Wanandoa jitahidini sana mfichiane madhaifu yenu mbele ya jamii

Wanandoa jitahidini sana mfichiane madhaifu yenu mbele ya jamii

Hao watadumu katika ndoa, kusemwa ni sehemu ya kukurekebisha, huwezi jua huyo mwanaume kwanini amseme mkewe vile, kuna wanawake ni wazembe sana hata makazini unamkuta binti mtanashati lakini namna anavyofanya kazi hadi asukumwe au afokewe, na wewe siku ukiolewa vumilia tu udipende kujibishana na mwanaume.
Nakubaliana na wewe, hao ndoa yao itadumu saana, tatizo wanawake wa sasa hawajui kwamba kumtii na kumheshimu mume ndio hatua ya kwanza kabisa ya kuboresha ndoa, sio tendo la ndoa kama ambavyo wengi hudhani, mwanaume anajiona fahari pale anapokoroma mwanamke anakaa kimya, huyo mwanamke inaonekana ana mafunzo toka kwao, wenye midomo mirefu ndio hawa tunasikia ndoa inadumu miezi 6 tu inavunjika
 
Upo sahihi mkuu...
Sasa turudi kwenye uhalisia, kama ni wewe ndie ungekuwa yule mwanamke...
1. Je, unge vunja doa?
2. Je, unge mshataki mumoe kwa kosa la kukudhalilisha?
Binafsi mimi nafikiri kwa hii scenario, hawa watu wana shida kuanzia ndani kwao. Na alicho kifanya mume wa huyo mama ni kulipuka kwasababu ana hasira zilizo jibeba.
Na mwisho nampongeza sana yule mama kwa kukaa kimya kwasababu pengine imemsaidia kuepuka mengi zaidi ya haya tulio simuliwa hapa.
Mkuu ndoa haivunjwi wala mume hashtakiwi. Ningekaa kimya halafu tukiwa nyumbani wawili namwambia. Kitendo chochote cha kudhalilisha mwenza iwe kimefanyika na mume au mke kinaishia kuwadhalilisha wote wawili.
Kama hapa mwanamke anaonekana mzembe na mwanaume ameonekana ana gubu hatari
 
Mkuu ndoa haivunjwi wala mume hashtakiwi. Ningekaa kimya halafu tukiwa nyumbani wawili namwambia. Kitendo chochote cha kudhalilisha mwenza iwe kimefanyika na mume au mke kinaishia kuwadhalilisha wote wawili.
Kama hapa mwanamke anaonekana mzembe na mwanaume ameonekana ana gubu hatari
Upo sahihi kabisa mkuu, na hiyo ndio namna pekee ya kumaliza tofauti kwenye ndoa.
Na hapa nimepata jibu kwamba, ingekuwa wewe ndie yule mwanamke basi pia ungakaa kimya na kisha kumtii mumeo ili kumpisha shetani, na kisha baada ya pale mkiwa nyumbani ungemuelekeza na kumkanya mumeo kwa lugha ya upole na upendo ili aweze kubadilika.
 
Hi guys..!
Natumaini mpo salama sana.!

Nilishauriwa nipunguze kuandika humu, ila Mungu ndiye ajuaye mbona nashindwa? Najikuta tu natamani kuwaandikia humu ili mfurahi ama la mjifunze jambo,
Mshauri wangu na rafiki yangu..! nimeuelewa ushauri wako barabara, but please understand me, writing is my passion..!!

Nije kwenye lengo la uzi, ilikuwa wiki iliyopita hivi, kuna wanandoa walikuja pahala ninapotafutia riziki yangu ya kila siku, na huduma waliyokuwa wanaihitaji mimi ndiye niliyepaswa niwahudumie.!!

Nikawakaribisha vizuri, nikawasikiliza shida yao, tukaongea vyema, ukafika muda wa kukagua documents zilizohitajika, hapo ndo kasheshe likaanza,
Yule dada akawa amesahau mkoba huko walipotoka, Mume akaanza; 'Na utakuwa umeacha pale dukani bila shaka, tatizo lako wewe 'fulani'(anamtaja jina) ni mzembe sana, na nilikuambia kuwa makini utaacha baadhi ya mizigo, si unaona sasa'.!?
Ikabidi kwanza nibaki nawashangaa, zaidi nikimshangaa yule mwanaume anavyomsema mkewe vile mbele yangu,
Na of course walikuwa na mizigo mingi, yule dada kusahau mkoba halikuwa kosa la jinai mpaka kuongeleshwa namna ile,

