Wananchi wa Zanzibar na ‘chaguo la tatu’ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wananchi wa Zanzibar na ‘chaguo la tatu’

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by M TZ 1, Jan 26, 2012.

 1. M

  M TZ 1 Member

  #1
  Jan 26, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Lula wa Ndali Mwananzela

  WANANCHI wa Zanzibar wanadhulumiwa na wanadhulimiwa kweli kweli. Wanalazimishwa kuchagua kati ya vitu viwili na ni vitu viwili peke yake. Matokeo yake wananchi wa Zanzibar hawana uchaguzi wa kweli na hata kunyimwa uchaguzi bora. Katika elimu ya mantiki (logic) kuna kitu kinaitwa ulaghai wa hoja (fallacies). Ulaghai wa hoja ni namna ya kauli au hoja ambayo inajengwa kwa makosa na wakati mwingine kwa makusudi ili kumlaghai msikilizaji. Ulaghai huo hufanywa kwa kutegemea kwamba wasikilizaji hawawezi kugundua kuwa wanalaghaiwa.

  Njia mojawapo ya kufanya ulaghai wa hoja ni kuwashambulia watu badala ya hoja. Kwa mfano, mtu anakuja nyumbani kwako na kukuambia kuwa nyumba yako ina ufa mkubwa wewe badala ya kuangalia kama kweli kuna ufa (kuiangalia hoja yake) unaanza kumshambulia. “Wewe ni mshamba mkubwa nyumba yangu iwe na ufa mimi? Wewe una kichaa nini?” ni namna mojawapo ya mashambulizi ambayo kitaalamu yanaitwa ad hominem (kumshambulia mtu). Sasa mtu asiyejua kufikiri vizuri anaweza kurukia tu juu juu “kweli mshamba huyo, kwanza katumwa” na wote wawili wanaweza kudhania wanaishughulikia hoja ya ‘nyufa’. Hoja ya nyufa inaweza tu kupanguliwa kwa kuangalia pale ambapo yule mtu alionesha na kudai kuwa pana nyufa. Kama kweli pana nyufa hata yule mtu angekuwa kichaa, mshamba, mwizi, au mhuni mmoja ukweli utabakia kuwa nyumba ina nyufa!

  Njia nyingine ya kuwalaghai watu kwa hoja ni ile ya kuwapa kile kinachoitwa “ulaghai wa njia mbili pekee”. Kwa kitaalamu hii inaitwa “the fallacy of false dilemma” yaani mtu anaambiwa kuwa vitu vya kuchagua ni vitu viwili tu. Mfano mzuri uko kwenye lugha yetu ya Kiswahili ambapo mtu anaweza kumwambia mwingine “bwana uchaguzi unao kusuka au kunyoa”. Sasa kwa haraka haraka mtu asiyefikiri anaweza kuamini kuwa anao uchaguzi wa ama “kusuka au kunyoa”. Mtoto anaweza kufikiria hivyo lakini mtu mzima anaweza akasema mbona kuna ‘kuchana?’, mbona kuna “kupunguza kidogo tu?”. Kumbe uamuzi wa “kusuka au kunyoa” ni njia panda ya uongo kwamba mtu anazo njia mbili tu za kuchagua.

  Sasa mtu au kundi la watu linaweza kutumia nguvu kubwa sana kuwashawishi watu kuwa zipo njia mbili tu za kwenda na njia nyingine yoyote ya tatu haipo au haiwezekani. Na kama imani hii inajengwa kwa muda mrefu sana wapo watu wanaamini pasipo shaka kweli wanazo njia mbili tu. Ni sawa sawa na mahali kwenye kijiji kimoja kulikuwa na mto na watu walikuwa wanatumia mahali fulani kuvuka kwa kutumia daraja walilojijengea. Kwa muda mrefu uchaguzi ulikuwa wa aina mbili tu kwamba kuvuka kwenda upande wa pili ilikuwa ni ama kutumia mtumbwi au kuogelea.

  Hadi alipokuja mtu na kuwaambia kwa nini watoto wao waliendelea kufa kwa kuogelea au mitumbwi kusombwa na maji? Kwa nini wasiamue kujenga daraja? Wale wanakijiji walianza kulalamika kuwa gharama za kujenga daraja ni kubwa sana na hawakuwa na wataalamu. Hadi yule mtu akawashawishi na kuwaonesha kuwa wakitafuta mahali ambapo upana wake si mrefu wangeweza kuangusha minazi miwili na kutoka hapo kuweka mbao na kujitengenezea daraja bila kutumia nguvu kubwa. Matokeo yake wakajipatia njia nyingine ya kwenda ng’ambo.

