Wananchi Msizomee CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wananchi Msizomee CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kichankuli, May 16, 2009.

 1. Kichankuli

  Kichankuli JF-Expert Member

  #1
  May 16, 2009
  Joined: Dec 18, 2008
  Messages: 856
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 45
  Jana mwenyekiti wa UDP Bwan John Momose Cheyo almaaruf Bwana Mapesa alinukuliwa akiwaambia wapiga kura wa Jimbo la Busanda kuwa wasiwazomee Viongozi wa CCM badala yake wawaambie "stop this non-sense". Mimi nilishindwa kumwelewa Bwana Mapesa alimaanisha nini kwa sababu mpaka wananchi wafikie kuzomea inamaana kinachoongewa na viongozi wa CCM kimeonekana kwao kuwa ni upuuzi. kwa hiyo kuzomea ni namna moja wapo ya kufikisha ujumbe kwa wahusika kwani wengi wa wapigakura hao hawafaamu lugha ya kiingereza (achilia mbali kutokuwa na Runinga wala fedha za kununulia magazeti kama alivyowabezxa Bwana Mkuchika) ambacho kingewawezesha kustopisha hizo non sense.Pia wangeweza kupiga makofi yasiyo na kikomo, kupiga kelele ya kumtaka mwogeaji asiendelee kuongea (japo hizi zinaweza kukusababishioa kuwekwa chini ya mikono ya polisi wa CCM wasiojua haki ya raia wa nchi hii)au kuondoka kwenye kikao
   
 2. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #2
  May 16, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Baba wa Taifa alishatushauri kwamba iwapo mtu mbabe ataendeleza kufanya ujinga wake basi dawa yake ni KUMZOMEA TU!

  Huyu Mapesa namtiliashaka sana siku hizi tangu awe mwenyekiti wa kituo cha demokrasia hasa zile senti alizokuwa anapewa na ccm kwa kisingizio cha kuimarisha kituo... nachoka kweli kweli

  Kwa kauli ya mapesa basi wazee wa propaganda watakuja wakisema kuwa wanaozomea ni wanachama walioshindwa kukubalika ndani ya chama.....

  Ah, nawaza tu!
   
 3. M

  Mafuchila JF-Expert Member

  #3
  May 16, 2009
  Joined: Apr 29, 2006
  Messages: 752
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Wasi wasi wangu ni kuwa, wanaozomea ni watu walioishiwa hoja, Wapinzani wana hoja za nguvu dhidi ya CCM. Suala la kushabikia kuzomewa kwa viongozi wa CCM na wale wanaodaiwa ni 'wananchi wenye hasira kali', linaweza kuigwa na makada wa CCM kwa kujificha kwenye kivuli kile kile cha 'wananchi wenye hasira kali'. Hili likifanyika, basi wapinzani ndio watakaokosa katika huu mchezo mzima wa kuzomeana majukwaani.
   
 4. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #4
  May 16, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Hapa umeongea "point" ila surfix ya "less" inaongezwa na ukweli kuwa asilimia kubwa ya wanabusanda hawaitaki ccm na wao wanajuana, sasa inakuwa ni vigumu kwa CCM wachache wa Busanda kuwa over power wananchi wote ambao wanataka mabadiliko. Hilo CCM hawawezi kulifanya sema wao wanaweza kusubiri mpaka siku ya kupiga kura halafu wakajitangaza wameshinda na kumwaga askari walinde amani kwa muda wa miaka miwili mpaka uchaguzi wa 2010. Hilo CCM wanaliweza kabisa kwani kwao amani ni second priority baada ya kulazimisha yale wanayoyataka wao unakumbuka Chaguzi za Zanzibar 1995,2000 & 2005?, jamaa hawakushinda ila walifanya yale ambayo huko mbeleni yanaweza ligharimu Taifa letu.

  Ni rahisi sana kutumia Bunduki na mabomu kutuliza watu wasifanye fujo lakini ni ngumu sana kutumia bunduki na mabomu kuwafanya watu wakusikiliza kama kiongozi wao na hatimaye kuendeleza nchi.

  Kwao CCM huu uchaguzi wa Busanda ni "lazima tushinde kwa vyovyote", kwani kushindwa vibaya ni picha mbaya kwa uchaguzi wa mwakani kwani hatutakuwa na Legitimacy ya kumanipulate "counts" na hivyo itakuwa ni hali ngumu kwetu.

  Hebu fikirini jinsi ambavyo watanzania wengi wa leo wanavyokuwa na furaha pale ambapo CCM inaposhindwa uchaguzi (TARIME). Dhahili kuwa CCM yangu ile iliyonifundisha Chipukizi sasa hivi haipendwi na mfano ninajiona mimi mwenyewe ambaye niliisha kuwa mwenyekiti wa vijana wa CCM katika shule moja ya sekondari kabla ya matawi ya umoja wa vijana kufutwa mashuleni baada ya kuanzishwa mfumo wa vyama vingi.

  Ukweli ni kwamba CCM itashinda urais kwa sababu ni rahisi sana kucheza na hesabu kutoka vijijini ila tunahitaji wabunge wengi wa Upinzani ili watuletee changamoto katika kuendesha nchi kwa misingi ya haki na usawa. Chama kimevamiwa na mamluki wa kutaka kujinufaisha binafsi hivyo hakina budi kikae kando na kujijenga upya, kwani hawa mamluki ni kama "Changudoa" anakupenda ukiwa katika nafasi ya kumpatia anachokitaka ukiishiwa anamfuata mwenye nacho. Ninaamini njia pekee ya CCM kujirekebisha ni kuwa nje ya madaraka hata kwa muhula mmoja ili wababkie wale wenye chama kwani kunguni wote wataachia ngazi kwa kukosa damu ya kunyonya.
   
 5. Makonyagi

  Makonyagi Member

  #5
  May 16, 2009
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wewe mlevi kweli wewe
  naona umeishiwa na hoja
   
 6. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #6
  May 16, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Watazomea kwenye boksi la kura? Hapo ndipo pana umuhimu.
   
 7. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #7
  May 16, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,596
  Likes Received: 3,887
  Trophy Points: 280
  we need new generation in these kind of political parties, hawa akina cheo(yo) Mrema, Lipumba wamesha exprire.The only thing that we are witnessing is fighting within this opposition parties.Jesus said "If a kingdom is divided against itself, that kingdom cannot stand.
   
 8. E

  Emma M. JF-Expert Member

  #8
  May 16, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 207
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuzomea kuna nafasi yake.
  Ni njia mojawapo ya ku-send message.
  Keep it up wananchi.

  Emma,
   
 9. Kichankuli

  Kichankuli JF-Expert Member

  #9
  May 16, 2009
  Joined: Dec 18, 2008
  Messages: 856
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 45
  Siyo kila uigaji kila mara unaweza kukuletea matokeo chanya, Tarime si waliiga kuruka na kutuo na Helkopta kwani waliambua nini. Wenye hoja wako wapi ambao wanawaambia wapigakura kuwa hawawezi kuangalia Runinga kwa sababu hawana umeme, hawawezi kusoma magazeti kwa sababu hayafiki na hata kama hayafiki hawana uwezo wa kuyanunua huku upande mwingine mwenzake akiwaeleza wapigakura kuwa wakimchagua mgombea wa CCM wataletewa umeme na kupatiwea mikopo ya SEDA.

  Kuna maneno mengine yanachoma roho hadi mtu mnafikiria kumpiga mtu manati
   
 10. M

  MtazamoWangu JF-Expert Member

  #10
  May 16, 2009
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 313
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  dalili zote zinaonyesha CCM wamechemsha na serikali ya bwana JK haina jipya..hapendwi ndani na nje ya chama..na hii ni ile zana aliyosema mwalimu kwamba zambi ya ubaguzi haiishi...JK alileta makundi ndani ya chama na wale aliokuwa nao kundini nao wameanzisha makundi yao....ni mtihani sana kwa CCM sasa hivi, kwani ili tuwakubali inabidi wafanye yale wasioyataka ikiwa ni pamoja na kuwatoa kafara wazamini wao.........
  bwana mapesa naekuna wakati anachemsha ila tusisahau unafiki wa kisiasa...we may not be with those who we think they are with us...wanachi waendelee kuwazomea tu maana inatuma ujumbe unaotakiwa....hata akienda JK wamzomee tu kama kule mbeya...unafiki mtupu...
   
 11. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #11
  May 16, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Maneno mazito sana, sasa hii zomea zomea kama ni kweli ni ya wananchi wa Busanda, nitaamini baada ya matokeo ya kura kwenye box na hapo ndipo wananchi wa Busanda watahitaji kupewa nafasi kuelimisha wananchi wengine wote wa Tanzania, as long as hao wazomeaji sio vijana 70 walowezi toka Tarime.

  Respect.

  FMEs!
   
 12. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #12
  May 16, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Mkuu sijakuelewa ktk maneno bold hapo?
  kuna ushahidi wowote kuhusu hao vijana walowezi 70 kutoka tarime???
   
 13. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #13
  May 16, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Kwani wewe umeweka ushahidi wowote wa kuzomewa kwa CCM? By the way unalala saangapi mkuu maana 24/7 umo humu Duh! Samahani kwa kukukwaza na hili swali lakini I am just curious! I mean you are all over all the times, Damn!

  FMES
   
 14. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #14
  May 16, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Ushahidi si ni sisi m wenyewe kutumia ocd kuwakamata makada wa chadema?
   
 15. M

  Magezi JF-Expert Member

  #15
  May 16, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  wananchi wa busanda mimi nawaomba wawe waangalifu ktk kupiga kura na kuzilinda. CCM ni maarufu sana kwa kuiba kura hasa vijijini sana. CHADEMA kueni waangalifu kwani mliweza kuwadhibiti tarime wembe ule ule utumike Busanda.

  Lazima mwangalie CCM kupitia tume ya uchaguzi wanaweza ku-locate majina sehemu wanazojua kwamba wapenzi wa CHADEMA hawata piga kura, hili nalo mliangalie kwa makini.
   
Loading...