Wananchi washangazwa na udikiteta unaofanywa na viongozi wa CHADEMA

Mtoa mada kakurupuka hivi wewe uko Arusha ipi, hii hii nayo ifahamu au kuna Arusha nyingine, hoja zilizotanda nchi nzima ni mgao wa umeme, wizi Jairo na ziara za Kikwete. Wewe hizo zako sijui umezichomoa wapi, kiukweli umejidhalilisha hakuna hata point. fikirie tena uandika hoja zenye maana vingenevyo hizo zote ni hoja mfu.
 
mTOA MAADA HANA AKILI TIMAMU, HATA KAMA ZIPO NI MTUMIA VIROBA UNAJUWA VIROBA HUPUNGUZA INTELLIGENCE YA MTU, CDM IPO KWA AJILI YA WATANZANIA , NANI AMETOKA NJE YA KILIMANJARO AKAENGULIWA SAANANE NI WA KILMANJARO NA ALIENGULIWA HECHE NI WA TARIME ALIACHWA , NO RESERACH NO RIGHT TO SPEAK NYIE VIJANA WA NAPE MMEPINDA

Ndiyo,huyu mleta mada ana lake jambo....anywats,nilienguliwa lakini ......................................................................................! ! !
 
Sometimes unaweza kujikuta unarelease adrenaline hormone & gastric juice kwenye Ini lako bure na ukapata peptic ulcers, threads kama hizi huwa sina cha kujibu wala kujenga zaidi ya kuziepuka.
Najitahidi kutafuta sehemu ya kuandika katikati ya mistari yake ila nimekoswa kabisa.
Kila la kheri mwanzilishi.
Naona kuna wakati mtu anadhani kuwa maaruf JF ndio kukubalika kwenye jamii
.
 
Wamekuwa wakijiuliza iweje kila jambo viongozi watake kulitolea uamuzi? - Pengine ingekuwa vizuri viongozi wa ccm wakaiga toka CHADEMA na kufanya maamuzi badala ya 'kulia'.

Wamekuwa wakikumbusha juu ya Zitto Kabwe .... kuzushiwa mambo mbalimbali ikiwemo ati Zitto amenunuliwa na CCM ...Hazushiwi mtu hapa, unakumbuka simu na emails za Zitto zilivyoanikwa kwenye mwanahalisi?

Wanahoji iweje baadhi ya wagombea ambao hutoka katika mikoa isio ya Kilimanjaro na Arusha huenguliwa katika uchaguzi huo?.Wanatoa mfano wa kuenguliwa kwa baadhi ya wagombea katika uchaguzi wa BAVICHA.. Heche anatoka Arusha, au Kilimanjaro?*****

Hii kweli inaonesha kuwa no intra-party demokrasi CHADEMA.Yaani mbunge hapaswi kuwa na mawazo yake tofauti ndani ya Bunge... Kuna tofauti kati ya mgongano wa mawazo na tofauti kwenye sera. Sera ni accummulation ya mitizamo tofauti toka kwa watu mbalimbali ndani ya kundi fulani. Na wakati wa kuandaa sera ndio mtu/watu wanatoa hayo mawazo tofauti na baada ya mchakato 'a consesus' inafikiwa kwa maana ya sera. Kwa mbunge kama Shibuda kusimama bungeni na kueleza mtizamo tofauti kisera when infact alikuwa na muda wa kufanya hivyo wakati wa uandaaji wa sera yenyewe ni 'sabotage'. Na huyu Shibuda amefanya hii sabotage sio mara moja au mbili, several times. Ni sawa na kung'oa reli baada ya kiberenge kupita. Na kama CCM ingekuwa muumini mzuri wa hicho unachikiita 'intra-party demokrasi' tusingekuwa tunasikia 'naunga mkono hoja mia kwa mia lakini sikubalini....'

Sasa jambo ambalo limetawala karibu magenge yote ya story hapa Arusha ni hili sakata la madiwani wa Arusha kukataa kupelekeshwa?...Wananchi wa Arusha wanataka amani ya kudumu sasa ili wajikite katika shughuli za maendeleo. Amani haipatikani bila haki.********

Hivyo, wananchi wanasema imefika wakati sasa kwa viongozi wa chadema kujivua gamba angalau ziwepo nyuso mpya zitakazoleta matumaini mapya.Na nyuso hizo ziwe za vijana atakaopambana na Nape wa CCM ambaye anaonekana kuwatishio sasa na viongozi waliopo sasa CDM wamezeeka na nguvu za kutawala jukwaa zinaisha. Nape anaweza kuwa tishio kwa ccm B, C au D lakini kamwe hawezi kuwa na lolote nje ya ccm! Na kama ccm wanaona Nape ni kifaa basi naweza mko kwenye matatizo makubwa kuliko ilivyodhaniwa hapo awali******.

