Wanaohama CCM ni vinyago - NAPE

Wanaohama CCM ni vinyago - NAPE

Nape majuzi alikuwa nyumbani kwao. Katika pita pita akakutana na Makonde mmoja aliyekuwa anauza vinyago. Alivutiwa sana na kinyago kimoja kilichokuwa kinafanana na panya, na kilichochongwa kwa ustadi kiasi ya kwamba hata manyoya ungedhani ni yenyewe; wacha kichwa, miguu, mkia na vingine. Akamwuliza huyo Makonde anauzaje hicho kinyago. Akaambiwa ni shillingi mia tano na mtu akisha kinunua hakirudishwi. Nape akaona hiyo ni bei poa kwani ni kama bei ya soda. Alilipa akaondoka nacho.

Hajafika mbali, maajabu yakaanza kutokea. Kila aina ya panya wakaanza kujitokeza majumabani , vichakani, mashimoni ana kwingine wakimfuata Nape. Akaingiwa na woga na kuanza kukimbia. Lakini wapi. Panya waliongezeka na kuongeza kasi yao. Woga ulimzidi huku akijiuliza afanye nini.

Hapo alipokuwa ni karibu na Mto Ruvuma. Basi akakikimbia kuelekea huko na panya walikuwa bado wanamfuata na wakiongezeka. Kufika kwenye kingo za mto huo mkubwa, ailikitupa kile kinyago majini na hapo ndipo maajabu yalipotokea. Wale panya wote waliokuwa wakimfuata, walikifuata kile kinyago huko majini, wakazama nakufa.

Kuona hayo, Nape ilikuwa ni kama amepatwa na wazimu. Aliondoka kwa kasi mithiri ya farasi, akielekea kwa yule Makonde. Mara kufika Makonde akawa mkali.

“Nilchema chirudishe”
“Tulia Baba. Una kinyago kinachofanana na Dr. Slaa. Nataka kwenda nacho Igunga”
“China. Tena nakwambia china kabisa”
Nape alizimia papo hapo.
 
Eti yule Profesa wao wa kutukana matusi atakuwemo? nasikia ameyatengenezea chorus kwa kesho atatoka ya yapi?
 
Nape ni Great thinker wa CCM,kabobea katika siasa za uenezi.
Nasubiri neno lingine leo na usisahau na mafisadi akina Maige au jina lao hujalipata?
 
Wakati mwingine najisikia kukoshwa na juhudi zisizo za kawaida za Nape kuipigania CCM. Kama alivyosema Mwalimu kuwa inabidi uwe mwendawazimu kuutetea ujamaa, hali hiyo inaweza kusemwa pia kwa CCM. Tukubali, nape ana kipaji maalum - hata kama kinaonekana majitaka kwa wengine. Swali gumu ni kuwa ndani kabisa ya nafsi yake hasa anaionaje hali halisi ya CCM ilivyo sasa na mparaganyiko unaokiandama bila simile? Manake hata "wenyewe" wenye chama chao wamejiweka kando wakipima upepo tu na kutoa kauli/majibu ya rejareja kujaribu kuzima mioto inayojitokeza hapa na pale. Hawana nia ya dhati ya kuimarisha chama wala kutimiza wajibu wao kwa wananchi - na hawajali wala hawajitokezi kumuunga mkono kwa nguvu na waziwazi katika juhudi zake za kukipodoa chama. Kama vile ameachwa awe "target" wakati wakulu wanapima upepo!
 
Jamani kumwabie nape hatumii akili ni kumwonea, naomba tuache. Akili mnazomshupalia azitumie hana, atafanyaje??

:laugh: lakini nyie jamani...:laugh: , mi chimo mwe, this's too funny! :laugh:....you made ma friday!
 
Hatuko hapa kutukanana ninaogea kitu mimi kama mimi. Huu ni ujinga inabidi tubadilike wote. Hawa CDM nao wanatafuta kitu. Je hata hicho kidogo walichopata wamesaidia nini jamii. Hatakujenga kinyumba cha mwalimu tu! acha kutukana bwana toa pointi sisi ni wasomi sawa?
Ninamashaka sana na elimu yako na upeo wako wa kufikiri na kujenga hoja. Hunan lolote la maana zaidi ya kutetea umagamba wako hapo. Umejifanya kuja na gia ya kutoegemea chama chochote wakati unaonyesha kabisa unachuki binafsi na cdm.

