Wananchi wangapi walikataliwa Kupiga Kura Igunga?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,362
39,082
Kuna madai ambayo tulianza kuyasikia siku ya J'pili wakati waupigaji kura kuwa watu walikuwa wanakataliwa kupiga kura kwa sababu mbalimbali. Na baadaye madai haya yametolewa na pande zote mbili hasimu (Katibu Mkuu Mukama kwa upande wa CCM, na Mwenyekiti Mbowe kwa upande wa CDM).

Natumaini wote hawa wana ushahidi wa madai haya; binafsi ningependa kujua tu je vyama hivi vilifanya utaratibu wa kufuatilia na kujua wale waliokataliwa kupiga kura ni kina nani na sababu za kukataliwa ni zipi na kwa kufanya hivyo kuweza kujua kwa kiasi fulani idadi ya watu waliokataliwa kupiga kura kwenye jimbo hilo.

Kuna mtu ana namba isije kuwa ni idadi ambayo ni negligible - isingeweza kubadilisha matokeo. Kwa mfano (kama ni watu 100 kwenye jimbo zima hata kama wote wangeruhusiwa kupiga kura na wote wangeipigia CDM bado matokeo yasingebadilika).

Sidhani kama kwenda baada ya uchaguzi kuuliza watu kama walikataliwa yaweza kuwa njia sahihi ya kujua kilichotokea siku ya uchaguzi. Ni matumaini yangu CDM walifanya utaratibu wa kuorodhesha watu waliokataliwa kupiga kura kwenye vituo mbalimbali siku ya Jumapili mbili ya Oktoba.
 
Godwine

JF-Expert Member
Jan 15, 2010
1,371
279
Cha msingi mfumo wa kuandikisha kupiga kura ungeboreshwa na kuweza kuruhusu ata watu kupiga kura online na virevile vitambulisho vipya vya nchi hii ndivyo viwe shahada ya kupiga kura
 
Bob G

JF-Expert Member
Oct 5, 2011
2,351
447
vyama vinafanya kazi kubwa saana ya kutoa elimu, Hayo ya Igunga ungeyajua bila vyama kwenda kufanya siasa!
 
nzitunga

Senior Member
Oct 31, 2010
193
52
Kuwapata waliokataliwa kupiga kura kwa maana ya waliokwenda kituoni na kukatazwa kunaweza kusiwe na maana sana.
Watu walikatazwa kupiga kura kwa namna nyingi sana
1. Kubadilisha utaratibu baada ya saa saba mchana ambao vyama pamoja na tume vilishakubaliana. Naamini kuna watu ambao walikuwa wanaenda theni wakakutana na waliokataliwa.
2. Uboreshaji wa daftari la mpiga kura.
3. CCM kununua vitambulisho vya wapiga kura. Na mtu aliyetangazwa amekufa baada ya kukataa kuuza kadi yake kwa balozi wa CCM ni mfano wa kutosha. Ni wangapi wameona dk ya mwisho majina yao hayapo?

Maoni yangu: Tume ya Uchaguzi inadidimiza Demokrasia. Historia itakuja kuwashuta siku moja
 
Regia Mtema

R I P
Nov 21, 2009
2,970
848
Mwanakijiji sijaelewa lengo lako hasa katik sredi hii ni nini?nikijua nitaweza kucomment zaidi

QUOTE=Mzee Mwanakijiji;2600564]Kuna madai ambayo tulianza kuyasikia siku ya J'pili wakati waupigaji kura kuwa watu walikuwa wanakataliwa kupiga kura kwa sababu mbalimbali. Na baadaye madai haya yametolewa na pande zote mbili hasimu (Katibu Mkuu Mukama kwa upande wa CCM, na Mwenyekiti Mbowe kwa upande wa CDM).

Natumaini wote hawa wana ushahidi wa madai haya; binafsi ningependa kujua tu je vyama hivi vilifanya utaratibu wa kufuatilia na kujua wale waliokataliwa kupiga kura ni kina nani na sababu za kukataliwa ni zipi na kwa kufanya hivyo kuweza kujua kwa kiasi fulani idadi ya watu waliokataliwa kupiga kura kwenye jimbo hilo.

