Wanandoa: Upangaji wa nguo chumbani

Wanandoa: Upangaji wa nguo chumbani

nzalendo

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2009
Posts
12,692
Reaction score
14,078
Yaani bedroom, mke hata awe mstaarab kiasi gani kikawaida huwa anameza nafasi ya uhifadhi wa nguo.

Kama ni kabati atajaza nguo zake mpaka wewe uhamie masandukuni na huko usipokuwa makini utakuta kaanza kuweka nguo zake inabidi uhamie kwenye mabegi.

Pia huko atajaza na kwa sababu wanaume hatutaki usumbufu wa kutafuta na kupekua nguo utampisha utafute namna ya kutundika nako huko atakufata utakosa nafasi ya kutundika.

Wakati huo chumba kitakuwa kama store, nyie wamama nyiee.

Vichwa vyenu made in wapiii?
 
aisee wewe ko hujamwambia mkeo unalalamika huku zungumza nae ikibid ongezen makabat...
 
Nunua kabati kubwa la ngua. Zako zitenge na za kwake. Ukiona bado anakufuata, kila unapotafuta zako changu changua na za kwake. Atakuhama.
 
Tengeneza la milango 6....ndo habari ya mjini hiyo milango mi 3 weka kwa watoto
 
hivi hilo kabati unaloongelea ni la aina gani..kwa mfano kama una kijichumba cha kuweka nguo na kimegawanywa makabati ya ukutani mawili..lake na lako...huo muingilianao unatokea wapi?....kutatua tatizo hili ni kujenga chumba maalumu kwa ajili ya kutunzia nguo.

wenzetu wazungu walishaliona hilo na kutafuta suluhisho la kudumu....tuwaige kwa haya machache mazuri.
 
Back
Top Bottom