Kilichonishangaza ni namna yule mwanamke alivyopokea yale masimango, akabaki 'eeh' sijui hata nimeachaje, nisamehe mume wangu, ngoja nirudi'..!
Nikashusha pumzi ndefu, Nikajiuliza, hivi hawa wanawake wenye nidhamu namna hii kumbe bado wapo??? Mungu awabariki sana!!
Nikasali kimya kimya, Mungu nihurumie mimi mja wako, naomba nipe huu moyo hata robo tatu tu, maana moyo wa hivii kiukweli sijabahatika kuwa nao..!!

Basii, yule mwanamke akaharakia kutoka, kurudi alikotoka kuufuata mkoba wake, nikabaki na yule mwanaume anajiongelesha, 'yaani wanawake huwa mnakuwa mna mambo mengi sana ya ajabu, sijui blah blah'..!
Hata sikutaka kumjibu, maana kwa namna alivyomgombeza mkewe nilijikuta namie namuona ni mtu wa ajabu sana,

Akawa anauliza kitu kwa upole kama sio yeye, ananisemesha vizuuuri, nikataka kumuambia wewe, hili sound hata haliniingii ngozi yako halisi nishaijua, don't pretend hapa kujikuta mwema.!!

Baada ya muda mfupi mkewe akawa amerudi, na pochi kafanikiwa kuikuta, aliiacha duka la nguo huko, bahati nzuri ikawa imetunzwa maana walikuwa wamenunua vitu vingi hapo nadhani, ndo maana wakawa wamekuwa marked wakatunziwa,

Nikajua suala limeisha, kumbe bado, ni anajaza kitu akiuliza anaambiwa fanya haraka bwana tunachelewa, dada mara apigiwe simu, apokee! Anaambiwa hivii unaanza na kupokea simu sahizi, hivii tutawahi kweli?? Mkewe anajibu kwa upole, alikuwa tu ananiuliza nimuelekeze tu wachukue ngapi zitatosha,

Yaani kwa kumtazama tu unajua kabisa siyo kumuheshimu mumewe, hapana! bali huyu dada anamuogopa mumewe maskiini,
Na wala umri wao siyo mkubwa sana utaona kabisa hii ndoa pengine bado mpya, nadhani labda ndiyo sababu ya mke kumuogopa mumewe kiasi kile mpaka inatia huruma.!

Anyway, hilo halinihusu sana, nimetaka tu kuwaambia ndugu zangu wapendwa, mliopo kwenye ndoa ama mahusiano yenye malengo hata na wale mliopo kwenye mahusiano ya 'kurukaruka',
Chondechonde.!! Jitahidini sana mfiche mikwaruzano yoyote mliyo nayo mbele za watu, fanyeni juu chini jamii isijue kile mnakipitia, nendeni mkayazungumzie sirini huko.!!

Ifikie mahali, siyo watoto wenu, majirani, wazazi, marafiki ama jamii inayowazunguka ipate habari Leo mmegombana, sijui mmetoleana lugha chafu, sijui kila mmoja kasema udhaifu wa mwenzie, Hell No'..!!


Kila mmoja ana madhaifu yake, tena wakati mwingine ni makubwa hata hayatatuliki, wala hayabebeki, kitendo cha kupiga kelele kuiambia dunia madhaifu ya mwenzio, humkomoi yeye, unajikomoa wewe mwenyewe, sababu mwisho wa siku wewe mpiga kelele ndo unayeenda kuishi naye na huo msalaba ni wako kuubeba hivyo ni jambo la busara zaidi kumfichia mwenzio mapungufu yake, hakikisha tusijue kabisaaa!! Na kama umeamua tujue sema mazuri yake basii, sifia hadii siyo poa! Mpaka tutamani kumpata kama yeye, lakini siri yenu mnabaki nayo moyoni wawili.!

Leo umemdharaulisha mbele ya jamii yake inayomzunguka, unategemea kesho, ile ile jamii imuheshimu?? Haiwezi kumuheshimu Yeye, na zaidi sana haitokaa ikuheshimu Wewe,
Msisahau ulimi ni kiungo kidogo lakini ndiyo chanzo cha uharibifu na uvunjifu mkubwa wa amani.!

Tupendane kwa dhati, tusameheane pasi kikomo, tusihesabiane mabaya na tuongozwe na Utii.!!