  Wananchi wa Zanzibar wanalazimishwa kuchagua kati ya CCM na CUF kama njia mbili pekee kwa maisha yao ya kisiasa na utawala. Kwa miaka sasa wananchi hao wameambiwa kuwa siasa za Zanzibar zitaamuriwa na vyama hivyo viwili peke yake na kuwa ni CCM na CUF tu ndio wenye mawazo bora kuhusu Zanzibar. Na kwa bahati mbaya sana tangu kurudi kwa mfumo wa vyama vingi siasa za Zanzibar zimetawaliwa na vyama hivyo viwili kana kwamba ndivyo vyenye ubia pekee wa kuitawala Zanzibar na wapo watu Zanzibar ambao hawawezi kufikiri kabisa (hawataki na hawana uwezo) nje ya CCM au CUF. Kwa watu hawa ni ama unaunga mkono CUF au CCM! Na vijana wameuziwa hizi njia mbili pekee!

  Kwa mara ya kwanza, hata hivyo, Zanzibar na hususan wananchi wa Jimbo la Uzini wanapewa nafasi ya kumchagua mgombea kutoka CHADEMA ambaye anakubalika na kuwakilisha mawazo tofauti na yale ya wana CCM na wana CUF. Ni chaguo la tatu, chaguo tofauti. Kwamba wananchi wa Uzini wanaitwa kufikiria kubadilisha kabisa siasa za Zanzibar kwa kuleta kwa mara ya kwanza chama tofauti na siasa tofauti na vile vile kutoa sauti tofauti kutoka Zanzibar. CHADEMA wameamua kumpitisha Mwalimu Ali Mbarouk Mshimba kuwa mgombea wa jimbo hilo. Wengine wanasema haiwezekani kwa sababu Zanzibar ni CCM au CUF lakini yumkini Zanzibar ikawa na nafasi kwa chama kingine!

  Sasa kwa kuangalia kwa haraka ni wazi kuwa Mshimba anaweza kuonekana hana nafasi kwa sababu eneo hilo ni ngome ya CCM. Lakini wananchi wa Uzini watamchagua yeyote alimradi anatoka CCM? Ni kweli wananchi wa Uzini hawawezi kuangalia njia ya tatu au chaguo la tatu kwa sababu wao na wazee wao waliapa kuchagua CCM bila kujali nani anasimamishwa? Je, wananchi wa Uzini watachagua CCM hata kama sera zake zimepitwa na wakati? Je, Mshimba anakuja na CHADEMA ana anakuja na sera gani kuhusu Zanzibar?

  Hatuna budi kuangalia Ilani ya Uchaguzi ya CHADEMA ya mwaka 2010 ambayo inatupa mwanga kidogo wa mawazo ya CHADEMA kuhusu wananchi wa Zanzibar. Ilani ya CHADEMA katika vipengele maalumu inazungumzia Zanzibar. Labda niweke hapa yale ambayo Ilani hiyo inadokeza ili wananchi wa Zanzibar wajue kuwa wakichagua mjumbe wa Baraza la Wawakilishi au mbunge kutoka CHADEMA wanachagua nini na atapigania nini.

  Serikali ya CHADEMA ina mpango madhubuti kabisa wa kuimarisha Muungano na kuhakikisha kuwa kero zote za Muungano zinaondolewa katika mwaka wa kwanza na kuachana na utaratibu wa kimazingaombwe unaofanywa na serikali ya CCM na kutishia Muungano wetu. Serikali ya CHADEMA itachukua hatua zifuatazo katika kuiwekea mazingira mazuri kwa maendeleo na katika kuimarisha Muungano:

  Suala la mafuta litaachwa mikononi mwa Serikali ya Zanzibar hasa tukizingatia kuwa visiwa hivi vina raslimali ndogo sana za kiuchumi. Masuala ya raslimali nyingine yatajadiliwa ili kuhakikisha kuwa Zanzibar inanufaika na raslimali za Tanzania na vile vile inatoa mchango wake sahihi katika uchumi wa taifa.

