Wanandoa wengi wanavaa pete lakini je, wajua kwanini wanavaa na maana yake ni nini?

Mwananchi wa chini

JF-Expert Member
Jul 23, 2013
227
597
Wakristo wengi au watu wengi tumekuwa tunaiga mambo mengi bila kutafuta kujua nikifanyacho ni nampendeza Mungu au ndio fashion tu za kila Siku kuiga??

Wengi watasema mbona wanandoa wanavaa Pete lkn je wajua kwann wanavaa na maana yake ni nini??

Wengi watajibu ni kuwa muaminifu au kwamba tayari umesha kuwa milki ya MTU mwingine so ajaye kwako tena akiiona aruke asikuguse kwakuwa umekuwa booked already

Jaman pete sio msingi Wa imani kwa wanaopenda au wanaotamani kumuona Mungu, na Pete sio kizuizi cha MTU kuwa mwaminifu maana wengi wao wanazo na wanazivua wakitaka kuvunja huo uaminifu wakimaliza wanazivaa na wavalishaji wanaendelea kuamini kweli mwenzi wake bado ni mwaminifu.

Na kipindi cha sasa wengi wakiwa nazo ndio wanatafutwa sana na wasiovaa either mwanaume akionekana kaoa amevaa ile Pete wanawake sasa ndio hawaogopi kabisaaa na wanawake walioolewa wakionekana na hizo Pete wanaume Wa sasa ndio shangwe hawawaogopi wanaona hawa ndio wanaofaa kuutimiza machafu yao.

Nisielezee sana Ila nakupa hii hapa usome na ujue unachokivaa kinampendeza Mungu au ndio vazi mojawapo LA shetani

Kumekuwa na maswali mengi juu ya chanzo hasa cha pete hiyo inayotumiwa katika harakati za ndoa’.

Wale walio na matazamo hasi juu ya matumizi ya pete, wamekuwa na sababu mbalimbali za kutetea msimamo huo hasa ni ile sababu kuwa “pete inafanya wazo la upendo kuwa la kinadharia” na ushahidi wa nje kuliko kuwa na chimbuko halisi la upendo wa ndani ya moyo. Lakini katika makala hii tutaona kwa kina juu ya historia halisi pete.

Pete ya ndoa ilianzishwa na watu wa Farao” Firauni” nchini Misri.
Historia inaonyesha kuwa karne ya 14, BC (kabla ya kristo), katika nchi hiyo ya Misri iliyo kaskazini mwa Afrika, watu wanchi hiyo chini ya mfalme wao Farao’ walianzisha utamaduni wa kuwekeana viapo vya uaminifu katika mahusiano yao ya kimapenzi na ndoa kwa kutumia pete.

Wananchi walilazimika kwenda kwenye ukingo wa Mto Nile ambapo huko walifanya matambiko ya kipagani na kuwekeana viapo vya uaminifu. Sherehe hiyo iliambatana na kuvalishana pete yenye umbo la duara baina ya mke na mume kwenye vidole vyao vya mkono wa kushoto.

Lengo, Maana yake’
Kwa kufanya hivyo wapagani wa Misri waliamini kuwa wameweka kiapo na ahadi ya kuto salitiana ambapo pia ilifuatiwa na kumvalisha mwanamke mkufu wa fedha na dhahabu au chuma kiunoni.
Umbo la duara la pete liliundwa hivyo kuashiria kuwa kifungo hicho cha ndoa ni cha milele kwa maisha yote.

Umbo la duara la pete na upagani’
Umbo hilo la duara la pete liliashiria imani kuwa viapo hivyo vilishuhudiwa na miungu miwili ya wamisri yaani mungu Jua’ na Mwezi ambao alama zake zilikuwa ni umbo hilo la duara la pete.

Pia uwazi huo wa pete “duara ya kati” ilimaanisha kuwa ndiyo mlango wa kuingilia katika maisha ya ndoa” na yakuwa ndoa hiyo na familia ijayo vinalindwa na miungu hiyo Jua’ na Mwezi daima.

Eneo la kuvaa pete na chimbuko lake’
Uamuzi wa kuvaa pete kwenye “kidole” kinachoitwa cha “Pete” ulifanyika kutokana na ushauri wa watalamu wa Sanyansi ya maumbile ya mwanadamu.

Wataalamu hao waliamini kuwa mshipa mkuu wa damu unaogawa damu mwilini toka moyoni (vein) unaunganika moja kwa moja na kidole hicho, hivyo pamoja na elimu ya kinajimu iliyotawala wakati huo bado ilishauriwa kuwa pete hiyo ivaliwe katika kidole hicho.