Kuna mtu ana namba isije kuwa ni idadi ambayo ni negligible - isingeweza kubadilisha matokeo. Kwa mfano (kama ni watu 100 kwenye jimbo zima hata kama wote wangeruhusiwa kupiga kura na wote wangeipigia CDM bado matokeo yasingebadilika).

Sidhani kama kwenda baada ya uchaguzi kuuliza watu kama walikataliwa yaweza kuwa njia sahihi ya kujua kilichotokea siku ya uchaguzi. Ni matumaini yangu CDM walifanya utaratibu wa kuorodhesha watu waliokataliwa kupiga kura kwenye vituo mbalimbali siku ya Jumapili mbili ya Oktoba.[/QUOTE]
 
Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,362
39,082
Si vizuri kwenda kwa kuamini tu; ni vizuri kuwa na japo ushahidi wa awali. Maana isije kuwa hakuna mtu aliyekataliwa kupigwa kura kama alienda kupiga kura. Sijali sana wale ambao hawakwenda kabisa kupiga kura; I'm more concerned na wale ambao walienda kupiga kura lakini hawakupiga kura. This number interests me much.
 
NewDawnTz

JF-Expert Member
Nov 15, 2010
1,668
362
Napata tabu sana kuwaza juu ya jambo hili kwa sababu kuu mbili

1. Ni ngumu kumuamini mkama....kama anaweza kusema lolote hata lenye kuingilia usalama wa taifa maadam apate "favor" ya wananchi, basi hashindwi kusema lolote ili kupata "sympathy" ya wananchi na kuonesha wao kama CCM na Serikali yao hawana tatizo lolote na watu kutokujitokeza kupiga kura

2. Kutokana na jambo la kwanza hapo juu nakosa mizani sahihi ya kupima pia taarifa ya Mbowe kwa kuwa itakuwa ni kusikia toka upande mmoja kutokana na kushindwa kumuamini mtoa kauli wa upande wa pili

Pamoja na hayo yote, bila kujali significance au insignificance ya idadi ambayo haijapiga kura, ni muhimu kufahamu hii ni haki ya kisheria na ya kikatiba kwa kila mtazania (hata awe ni mmoja tu kati ya watanzania wote) na kuwa na mfumo (kwa namna na tafsiri yoyote ile) ambao utamnyima kuitumia haki hii ni kosa kubwa sana (ukiachilia mbali la kisheria lakini pia la kibinadamu)...

Cha muhimu ni kuhakikisha mifumo yetu inaruhusu watu kupiga kura na sheria zitekelezwe (kama zipo) dhidi ya yeyote atakaeonekana kuzuia haki hii kwa namna iwayo yote (kwa maneno au kwa vitendo) bila huruma wala kujali anatoka chama gani......na hapa ndipo ugumu na kazi ilipo
 
Regia Mtema

R I P
Nov 21, 2009
2,970
848
Si vizuri kwenda kwa kuamini tu; ni vizuri kuwa na japo ushahidi wa awali. Maana isije kuwa hakuna mtu aliyekataliwa kupigwa kura kama alienda kupiga kura. Sijali sana wale ambao hawakwenda kabisa kupiga kura; I'm more concerned na wale ambao walienda kupiga kura lakini hawakupiga kura. This number interests me much.

Ni kweli kabisa kuna watu walikataliw kupiga kura ila kwa takwimu sidhani sisi kama CHADEMA tunazo kwakuwa kwa bahati mbaya hatukuweka rekodi.Wale tuliokuwa tunazunguka kwenye vituo vya kupitia kura na kukuta changamoto hii tulichokuwa tunafanya ni kutoa tu taarifa kw waratibu wa Kampeni nawao sina hakika kama watakuwa na takwimu.We were not smart kukumbuka kuweka takwimu..
 
Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,362
39,082
Ni kweli kabisa kuna watu walikataliw kupiga kura ila kwa takwimu sidhani sisi kama CHADEMA tunazo kwakuwa kwa bahati mbaya hatukuweka rekodi.Wale tuliokuwa tunazunguka kwenye vituo vya kupitia kura na kukuta changamoto hii tulichokuwa tunafanya ni kutoa tu taarifa kw waratibu wa Kampeni nawao sina hakika kama watakuwa na takwimu.We were not smart kukumbuka kuweka takwimu..

Lengo langu ni kujaribu kupata picha tu ya extent ya tatizo lilikuwa kubwa kiasi gani kama kuweza kuathiri matokeo. Kwa mfano katika mizunguko yako siku ile tatizo la watu kukatawaliwa kupiga kura lilikuwa kubwa kiasi gani? Unaweza ukanipa kisio la chini tu kwa mfano kwenye kituo kimoja kulikuwa na watu kama wangapi ambao hawakuweza kupiga kura au kuja kulalamika kuwa wamekataliwa kupiga kura? Au niulize kinyume chaka ni mara ngapi ulilazimika kutoa taarifa kwa wahusika kuhusu watu kukataliwa kupiga kura?
 
politiki

JF-Expert Member
Sep 2, 2010
2,376
1,504

mkifika mahakamani hili ndio litakuwa swali la kwanza jaji kukuuliza kuhusu idadi ya watu ambao walizuiwa kupiga kura na pili je mnayo mikanda ya
statement ya mukama kuwa chadema imeagiza makomando na watu wa kujitoa mhanga kutoka Afghanistan ??hiyo inaweza kutumika kama
ni kauli za kutishia amani na kuwatisha wananchi kushiriki kwenye uchaguzi endapo Bw.Mukama hatashindwa kuthibitisha kauli yake.
 
Regia Mtema

R I P
Nov 21, 2009
2,970
848
Lengo langu ni kujaribu kupata picha tu ya extent ya tatizo lilikuwa kubwa kiasi gani kama kuweza kuathiri matokeo. Kwa mfano katika mizunguko yako siku ile tatizo la watu kukatawaliwa kupiga kura lilikuwa kubwa kiasi gani? Unaweza ukanipa kisio la chini tu kwa mfano kwenye kituo kimoja kulikuwa na watu kama wangapi ambao hawakuweza kupiga kura au kuja kulalamika kuwa wamekataliwa kupiga kura? Au niulize kinyume chaka ni mara ngapi ulilazimika kutoa taarifa kwa wahusika kuhusu watu kukataliwa kupiga kura?

To be honest,I can't tell,sina takwimu!
 
politiki

JF-Expert Member
Sep 2, 2010
2,376
1,504
To be honest,I can't tell,sina takwimu!

kamanda mtema mnatutisha kidogo jamani chama makini hakitakiwi kutoa majawabu kama haya yasiyojitisheleza. wewe ni mbunge tunategemea
kuwa huko jikoni sasa inakuwaje makamanda wengine wanakwenda na info. frontline bila kuwa brief nyie wenyewe kwa wenyewe kwanza ili nyie
wote muwe na coherent message. basi tunategemea utawasiliana na wahusika ili tupate majawabu ya uhakika.
 
TIMING

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
22,850
8,678
To be honest,I can't tell,sina takwimu!
Thank you Regia for being honest

hakuna haja ya kupika data, and unaeleweka kwani kwa mfumo wa maisha ya bongo, ni vigumu sana hata kujua kaya moja (hasa za wasiojua kusoma au kuandika kama Igunga ina watu wangapi

Nevertheless, you can do post election data collection mnaweza kuwa na pa kuanzia
 
TIMING

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
22,850
8,678
kamanda mtema mnatutisha kidogo jamani chama makini hakitakiwi kutoa majawabu kama haya yasiyojitisheleza. wewe ni mbunge tunategemea
kuwa huko jikoni sasa inakuwaje makamanda wengine wanakwenda na info. frontline bila kuwa brief nyie wenyewe kwa wenyewe kwanza ili nyie
wote muwe na coherent message. basi tunategemea utawasiliana na wahusika ili tupate majawabu ya uhakika.
mkuu uko sawa kweli hapo?

