Wamekuwa wakijiuliza iweje kila jambo viongozi watake kulitolea uamuzi? - Pengine ingekuwa vizuri viongozi wa ccm wakaiga toka CHADEMA na kufanya maamuzi badala ya 'kulia'.
Wamekuwa wakikumbusha juu ya Zitto Kabwe .... kuzushiwa mambo mbalimbali ikiwemo ati Zitto amenunuliwa na CCM ...Hazushiwi mtu hapa, unakumbuka simu na emails za Zitto zilivyoanikwa kwenye mwanahalisi?
Wanahoji iweje baadhi ya wagombea ambao hutoka katika mikoa isio ya Kilimanjaro na Arusha huenguliwa katika uchaguzi huo?.Wanatoa mfano wa kuenguliwa kwa baadhi ya wagombea katika uchaguzi wa BAVICHA.. Heche anatoka Arusha, au Kilimanjaro?*****
Hii kweli inaonesha kuwa no intra-party demokrasi CHADEMA.Yaani mbunge hapaswi kuwa na mawazo yake tofauti ndani ya Bunge... Kuna tofauti kati ya mgongano wa mawazo na tofauti kwenye sera. Sera ni accummulation ya mitizamo tofauti toka kwa watu mbalimbali ndani ya kundi fulani. Na wakati wa kuandaa sera ndio mtu/watu wanatoa hayo mawazo tofauti na baada ya mchakato 'a consesus' inafikiwa kwa maana ya sera. Kwa mbunge kama Shibuda kusimama bungeni na kueleza mtizamo tofauti kisera when infact alikuwa na muda wa kufanya hivyo wakati wa uandaaji wa sera yenyewe ni 'sabotage'. Na huyu Shibuda amefanya hii sabotage sio mara moja au mbili, several times. Ni sawa na kung'oa reli baada ya kiberenge kupita. Na kama CCM ingekuwa muumini mzuri wa hicho unachikiita 'intra-party demokrasi' tusingekuwa tunasikia 'naunga mkono hoja mia kwa mia lakini sikubalini....'
Sasa jambo ambalo limetawala karibu magenge yote ya story hapa Arusha ni hili sakata la madiwani wa Arusha kukataa kupelekeshwa?...Wananchi wa Arusha wanataka amani ya kudumu sasa ili wajikite katika shughuli za maendeleo. Amani haipatikani bila haki.********
Hivyo, wananchi wanasema imefika wakati sasa kwa viongozi wa chadema kujivua gamba angalau ziwepo nyuso mpya zitakazoleta matumaini mapya.Na nyuso hizo ziwe za vijana atakaopambana na Nape wa CCM ambaye anaonekana kuwatishio sasa na viongozi waliopo sasa CDM wamezeeka na nguvu za kutawala jukwaa zinaisha. Nape anaweza kuwa tishio kwa ccm B, C au D lakini kamwe hawezi kuwa na lolote nje ya ccm! Na kama ccm wanaona Nape ni kifaa basi naweza mko kwenye matatizo makubwa kuliko ilivyodhaniwa hapo awali******.