Kuenea kwa tendo hilo la uvaaji pete
Utamaduni huu wa kuvaa pete ulianza kuenea duniani baada mfalme Alexander, kuvamia nchi ya Misri, ambapo mambo yalovutia utawala huo ni pete ya ndoa.
Baadae Wagiriki walichukua utamaduni huo na kuubadilisha kidogo huku wakiwa na hofu ya kuwaudhi miungu hao Jua na Mwezi.

Miongoni mwa mambo yalofanywa kuhamasisha matumizi ya pete hiyo ni tendo la kuibadilisha jina na kuiita pete hiyo jina la kigiriki “evena amoris” yaani mshipa wa penzi” na kuruhusu itengenezwe kwa matirio tofauti kama pembe za ndovu, mifupa ya miguu, ngozi za wanyama nk.

SWALI:

Leo hii watoto wa Mungu wamechukua ibada hiyo’ na kuiweka katika maisha yao??????

“Unapovaa pete’ fanya ukijua kuwa haina chimbuko utakatifu’

KWA UFUPI:

Pete ya harusi haina maagizo au utakatifu wa Kibiblia. Inapata asili yake katika kipagani, ambayo ni kinyume na Mungu.

Pete ya harusi ni amri ya ulimwengu. Mungu anasema hatutakii maagizo ya dunia.

Pete ya harusi inaashiria ishara ya uongo ya muungano usio na mwisho, wa milele. Mungu anasema kwamba muungano wa ndoa ni kwa muda tu ni mpaka kifo kitutenganishe

Pete ya harusi ina kinga kidogo na ya kudumu chini ya mtihani.

Kuvaa kwa pete ya harusi ni hatua ya kwanza kwa watu wengi katika kuvaa aina zote za mapambo mengine ya Biblia yaliyokatazwa.

Pete ya harusi si sehemu muhimu ya kanuni za Biblia.


Baadhi watalalamika, "Lakini yangu au" Kanisa langu limeongeza mazoezi haya kwa miaka. Kwa kweli, karibu sana uondoke katika kudanganywa huko utapotea vua mapete hayo iwe Pete kidoleni,puani,masikioni n.k uliyonayo mfuate Yesu.
 

Attachments

  • ring.jpg
    ring.jpg
    23.2 KB · Views: 148
  • ri.jpg
    ri.jpg
    19.7 KB · Views: 126
Kuna wakristo wanasema kusuka nywele ni dhambi,kuvaa mikufu na hereni ni dhambi,kuvaa mavazi mazuri yanayovutia ni dhambi,cheki huyu naye anasema kuvaa pete ni dhambi lakini watu wa zamani kama Rebeka mke wa Isakaalivishwa pete na vito vingine vya urembo.
Ukristo wa sasa kwa wingi umelenga kuwafanya watu wawe watumwa na washamba kwa mihemko ya viongozi wa makanisa fulani
kama pete ni dhambi basi wakristo wote wamepotea na moto unawasubiri maana makanisa yote watu wanavaa pete(labda uko kwenu)
Mwisho:msimamo wangu ni mmoja mke wangu atavaa pete heleni na vito vyote mimi pia pete navaa
Ifike mahali tukatae utumwa wa dini hii tutafanywa misukule tukiwa hai
 
Mtume Paulo anasema, yamkini wako ma bwna wengi wanao abudiwa lakini sisi tunaye bwna mmoja yaani Yesu kristo, yamkini kuna miungu wengi wanao abudiwa lakini sisi tunaye Mungu mmoja, hvyo, hiyo miungu jua cjui mwezi cc hatitambui
 
Katika Biblia tuanza
Luka 15:22 Lakini baba yake akawaambia watumwa, ‘Leteni upesi kanzu bora zaidi na kumvika, pia mvisheni pete mkononi na viatu miguuni.

Unataka kuniambia Yesu alikuwa hajui unachosema wewe hadi akatumia kwenye mfano wake?
Ayubu 42:11 Ndugu na dada zake wote pamoja na rafiki zake wote wa zamani wakaja kwake na kula pamoja naye nyumbani mwake. Wakampa pole na kumfariji kwa sababu ya mateso yote ambayo Yehova alikuwa ameruhusu yampate. Kila mmoja wao akampa kipande cha fedha na pete ya dhahabu.

Ayubu naye alikuwa hajui hicho?

Hagai 2:23 “‘Siku hiyo,’ asema Yehova wa majeshi, ‘nitakuchukua, mtumishi wangu Zerubabeli mwana wa Shealtieli,’ asema Yehova, ‘nitakufanya kuwa kama pete ya muhuri, kwa sababu nimekuchagua wewe,’ asema Yehova wa majeshi.”

hagai hakujua chanzo hicho pia?

