Wananchi wengi wanaunga mkono tozo, maneno ya maadui na vibaraka wa mabeberu yapuuzwe

njaakalihatari

JF-Expert Member
Feb 12, 2019
4,084
8,663
Baada ya kuona nchi inapiga hatua kwa kasi chini ya Rais mpendwa wa awamu ya sita, madaui wa taifa kupitia vibaraka wao wameibuka kwa kasi sana

Mama hata halali kabisa akiwaza jinsi ya kuwaletea maendeleo hili lilithibitishwa na Gerson Msigwa lakini bado kuna wajinga wanalalamika tu

Tozo zinazotozwa kwa sasa siyo nyingi na manufaa yake yanaonekana, barabara zinajengwa kwa kasi, umeme wa uhakika, maji, huduma za afya zimeboreshwa mno.

Ndege 5 zinakuja za kuboresha ATCL tena zimenunuliwa cash sasa jiulize ni nchi ngapi zina uwezo wa kununua cash hizo ndege ni uzalendo wetu umoja na mshikamano watanzania umefanikisha hilo

Tusiwasikilize mabeberu na vibaraka wao wasiotutakia mema, tumsapoti Rais wetu na jembe lake genius kabisa Field marshall Mwigulu Nchemba ambaye kapaisha sana mapato ya serikali kwa kipindi kifupi ama kwa hakika huyu ndiye Rais ajaye

Tozo wananchi tumeridhia sababu kazi yake tunaiona na tunaamini kwamba pesa haziliwi kwani kuna uwajibikaji mkubwa mno kwenye awamu hii ya sita majizi yote yamekatiwa mirija, nidhamu ya kazi iko juu,morale hata mawazirini wanyeyenyekevu sana kwa raia hawana majibu ya dharau

Tunashauri vyanzo vingine vya TOZO pia viendelee kufatiliwa kwa karibu na kwa kuanzia bando za simu atleast GB 1 iwe 3000 au 4000 itakuwa bado ni himilivu sana na bei nafuu mno kwa viwango vya Afrika.

MR TOZO.jpg
 
Baada ya kuona nchi inapiga hatua kwa kasi chini ya Rais mpendwa wa awamu ya sita,madaui wa taifa kupitia vibaraka wao wameibuka kwa kasi sana
Ukiwa unaishi kwa shemeji ni lazima utakuwa na mawazo haya, kwa kuwa kazi yako kubwa ni kula na kulala tu, gharama halisi za maisha utazijulia wapi!?
 
Ukiwa unaishi kwa shemeji ni lazima utakuwa na mawazo haya, kwa kuwa kazi yako kubwa ni kula na kulala tu, gharama halisi za maisha utazijulia wapi!?
Sasa huyo shemeji yeye pesa anatoa wapi we kibaraka wa mabeberu??
 
Baada ya kuona nchi inapiga hatua kwa kasi chini ya Rais mpendwa wa awamu ya sita,madaui wa taifa kupitia vibaraka wao wameibuka kwa kasi sana...
Tena wa Vijijini maana ndio wanufaika wakubwa..

Ukisema tozo sijui loop lopo kibao unaoneshwa miradi na Serikali huwa haifichi inasema mradi huu wa darsa au kituo Cha afya ni pesa ya tozo.
 
Baada ya kuona nchi inapiga hatua kwa kasi chini ya Rais mpendwa wa awamu ya sita,madaui wa taifa kupitia vibaraka wao wameibuka kwa kasi sana

Mama hata halali kabisa akiwaza jinsi ya kuwaletea maendeleo hili lilithibitishwa na Gerson msigwa lakini bado kuna wajinga wanalalamika tu

Tozo zinazotozwa kwa sasa siyo nyingi na manufaa yake yanaonekana, barabara zinajengwa kwa kasi, umeme wa uhakika, maji, huduma za afya zimeboreshwa mnoo

Ndege 5 zinakuja za kuboresha ATCL tena zimenunuliwa cash sasa jiulize ni nchi ngapi zina uwezo wa kununua cash hizo ndege,ni uzalendo wetu umoja na mshikamano watanzania umefanikisha hilo

Tusiwasikilize mabeberu na vibaraka wao wasiotutakia mema, tumsapoti Rais wetu na jembe lake genius kabisa Field marshall Mwigulu nchemba ambaye kapaisha sana mapato ya serikali kwa kipindi kifupi ama kwa hakika huyu ndiye Rais ajaye

Tozo wananchi tumeridhia sababu kazi yake tunaiona na tunaamini kwamba pesa haziliwi kwani kuna uwajibikaji mkubwa mno kwenye awamu hiiya sita majizi yote yamekatiwa mirija, nidhamu ya kazi iko juu,morale hata mawazirini wanyeyenyekevu sana kwa raia hawana majibu ya dharau

Tunashauri vyanzo vingine vya TOZO pia viendelee kufatiliwa kwa karibu na kwa kuanzia bando za simu atleast GB 1 iwe 3000 au 4000 itakuwa bado ni himilivu sana na bei nafuu mno kwa viwango vya afrika

Naunga mkono viwango vya tozo vipandisbwe kwa asilimia mia ili tuongeze kasi ya maendeleo ya nchi yetu pendwa ya Tozonia.

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Umasikini na masikini si sifa nzuri kwa nchi

Nchi ikiongeza makato, inapunguza uwekezaji na wawekezaji
 
Back
Top Bottom