  Serikali ya CHADEMA itaitisha mkutano maalum wa pamoja wa Baraza la Wawakilishi na Bunge la Muungano na wadau wengine ili hatimaye kukaa chini kama ndugu wamoja na kujadili masuala yenye matatizo yanayohusu Muungano. Kutakuwa na kikao cha Pamoja cha Uongozi wa Taifa mara mbili kwa mwaka.•

  Serikali ya CHADEMA itahakikisha kuwa vikwazo mbalimbali ambavyo vinaonekana kutatiza ufanyaji wa biashara na uwekezaji katika visiwa hivyo vinaondolewa.

  11.2 Unguja
  Kwa vile Unguja ni eneo la kihistoria na historia yake imefungamana kabisa na historia ya Tanzania bara na pwani ya mwambao juhudi za wazi zitafanyika ili kulinda tunu hiyo ya kihistoria. Hii ni pamoja na:

  Kufanya ukarabati wa majengo na maeneo ya kihistoria yaliyoko Unguja ili kuhakikisha yanaingizwa na kutunzwa katika mfumo wa kisasa ili yaendelee kuwa ni urithi kwa vizazi vijavyo.

  Kwa kushirikiana na serikali ya Zanzibar, tutatenga eneo jipya kwa ajili ya ujenzi wa Jiji la Kisasa la Zanzibar (Zanzibar City) kwenye eneo ambalo litakubaliwa na Serikali ya Zanzibar ili hatimaye kujenga jiji la kisasa visiwani humo ambalo litakuwa ni kitovu cha utalii wa maeneo ya kisasa na yale ya kihistoria.

  11.3 Pemba
  Mji wa Pemba ni mji ambao bado haujaingizwa vizuri kabisa katika uchumi wa nchi na umeendelea kubakia mahali penye kuahidi mafanikio bila kuyatoa. Chini ya Serikali ya CHADEMA Pemba itatengwa maalumu kuwa kitovu cha biashara ya mambo ya fedha (Financial Centre) ili kushindana na maeneo kama ya UAE, Saudi Arabia, Qatar n.k Lengo letu ni kuhakikisha kuwa Pemba inakuwa ni makao makuu ya taasisi mbalimbali za kifedha na makampuni mbalimbali. Ili kutimiza adhma hii

  Kuanzia Bajeti ya 2011/2012 upembuzi yakinifu utafanywa ili kuona ni jinsi gani mkongo wa mawasiliano ambao unapita katika bahari ya Hindi unaweza kuchepushwa kuelekea Pemba na hivyo kuipatia Pemba njia za ‘fibre optics’ na kurahisisha mawasiliano.

  Kwa kushirikiana na Serikali ya Zanzibar utawekwa mfumo maalum wa kodi mbalimbali kwa ajili ya Pemba kuwa kivutio cha uwekezaji wa taasisi za fedha. Lengo ni kufanya Pemba kuwa ni eneo la unafuu wa kodi (Tax Haven) kwa makampuni ya ndani na ya kimataifa. Ili kuhakikisha hili linafanikiwa tutahakikisha kunakuwepo na umeme wa kudumu, huduma safi ya maji, tiba na udhibiti wa kisasa ili kuhakikisha kuwa Pemba haitotumiwa na wahalifu wa kimataifa katika masuala ya kodi.

  Kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Serikali ya Muungano itahakikisha kuwa miji ya Chake Chake na Wete inapatiwa ujenzi wa majengo ya kisasa pamoja na miundo mbinu ya kisasa na huduma za kuaminika za usafiri kati yake ya
  Tanga.

  Ni wazi kwamba, kwa vile Serikali hiyo ya CHADEMA haijaundwa basi wale wagombea na wabunge wa CHADEMA wanaendelea kusimamia na kupigania yale. Je, haya ni bora kulinganisha na yale yanayopendekezwa na CCM na CUF? Nina uhakika wapo watu Zanzibar ambao hawakubaliani na siasa za CCM wala zile za CUF na kwa muda mrefu wamekuwa wakisubiri nafasi ya kuchagua kitu kingine.

  Lakini, hakuna mtu atakayekuja kutoka akhera kuwaambia nani wamchague; hatakuja mtu kutoka peponi kuwaambia waangalie chaguo jingine. Wao wenyewe kama binadamu wenye uwezo wa kufikiri wanatakiwa kuitikia wito wa kihistoria wa kuangalia kama kuendelea na watu wale wale, wenye sera zile zile na kutoka chama kile kile kumekuwa na manufaa kwao. Wafanye ambacho Watanzania wengine wamekifanya hata sehemu ambazo ziliaminika ni ngome za CCM; waliikataa.

  Wananchi wa Uzini wakituma ujumbe huo watakuwa wamewapa wananchi wa Zanzibar kile ambacho Mapinduzi yalipigania yaani uhuru wa kuamua na kuwa na utu bila kulazimishwa kufanya siasa ambazo hazina manufaa. Hili nina uhakika litafanywa na wazee na vijana na kuwa wataamua kuendelea kuambia kuwa njia pekee ni hizo mbili walizozizoea kwa karibu miaka hamsini sasa au kuna njia ya tatu bora. Nani atawaongoza? Je, itakuwa ni sawa na kusaliti? Je, kuchagua chama kingine nje ya CCM na CUF ni kutokuwa mwaminifu kwa Zanzibar? Well, kila kitu kina mwanzo wake, na tusipoangalia tunaweza kuwa mashahidi wa kitu kipya kabisa Zanzibar!

  Zanzibar imepewa chaguo la tatu!

  SOURCE: Raia Mwema
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Jan 27, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,396
  Trophy Points: 280
  Well nikweli wamepewa chaguo la tatu; maana kwa muda mrefu wanalazimishwa kuchagua kati ya vitu viwili pekee; CHADEMA inawapa chaguo la tatu.
   
 3. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #3
  Jan 27, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Hapana Mwanakijiji, Chadema inawapa chaguo la pili; chaguo la kwanza ni CCM/CUF ambao waliamua kuzika tofauti zao na kuwa kitu kimoja.
   
 4. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #4
  Jan 27, 2012
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Mmh? Mzee Mwanakijiji unafikiri kweli Chadema inaweza kukubarika Zanzibar? maana kila nikiwaza propaganda zilizoenezwa na CCM kwa kushirikiana na CUF kuwa CDM ni chama cha kidini na ni chama cha kikanda....alafu napiga picha wananchi wa pemba na unguja
  kwa jinsi walivyoishika dini ya kiislaam na kwa wanavyoipenda CUF huku ukizangatia wengi wao walivyo na uelewa mdogo! Sidhani
  kama CDM inaweza kubalika Zanzibar. Anyway huu ni mtizamo wangu tu....niko teyari kusahihishwa
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Jan 27, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,396
  Trophy Points: 280
  Mshikachuma, chama chochote kingine kinaweza kukubalika Zanzibar. HIstoria inaonesha hivyo. Zanzibar haijawahi kuwa sehemu ya vyama viwili tu. Ni baada ya kurudi kwa vyama vingi ndio watu walilazimika kugawanyika katika makundi ya sehemu mbili tu ama uko CCM au uko CUF. Lakini kuna watu wengi tu wasiokubalia na na CCM au CUF. Sasa baada ya CCM na CUF kuwa upande mmoja (kama Mag3 anavyoonesha) ni wazi kuwa bado wapo watu wanaotafuta chaguo mbadala la ushirika huo. Naamini CDM ikicheza vizuri na kuzungumza lugha tofauti (siyo haya ya kuimba "anti Muungano, anti-Tanganyika) nina uhakika wapo watu ambao wataiunga mkono.
   
 6. T

  Topical JF-Expert Member

  #6
  Jan 27, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kwanza hii makala mwandishi ni wewe mwenyewe..reading between the lines??

  Halafu una weka comment wewe wa kwanza..kazi kwelikweli (talking about...)

  Swala la msingi chadema wako tayari kushiriki SUK wakishinda? then wakubali kuolewa kama wanavyosema (popular saying)
   
 7. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #7
  Jan 27, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,696
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Is it a must kushiriki kwenye hiyo serikali? Au maana ya SUK ni kutawala nchi without checks and balance? UK wana serikali ya mseto still labour ni wapinzani!
   
 8. k

  kicha JF-Expert Member

  #8
  Jan 27, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 511
  Likes Received: 536
  Trophy Points: 180
  unajua nyie chadema mie nashindwa kuwaelewa kabisa, haki hizo za zanzibar ambazo umezitaja kuwa chadema watazishughulikia ni kweli kua kila kukicha zanzibar inalia nazo, cha ajabu wanapoziwakilisha ndo nyienyie mnaoanza kuwaponda na kuona kama si watu, mara sawa na kigamboni na mengine mengi, ninavoelewa mimi ktk kutafuta ukombozi si wapiganaji wote ni wahalisia wengine ni vibaraka na wasaliti hata zanzibar na sehem yoyote duniani wapo mkiwemo nyie chadema mifano mnaielewa mnavolia na kina shibuda na wengineo, sasa hii dhambi ya kujifanya mnauhubiri ukweli wakati haupo moyoni ndo inayoangamiza hilitaifa la tanzania ambalo viongozi na serkali vimekua vkilaumiwa kila leo kwa kushindwa kujali utaifa na maslahi ya mwananchi wa kawaida wa hali ya chini, mifano iko mingi kulithibitsha hili, binafsi nawaheshimu baadhi ya viongozi wa chadema kwa vitendo na kauli zao zenye nia safi hata kwa macho tu unaweza kupata hisia hizo, lkn kiukweli wengi ya wanachama wengine mkiwemo humu jf mnakua mna ushabiki mwingi tu na porojo kwa sababu hakuna kimblio jengine kwenu kutokana na mateso ya ccm.miongoni mwa wanachoona tatizo zenji ni muungano so wanapojaribu kutoa hisia zao wasionekane watu wa ajabu, ni sawa na mh lema au na wengineo wanapodai haki zao kwa mikoa na taifa lao dhidi ya ya ufisadi, na mengineyo.
   
 9. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #9
  Jan 27, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Chadema Zanzibar itakubalika tu labda muungano ufe
   
 10. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #10
  Jan 27, 2012
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Fafanua kwa kutujengea mahoja! itakubalika ki vipi? ikiwa karibu wananchi wote wa ZNZ wamelishwa propaganda dhidi ya CDM?
   
 11. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #11
  Jan 27, 2012
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Topical,unaushahidi gani kama huyu aliyeandika makala hii ni Mzee mwanakijiji? maana kusoma between the line au mpangilio
  wa maandishi hakuwezi kufanya aliyeandika ni Mzee mwanakijiji.
   
 12. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #12
  Jan 27, 2012
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Mzee mwanakijiji,ahsante na nimekuelewa! ila sijaridhika na ulichokisema! naona kama umenipa majibu mepesi kwenye maswali
  magumu. Tukubari tukatae jamii ya kiislaam imelishwa propaganda yenye sumu kali sana against CDM! unakumbuka uchaguzi
  wa mwaka 2010? unakumbuka uchaguzi mdogo wa Igunga? Unakumbuka tamko la BAKWATA kuhusiana na mama Fatuma kimario? Unasikiliza yanayosemwa na Radio Imani na Radio Kheri?....yaani sumu waliyoimwaga ccm dhidi ya CDM kwa hawa ndugu
  zetu'Mungu ndiyo anajua! cha kusikitisha na hawa ndugu zetu wamekubali na wanaiona CDM kama hadui yao namba moja....au
  utafikiri hiyo CDM ndiyo inatawala kwa sasa au utafikiri hiyo CDM imewahi kutawala nchi hii na wakati inatawala imewahi kufanya
  jambo baya sana dhidi ya hawa ndugu zetu. Kwahiyo ukinipa majibu mepesimepesi kuwa CDM inaweza kukubarika ZNZ bila kwanza
  kuangalia na kukumbuka hayo yote niliyokuorodheshea hapo juu itakuwa tunadanganyana mchana kweupe!
  Binafsi nitapenda sana oneday CDM ikubalike Zanzibar
   
 13. c

  chakupewa Member

  #13
  Jan 27, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo ninaloona ni moja tu, ni kutumia mtandao zaidi kuliko uhalisia, Wazanzibari wanasifa/aibu moja tofauti na watanganyika, wao wanataka wakuone, wakupime, ikiwemo kukuuliza na kuwapa jawabu, ili wajue mustakbali wao, watanganyika ni rahisi kuwapiga propaganda na kukufuata, sasa chadema waende Zanzibar wakutane na wazanzibari, pengine linaweza kuwa chaguo la tatu, na ikiwezekana "CHAUSITA" nao waende wawe chaguo la nne, hapo demokrasia itakuwa kede kede.

  Ila lazima waelewe pale ni chimbuko la siasa, wanaoweza kupanga mipango ya pale na kuwasukuma Wazanzibari ni wamarekani na waingireza tu kwa ushirikiano wao
   
 14. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #14
  Jan 27, 2012
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0

  mmh! kwahiyo wataka kutuambia CDM na vyama vingine hawawezi kuiteka siasa ya zanzibar hadi wawashirikishe US na UK?
  Hebu tufafanulie kidogo....naona kama umetuacha njia panda
   
Loading...