Mkuu wangu FJM nimefurahi sana kwani umejibu hoja kikubwa na kwa usahihi kabisa, umeonyesha ukomavu wa CDM kwa kujibu fact nono zinazo pagusa kulekule kulipochokozwa. Ila naomba nami niongezee zege kidogo kwa ajili ya kufanya finishing ya majibu ya mada husika kupitia muongozo wa majibu yako makini kama ifuatavyo mkuu wangu:

1.Hapo Kwenye alama ya ***** Pia vijana walioenguliwa uchaguzi Bavicha ushahidi wa sababu za kuenguliwa ulishatolewa kupitia magazeti ukiainisha mchakato wote wa rushwa kupita Mpesa na Tigo uliofanywa na wahusika wote walioenguliwa.

2.Hapo kwenye alama ya ****** Ayo magenge yote ya story ya Arusha anayoyataja muandishi husika ndo wale watu 30 tu (na picha zilionyesha hapa JF) waliohudhuria shughuli ya kujipongeza kufanikisha muafaka feki yaani kale kashughuli kalichofanyika nje ya Ofisi ya Halmashauri ya Arusha mjini hivi majuzi???

3.Hapo kwenye alama ******* Sura za ya zamani inayopingwa ni Slaa kwa sababu amekua akionyesha matumaini mapya na imani kwa watanzania wengi wanaopenda haki. Sura hii ya Slaa(old wine in lattest bottle) inapingwa kwa sababu ni Mwiba kwa mafisadi ya nchi hii. Sera ya kujivua Gamba ni sera ya CCM haina nafasi CDM. Nape hafai kufananishwa na kijana yeyote ndani CDM kwani hasogei hata nukta moja, ukweli wake unajulikana na any reasonable man.
 
Sira G, Mara nyingine tambua ya kuwa wote waliopo JF si wapo na masikio, macho na akili zisizo katika mwanga, naomba ni kiri kwa imani na uwelewa wangu kuwa JF ni sehemu ya watu makini. Ni dhahiri kwa wenye kujua mbwa wa mwenyewe apati chakula majalalani na ukimwona jalalani ujue ni koko, wewe kama wewe kwa maoni yako naweza kukiri ni sawa, huo ni mtazamo wako, yaliyoandikwa hapo ni kama mtu anapiga stori kwa mama ntilie kisha anaondoka akijua amepata mada wakilishi. Inahitaji kila jambo utafakari katika ubongo wako kabla ya kuleta hapa, hiyo ni kazi ya ubongo, au pengine wenzetu hutumia kichwa kama pickup, mie sijui. Lukolo amejaribu kukupa kibatari kama giza kabisa anzia hapo!! au moshi mwingi? Kuibadilisha hii nchi inahitaji viboko kwani hata sheria mnaziweka nyie wenyewe hamzitaki, mnapiga kelele kwa jirani yako kuwa kiuka za kwake, umejua je? Unafiki mtupu
 
Yani unajilazimisha tukuone kwamba upo nasi hapa Arusha wakati ipo wazi unapatikana makao makuu hapo. Hao wana Arusha unaowataja mara mia mia ndio wale 29 ukijumlisha na wewe mnakamilisha idadi ya watu 30 yaani ile idadi kamili iliyohudhuria kamkutano cha kupongeza muafaka feki uliyofanyika hapa Nje ya ofisi za halmashauri ya arusha ivi majuzi???
Pia ukirudi uko unapopaita mtaani kwa hao wanaArusha 29 waambie kwamba wewe SIRAJI umekosea na umewadanganya kwani SAANANE aliyeenguliwa Bavicha ni mtu wa KILIMANJARO na aliyebakizwa yaani HECHE ni mtu wa TARIME kulekule kwa kina CHACHA WANGWE tofauti na ulivyowaeleza hapo awali.
 
Hao wananchi wengi mlikutana nao kwenye baa gani.
Hao wananchi wengi ni wale 29 ukimjumlisha na yeye SIRAJI mwenyewe wanakua 30 yaani ile idadi ya wananchi waliohudhuria kale kamkutano cha kupongeza muafaka feki kalichofanyika hapa nje ya ofisi za halmashauri ya arusha ivi majuzi(picha ziliwekwa humu JF)
 
Mimi mwenyewe nilikuwa napenda sana CHADEMA, lakini tangu walivyomuua Chacha Wangwe moyo wangu umekasirika sana.
Anayehusishwa na kifo cha CHACHA WANGWE ni MALYA ambaye ni usalama wa taifa, Je muajiri wake ni nani?? je muajiri wake mkuu ni wa chama gani???
 
