Uchaguzi 2020 Wananchi wamkataa Diwani na Mbunge mbele ya Rais Magufuli kata ya kiloleni Busega

Huliza

JF-Expert Member
May 5, 2017
392
982
Rais Magufuli akiwa anaelekea Mwanza amewashawishi wananchi wamchague diwani wa ccm na Mbunge wa ccm lakini wananchi hao wamezomea na kukataa mbele ya Rais Magufuli

Wananchi hao wa kata ya kiloleni jimbo la Busega ambalo mgombea wao pendwa Bwana chegeni amekatwa jina lake wakati aliongoza kura za maoni wamekasirika mbele ya Rais kwa kuzomea

Mwananchi mmoja ameomba kuelezea tatizo ,Mwananchi huyo wa ccm amesema mbunge na diwani wa ccm bwana Magoti hawafai

Rais amesisituza wakichagua mgombea mungine watajuta

Akitumia kilugha ambacho mimi sikuelewa ni lugha gani akiweka msisitizo,Aidha lugha hiyo ya utamaduni bado haikusaidia zomea zomea hiyo

Muda huu yupo live TBC saa tano

Wananchi wameweka ngumu na Rais anasema hatapeleka lami

Wananchi wanamjibu hatumtaki wala hatumchagui Bwana Magoti diwani

Kazi kazi kweli kweli
 
Umeongeza chumvi, mwananchi kasema hawana matatizo na hao waliopitishwa na chama ila wakishachaguliwa hawafanyi mikutano
Wewe ni mwana ccm au chadema?
Kama ni chadema endelea kuwa chadema

Kama ni mwana ccm kama mimi yakupasa kutoa ushauri na sio kutoa taarabu na ngonjera za kujibishana na mleta uzi

Je mleta uzi ameandika uwongo,Nawe umekili ni kweli kuna tatizo

Sasa kama kuna tatizo kwanini alirudishwa diwani ambaye hakupita kura za maoni na mbunge

Kuna matatizo tunasababisha wenyewe ,
 
Back
Top Bottom