Wanandoa: Upangaji wa nguo chumbani

Wanandoa: Upangaji wa nguo chumbani

Chumba na sebule tena ya kupanga walk in closet inatoka wapi. Hayo ndio maisha wengi wetu.

Hapo unauwezo wa kununua bundle + unamiliki smartphone.
Chumba na sebule watoto wako wanalala wapi?
Mwanaume jiongeze.
 
hili ni la kujadiliwa hapa haswaaa wengi ni wahanga wa hili tatizo kwa kweli nimejikuta nimecheka mpakaaaaaaa
 
Taabu ipo kwenye sox...halafu uwe una haraka..ushaiona nyeupe unaamua kuivaa...tafuta enzake huioni,,,,kila ukipekua zinatoka nyeusi,:A S angry:


Haa...haaa...ndio uamue kuvaa nyeusi sasa kuokoa muda....vinginevyo zitafute kabla hujalala...
 
Ukishagundua tatizo ndio mwanzo wa kuanza kulitatua, hivyo basi ni kuwa na masterbedroom kubwa yenye kabati kubwa kulingana na mahitaji yenu au kama ni kabati la kawaida siku zote kwenye kabati lazima kuwe na kiongozi ambae kazi yake ni kufanya arrangement, in this case huyo huyo mwanamke unamwachia jukumu yeye atajua namna ya kuzipangalia hizo nguo zenu


Mkubwa una mke? Kama unaye basi mna muda mfupi sana tangu mwe pamoja, tuulize sisi tunaojukuu, ni shida.
 
Inafaa lijadiliwe maana linatugusa wengi, chumba kinakuwa min store! Khaaa!


vyumba vinakuwa min store kwakuwa wanaume wengi ni rafu sana mkivua nguo mnatupa mliposimama wakati huo!
kisa mwanamke hajapanga! hivyo kila ukivua kama hayupo huwezi kuweka nguo kwa ustaarabu?
usafi wa chumbani unahitaji sana ushirikiano wapendwa. mf mke katangulia kutoka home wewe umelala then ukiamka unaacha kitanda kama kiota cha ndege kisa mwanamke hayupo? mwishowe mnalalamika humu.

hamna watu wanakera kama wanaume wanajifanyaga kama watoto wadogo , mara waingie na viatu ndani wakati kusafi, anakula haupo akidondosha chakula alipokaa andaondoka kama kuku asubir ukija alalamike nyumba chafu looo, akioga bafuni hata kusukuma maji na broom hakuna jaman wanaume mbadilike kuna vitu mwanamke anatakiwa afanye lakini vingine vinavyokuhusu wewe fanya hapohapo
 
aisee Kama umeniona hivi yani kila kona ya chumba nimejimilikisha, kumbe tupo wengi
 
Yaani bedroom, mke hata awe mstaarab kiasi gani kikawaida huwa anameza nafasi ya uhifadhi wa nguo.

Kama ni kabati atajaza nguo zake mpaka wewe uhamie masandukuni na huko usipokuwa makini utakuta kaanza kuweka nguo zake inabidi uhamie kwenye mabegi.

Pia huko atajaza na kwa sababu wanaume hatutaki usumbufu wa kutafuta na kupekua nguo utampisha utafute namna ya kutundika nako huko atakufata utakosa nafasi ya kutundika.

Wakati huo chumba kitakuwa kama store, nyie wamama nyiee.

Vichwa vyenu made in wapiii?

Mkuu nilidhani ni mimi tu ndo nakumbana na hii hali, kumbe tuko lukuki!!
 
Taabu ipo kwenye sox...halafu uwe una haraka..ushaiona nyeupe unaamua kuivaa...tafuta enzake huioni,,,,kila ukipekua zinatoka nyeusi,:A S angry:

Kwenye sox apo nibonge ya mtihani.ata ninunue pea tano najikuta kila pea imebaki moja nyingine ishapotea.
 
Nikioa nitajua, sasa nguo nanyoosha nikiitaka
 
Back
Top Bottom