Wanandoa jitahidini sana mfichiane madhaifu yenu mbele ya jamii

Wanandoa jitahidini sana mfichiane madhaifu yenu mbele ya jamii

Kwa hiyo wewe ulitaka mmoja akipanda juu mwenzake nae apande juu? Mkuu upo kwenye ndoa? Kumbuka hapo hawapo wenyewe na mmoja ameshaonyesha udhaifu wake, unadhani ni busara kwa huyu dada kuanza majibizano mbele za watu?

Tuanzie hapo kwanza!!
Aanze majibizano.!? Hell No'..!!
Nimefurahishwa na unyenyekevu wake na sikutegemea hilo..!
Mbona mnajibu kama vile nina support ugomvi.? Nadhani hamjaipata maana ya nilichomaanisha.!

Ndiyo nipo kwenye ndoa, ila sijawahi karipiwa mbele za watu hata siku moja.!
 
Mkuu hili swali na huu mtazamo ni sawa na ninaokutana nao kwa wale makungwi wa kitchen parties, asilimia kubwa hawana ndoa au wameachika.

Ila utakuta wao wanafundisha jinsi ya kuhakikisha mwanamke haachwi na mume (kulinda ndoa)
tena bahati nzuri wanawafundisha kulinda ndoa zao na siyo vice versa, hilo siyo tatizo kubwa Mr. Don C..!!
 
That is cumulative stress of doing/saying the same thing over and over. Wewe ni msichana usiyekuwa na stress ya kuishi na mtu asiyetaka kujifunza na kubadilika. Omba upate mtu tofauti wakati wako utakapofika. Ukipata aina hiyo ya kutotaka kujifunza utarudi hapa kufungua uzi wa kulaumu.
Hi guys..!
Natumaini mpo salama sana.!

Nilishauriwa nipunguze kuandika humu, ila Mungu ndiye ajuaye mbona nashindwa? Najikuta tu natamani kuwaandikia humu ili mfurahi ama la mjifunze jambo,
Mshauri wangu na rafiki yangu..! nimeuelewa ushauri wako barabara, but please understand me, writing is my passion..!!

Nije kwenye lengo la uzi, ilikuwa wiki iliyopita hivi, kuna wanandoa walikuja pahala ninapotafutia riziki yangu ya kila siku, na huduma waliyokuwa wanaihitaji mimi ndiye niliyepaswa niwahudumie.!!

Nikawakaribisha vizuri, nikawasikiliza shida yao, tukaongea vyema, ukafika muda wa kukagua documents zilizohitajika, hapo ndo kasheshe likaanza,
Yule dada akawa amesahau mkoba huko walipotoka, Mume akaanza; 'Na utakuwa umeacha pale dukani bila shaka, tatizo lako wewe 'fulani'(anamtaja jina) ni mzembe sana, na nilikuambia kuwa makini utaacha baadhi ya mizigo, si unaona sasa'.!?
Ikabidi kwanza nibaki nawashangaa, zaidi nikimshangaa yule mwanaume anavyomsema mkewe vile mbele yangu,
Na of course walikuwa na mizigo mingi, yule dada kusahau mkoba halikuwa kosa la jinai mpaka kuongeleshwa namna ile,

Kilichonishangaza ni namna yule mwanamke alivyopokea yale masimango, akabaki 'eeh' sijui hata nimeachaje, nisamehe mume wangu, ngoja nirudi'..!
Nikashusha pumzi ndefu, Nikajiuliza, hivi hawa wanawake wenye nidhamu namna hii kumbe bado wapo??? Mungu awabariki sana!!
Nikasali kimya kimya, Mungu nihurumie mimi mja wako, naomba nipe huu moyo hata robo tatu tu, maana moyo wa hivii kiukweli sijabahatika kuwa nao..!!

Basii, yule mwanamke akaharakia kutoka, kurudi alikotoka kuufuata mkoba wake, nikabaki na yule mwanaume anajiongelesha, 'yaani wanawake huwa mnakuwa mna mambo mengi sana ya ajabu, sijui blah blah'..!
Hata sikutaka kumjibu, maana kwa namna alivyomgombeza mkewe nilijikuta namie namuona ni mtu wa ajabu sana,

Akawa anauliza kitu kwa upole kama sio yeye, ananisemesha vizuuuri, nikataka kumuambia wewe, hili sound hata haliniingii ngozi yako halisi nishaijua, don't pretend hapa kujikuta mwema.!!

