Carleen
JF-Expert Member
- Nov 6, 2018
- 8,592
- 29,545
Hi guys..!
Natumaini mpo salama sana.!
Nilishauriwa nipunguze kuandika humu, ila Mungu ndiye ajuaye mbona nashindwa? Najikuta tu natamani kuwaandikia humu ili mfurahi ama la mjifunze jambo,
Mshauri wangu na rafiki yangu..! nimeuelewa ushauri wako barabara, but please understand me, writing is my passion..!!
Nije kwenye lengo la uzi, ilikuwa wiki iliyopita hivi, kuna wanandoa walikuja pahala ninapotafutia riziki yangu ya kila siku, na huduma waliyokuwa wanaihitaji mimi ndiye niliyepaswa niwahudumie.!!
Nikawakaribisha vizuri, nikawasikiliza shida yao, tukaongea vyema, ukafika muda wa kukagua documents zilizohitajika, hapo ndo kasheshe likaanza,
Yule dada akawa amesahau mkoba huko walipotoka, Mume akaanza; 'Na utakuwa umeacha pale dukani bila shaka, tatizo lako wewe 'fulani'(anamtaja jina) ni mzembe sana, na nilikuambia kuwa makini utaacha baadhi ya mizigo, si unaona sasa'.!?
Ikabidi kwanza nibaki nawashangaa, zaidi nikimshangaa yule mwanaume anavyomsema mkewe vile mbele yangu,
Na of course walikuwa na mizigo mingi, yule dada kusahau mkoba halikuwa kosa la jinai mpaka kuongeleshwa namna ile,
Kilichonishangaza ni namna yule mwanamke alivyopokea yale masimango, akabaki 'eeh' sijui hata nimeachaje, nisamehe mume wangu, ngoja nirudi'..!
Nikashusha pumzi ndefu, Nikajiuliza, hivi hawa wanawake wenye nidhamu namna hii kumbe bado wapo??? Mungu awabariki sana!!
Nikasali kimya kimya, Mungu nihurumie mimi mja wako, naomba nipe huu moyo hata robo tatu tu, maana moyo wa hivii kiukweli sijabahatika kuwa nao..!!
Basii, yule mwanamke akaharakia kutoka, kurudi alikotoka kuufuata mkoba wake, nikabaki na yule mwanaume anajiongelesha, 'yaani wanawake huwa mnakuwa mna mambo mengi sana ya ajabu, sijui blah blah'..!
Hata sikutaka kumjibu, maana kwa namna alivyomgombeza mkewe nilijikuta namie namuona ni mtu wa ajabu sana,
Akawa anauliza kitu kwa upole kama sio yeye, ananisemesha vizuuuri, nikataka kumuambia wewe, hili sound hata haliniingii ngozi yako halisi nishaijua, don't pretend hapa kujikuta mwema.!!
Baada ya muda mfupi mkewe akawa amerudi, na pochi kafanikiwa kuikuta, aliiacha duka la nguo huko, bahati nzuri ikawa imetunzwa maana walikuwa wamenunua vitu vingi hapo nadhani, ndo maana wakawa wamekuwa marked wakatunziwa,
Nikajua suala limeisha, kumbe bado, ni anajaza kitu akiuliza anaambiwa fanya haraka bwana tunachelewa, dada mara apigiwe simu, apokee! Anaambiwa hivii unaanza na kupokea simu sahizi, hivii tutawahi kweli?? Mkewe anajibu kwa upole, alikuwa tu ananiuliza nimuelekeze tu wachukue ngapi zitatosha,
Yaani kwa kumtazama tu unajua kabisa siyo kumuheshimu mumewe, hapana! bali huyu dada anamuogopa mumewe maskiini,
Na wala umri wao siyo mkubwa sana utaona kabisa hii ndoa pengine bado mpya, nadhani labda ndiyo sababu ya mke kumuogopa mumewe kiasi kile mpaka inatia huruma.!
Anyway, hilo halinihusu sana, nimetaka tu kuwaambia ndugu zangu wapendwa, mliopo kwenye ndoa ama mahusiano yenye malengo hata na wale mliopo kwenye mahusiano ya 'kurukaruka',
Chondechonde.!! Jitahidini sana mfiche mikwaruzano yoyote mliyo nayo mbele za watu, fanyeni juu chini jamii isijue kile mnakipitia, nendeni mkayazungumzie sirini huko.!!
Ifikie mahali, siyo watoto wenu, majirani, wazazi, marafiki ama jamii inayowazunguka ipate habari Leo mmegombana, sijui mmetoleana lugha chafu, sijui kila mmoja kasema udhaifu wa mwenzie, Hell No'..!!
Kila mmoja ana madhaifu yake, tena wakati mwingine ni makubwa hata hayatatuliki, wala hayabebeki, kitendo cha kupiga kelele kuiambia dunia madhaifu ya mwenzio, humkomoi yeye, unajikomoa wewe mwenyewe, sababu mwisho wa siku wewe mpiga kelele ndo unayeenda kuishi naye na huo msalaba ni wako kuubeba hivyo ni jambo la busara zaidi kumfichia mwenzio mapungufu yake, hakikisha tusijue kabisaaa!! Na kama umeamua tujue sema mazuri yake basii, sifia hadii siyo poa! Mpaka tutamani kumpata kama yeye, lakini siri yenu mnabaki nayo moyoni wawili.!
Leo umemdharaulisha mbele ya jamii yake inayomzunguka, unategemea kesho, ile ile jamii imuheshimu?? Haiwezi kumuheshimu Yeye, na zaidi sana haitokaa ikuheshimu Wewe,
Msisahau ulimi ni kiungo kidogo lakini ndiyo chanzo cha uharibifu na uvunjifu mkubwa wa amani.!
Tupendane kwa dhati, tusameheane pasi kikomo, tusihesabiane mabaya na tuongozwe na Utii.!!
Wishing you a very blessed long weekend ahead.!!