Wananchi washangazwa na udikiteta unaofanywa na viongozi wa CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wananchi washangazwa na udikiteta unaofanywa na viongozi wa CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by siraji, Jul 24, 2011.

 1. s

  siraji Member

  #1
  Jul 24, 2011
  Joined: Mar 13, 2010
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huku mitaani wananchi wameduwazwa na udikiteta unaoendelezwa na uongozi wa juu ndani ya chama hicho.Wamekuwa wakijiuliza iweje kila jambo viongozi watake kulitolea uamuzi?.Wananchi hapa mtaani wamekasirishwa na kitendo cha katibu wa CHADEMA kuonyesha usaliti wa demokrasia kwani amekuwa akihubiri kuwa serikali inahujumu demokrasia hapa nchini kumbe na yeye ndani ya chama chake hakuna demokrasia kabisa.

  Wananchi wamekuwa wakitolea mifano mambo kadhaa ambayo yamewahi kutokea ndani ya chama hicho na bado kikaendelea kuyafumbia macho huku suluhisho kikitoa vitisho vya kuwafukuza wanachama ambao wanaonekana kuhoji juu ya mwenendo ndani ya chama hicho.
  1.Wamekuwa wakikumbusha juu ya Zitto Kabwe alivyozuiwa na kikundi cha ati wazee wa chama asigombee uenyekiti na baadaye kuzushiwa mambo mbalimbali ikiwemo ati Zitto amenunuliwa na CCM nadhani tunayakumbuka haya kwani Zitto amepita katika kipindi kigumu mno.

  2.Pia, wananchi wamekuwa wakikumbushana juu ya lile tukio la Marehemu Chacha Wangwe alipohoji juu ya matumizi ya fedha za ruzuku ya chama kufaidisha watu wachache wa makao makuu huku ofisi za mawilayani na mikoa zikuwa katika hali mbaya kama sio taabani.Chacha Wangwe alizuliwa kashfa nyingi na kusema kwamba alikuwa amenunuliwa na CCM.Na alipotaka kutumia haki yake ya kidemokrasia kwa kutangaza kuwania uenyekiti ndani ya chama hicho mengi yalimkuta nadhani tunayakumbuka.

  3.Wananchi pamoja na wapenzi wa CDM wamekuwa wakizungumzia uchaguzi wa ndani ya chama hicho.Wanahoji iweje baadhi ya wagombea ambao hutoka katika mikoa isio ya Kilimanjaro na Arusha huenguliwa katika uchaguzi huo?.Wanatoa mfano wa kuenguliwa kwa baadhi ya wagombea katika uchaguzi wa BAVICHA, wanasema udikiteta na upendeleo ndio ulitumika kuwaengua baadhi ya wagombea uenyekiti na kupitisha wale wasioweza kuhoji mwenendo wa mambo ndani ya chama hicho na si vinginevyo.Vijana wengi walidhani CDM ndio kimbilio lao kumbe wamebaini walipotea na sasa wameanza kusambaratika wengine juzijuzi tu wamejiunga na chama cha SAU na tumeona wamepewa ujumbe wa sekratirieti na wengine hivi karibuni tutawasikia NCCR-Mageuzi na CCM.

  4.Jambo lingine ambalo nimekuwa nikilisikia kwa wananchi mara kwa mara suala la Mh Shibuda.Hii kweli inaonesha kuwa no intra-party demokrasi CHADEMA.Yaani mbunge hapaswi kuwa na mawazo yake tofauti ndani ya Bunge.Hapaswi kupingana na wenzake hata kama wanazungumza pumba.Wananchi wamekuwa wakihoji iweje CDM imekuwa ikiponda CCM kuwa wabunge wake ni ndio mzee wakati wa kwao hawawapi fursa ya kutoa mawazo yao au kueleza bila kubughudhiwa na chama kile wananchoamini ni sahihi?.Hapa wananchi wengi wanaona CDM si mbadala wa CCM hata kidogo na mbadala hajazaliwa labda CCM yenyewe ipasuke vipande na hapo mbadala ndio utakuwepo na upinzani wa kweli sio wa Ze- Comedy utaonekana.Wanahoji hivi mbunge kutofautiana kidogo na msimamo wa chama chake ni dhambi?.Je mbunge alienda bungeni kusimamia maslahi ya chama au ya kwao wananchi?.Mimi mfanyabiashara hapa Arusha sina jibu labda wanachadema hasa viongozi wa juu wajitokeze na kujibu haya.