Wishing you a very blessed long weekend ahead.!!
Tumejifunza kitu lakin na wewe haujafanya vyema kuyaleta matatizo/madhaifu ya wateja wako, ungekaa nayo hukohuko kulinda privacy zao.

Siku nyingine deal na kazi yako siyo kubeba madhaifu ya watu kuja kuyamwaga huku huo ni umbea na haukubaliki katika kazi hasa hizo zinazohusisha watu wengi.
 
Mkuu, kama upo kwenye ndoa naamini utaungana nami kwamba hilo ni jambo dogo sana.
Na kwenye ndoa hapahitaji mashindano wala ujuaji mwiiiingi ambao huweza ukapelekea shida kubwa zaidi.
Zipo ndoa nyingi ambazo zinavumiliwa kwa sababu tofauti tofauti, na ingekuwa kila jambo linapo tokea ama kauli mbaya inapo tokea ni kukimbilia kwenye hizo mnaita haki/sheria/dawati and ect basi bilashaka ndoa nyingi zingekuwa zimesha vunjika.
Na, yawezekana msimuliaji ameona hili ni jambo la ajabu na kubwa kwake kwasababu pengine bado hajaingia kwenye ndoa.
Mkuu mambo madogo madogo haya ndio yanayochangiaga kudhoofisha ndoa. Kitendo cha kuwaonyesha watu wa nje kwamba mwenza wako (mume au mke wako)ni mjinga au mzembe unakua umeishusha thamani yake na yeye anaweza kuathirika kisaikolojia. Tusipokubali kutibu mambo madogo madogo haya tunajiweka sehemu mbaya
 
Kuna wanawake ni wazembe toka wakiwa makwao na hawabadiliki, na kuna wanaume ambao hasira zao ni kusema akisema nyongo yake inatulia na maisha yanasonga, wasichana wengi wa kileo wanapenda kushindana na wanaume katika kuongea haswa mkiwa katika ugomvi
Mkuu ukiona mnaanza kushindana ndani ya nyumba ujue ndoa imeshapoteza uelekeo.
Bora kukaa chini na katatua changamoto kuliko kulumbana
 
Mkuu mambo madogo madogo haya ndio yanayochangiaga kudhoofisha ndoa. Kitendo cha kuwaonyesha watu wa nje kwamba mwenza wako (mume au mke wako)ni mjinga au mzembe unakua umeishusha thamani yake na yeye anaweza kuathirika kisaikolojia. Tusipokubali kutibu mambo madogo madogo haya tunajiweka sehemu mbaya
Uko sawa, lakini nanyi mjifunze kuwa smart, unakuta mwanamke mnatoka nae vizuri mnaenda kusalimia mgonjwa, mnafika huko eti ndio anaanza kukwambia nimesahau matunda mliyokuwa mmeandaa kwa ajili ya mgonjwa, haya matabia huwa yanaudhi sana
 
Maisha ya kuogopana mabaya sana, ndoa ni muungano wa marafiki wawili wanaopendana wajinsia mbili tofauti.....
 
Nilipofikia sehemu unasema moyo wa hivyo huna nikaishia hapo hapo, sasa kama wewe mwenyewe huo moyo huna unawezaje kutushauri wengine? Umechemka sana.
atakua alikua anaandika script ya bongo movie. ila kitu NDOA hata yeye binasi hakijui wala kukifahamu zaidi ya kukisikia.
 
Napongeza ujasiri wa huyo mwanamke ..ila sidhani Kama ilikuwa busara mwanaume kufanya hayo aliyoyafanya.
 
Uko sawa, lakini nanyi mjifunze kuwa smart, unakuta mwanamke mnatoka nae vizuri mnaenda kusalimia mgonjwa, mnafika huko eti ndio anaanza kukwambia nimesahau matunda mliyokuwa mmeandaa kwa ajili ya mgonjwa, haya matabia huwa yanaudhi sana
Kwa kweli hili linaudhi, sasa matunda ya mgonjwa unayasahau vipi tena baada ya kuyaandaa?
Huyu mwanamke mvumilie... mkishafika nyumbani mpe maneno kama aliyopewa yule contractor 😆😆
 
Kuna kitu kinaitwa Ustaarabu hichi ni mtiani mgumu sana unaweza ukawa mstaarabu alafu ukakutana na wanadamu si wastaarabu ukajuta maishani.
 
Back
Top Bottom