Wanaohama CCM ni vinyago - NAPE

Wanaohama CCM ni vinyago - NAPE

Si ndio hapo sasa.

Huyu bwana anajionyesha ambavyo hajakomaa kisiasa.

Mkuu,a drowning man will clutch a straw, nyinyiem imefilisika fikra afu ndo muda huohuo M4C inakuja kwa magnitude ya ajabu,watafanya nini sasa,yamebaki matusi tu,waache watukane weee sisi zetu sera na elimu kwa umma
 
Nape.unapaswa pia kutuambia waliobaki CCM ni akina nani,hii inaonyesha wazi ya kuwa MFA MAJI HAACHI KUTAPATAPA,kwa hal hii mpaka mwaka 2015 nina uhakika asilimia sabini ya wapiga kura wa nchi hii watakuwa wameshatukanwa sana na wewe nape,na hapo starajii aliyetukanwa kumpa kura aliyemtukana,kwa mwenye akili hii ni dalili ya CCM kuaga watanzania kutoka ikulu kwa staili ya matusi
 
13) Wachumia matumbo
14) Wakandamizaji wa wanyonge
15)
 
Anaenda kuandaa mikutano analalamika utafikiri wananchi ndio wenye mamlaka na mahakama.
Kikwete ni bosi wako mko pamoja kwenye vikao na serikali.
Ni nani hao walioamua kesi za uchaguzi ziishe ndani ya miaka miwili?je ni wananchi?
Nape acha kutuzuga tuna akili sasa.
V8 unalotembelea unajua ni nani kanunua?au unafikiri ni kipindi cha zidumu fikra za mwenyekiti?
 
Nape leo ametoa jina jipya kwa wanaohama ccm kuwa ni vinyago na vinyago haviwezi kuwatisha hilo ni jina la pili ndani ya wiki moja baada ya kuwaita kuwa ni Oil chafu ametoa kauli hiyo alipokuwa anahutubia wakazi wa makambako mkoa wa Njombe.
Mytake na bado atatoa majina mpaka achoke mwaka huu kimenuka kimenuka tu.
Source ITV

Hata akina Ghadafi na Gbagbo walipoona maji yamewafika shingoni, walikuja na kauli za namna hii. People's power!!!!!!!!!!
 
Nape leo ametoa jina jipya kwa wanaohama ccm kuwa ni vinyago na vinyago haviwezi kuwatisha hilo ni jina la pili ndani ya wiki moja baada ya kuwaita kuwa ni Oil chafu ametoa kauli hiyo alipokuwa anahutubia wakazi wa makambako mkoa wa Njombe.
Mytake na bado atatoa majina mpaka achoke mwaka huu kimenuka kimenuka tu.
Source ITV

Au labda ni mende na panya kama waliokuwa wakimpinga Gadaffi
 
Deffensive ya ccm imepwaya kwa hiyo chadema wanafunga hata magoli ya mbali
 
Nape leo ametoa jina jipya kwa wanaohama ccm kuwa ni vinyago na vinyago haviwezi kuwatisha hilo ni jina la pili ndani ya wiki moja baada ya kuwaita kuwa ni Oil chafu ametoa kauli hiyo alipokuwa anahutubia wakazi wa makambako mkoa wa Njombe.
Mytake na bado atatoa majina mpaka achoke mwaka huu kimenuka kimenuka tu.
Source ITV

Aendelee kuyatoa tu tutayatunza mwaka 2015 tutamkumbusha na matokeo ya vinyago na oil chafu yatapatikana kwani hakuna haja ya kubishana nae kwa mameno bali vitendo!
 
Si busara kwa mwanasiasa yeyote yule kutukana wapiga kura. Kwa namna hiyo, hata wale ambao ni wanachama wanaweza kukerwa na matusi ya mwanasiasa huyo na kuamua kukiacha chama.

Si anajua dawa yao ni ubwabwa, kanga na kepu ndo maama kuwatukana haoni tabu!
 
Nape najua ni kijana mdogo ambaye anajipambanua kama kijana wa wakati huu. Mwanasiasa anayedai amejijenga kwa nguvu zake mwenye, wakati mwingi akidai wazee ndio sababu ya kuzorota uchumi na kuanguka kwa maadili makubwa ya uongozi.

Nape amekuwa kijana ambaye anathibitisha elimu, maadili, utu na heshima kwa watu anaotaka kuja kuwaongoza hana. Nape anatakiwa atafakari sana kwa nini ameshindwa kuchaguliwa hata na kundi dogo la wanachama wake kupeperusha bendera ya chama chake Ubungo-Ulimi wenye dharau, sifa, majivuno, kujiamini kupindukia na sasa kuwatukana watanzania.