  5.Sasa jambo ambalo limetawala karibu magenge yote ya story hapa Arusha ni hili sakata la madiwani wa Arusha kukataa kupelekeshwa.Jambo hili limevuta hisia za watu wengi hapa na katika vyombo vya habari.Wananchi wamekasirishwa na kitendo cha viongozi wa CDM kuwatishatisha viongozi wao kwa kutaka kuwavua madaraka yao.Wananchi wengi sana hapa Arusha wanauliza hivi tulichagua viongozi hawa ikiwemo mbunge kutumikia chama au sisi wana Arusha?.Iweje chama kiwalazimishe madiwani wake kutanguliza maslahi ya chama badala ya maslahi yetu?.Sisi hatutaki vurugu kila kukicha ambazo zinapelekea kuuwawa kwa ndugu zetu.Wananchi wa Arusha wanataka amani ya kudumu sasa ili wajikite katika shughuli za maendeleo.Wananchi wengi wanaamini madiwani ambao wameshika vyeo hapa Arusha wakiongozwa na Naibu Meya Mh Estomih Mallah litakuwa suluhisho la mikwaruzo mingi ambayo imetokea hapa Arusha.Hivyo chama kuwalazimisha madiwani wavue vyeo walivyovipata kwa njia halali wakiongozwa na nia thabiti kabisa ya kujenga Arusha yetu ni kusaliti demokrasia na kuwasaliti wananchi waliowachagua kuungana na wale wa kutoka CCM ili kuleta maendeleo jijini.

  Hivyo, wananchi wanasema imefika wakati sasa kwa viongozi wa chadema kujivua gamba angalau ziwepo nyuso mpya zitakazoleta matumaini mapya.Na nyuso hizo ziwe za vijana atakaopambana na Nape wa CCM ambaye anaonekana kuwatishio sasa na viongozi waliopo sasa CDM wamezeeka na nguvu za kutawala jukwaa zinaisha.Pia, wanashauri utaratibu wa viongozi kupenda kuingilia mambo ya chini kama maamuzi yanayofikiwa na madiwani wao ukome kwani utakifanya chama kiondoke kwa wananchi na kubaki chini kuwa kampuni ya watu kama kilivyokuwa huko nyuma.Wanashauri structure ya chama ibadilishwa na maamuzi yawe yanafuata approach ya bottom-up badala ya sasa ya juu-chini.Wanasema utaratibu huu unalenga kuwatafutia umaarufu viongozi wa juu ili kila kitu waonekaneonekane na hawakotayari kuona mtu mwingine ndani ya chama akiibuka na kuwa maarufu zaidi yao.Wanasema udikiteta unakiua CHADEMA taratiiibu sawa na ugonjwa wa kansa kwa binadamu.

  Mie nimewasilisha kilio cha wananchi waliowengi wasioweza kufika hapa jamvini wadau!!!

  5.Wananchama wa CDM na watanzania kwa
   
 2. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #2
  Jul 24, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,935
  Likes Received: 351
  Trophy Points: 180
  Hao wananchi wengi mlikutana nao kwenye baa gani.
   
 3. Mumwi

  Mumwi JF-Expert Member

  #3
  Jul 24, 2011
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 593
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huyo katumwa na Nnape
   
 4. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #4
  Jul 24, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,393
  Likes Received: 1,549
  Trophy Points: 280
  cdm inawanyima usingizi!
   
 5. s

  siraji Member

  #5
  Jul 24, 2011
  Joined: Mar 13, 2010
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wanajamvi ni vyema tukajikita kwenye hoja za wananchi na tusipambane na mtoa mada.Mimi nimewasilisha malalamiko ya wananchi ambao nimekuwanikisikia wakiyatoa dhidi ya CHADEMA.Nimekuwa nikiwasikia mitaani na kuyachukua nikayamwaga hapa jukwaani jinsi yalivyo.Tusipuuze hoja zao kama tunakitakia mema CHADEMA.
   