kwa weledi wako unadhani in 3 days unaweza kuwa na statistics za waliokosa kupiga kura? then ujue na sababu ya kukosa (considering eligibility criteria) ??

kama kuhesabu makarasi yakiyo kwenye maboksi imezidi 36 hours, how would head counts from the whole constituent work faster? tena without all attention na pesa?

swali la mwanakijiji ni muhimu sana, tena sana tu na by december wajuvi watagundua
 
FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
74,138
75,105
Kuna madai ambayo tulianza kuyasikia siku ya J'pili wakati waupigaji kura kuwa watu walikuwa wanakataliwa kupiga kura kwa sababu mbalimbali. Na baadaye madai haya yametolewa na pande zote mbili hasimu (Katibu Mkuu Mukama kwa upande wa CCM, na Mwenyekiti Mbowe kwa upande wa CDM).

Natumaini wote hawa wana ushahidi wa madai haya; binafsi ningependa kujua tu je vyama hivi vilifanya utaratibu wa kufuatilia na kujua wale waliokataliwa kupiga kura ni kina nani na sababu za kukataliwa ni zipi na kwa kufanya hivyo kuweza kujua kwa kiasi fulani idadi ya watu waliokataliwa kupiga kura kwenye jimbo hilo.

Kuna mtu ana namba isije kuwa ni idadi ambayo ni negligible - isingeweza kubadilisha matokeo. Kwa mfano (kama ni watu 100 kwenye jimbo zima hata kama wote wangeruhusiwa kupiga kura na wote wangeipigia CDM bado matokeo yasingebadilika).

Sidhani kama kwenda baada ya uchaguzi kuuliza watu kama walikataliwa yaweza kuwa njia sahihi ya kujua kilichotokea siku ya uchaguzi. Ni matumaini yangu CDM walifanya utaratibu wa kuorodhesha watu waliokataliwa kupiga kura kwenye vituo mbalimbali siku ya Jumapili mbili ya Oktoba.

Wewe si mwandishi kwanini hufatilii utuletee hapa habari. Unatuuliza sisi? Unanchekesha!
 
FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
74,138
75,105
Ni kweli kabisa kuna watu walikataliw kupiga kura ila kwa takwimu sidhani sisi kama CHADEMA tunazo kwakuwa kwa bahati mbaya hatukuweka rekodi.Wale tuliokuwa tunazunguka kwenye vituo vya kupitia kura na kukuta changamoto hii tulichokuwa tunafanya ni kutoa tu taarifa kw waratibu wa Kampeni nawao sina hakika kama watakuwa na takwimu.We were not smart kukumbuka kuweka takwimu..

Nyie mlikuwa "smart" kutazama Rostam hajafanya nini! maana hiyo ndio report uliyotuletea hapa JF kutoka huko.
 
Daudi Mchambuzi

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
61,292
124,869
Ni kweli kabisa kuna watu walikataliw kupiga kura ila kwa takwimu sidhani sisi kama CHADEMA tunazo kwakuwa kwa bahati mbaya hatukuweka rekodi.Wale tuliokuwa tunazunguka kwenye vituo vya kupitia kura na kukuta changamoto hii tulichokuwa tunafanya ni kutoa tu taarifa kw waratibu wa Kampeni nawao sina hakika kama watakuwa na takwimu.We were not smart kukumbuka kuweka takwimu..
Safi sana dada angu, wachache sana wanakiri makosa pale wanapokosea.
 
Daudi Mchambuzi

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
61,292
124,869
kamanda mtema mnatutisha kidogo jamani chama makini hakitakiwi kutoa majawabu kama haya yasiyojitisheleza. wewe ni mbunge tunategemea
kuwa huko jikoni sasa inakuwaje makamanda wengine wanakwenda na info. frontline bila kuwa brief nyie wenyewe kwa wenyewe kwanza ili nyie
wote muwe na coherent message. basi tunategemea utawasiliana na wahusika ili tupate majawabu ya uhakika.
Amekiri makosa ya kibinadamu kuhusu takwimu sioni umuhimu wa kumkomalia namna hii. Huyu dada kaonyesha political maturity.
 
2 Reactions
Reply
Top Bottom