Wanaohama CCM ni vinyago - NAPE

DOMA

JF-Expert Member
Mar 17, 2011
944
365
Nape leo ametoa jina jipya kwa wanaohama ccm kuwa ni vinyago na vinyago haviwezi kuwatisha hilo ni jina la pili ndani ya wiki moja baada ya kuwaita kuwa ni Oil chafu ametoa kauli hiyo alipokuwa anahutubia wakazi wa makambako mkoa wa Njombe.
Mytake na bado atatoa majina mpaka achoke mwaka huu kimenuka kimenuka tu.
Source ITV
 
Nape anasema kinyago ukichonga mwenyewe hakikutishi. Anamaana waanzilishi wa vyama vya cdm,cuf, nccr,cck..... nk wote hawawezi kuiangusha ccm, ameyasema hayo ktk mkutano uliofanyika makambako mkoa wa Njombe leosource:Taarifa ya habari ITV&TBC.
 
Jamani huyo Nape muacheni.
Ni bahati mbaya kwa CCM kwamba kila katibu muenezi wao huwa ni mtu wa ajabu ajabu.

Kwa nini hasemi sababu ya watu wazima wote kuwa wanachama wa CCM miaka ya nyuma? Asije kuwa kama Makamba kushindwa kusema sababu ya kufukuzwa ualimu wake!
 
Kama hatishwi na kinyago kwa nini wameamua kuwafuata CDM Pale CDM square? si walale tu bwana waone nguvu ya kinyago
 
Kwani alitegemea watoke kuzimu au? Yaani jamaa hata hawezi kufikiri!!! Enzi zile kila mtu alikuwa mwanachama wa ccm iwe unataka au hutaki, hupati kazi, huendi chuokikuu, hufanyi lolote la kukuendeleza bila kuwa mwanachama wa CCM sasa alitegemea waanzilishi wasiwe CCM kipindi hicho??
 
Mimi sioni kama katukana, naona katumia nahau hapo wala msimuhukumu. Na anaposema tumetoka CCM sikatai ni kweli ila tatizo linakuja anaposema hatuwezi kuiangusha CCM ndipo ninapokumbuka kuwa yeye ni Vuvuzela kumbe hatumii kichwa katika kuchanganua akipulizwa anatoa sauti tuuuuu ikiwa ya ng'ombe au ya binadamu yeyote Vuvu litaitika tu. Mwambieni carolite inaleta cancer ya ngozi ajitahidi kupunguza
 
nape hujui kabla ya uhuru kulikua na vyama vingi?hata ccm imeundwa na TANU na ASP!akili mgando hiyo
 
Njombe watu wana shida ya barabara, huduma ya afya, umeme, bei ya mafuta ya taa iko juu, soko la mazao ya kilimo hakuna lakini Nape anaona jambo la maana kuzumza ni historia ya vyama vya upinzani! Yaani ametoa Mtaa wa Lumumba kwenda Njombe kuongea hizo porojo? CCM hawana jingine la kuwaambia wananchi?

Tallking of historia ya vyama vya upinzani, Nape anaweza kueleza CCJ, waanzilishi wake nani?
 
Hoja ya nape haina mashiko kwani ikumbukwe kuwa CCM yenyewe ilianza kama TAA baadae ukawa TANU na Baadae ndo ccm,pia mabadiliko ya kisiasa toka mfumo wa chama kimoja kuwa vyama vingi,kutokana na ukasukuku wa ccm wa kuunda madokment yasiyotekelezeka yanayojaza mfuko ya viongozi.Pia ikumbukwe hata ROME empire chini ya kanisa katoliki baada ya kukithiri kwa unyonyaji KING MARTIN LUTHER akaamua kuunda kanisa jipaya,SO NAPE ACHA UVIVU WA KUFIKIRI NA KUKURUPUKA CCM NI SAWA NA GAMBA LA NYOKA ANAYETOA GAMBA NA KUBAKI NA SUMU YENYE MADHARA.HUNA JIPYA NAPE.
 
Kweli hatumii Akili, Nchi yetu ilikuwa ya Chama kimoja tangu 1961... Wote waliotaka Vyama Vingi walikimbilia Nje na walisha poteza Maisha yao.

Wengi watatoka CCM sababu kama yeye Mwenyewe
 
Yeye ndiye kinyago na hajajifahamu.
Chadema inasonga mbele na hajajua ataokoka vipi na fagio la M4C
 
nape leo ametoa jina jipya kwa wanaohama ccm kuwa ni vinyago na vinyago haviwezi kuwatisha hilo ni jina la pili ndani ya wiki moja baada ya kuwaita kuwa ni oil chafu ametoa kauli hiyo alipokuwa anahutubia wakazi wa makambako mkoa wa njombe.
Mytake na bado atatoa majina mpaka achoke mwaka huu kimenuka kimenuka tu.
Source itv
vinyago uchongwa kama hao ni vinyago basi waliovichonga ni wao ccm na vinyago ndio taswira halisi ilivyo katika ccm.
 
Yani ameamua kuwatania ndugu zetu wa Kusini ambao ni wachongaji wazuri wa vinyago na ukizingatia M4C imeshamiri huko hivisasa.
 
hii hina tofauti na ile ya lusinde kule meru, kuwa ni dalili za kushindwa ameamua kutoa matusi tusubiri tuone baada ya kusema atawashikisha ukuta kule mwanza tusubiri tutasikia mengi mwaka huu na kuendelea
 
Kweli ccm inamilikiwa na nape? Hakuna ccm bila nape kweli lichama langu limekufa!
 
Back
Top Bottom