 6. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #6
  Jul 24, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,125
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Hili Suala la Chacha Wangwe nafikiri linahitaji elimu ya ziada kwa wananchi. Hivi kweli kama Chacha Wangwe angekuwa aliuawa na viongozi wa CHADEMA, CCM wangeliacha tu lipite hivhivi? Si ungekuwa ndo mtaji wao wa kisiasa? Ilikuwaje yule aliyekuwa na Chacha kwenye gari aliachiwa? Tena kwa msamaha wa rais? Huyu Rais ina maana anafagilia ugaidi?

  Taarifa zisizo rasmi zinasema Malya ni usalama wa Taifa, ninachojiuliza hapa, ni vipi usalama wa taifa atumiwe na chadema katika masuala ya mauaji ya mtu asiye na hatia? Nafikiri at a time tuwe makini na hoja tunazozitoa. Vinginevyo mimi naweza kusema kwamba Chacha Wangwe aliuawa na Kikwete, kwa kuwa alimpa msamaha muuaji? Na tena usalama wa taifa ni wafanyakazi wa Ikulu, bila shaka alitumwa na Ikulu kwenda kumuua Chacha.

  Ninaamini wangekuwa CHADEMA ndo waliomuua Chacha basi, Mallya angewekwa sawa aseme kila kitu halafu polisi wangetangaza kwenye magazeti kwamba Chadema ndio waliomuua Chacha. Na huo ungekuwa ndo mwisho wa CHADEMA katika anga za siasa. Maana CCM zao ni kutafuta weak points za CHADEMA na kuzitumia kwenye kujijenga. Sasa wasingeitumia hiyo?
   
 7. N

  Ngoks Member

  #7
  Jul 24, 2011
  Joined: Jul 21, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hakuna chama duniani ambacho hakina katiba, sera, kanuni, mwongozo n.k. Mtu yeyote anayepinga uongozi na mambo tajwa hapo juu, yapaswa ajiengue, au asubiri uchaguzi agombee. CDM HAINA UBAGUZI WA AINA YOYOTE!
   
 8. Henry Kilewo

  Henry Kilewo Verified User

  #8
  Jul 24, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 888
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Yaani mkikaa huko chumbani kwenu na wake zenu mnawaza kuishambulia chadema? Ila kwakuwa ni chama makini hoja kama hizi ambazo hazina mashiko kwetu hazina nafasi wala kwa wananchi wa ARUSHA hazina nafasi. Chuki binafsi haziwezi kushindana na umma hata siku moja. So endelea kukuza kipaji chako cha propaganda
   
 9. F

  FJM JF-Expert Member

  #9
  Jul 24, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,090
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Wamekuwa wakijiuliza iweje kila jambo viongozi watake kulitolea uamuzi? - Pengine ingekuwa vizuri viongozi wa ccm wakaiga toka CHADEMA na kufanya maamuzi badala ya 'kulia'.

  Wamekuwa wakikumbusha juu ya Zitto Kabwe .... kuzushiwa mambo mbalimbali ikiwemo ati Zitto amenunuliwa na CCM ...Hazushiwi mtu hapa, unakumbuka simu na emails za Zitto zilivyoanikwa kwenye mwanahalisi?

  Wanahoji iweje baadhi ya wagombea ambao hutoka katika mikoa isio ya Kilimanjaro na Arusha huenguliwa katika uchaguzi huo?.Wanatoa mfano wa kuenguliwa kwa baadhi ya wagombea katika uchaguzi wa BAVICHA.. Heche anatoka Arusha, au Kilimanjaro?

  Hii kweli inaonesha kuwa no intra-party demokrasi CHADEMA.Yaani mbunge hapaswi kuwa na mawazo yake tofauti ndani ya Bunge... Kuna tofauti kati ya mgongano wa mawazo na tofauti kwenye sera. Sera ni accummulation ya mitizamo tofauti toka kwa watu mbalimbali ndani ya kundi fulani. Na wakati wa kuandaa sera ndio mtu/watu wanatoa hayo mawazo tofauti na baada ya mchakato 'a consesus' inafikiwa kwa maana ya sera. Kwa mbunge kama Shibuda kusimama bungeni na kueleza mtizamo tofauti kisera when infact alikuwa na muda wa kufanya hivyo wakati wa uandaaji wa sera yenyewe ni 'sabotage'. Na huyu Shibuda amefanya hii sabotage sio mara moja au mbili, several times. Ni sawa na kung'oa reli baada ya kiberenge kupita. Na kama CCM ingekuwa muumini mzuri wa hicho unachikiita 'intra-party demokrasi' tusingekuwa tunasikia 'naunga mkono hoja mia kwa mia lakini sikubalini....'

