Wananchi washindwa kupita kwenye Mto Kinyerezi kwa siku tatu

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,814
11,991

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amewaagiza TARURA kuhakikisha wanajenga daraja kwa haraka eneo la Tabata kinyerezi ili wananchi wapate mahali pa kupita na kuepusha maafa kwa wananchi ambao wamekuwa wakikatiza huku maji mengi yakiwa yanapita.

Chalamila ametoa maagizo hayo kwa TARURA Mara baada ya kufika eneo hilo na kuona watu wanabebwa ili waweze kuvuka eneo hilo.

“Timu ya mkurugenzi, TPDC, team ya Tanesco, team ya tarura ili angalau kuona kwa pamoja nini kinachoweza kufanyika na jambo la tatu kama tukishajithibitishia tarura maana yake immediately Jumatatu asubuhi wawepo kwa ajili ya kudesign kivuko,” Chalamika

Awali, Chalamila alitembelea vituo Vya kuzalisha umeme Vya Kinyerezi one na Kinyerezi two na kutoa maagizo kwa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kuondokana na umeme wa gharama kubwa ambao umekuwa kero kwa wananchi.

Amesema “Tuondokane na umeme wa gharama kubwa kwa wananchi na Sasa tuwekeze zaidi kwenye umeme ambao mwananchi anaweza akauaccess kwa gharama ndogo zaidi kwa maana tukaangalia accessibility lakini na affordability ili kuweza kukidhi mahitaji ya wananchi na viwanda.”

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Miradi Tanesco, Mhandisi Didas Lyamuya anaelezea mikakati yao kuhakikisha umeme wa uhakika unapatikana.

Amesema “Tuna mipango na kazi ambazo tunaendelea nazo kwenye baadhi ya mitambo ili tuweze kufikia megawatt 185, pia tutaongeza mitambo mingine ya transformer ili wananchi wa Dar es salaam waweze kupata umeme wa uhakika."

Nao baadhi ya wananchi wa kinyerezi wanaelezea adha ya miundombinu kipindi cha mvua, Zuhura Shombi anasema "Leo ni siku ya tatu wa ng’ambo wa ng’ambo wa huku wa huku , huu mit Ni kero sana tunaomba mkuu wa mkoa utuletee daraja.”
 
Back
Top Bottom