabwenyenye wana kiu sanaa na rasimali zetu ndipo wanaungana na mtandao wenye mrengo kama ya kwao wenye kujiita wana demokrasia.

3. Ni taasisi Fulani Fulani zisizo za kiserikali ambao wanatumiwa na wana siasa kwa nyakati tofauti kuja kupotosha umma kuhusu dhana ya demokrasia na utawala wa RAIS MAGUFULI zipo taasisi za kidini na zisizo za kidini kama mnafuatilia mambo kiundani mmemsikia padri Fulani kwa nyakati tofauti amesikika kuupinga utawala wa MAGUFULI hadharani lakini siyo kosa lake ni kosa la waliomtuma.
Hili kundi lina ushirikiano mkubwa na kundi la pili kwa kuwa waga kuna vikao wanafanya kwa usiri Mkubwa na ndipo wakishapewa au wakishaaidiwa vitu Fulani unawasikia wakiropoka bila ata mantiki ya kutuunganisha sisi wananchi hivyo nitoe rai yangu kuvionya hizi taasisi ambao wanashirikiana kwa namna moja au nyingine na hii genge la MBOWE na wenzake kuacha Mara moja kwa kuwa wao ni taasisi bila kujali ya serikali au siyo ya ki serikali kazi yao ni kutuunganisha na si kutugawa na kuleta uchochezi.

4. Baadhi ya vyombo vya habari hapa utakuta kuna media zimenunuliwa na kuna wana habari pia na magazeti yamenunuliwa ili kupambana na serikali ya awamu ya tano juzi tuu ni mfano halisi baada ya waziri NAPE kuvifungia baadhi za station za radio zilizoripoti habari za kichochezi na hili kundi hushirikiana kwa karibu na kundi la pili kwa nyakati na sehemu tofauti.

Kila siku ukisoma gazeti Fulani ambye mmiliki wake ni kiongozi wa chama Fulani utaona na kujiiridhisha kuwa wanapambana na serikali ya awamu ya tano. Rai yangu kwa wanahabari wote kuacha mara moja mambo au kutoripoti kabisa habari za kichochezi zenye mrengo wa kutugawa katika taifa letu pia niwaonye wamiliki wa vyombo vya habari kuacha utashi wa kisiasa kuvitumia vyombo vyao kuripoti au kuandika habari za kichochezi zenye mrengo wa kuligawa taifa letu.

Safari ya kuelekea kwenye uchumi wa kati bado inaendelea:

Ni wako kijana mtiifu,mzalendo na mwanaharakati wa kweli.

SIMON MATO-0762189733.
Unajipaisha kwa kutoa onyo tu?

Wengine huwa wanawafata na kuwapiga hadharani. Ndo malengo yanakamilika!

Huo wa kwako ni uchochezi
Maana hata hao wafanyabiashara hujawataja!
 
Back
Top Bottom