Ungekuwa na akili ungetambua kuwa cdm wanasambaza elimu ya uraia kwa wananchi na kuwaelimisha juu ya umuhimu wa katiba mpya. Sasa ulidhani kazi ya vyama vya siasa ni nini? Na kazi ya ruzuku ni nini?

Acha unafiki na umagamba wako. Unaonekana kabisa unafaidika na ccm kuwepo madarakani ndio maana unachukizwa sana na hizi harakati za cdm. Mkafie mbele huko.
 
Kumekuwa na mfululuzo wa kauli zisizo na heshima wala malengo ya kujenga nchi yetu ya Tanzania kutoka kwa katibu wa itakadi na uenezi wa CCM bwana Nape nnauye.

Mengi ameyasema toka kipindi kirefu ila kwa wiki mbili hizi kuna maneno aliyoyatoa kwa wanachama walioihama CCM yaani walioamua kuwa gwandalised na kukataa kuwa gambalised na mfumo wa CCM.

Tunakuomba na nijukumu lako pia bwana Nape kuja humu na kutuambia ili tupate kutambua oil safi iliyobaki CCM ni ipi?Maana oil chafu umeshaiweka wazi kwa mujibu wa akili na upeo wako.

Nawasilisha.
 
Oil safi ya kwanza labda yeye(Nape).
The unseen is illutrated by the seen.
 
Kwani kazi ya Oil kwenye injini!

Dr. Slaa alikuwa Oil Chafu tukaiweka kwenye Injini yetu CHADEMA. hatujaongeza STP wala nini! Injini inavyofanya kazi wadau si mnaiona!
 
Kumbe huyu jamaa pia ni mcheza shoo??
3.JPG
Hamna kitu! Wenzake wameweka mguu wa kulia mbele yeye wa kushoto!. Anakiangusha chama chao
 
Arusha tuliitwa panya na ocd Zuberi ikaundwa tume ya kumchunguza mpaka leo kimya...mwanza waliambiwa atawashika ukuta baada ya kumzomea, aliwahi kusema hawezi kuhamia chama cha wachaga, akawaita wanao hamia chadema mizingo mara oil chafu mara vinyango kesho sijui atawaita je..ikumbukwe huju ni kiongozi wa kitaifa ambae raisi aliwahi kusema sauti ya nape ni sauti ya kikwete inamaana maneno ya nape na matusi yte yana baraka za JK..

Sikilizeni watanzania,miaka ya tisini na mwanzoni mwa elfu mbili ccm walisema wapinzani wanamatusi wasisikilizwe.Hivyo kwa kuwa ccm ya sasa ina matusi hatuna budi sisi watanzania kuto wasikiliza viongozi wote wa ccm.MWAKA 2015 NI MBALI SANA.
 
Ninamashaka sana na elimu yako na upeo wako wa kufikiri na kujenga hoja. Hunan lolote la maana zaidi ya kutetea umagamba wako hapo. Umejifanya kuja na gia ya kutoegemea chama chochote wakati unaonyesha kabisa unachuki binafsi na cdm.

Ungekuwa na akili ungetambua kuwa cdm wanasambaza elimu ya uraia kwa wananchi na kuwaelimisha juu ya umuhimu wa katiba mpya. Sasa ulidhani kazi ya vyama vya siasa ni nini? Na kazi ya ruzuku ni nini?

Acha unafiki na umagamba wako. Unaonekana kabisa unafaidika na ccm kuwepo madarakani ndio maana unachukizwa sana na hizi harakati za cdm. Mkafie mbele huko.

Wewe nawe hujanielewa mimi sipendi kabisa mahali tupo sasa ninataka maendeleo si ya kuongea ongea tu. Iwe CDM au CCM. Mimi nimepigia kura CDM lakini kinachonishangaza sasa hivi sioni faida yoyote. Zaidi ya kutafuta sifa tu kwenye majukwaa. Huo ni mtazamo wangu. Sawa jamani?
 
hata vichaa hawakuanza siku moja,nape amechanganyikiwa kabisa,masikini siku zote ni vinyago kwa akiri za matajiri.mafisadi wanahaha,subiri dawa yao iko kitchen inachemka.
 
Duh! Hao vinyago wanaozidi kupungua bila kurejea/kufanya mikakati ya kuongeza vinyago wengine wapya, yeye haoni ni pigo kwa chama. Kwa kweli ulevi wa madaraka ni noma!
 
Back
Top Bottom