  Sasa jambo ambalo limetawala karibu magenge yote ya story hapa Arusha ni hili sakata la madiwani wa Arusha kukataa kupelekeshwa?...Wananchi wa Arusha wanataka amani ya kudumu sasa ili wajikite katika shughuli za maendeleo. Amani haipatikani bila haki.

  Hivyo, wananchi wanasema imefika wakati sasa kwa viongozi wa chadema kujivua gamba angalau ziwepo nyuso mpya zitakazoleta matumaini mapya.Na nyuso hizo ziwe za vijana atakaopambana na Nape wa CCM ambaye anaonekana kuwatishio sasa na viongozi waliopo sasa CDM wamezeeka na nguvu za kutawala jukwaa zinaisha. Nape anaweza kuwa tishio kwa ccm B, C au D lakini kamwe hawezi kuwa na lolote nje ya ccm! Na kama ccm wanaona Nape ni kifaa basi naweza mko kwenye matatizo makubwa kuliko ilivyodhaniwa hapo awali.
   
 10. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #10
  Jul 24, 2011
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  mTOA MAADA HANA AKILI TIMAMU, HATA KAMA ZIPO NI MTUMIA VIROBA UNAJUWA VIROBA HUPUNGUZA INTELLIGENCE YA MTU, CDM IPO KWA AJILI YA WATANZANIA , NANI AMETOKA NJE YA KILIMANJARO AKAENGULIWA SAANANE NI WA KILMANJARO NA ALIENGULIWA HECHE NI WA TARIME ALIACHWA , NO RESERACH NO RIGHT TO SPEAK NYIE VIJANA WA NAPE MMEPINDA
   
 11. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #11
  Jul 24, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 9,588
  Likes Received: 2,924
  Trophy Points: 280
  Hao wana ccm walio kutuma kuleta upuuzi huu ulikaa nao msikiti gani?
   
 12. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #12
  Jul 24, 2011
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Anaza Mayai on work!
   
 13. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #13
  Jul 24, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  Mimi mwenyewe nilikuwa napenda sana CHADEMA, lakini tangu walivyomuua Chacha Wangwe moyo wangu umekasirika sana.
   
 14. M

  Maga JF-Expert Member

  #14
  Jul 24, 2011
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 323
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Bado tuna safari ndefu kwenda kwenye mnara wa uelevu
   
 15. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #15
  Jul 24, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 36,241
  Likes Received: 14,481
  Trophy Points: 280
  wewe siraji sijui miraji .. ni mtoto wa make yupi? wa kwanza ? au yule mwingine
   
 16. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #16
  Jul 24, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 10,999
  Likes Received: 1,881
  Trophy Points: 280
  Mkuu achana nae huyo hawajui nini maaana ya katiba ya chama.
   
 17. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #17
  Jul 24, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 10,999
  Likes Received: 1,881
  Trophy Points: 280
  Una USHAHIDI au una copy na kupest? Mtu mzima hovyoo.
   
 18. s

  sweke34 JF-Expert Member

  #18
  Jul 24, 2011
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 2,530
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  unazungumzia wananchi wachache wanachama wa CCM au wananchi wanachama wa CHADEMA?
   
 19. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #19
  Jul 24, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,883
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 135
  ni heri kuwa mchawi kuliko kuwa mnafiki. Unalipwa kiasi gani kwa huo unafiki?
   
 20. M

  Molemo JF-Expert Member

  #20
  Jul 24, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,256
  Likes Received: 380
  Trophy Points: 180
  acha maneno ya kitapeli ndugu yangu.Hivi unamwamini Mungu kweli? Umeandika kama mpagani.Hela za rushwa hakika zitakuangamiza.
   
Loading...