Baada ya muda mfupi mkewe akawa amerudi, na pochi kafanikiwa kuikuta, aliiacha duka la nguo huko, bahati nzuri ikawa imetunzwa maana walikuwa wamenunua vitu vingi hapo nadhani, ndo maana wakawa wamekuwa marked wakatunziwa,

Nikajua suala limeisha, kumbe bado, ni anajaza kitu akiuliza anaambiwa fanya haraka bwana tunachelewa, dada mara apigiwe simu, apokee! Anaambiwa hivii unaanza na kupokea simu sahizi, hivii tutawahi kweli?? Mkewe anajibu kwa upole, alikuwa tu ananiuliza nimuelekeze tu wachukue ngapi zitatosha,

Yaani kwa kumtazama tu unajua kabisa siyo kumuheshimu mumewe, hapana! bali huyu dada anamuogopa mumewe maskiini,
Na wala umri wao siyo mkubwa sana utaona kabisa hii ndoa pengine bado mpya, nadhani labda ndiyo sababu ya mke kumuogopa mumewe kiasi kile mpaka inatia huruma.!

Anyway, hilo halinihusu sana, nimetaka tu kuwaambia ndugu zangu wapendwa, mliopo kwenye ndoa ama mahusiano yenye malengo hata na wale mliopo kwenye mahusiano ya 'kurukaruka',
Chondechonde.!! Jitahidini sana mfiche mikwaruzano yoyote mliyo nayo mbele za watu, fanyeni juu chini jamii isijue kile mnakipitia, nendeni mkayazungumzie sirini huko.!!

Ifikie mahali, siyo watoto wenu, majirani, wazazi, marafiki ama jamii inayowazunguka ipate habari Leo mmegombana, sijui mmetoleana lugha chafu, sijui kila mmoja kasema udhaifu wa mwenzie, Hell No'..!!


Kila mmoja ana madhaifu yake, tena wakati mwingine ni makubwa hata hayatatuliki, wala hayabebeki, kitendo cha kupiga kelele kuiambia dunia madhaifu ya mwenzio, humkomoi yeye, unajikomoa wewe mwenyewe, sababu mwisho wa siku wewe mpiga kelele ndo unayeenda kuishi naye na huo msalaba ni wako kuubeba hivyo ni jambo la busara zaidi kumfichia mwenzio mapungufu yake, hakikisha tusijue kabisaaa!! Na kama umeamua tujue sema mazuri yake basii, sifia hadii siyo poa! Mpaka tutamani kumpata kama yeye, lakini siri yenu mnabaki nayo moyoni wawili.!

Leo umemdharaulisha mbele ya jamii yake inayomzunguka, unategemea kesho, ile ile jamii imuheshimu?? Haiwezi kumuheshimu Yeye, na zaidi sana haitokaa ikuheshimu Wewe,
Msisahau ulimi ni kiungo kidogo lakini ndiyo chanzo cha uharibifu na uvunjifu mkubwa wa amani.!

Tupendane kwa dhati, tusameheane pasi kikomo, tusihesabiane mabaya na tuongozwe na Utii.!!

Wishing you a very blessed long weekend ahead.!!
 
Kweli mkuu ndoa inahitaji kuvumiliana ila huyo jamaa anachofanya ni kumdhalisha mwenzie na hiyo inaweza pelekea ndoa kuanza kuyumba (kwa kuwa anatoa nafasi hadi kwa watu wa nje kuivuruga au mke pia anaweza kuchoka maana sio kwamba ana nidham tuu bali ana hofu pia )
Jamaa angemsema mkewe wakiwa wawili peke yao mke angemheshimu sana na kumwelewa zaidi na huo ndio uanaume😎
Absolutely,
Na Mimi maana yangu ilikuwa hiyo.! Haikuwa na haja ya kumkaripia mbele yangu! Wangeenda tu kumalizana huko mbele wakiwa peke yao! Na mke ni mstaarabu kafanya kitendo cha kijasiri ingekuwa ni wale vichwa panzi pasingetosha..!!
 
That is cumulative stress of doing/saying the same thing over and over. Wewe ni msichana usiyekuwa na stress ya kuishi na mtu asiyetaka kujifunza na kubadilika. Omba upate mtu tofauti wakati wako utakapofika. Ukipata aina hiyo ya kutotaka kujifunza utarudi hapa kufungua uzi wa kulaumu.
Amina mkuu,
Na Mungu aniepushe maana nitapata ugonjwa wa moyo mapema sana nahisi.!
 