Mimi mwenyewe nilikuwa napenda sana CHADEMA, lakini tangu walivyomuua Chacha Wangwe moyo wangu umekasirika sana.

Mkuu ili umelisema makusudi ili kutimiza terms of reference lakini ukweli unaujua kabisa kwamba mipango ya kifo cha Wangwe iliratibiwa na Makamba akishirikiana na UWT. Kulikuwa na masuala mawili hapa, kwanza walimuua kulipiza kisasi kwa kutapeliwa (nitaeleza zaidi hapa chini) pili walitaka kuitumia nafasi hiyo kuisambaratisha Chadema (kwa hili waligonga ukuta).

Kwa nini CCM walimuua Wangwe? Wangwe alivuta mshiko wa kutosha kutoka CCM ili aanzishe zali ambalo lengo lake ilikuwa ni kuisambaratisha Chadema. Aliyokuwa anayasema na kuyasimamia Wangwe yalipikwa na CCM. Walipoona kwamba lengo lao halijatimizwa na Wangwe kama walivyokubaliana naye (Wangwe aliisha shindwa kwenye hoja aliyokuwa ameianzisha), ikabidi wafanye mpango wa kumuua. Kilichomuua Wangwe ni uroho wa pesa, zilimtokea puani. Muuaji wa Wangwe kwa historia yake ni mtu aliyepelekwa kusomea ujasusi na serikali ya CCM huko Libya. Wangwe kwa kutokujua alikuwa anashirikiana nayeDeus) lakini wakati ulipofika, ilibidi afanye kazi yake.

Tafadhali usiseme ukweli hauujui!!!!

Tiba
 
Kwani katiba ya Chadema inasemaje kuhusu hilo? Na kama hiko kimya, inakuwaje?
 
Nawaambia Mnao - post humu chochote kile ambacho ni ANTI CHADEMA; mnatafuta ugomvi jamvini.

HAPA wimbo ni kusifu chadema.

Ukisifu Chadema; umeongea JEMA.

Ukikashifu CCM umeongea SAWASAWA.

Ila ukisifia/pongeza CCM au Serikali na Kubainisha changamoto za chadema; itakuwa unatafuta majibu ya kukosoa thinking yako.

In this forum.

IQ strong ni ile ya ku support chadema [hata kama itabainishwa changamoto; kufumbia moto changamoto hiyo na kukashifu CCM na Serikali

IQ dhaifu ni ile ya Kusupport CCM na Serikali na kubainisha changamoto za chadema.

Gr8 thinkers huwa wanapokea criticism na kutoa credit where necessary. If you cannot do that, then utajiita tu great thinker; kumbe Tanker
 
Wanajamvi ni vyema tukajikita kwenye hoja za wananchi na tusipambane na mtoa mada.Mimi nimewasilisha malalamiko ya wananchi ambao nimekuwanikisikia wakiyatoa dhidi ya CHADEMA.Nimekuwa nikiwasikia mitaani na kuyachukua nikayamwaga hapa jukwaani jinsi yalivyo.Tusipuuze hoja zao kama tunakitakia mema CHADEMA.

Ni vizuri kukupuuza saana wewe binafsi na sio hao wananchi. Wananchi wameshaonyesha mtazamo wao kuhusu CDM kupitia kwa maandamano na mikutano ya hadhara. Hao wengi wako sijui ni wapi. CDM kinafuata kanuni na katiba ya chama.
 
Tatizo la Jf ya sasa ukiikosoa cdm unaambulia matus, ukikosoa ccm wanafurahai. Kuna ushauri mzuri unatolewa kama wana cdm tuupokee na kama kujibiwa ujibiwe na hoja. Cdm inaongozwa na watu na co malaika. Kuna baadhi wanataka kila siku ziwe post za kuisifia cdm kana kwamba haina mapunguzu.
 
Mimi mwenyewe nilikuwa napenda sana CHADEMA, lakini tangu walivyomuua Chacha Wangwe moyo wangu umekasirika sana.

Waliomuua Chacha Wangwe ni nyie CCM, na sasa hivi mnamchochea Shibuda akosane na viongozi wake ili naye mumuue kisha muwasingizie CDM kama kawaida yenu.Halafu wewe mbwiga hilo jina hulitendei haki, akina Mwita siyo wajinga wajinga hivyo
 
Hivi kwa nini hawa wajamaa hawaulizi kuhusu CUF, TLP etc..Ni CHADEMA tuuu...!! hofu ya nini wandugu??
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom