Wananchi wanaomjua Hamza wanasema alikuwa mtu mzuri, mwana CCM kindakindaki na Mmiliki wa mgodi

Mbuzi kala mkeka! wameamua kumtosa kada wao eti gaidi! polisiccm peponi kwenu kamwe hamuwezi kufika hata kwa dawa!
 
Mimi sidhani kama Polisi walifanya upelelezi wo wote! Tukio zito kama hilo haliwezi kuchunguzwa kwa muda mfupi namna hiyo ndiyo maana majibu yaliyotolewa ni mepesi sana.
 
hivi mlitegemea polisi walete majibu gani???? mlimsikia hamza alivyokuwa anatuma taarifa kwa siro..........ukiangalia ile clip dk za mwishoni hamza alianza kujisalimisha....ili akamatwe akaseme ukweli.....wakatumia nafasi hiyo kumlipua.....walishindwa wapi kumlenga mikono?? kwanza polisi wetu ni hovyo sana...hata shabaha hawana....... polisi hawezi kujichunguza kabisa......na pia tunae RAIS DHAIFU mno.....kiumbe dhaifu......
 
samahani kwa kuandika hivi....simhukumu marehemu Hamza wala kuitetea Serikali najaribu kuwaza tofauti nakujenga hoja fulani.

Elchapo na kundi lake la Sinaloa Cartel kule kwao ni watu wema sana na walijitoa sana kusaidia jamii..Pablo naye pia alikuwa mtu mwema sana pale kwao, Osama binladen wapo wamilioni ya watu wanaamini binladen ni mtu mwema na ameonewa tu na USA na alikuwa akitetea haki zao....wapo majambazi mtaani tunaishi wao ni wati wema sana na hatujui lolote kuhusiana na dark side yao....wale vijana wa 11sept baadhi waliishi Germany na mama aliyekuwa jirani yao aka mpangaji mwezao alisema walikuwa vijana safi sana, wakalimu sana nk....

Kama tunaamini Hamza kaonewa na sio Gaidi basi ni vyema mmoja wetu akadai justice for Hamza kwa either kufungua kesi kudai uchunguzi huru au ukweli wa jambo...kesi sio lazima iwe Tanzania popote pale tunaweza kufungua kudai justice for Hamza....
Issue ya Hamza kudhulumiwa ilianzia mitandaoni kwa raia na mamlaka zinakuja kutumbia Hamza ni gaidi, tuamini mtandaoni au Serikali... wanaharakati wetu ambao wengi wanasheria, wanaharakati wetu kule twita kwanini wasiidai haki ya Hamza kwa kukusanya ushahidi na kuishitaki serikali.?
 
Wanaomtetea muuaji Hamza, Wamesikia yaliotokea leo huko New Zealand??? Mjamaa kajidai kuchoma watu visu kwa shopping mall. Polisi hawakumkawiza na hawakua na muda wa ETI tumkamate tukamhoji.. wamempeleka kuzimu fasta.
Alichofanya hamza ni uhalifu,ila namna ambavyo suala lake limetazamwa sio sahihi hasa ukizingatia kwamba kuna vyanzo vingi sana vya taarifa ambazo zinaelekeza kabisa kwamba hii kesi inaweza kuwa kama ile kasi ya kila Abdalah Zombe isipokuwa tu huyu amekuwa na ujasiri wa kuchukua sheria mikononi.
 
Najaribu kuwaza tuu kwa sauti ya chinichini......ivi kwa nnavowafaham magaidi hao wenyewe hasa kina alshabab au boko haram.....kweli kabisa kashika mashine gani mbili zina risasi za kutosha wale raia wote pale mbele yake anawatizama tuu???.....mmmmhhh sijui bana
 
Wanaomtetea muuaji Hamza, Wamesikia yaliotokea leo huko New Zealand??? Mjamaa kajidai kuchoma watu visu kwa shopping mall. Polisi hawakumkawiza na hawakua na muda wa ETI tumkamate tukamhoji.. wamempeleka kuzimu fasta.
Usiseme "mjamaa"wala mbepari sema: gaidi!
 
Back
Top Bottom