Wananchi wenye vilio wamlilie nani?

mzamifu

JF-Expert Member
Mar 10, 2010
6,379
3,826
Wana Jf, kama mnakumbuka kipindi Mrema akiwa waziri wa mambo ya ndani wananchi wenye vilio walijipamga foleni ndefu kumlilia asikilize vilio vyao.

Walipata ahueni japo kwa kusikilizwa tu. Walimshangilia na kumpenda hata kama Mrema alikosea hapa na pale. Mrema alikuwa maarufu kwa kutoa siku saba kwa waliotuhumiwa.

Leo hii kuna wananchi wana vilio vingi tu sasa hawajui wa kumlilia. Chadema wamegundua hilo wanajaribu kuchukua jukumu hilo japo tofauti na staili ya Mrema. Je, wale waliochaguliwa wanajua wajibu wao kwa wananchi? Hivi wanaweza kukana kuwa wananchi hawana vilio?

There are so many unanswered cries!
 
Andiko zuri sana hili. Sasa hivi hakuna kiongozi wa juu ambaye yupo kusikiliza shida ya mtu mmoja mmoja. Na wenye matatizo hayo ni wengi lakini wamekata tamaa. Utaratibu wa CCM wa kuitaka Serikali ishughulikie matatizo hayo haupo kabisa umesahaulika. Hata Mzee Ruksa alikuwa ameweka utaratibu wa kukutana na mwananchi mwenye tatizo pale Lumumba kila Alhamis. Viongozi wa sasa wanadhani jukumu lao ni kujenga barabara, SGR, kutafuta mikopo na wawekezaji, basi; wakati wengi wa wananchi mmoja mmoja wana matatizo ya kufa mtu! Siku moja ama CCM au chama mbadala kitairudisha Tanzania kwenye mstari wa utawala halisi. Ni suala la muda tu!
 
Wana Jf, kama mnakumbuka kipindi Mrema akiwa waziri wa mambo ya ndani wananchi wenye vilio walijipamga foleni ndefu kumlilia asikilize vilio vyao.

Walipata ahueni japo kwa kusikilizwa tu. Walimshangilia na kumpenda hata kama Mrema alikosea hapa na pale. Mrema alikuwa maarufu kwa kutoa siku saba kwa waliotuhumiwa.

Leo hii kuna wananchi wana vilio vingi tu sasa hawajui wa kumlilia. Chadema wamegundua hilo wanajaribu kuchukua jukumu hilo japo tofauti na staili ya Mrema. Je, wale waliochaguliwa wanajua wajibu wao kwa wananchi? Hivi wanaweza kukana kuwa wananchi hawana vilio?

There are so many unanswered cries!
Wananchi wanalia na kilio chao kimefika juu
 
CCM ni sawa kabisa na mama wa kambo aliyekuwa na roho mbaya. Yeye pesa zote za matumizi na matunzo ya watoto nyumbani anazopewa na mumewe anaamua kizutumia kwa starehe zake binafsi, wakati watoto wakiandamwa na utapiamlo.
 
Back
Top Bottom