Kutoka 35:22 Nao wakaendelea kuja, wanaume pamoja na wanawake, kila mtu aliyekuwa na moyo wa kutoa kwa hiari akaleta bizimu, vipuli, pete, na vito vingine, kutia ndani vito vya dhahabu vya kila aina. Wote wakamletea Yehova matoleo yao ya dhahabu.



acheni kupotosha watu!
waisraeli hakuja pia?
 
Wapi Biblia imetaja Mahali
STORI KAMILI SOMA SURA NZIMA YA MWANZO 24 UTAELEWA HAPA NAKUPA KAMSTARI KADOGO TU ILI UJUSOMEE MWENYEWE

MWANZO 24
.* 51 Rebeka ndiye huyu hapa. Mchukue uende, na awe mke wa mwana wa bwana wako, kama Yehova alivyosema.” 52 Mtumishi wa Abrahamu aliposikia maneno yao, mara moja akainama chini kifudifudi mbele za Yehova. 53 Na mtumishi huyo akaanza kutoa vito vya fedha na dhahabu na mavazi na kumpa Rebeka, naye akampa ndugu yake na mama yake vitu vyenye thamani.
 
Msabato umefulia lini MTU aliyevaa Pete ameanza abudu huyo mungu jua.. Yani wasabato na hekaya za elen g white ni uzezeta wa qnet
 
Kristo mwisho wa sheria! Yani kumtumikia Mungu inakuwa kama adhabu eti watu waishi ki primitive ili uwe mtakatifu! Hamna hiyo bwana ukiona sehemu sheria zimezidi kuliko NEEMA na Imani hapo ujue hakuna Yesu
Kuna wakristo wanasema kusuka nywele ni dhambi,kuvaa mikufu na hereni ni dhambi,kuvaa mavazi mazuri yanayovutia ni dhambi,cheki huyu naye anasema kuvaa pete ni dhambi lakini watu wa zamani kama Rebeka mke wa Isakaalivishwa pete na vito vingine vya urembo.
Ukristo wa sasa kwa wingi umelenga kuwafanya watu wawe watumwa na washamba kwa mihemko ya viongozi wa makanisa fulani
kama pete ni dhambi basi wakristo wote wamepotea na moto unawasubiri maana makanisa yote watu wanavaa pete(labda uko kwenu)
Mwisho:msimamo wangu ni mmoja mke wangu atavaa pete heleni na vito vyote mimi pia pete navaa
Ifike mahali tukatae utumwa wa dini hii tutafanywa misukule tukiwa hai
 
kumbe ili asisiwa na farao ... safi Sana " Though Mimi ni melelewa na wazazi wenye imani ya kiislam " Ijapo kuwa mimi mwenyew imani yangu ni haba kuhusu dini hizi mbili zilizoletwa na hawa watesi wetu (waarabu na wazungu)

lakini mkuu naomba nikushukuru kwa hili bandiko lako ..Namimi ukifika wakati wangu wa kuoa nitaivaa hiyo pete na kumvisha mwenzangu pia ..kwa minajili ya kumuenzi farao .. Maana farao hakuwa mtu mbaya kama namna ambavyo tuna aminishwa kwenye hiyo misahafu yenu"..
Farao ni kiongozi Ambaye alifanikiwa kwa kiasi kikubwa kuitangaza africa na kuiachia urithi mkubwa sana Anna Mpaka leo bado unainufaisha ..

. Wazungu na waarabu wanampinga haswaa kwa kuwa alikuwa mtu mwenye nguvu na ambaye alikuwa na utawala uliochochea maendeleo makubwa sana kuliko wao"....,So wakaamua kusafiri na ule msemo usemao ukitaka kumuua mbwa wako basi mpe Jina baya
 
Kuna wakristo wanasema kusuka nywele ni dhambi,kuvaa mikufu na hereni ni dhambi,kuvaa mavazi mazuri yanayovutia ni dhambi,cheki huyu naye anasema kuvaa pete ni dhambi lakini watu wa zamani kama Rebeka mke wa Isakaalivishwa pete na vito vingine vya urembo.
Ukristo wa sasa kwa wingi umelenga kuwafanya watu wawe watumwa na washamba kwa mihemko ya viongozi wa makanisa fulani
kama pete ni dhambi basi wakristo wote wamepotea na moto unawasubiri maana makanisa yote watu wanavaa pete(labda uko kwenu)
Mwisho:msimamo wangu ni mmoja mke wangu atavaa pete heleni na vito vyote mimi pia pete navaa
Ifike mahali tukatae utumwa wa dini hii tutafanywa misukule tukiwa hai
Ukilifuatilia sana suala la Rebeka kuvaa Pete unaweza kuta kuna upagani ndani yake utakubali kuwa Pete ni upagani kama mtoa mada anavyosema?
 
Back
Top Bottom