Wengine kuchukulia vitu poa ni anasa, vitu vidogo wanavifanyia amplification mpaka..
You as a woman you can't change your man because you love him, ila sisi men we change ourselves because we love you
Exactly Vinci rafiki yangu.!!
Na Mungu awasaidie kubadilika.!!
 
Umenielewa lakini? Asiyetaka kujifunza ni huyo mwanamke. Mumewe inabidi arudie mambo yaleyale. As a result, ana chronic stress. Ndio maana haoni tena sababu ya kuongelea faraghani. Ameshaongelea faraghani mara nyingi lakini haikusaidia....
Amina mkuu,
Na Mungu aniepushe maana nitapata ugonjwa wa moyo mapema sana nahisi.!
 
Ila Mungu sisi wanawake alituumba na natural love, mwanaume wanaweza kuwa anakutesa ila ukifika kwa mashoga basi unamsifia, unamwongezea hata sifa ambazo hana.aonekane the best.

All in all haipendezi kumsema mtu vibaya mbele za watu, mapungufu yake mseme mkiwa nyumbani inatosha, iwe ndoa au mahusiano usiri ni muhimu sana.
 
Aanze majibizano.!? Hell No'..!!
Nimefurahishwa na unyenyekevu wake na sikutegemea hilo..!
Mbona mnajibu kama vile nina support ugomvi.? Nadhani hamjaipata maana ya nilichomaanisha.!

Ndiyo nipo kwenye ndoa, ila sijawahi karipiwa mbele za watu hata siku moja.!
Ok, sasa ulitaka huyo dada afanyaje/ajibuje? Maana huenda tayari anajua hulka za mume wake. Unadhani angetakiwa kutumia approach gani?

Tunachotakiwa kukumbuka ni kwamba, kila ndoa ni tofauti na nyingine. Hata kwako yapo mnayafanya ambayo mwingine akiwaona anaweza kuwashangaa.
 
Kama alikumbushwa akaleta ujuaji ulitaka huyo mwanaume afanyeje? Tena huenda alimkumbusha kwa lugha ya upendo zaidi unavyofikiria wewe, na huyo mwanamke amejifanya lofa hapo mbele yako kwasababu kalifaham kosa lake ila huenda ni gaidi zaidi ya huyo mwanaume unapomkuta anga zake, ndio maana wanazeeka wote maana tabia wanaendana
😂 😂
Hivyo, nawe una support watu kugombana mbele za watu?
Hata kama umesema mara 100, bado ni mwenza wako unapaswa umvumilie kwa hali zote.!!
 
Umenielewa lakini? Asiyetaka kujifunza ni huyo mwanamke. Mumewe inabidi arudie mambo yaleyale. As a result, ana chronic stress. Ndio maana haoni tena sababu ya kuongelea faraghani. Ameshaongelea faraghani mara nyingi lakini haikusaidia....
Ndiyo nimekuelewa vizuri kabisa.! Na suala la kutenda jambo lile lile kila siku unalokatazwa ni a way too stressing for both male and female.!
Ahsante..!
 
Ok, sasa ulitaka huyo dada afanyaje/ajibuje? Maana huenda tayari anajua hulka za mume wake. Unadhani angetakiwa kutumia approach gani?

Tunachotakiwa kukumbuka ni kwamba, kila ndoa ni tofauti na nyingine. Hata kwako yapo mnayafanya ambayo mwingine akiwaona anaweza kuwashangaa.
Sawa Mr. Elli, nimekuelewa vizuri kabisa.!!
Amani ya Bwana ikae nawe.!
 
Maranyingi sana huwa nasoma hizi mambo za washauri wa wanandoa, na mwisho huwa napenda kuuliza hivi....
J, wewe upo kwenye ndoa??
Maana naona hapo nikama umem beza huyo mwanamke aliye jishusha mbele ya mumewe, na pengine kujishusha huko ndipo panapo ifanya ndoa yake iendelee kuwa hai leo hii.
Ndoa inahitaji kuvumilliana, na tabia ya mtu huwa ni ngumu kuibadilisha
Hawa ndio kama wale akina Joyce kiria au Bi chau au akina Mboni..Wajuaji wa ndoa wakat zao either zimewashinda au hawana kabisaa
 
Asilimia chache Sana ya wanawake wanapenda wanaume wabembelezaji.
Ile kukoroma koroma tu inakuongezea credit.
Ni kama huyu wangu anapenda sana nimkoromee

mfano anaweza kufanya kitu cha kijinga makusudi ili nimkoromee nikijikausha unamsikia ananiigilizia jinsi ninavyomkaripia
 
Back
Top Bottom