Mleta mada umeongea kwa kujiamini kama unayejua vitu kumbe huna lolote.
Je, unajua kama kuna makandarasi wamekabidhi kazi kwa serikali na serikali za mitaa (Halmashauri) tangu Agosti 2016 lakini hadi leo hawajalipwa.Kila wakifuatilia wanaambiwa akaunti hazijaingiziwa pesa?
Je, unajua kama zaidi ya 70% ya miradi ya maendeleo katika bajeti ya mwaka huu akaunti zake hazina hata senti tano?
Je, kwanini serikali imeshindwa kukopesheka huko nje inataka kukopa katika benki za ndani?Hoja yako ya kuogopa kuwaongezea mzingo watz ni dhaifu sana.Mikopo ya taasisi kubwa za kifedha nje ya nchi riba zake ni chini ya 6% wakati benki zetu ambazo serikali inataka kukopa riba zake ni zaidi ya 12%.Hiki ni kiashiria kuwa huko nje wamenyimwa kukopeshwa.
Je, Kama nchi bado ina fedha za kutosha,nini sababu ya kutopandisha watumishi madaraja pamoja na nyongeza ya mshahara ya kawaida?
Je, kwanini serikali ibane matumizi kupita kiasi na tusione huduma au maendeleo ambayo huko nyuma hatukuwahi kuyaona? Tumeshuhudia kuondolewa kwa watumishi hewa, kuondolewa kwa posho ,kukataza safari za nje,kuondoa semina na hafla .Lakini cha kushangaza madawa hosoitalini hali mbaya, mikopo kwa wanafunzi hali mbaya, kutoajiri ,akiba ya fedha za kigeni BOT imeshuka kuliko kawaida n.k bado unataka tusema hali ya uchumi ni shwari!!