Wanao Pora Fedha na Mali za Marehemu kwenye ajali

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2016
Posts
17,016
Reaction score
26,192
Ajali ya mtu wangu wa karibu ilitokea Korogwe, michungwani Tanga miaka 4 iliyopita. Wale wakaazi wa Pale , ilikuwa saa 11 alfajiri, wakafika wakapora simu, pochi , begi na kadhalika, yule mtu wangu akafia muhimbili baada ya wiki moja, alifia ICU.

Ndugu zangu wa Michungwani pale Tanga, hivi mnajisikiaje kula hela yenye damu?
Mnawezaje kupora mgonjwa mahututi na kula hela na wake zenu kitanddani mkiwa uchi?

Ajali ya Same juzi jumamosi, watu wameungua, manusura wanakwambia watu wamekuja kupora hela na hawa hangaiki na kuokoa watu, wote wanaodhulumu na kula fedha zenye damu, laana hiyo itakula viziza vyao mpaka cha nne.
 
Hakuna mijitu mipumbavu kama mitanzania,hapohapo ikisikia kelele za mwizi,mwizi itakusanya mawe kwenda kuponda na kutia tairi na petroli..Kweli hii ni miongoni mwa nchi ambazo raia wake wana kiwango kidogo cha IQ
 
Imekua kama Kawaida hiyo kwenye ajali watu wanaibia sana maiti, kuna ajali ya Bus na lori ilitokea veyula Dom mwaka 2022 kondakta na watu kama 6 walifariki waliokua wamekaa pale mbele kwenye godoro , jamaa walimsachi kondakta wakamuibia pesa 500k+
 
Kuna dereva mwenzetu Lori ilihama njia kidogo...wana kijiji wakamvamia analia anaomba msaada...raia wako busy kuiba mizigo......kama haitoshi wakamkimbiza na kumuua......
Unyama huu umeletwa na hali ngumu ya maisha iliosababishwa na ccm kuachia umaskini wa kutisha huku kuna wale wasiolipa kodi na mishahara minono. Tofauti ya kipato i kubwa sn.
 
Yaani wewe kila kitu ni CCM!?? Roho mbaya haina chama. Uporaji sio Tanzania tu.. pata ajali kwenye karibu nchi zote kusini mwa jangwa la Sahara uone kitachotokea... kuna mambo mengine ni ya mtu binafsi zaidi haina uhusiano na CCM wala chama kingine cha siasa. Watu waliteketea kwa moto Morogoro ila hadi leo gari la mafuta likipinduka watu huenda kupora mafuta
 
Kweli baadhi yetu watanzania ni viazi kabisa yaani, hatuna chembe ya aibu ndiyo maana na ccm wana tuona kama matako Yao.
 
Unyama huu umeletwa na hali ngumu ya maisha iliosababishwa na ccm kuachia umaskini wa kutisha huku kuna wale wasiolipa kodi na mishahara minono. Tofauti ya kipato i kubwa sn.
Yaani wewe kila kitu ni CCM!?? Roho mbaya haina chama. Uporaji sio Tanzania tu.. pata ajali kwenye karibu nchi zote kusini mwa jangwa la Sahara uone kitachotokea... kuna mambo mengine ni ya mtu binafsi zaidi haina uhusiano na CCM wala chama kingine cha siasa. Watu waliteketea kwa moto Morogoro ila hadi leo gari la mafuta likipinduka watu huenda kupora mafuta
Sijui ulimsoma mdau ukamuelewa?wakati mwingine tenganisha siasa na uhalisia.

Hali ngumu husababisha kiumbe kukosa utashi wa hekima na busara,sera mbovu za vyama tawala ndiyo husababisha hizo hali ngumu kwa wananchi lazima ulikubali hilo,hapo chini umemaliza kwa mfano dhahiri kabisa namna hali ilivyo ngumu ktk wanaoenda kuchota mafuta humkuti mtoto wa mkuu wa mkoa wilaya ded wala das kwa sababu baba na mama zao wapo kwenye chain ya ulaji ya ccm utakuta ni hao hao maskini waliokosa nyuma wala mbele.
 
Yaani wewe kila kitu ni CCM!?? Roho mbaya haina chama. Uporaji sio Tanzania tu.. pata ajali kwenye karibu nchi zote kusini mwa jangwa la Sahara uone kitachotokea... kuna mambo mengine ni ya mtu binafsi zaidi haina uhusiano na CCM wala chama kingine cha siasa. Watu waliteketea kwa moto Morogoro ila hadi leo gari la mafuta likipinduka watu huenda kupora mafuta
Hata wewe naamin ushapora fedha maiti.
 
Hakuna mijitu mipumbavu kama mitanzania,hapohapo ikisikia kelele za mwizi,mwizi itakusanya mawe kwenda kuponda na kutia tairi na petroli..Kweli hii ni miongoni mwa nchi ambazo raia wake wana kiwango kidogo cha IQ
Umewahi kuibiwa?

Tuanzie hapo kwanza
 
Umeandika nn sasa? Kwa hiyo kama umewahi kuibiwa?
Umewahi kuibiwa Mali yoyote .?

Pengine hujawai kuibiwa na hujui kadhaa ya kuibiwa Mali.

Aliyesema mwizi akatwe mikono hakukosea

Tia kiberiti wezi wote.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom