Wananchi wa Bumbuli waanza kumchoka January Makamba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wananchi wa Bumbuli waanza kumchoka January Makamba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by NOT FOUND, Mar 20, 2011.

 1. NOT FOUND

  NOT FOUND Senior Member

  #1
  Mar 20, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 158
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Habari zenu wana J.F

  Wiki iliyopita nilikuwa Bumbuli jimboni kwa ndg Makamba, kwa kweli niliyoyakuta huko ni mambo ya ajabu.

  Bumbuli ni sehemu ambayo naifahamu vilivyo kutokana na kuishi huko miaka kadhaa wakati nikisomea Medical Assistant pale COTC na Baadae kufanya kazi Bumbuli Hospital.

  cha kwanza barabara ya kufika huko ni mbaya huwezi ukaamini, yaani wakati wa mvua huwa gari zinaishia umbali wa kilometa 30, kutoka bumbuli stend katika eneo la Soni.

  Pia kuna shida ya maji utadhani ni jangwani, jimbo hili lina mito na chem chem kila kona lakini sasa hivi chem chem zote zimekufa kutokana na ukataji wa miti uliokithiri, na hata mto mkubwa uliopo haujafanyika utaratibu wowote wa kuvuna maji ya kuwasaidia wananchi.

  Baada ya kukupa hiyo intro fupi, sasa twende upande wa pili wa niliyoyakuta kuhusu ndugu Januari.

  Kwanza kabisa huyu jamaa mara baada ya kupitishwa (HAKUPIGIWA KURA KWA KUWA ALIKUWA PEKE YAKE) kuwa Mbunge, alihamisha ofisi ya mbunge kutoka Bumbuli na Kuipeleka Soni, tafsiri ya wengi hapa ni kwamba amekimbia kukaa na wananchi wake kwani Bumbuli ni katikati ya Mgwashi na Soni tarafa ambazo pia ni sehemu ya Jimbo hili.

  ikumbukwe kwamba tangu kuanzishwa kwa jimbo la Bumbuli miaka zaidi ya 15 iliyopita, ofisi ya Mbunge ilikuwa pale pale Bumbuli, lakini ndg Januari alipochukua ubunge akaamua kuihamisha na kuipeleka sehemu ambapo access na wananchi wake ni ndogo sana.

  Suala la pili ambalo nimelipata kutoka kwa vijana wengi waliokuwa wakimpigia debe Januari wakati wa kura za maoni, ni kwamba Ndg Januari ameanza kujivuna kupita maelezo, kiasi kwamba wale vijana ambao alikuwa nao bega kwa bega usiku kucha katika kuhakikisha kwamba mzee Shelukindo anang'oka, aliwatupilia mbali.

  Katika kulithibitisha hili, Ndg Januari alitembelea vijiji vilivyoko maeneo ya jirani na pale wanapotoka (Mahezangulu), wakati anaondoka, alipopita Bumbuli, alijidai kasinzia kwenye gari ili asiweze kusalimiana na wananchi ambao kipindi cha nyuma alikuwa na mazoea kusalimiana nao.

  Zaidi ya hayo jamaa hana mikakati yoyote ya Maendeleo kwa jimbo lake, vijana wengi wameponda utaratibu alioanzisha wa kuwasiliana na wananchi wake kwa namba ya simu hizi za kutuma ujumbe kwenda 15***, pamoja na kuwasiliana nao kwa kupitia website kwa kuwa sehemu kubwa ya wananchi wake ni masikini ambao hawana hata umeme na hata mtandao wa simu kupatikana ni kwa shida.

  Pia imedaiwa kwamba ndg Januari amekuwa akitembelea shule zilizopo ndani ndani na kuishia kukagua madaftari ya wanafunzi badala ya kuhakikisha anaanzisha utaratibu wa upatikanaji wa vitabu na walimu.

  Pia kubwa lingine ambalo wananchi wamemponda na kuanza kumchoka ni kwamba, baada ya kuapishwa kuwa mbunge, hajawai hata kujitokeza kuwashukuru wananchi wake kwa kuamua kumuunga mkono, jambo hili limewakera vijana na wazee wengi wa jimbo la Bumbuli kiasi cha kusema kama ataendelea hivi hivi asahau kuchaguliwa tena mwaka 2015.

  Vijana wengi ambao walimpachika jina la Obama wa Bumbuli, sasa hivi wameanza kumpa majina mengi kama Shalo Baro, Brazamen, Bishoo n.k, kutokana na kitendo chake cha "kuwapotezea" na "kujidai"

  KUFUATIA MAMBO HAYA YALIYOJITOKEZA, KUBWA LIKIWA LA KUHAMISHA OFISI, KUWACHUNIA WANANCHI, NA KUTOKWENDA KUTOA SHUKRANI, LIMEIBUKA KUNDI KUBWA LA VIJANA AMBAO WAPO KWENYE MCHAKATO WA KUMWANDIKIA BARUA MWENYEKITI WA CHADEMA MH. MBOWE PAMOJA NA KATIBU MKUU DR. SLAA, ILI WAWAPE SUPPORT YA KUFUNGUA TAWI LA CHADEMA BUMBULI, VIJANA WENGI WALISIKIKA WAKISEMA "TATIZO SIO SHELUKINDO, TATIZO SIO JANUARI, TATIZO NI CCM"

  MY TAKE:
  INGAWA MIMI SIO MZALIWA WA BUMBULI, LAKINI KWA KUWA BUMBULI NI SEHEMU AMBAPO NIMEISHI NA KUFANYA KAZI, NIMEKERWA NA KITENDO CHA NDUGU JANUARI KUWASUSA WANANCHI WAKE, HUKU AKISIKIKA KWENYE VYOMBO VYA HABARI KUHUSIANA NA SUALA LA DOWANS NA TANESCO, PAMOJA NA LILE LA KUHAMISHA OFISI ILI ASIWEZE KUSIKILIZA MATATIZO YA WANANCHI WA BUMBULI.

  NAWAPA SUPPORT VIJANA WALIOAMUA KUANZISHA MCHAKATO WA KUFUNGUA TAWI LA CHADEMA BUMBULI, KWA KUWA NDUGU JANUARI AMESHAONA YA KWAMBA UWAKILISHI WAKE KWA WANA BUMBULI, HAUNA UPINZANI KWANI HATA KUSIMAMA KWENYE UBUNGE ALIKUWA MGOMBEA PEKEE ALIYEPITA BILA KUPINGWA.
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Mar 20, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Where is Selemani when you need him?
   
 3. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #3
  Mar 20, 2011
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,483
  Likes Received: 764
  Trophy Points: 280
  Swali ni moja tu? hivi baada ya kuandika haya umejisikiaje?
   
 4. M

  MZAWATA JF-Expert Member

  #4
  Mar 20, 2011
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 555
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  mkuu ww ni shujaa na mkweli, huyu jamaa washamchoka longtime kwan huyu kijana kwa anakoelekea ni sawa na baba yake tu
   
 5. C

  CHESEA INGINE Senior Member

  #5
  Mar 20, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 180
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Na bado ni asubuhi!
   
 6. only83

  only83 JF-Expert Member

  #6
  Mar 20, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
   
 7. Lukansola

  Lukansola JF-Expert Member

  #7
  Mar 20, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 5,456
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Kwani wewe umekisiaje baada ya kuandika haya?
   
 8. U

  Uswe JF-Expert Member

  #8
  Mar 20, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  wakome, walikua wanampigia d
  ebe wa nini, 'if you dont use your brain you will use your feet' wacha wahifunze kwanza
   
 9. n

  nndondo JF-Expert Member

  #9
  Mar 20, 2011
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 1,250
  Likes Received: 535
  Trophy Points: 280
  Hata mimi nimefurahishwa sana na matendo ya January kama kweli ndio haya, maana hakuna watu wanafiki kama wananchi wa Bumbuli, yaani mzee wa watu kaongoza vita kubwa sana dhihi ya unyonyaji wetu sisi wote, walichofanya ni kumdhalilisha kwa namna ya ajabu leo wanasema nini? kwanza nasikia hao wenyewe huko sio kwao dingi alikuja kutoke iringa kama manamba, sasa leo wanamtakia nini. Heko January mwendo mdundo kama watu wenyewe hawana internet ama skype na hawajanunua ipads sasa wewe ufanye nini? kwanza kitabu chenyewe cha kuwaombea misaada umekiandika kiingereza sasa kama wao wanajua kisambaa tu wewe ufe? halafu watamchaguaje muwakilishi asiyeongea lugha yao? imekula kwao teh teh tehe kweli wajinga ndio waliwaao.. kula kwa kwenda mbele hayo mambo ya 2015 watajiju wakati huo dili lako la Dowans litakua lisha tiki huku wao umaskini ukwaparami mpaka kwenye kope
   
 10. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #10
  Mar 20, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  janu endelea na kasi hiyo mpk 2015, usilegeze
   
 11. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #11
  Mar 20, 2011
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0


  You don't get any better niggler. All we ever see from you is this half baked mystical twaddle.

  Why don't you actually stop and analyse the stuff you write before you post it?   
 12. S

  Selemani JF-Expert Member

  #12
  Mar 20, 2011
  Joined: Aug 26, 2006
  Messages: 871
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Hamkuweka mgombea 2010 (Slaa ain't no dummy), and I double dare you kuweka mgombea Chadema Bumbuli 2015, u will be obliterated. Thats all I can say.

  The rest is nonsense! Hii post imekaa kimajungu.

  Waswahili bhaana, u blame Mbunge for actually visiting schools and look at madaftari ya wanafunzi. What is wrong with that? lol. Some majungu are so stupid. Kama unataka kumpiga mtu fitina, find something tangible.

  By the way, ungekuwa kada wa CCM, wadau wa Chadema humu ndani wangekwambia UMETUMWA wewe--your 7th post jamvini ni jungu.
   
 13. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #13
  Mar 20, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Nimjuavyo huyu January ataishia kuwashangaa wananchi anaowawakilisha kama alivyojishangaa yeye na wabunge wengine kuingia mjengoni (Bungeni). Yakimkuta yaliyomfika Mmarekani mwenzie Masha ndiyo atapokoma kushangaa.
   
 14. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #14
  Mar 20, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mkuu hii msg ungeandika kisambaa halafu tukaisambaze bumbuli... mijitu haitumii akili hata kidogo!!!:smash:
   
 15. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #15
  Mar 20, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,465
  Likes Received: 19,847
  Trophy Points: 280
  kula bata mreya janiuarya makeimba.
  Sharo Biiiiii
   
 16. Mzee Wa Rubisi

  Mzee Wa Rubisi JF-Expert Member

  #16
  Mar 20, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,754
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Mchumia juani..............
   
 17. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #17
  Mar 20, 2011
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,795
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Wanalo Hilo! Waliambiwa hawakusikia. Fulana, Kofia na Pilau Vikawaponza. Na Bado!

  'sasa waliaa,
  ati wasema umepata mume kachalaa,
  walia nini ee,
  shauri yako Mume umemchagua mwenyewee x 2...'
   
 18. xhuma

  xhuma Member

  #18
  Mar 21, 2011
  Joined: Aug 22, 2010
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Selemani kuna harufu ya hasira kwenye hili jibu lako, sasa majungu yapo wapi hapo? Mbunge hajawezesha wananchi wake, hawana simu na sehemu kubwa haina umeme wala maji halafu anawaambia wamtumie kero kwa meseji, hiyo njia ya mtandao aliyoweka anajua asimia ngapi kule bumbuli ina uwezo wa kupata mtandao wa intanet? kama unamsaidia kujibu jibu hoja na uoneshe lipi ni jungu sio kuchanganya kiswahili na kingereza, wengine hata hatukuelewi!
   
 19. S

  Selemani JF-Expert Member

  #19
  Mar 21, 2011
  Joined: Aug 26, 2006
  Messages: 871
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Ushabiki ukizidi tunakuwa kama wehu. Najua hili ni jamvi la Chadema, but irrationality will not save us.

  Umesema Bumbuli kuna shida ya maji na barabara mbovu, halafu u blame Mbunge Makamba (Who was just elected last year) and then you go and praise Mzee Shelukindo kuwa ni mpiganaji but he was mbunge for 15 years? How do u explain that kind of intellectual dishonesty?

  Huku Tegeta kwetu kuna shida ya maji, as the matter of fact, tunanunua maji kila siku. But It would be stupid to blame that on Halima Mdee, she just started ubunge.

  Maybe its not really worthy arguing with this kind of thinking/posting. The motive of mtoa mada ni kupaka matope.

  Mtoa hoja anasema mbunge hana mikakati yoyote ya kuleta maendeleo, this is FALSE. Mtoa hoja kaamua kutudanganya, mipango ya kuleta maendeleo ipo hadi kwenye kitabu. Ukiamua kupiga fitina ungesema kwamba mipango ya kuleta maendeleo haitekelezeki, hapo labda tungekuelewa. Ndio maana nikasema hii post imekaa kimajungu.
   
 20. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #20
  Mar 21, 2011
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Nimetaka kushangaa wiki iishe bila the usual January bashing!

  JF imezidi kwa wivu maana sioni sababu hapa ni purely wivu. Kuna mpunge wa rufiji tangu aingie keshafanya nini?

  Man this hate is beyond reason
   
Loading...