Nape unasema leo vinyago ndio wanatoka CCM, umewahi kutumia maneno kama kushikishwa ukuta, ukanda, ukabila nk. Naona inakubidi urudi shule usome nini maana ya kuwa kiongozi wa umma kiongozi unayetegemea kuongoza watu, mwana siasa wa kizazi cha sasa karne ya 21 na kuendelea.

Ulimi kaka utakuponza sana, kuliko hata hao wazee unaowaona hawana akili.

Najua utajisikia vibaya, lakini ninyi hamuharibu tu chama chenu mnataka taifa la matusi, dharau na udhalilishaji. Ukijaribu kuangalia maneno unayotumia wewe , Wasira, Lusinde, Nchemba nk yanasikitisha sana.

Watanzania hawatakubali kutukanwa kwa sababu yeyote ile. Ni haki ya mtanzania kuwa CUF, TLP, CCM, CDM, TADEA Nk na kupewa heshima na haki yake. Hakuna mtanzania kinyago hata kama serikali ya CCM imenyima haki zake za msingi ili imeone kinyago. Ukinyago wa watanzania ni wakutengeneza ndio watanzania wanaonekana vinyago wanapodai, shule bora, maji, barabara, huduma bora za afya maisha bora na utekelezaji wa makusanyo ya kodi zao.

Nape siasa sio matusi

Chief Mkwawa wa Kalenga- Ukiishiwa sera hutukana-ndio kauli za kushindwa
 
Dogo hana ujanja, na sera hana sera.
 
Si busara kwa mwanasiasa yeyote yule kutukana wapiga kura. Kwa namna hiyo, hata wale ambao ni wanachama wanaweza kukerwa na matusi ya mwanasiasa huyo na kuamua kukiacha chama.
Kwa Mheshimiwa Nape maneno kama "wanashika shika ukuta, Oil chafu, vinyago na mengine mengi atakayo yaibua yatakuwa ya kawaida. Uzuri ni kwamba yanaashiria kitu kimoja tu, kuanguka kwa CCM. Na sasa naaza kuona kuwa wanasiasa wengi wa Africa hawapendi kabisa kupingwa; kwa maana kila atakaye wapinga, mara utasikia ni wahuni, ni panya, ni watu wa kariakoo. CDM kaza kamba wanakaribia kuhema.
 
Mchambuzi umenenaa!!! kumbe CCM bado imebakiza watu kama wewe?! au uko peke yako!!
 
Nape, sina mamlaka ya kukulaani ila nasema: Watu wanaondoka CCM kwa sababu ya ufisadi na mateso mnaotufanyia. Mmetuibia kwa miaka mingi na sasa tumeamua kutafuta njia nyingine maana nyinyi ni mbwa mwitu katika ngozi ya kondoo. Wewe unatuita sisi tulioamua kutoka katika kundi la mbwa mwitu na wewe unatuita sisi viumbe wa Mungu vinyago. Sisi tutaendelea kuwa binadamu ila wewe uliyetuita sisi vinyago naomba, mapigo yaliyoandikwa katika maandiko matakatifu yawe juu yako. Maana Mungu anasema usikifananishe kitu chochote alichokiumba Mungu na kinyago.
Ee Mungu tuangalie, watesi wetu wameanza kutuita sisi vinyago.
 
nduyangu kwanzaheshima kwako huondio ukweriambaounapashwa usemwekwasauti kubwasana.ccm wameishiwasera zakuongoza taifa nivigumu kutofautisha kaulizao na zamateja maanapamoja na maneno yaliyosemwa na lusinde hayatofautishwi na maneno ya mateja na hakuanzia hapotu pia aliwahikusema bungeni ati wabungewa wapimweakiri akiimanisha kutofautianakwahoja kwa ccm(wegi) na wabunge wa chadema je? kamakweri harikuwatusi kama angetofautiana na babayake angeweza kusema baba kapimwe akiri,mama kapimweakiri mh.spika kapimwe akiri.Hiyonikuonesha kwamba ccm hawawezi hatakukemeana matusi kwawapinzani nisawa siyo kwawana ccm.JENISAWA
 
Chifu pole sana kama unaipenda CCM lakini hao uliowataja na Nape na wengine wengi wao ndio wenzako!.
Waliogundua wanahama.
Maana utaambiwa una wivu wa kike!.
 
mimi sioni kama katukana, naona katumia nahau hapo wala msimuhukumu. Na anaposema tumetoka ccm sikatai ni kweli ila tatizo linakuja anaposema hatuwezi kuiangusha ccm ndipo ninapokumbuka kuwa yeye ni vuvuzela kumbe hatumii kichwa katika kuchanganua akipulizwa anatoa sauti tuuuuu ikiwa ya ng'ombe au ya binadamu yeyote vuvu litaitika tu. Mwambieni carolite inaleta cancer ya ngozi ajitahidi kupunguza

mwacheni atukane tu
 
Back
Top Bottom