Sasa hivi kuna miradi gani mikubwa inayoendelea katika Taifa letu? Tulizoe, wakati wote huku kuna mamia ya kilometa za lami zinajengwa, kule daraja la Kigamboni, kule bomba la gas, kule hospitali ya moyo, kule ujenzi wa daraja, huku chuo kikuu UDOM, huku ujenzi wa barabara ya mabasi yaendayo kasi, n.k. Sasa hivi ni miradi gani mikubwa inayoendelea nchini? Maana inawezekana kuna miradi mikubwa inaendelea kwenye baadhi ya maeneo ya nchi lakini watu hatupewi taarifa!
Yalipokuwa yanafanyika hayo, tuliona ni machache na madogo mno, tulitarajia serikali hii ije na mambo mengi zaidi na makubwa zaidi.